Mkutano mkubwa injili kutoka kwa Mhubiri Maarufu wa Kenya Nabii Ezekiel Odero uliokuwa ukiendelea wapigwa stop na Serikali

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,252
20230713_164551.jpg


Mkutano mkubwa wa Injili uliokuwa ukiendelea katika viwanja vya shule ya msingi Ngarenaro jijini Arusha na Mhubiri maarufu toka Kenya Nabii Ezekiel Odero umepigwa marufuku na serikali mchana huu.

Wakiwa katikati ya mahubiri ghafla ilitangazwa kuwa ni marufuku kuendelea na maombi hayo jambo liloshtua idadi kubwa ya watu walio kuwa wakisikiliza mahubiri hayo.
Idadi kubwa ya watu waliokuwa wametoka mikoani Walipigwa na Butwaa wasijue cha kufanya na wapi waende.

Awali Nabii huyo Akiongea na wandishi wa habari jijini hapa juu ya Ujio wa mkutano wake wa kiinjili ,aligoma kuzungumzia masahibu yaliyompata nchini kenya akihusishwa na sakata la mchungaji mwenzake,Paul Makenzie anayeshikiliwa na polisi akihusishwa kusababisha vifo vya raia wa Kenya zaidi ya 300 wasio na hatia ambao walikuwa waumini wake.

Mhubiri huyo ambaye anakanisa lenye uwezo wa kuingiza waumini elfu 45 kwa mkupuo mmoja nchini kenya, ameahidi kusaidia ufadhili wa kukarabati madarasa yenye changamoto katika shule hiyo Ya Ngarenaro baada Ya kubaini kwamba upo uhijitaji wa kuboresha shule hiyo.

Mchungaji Ezekiel ambaye ni mkazi wa Mombasa nchini Kenya,alisema kuwa amekuja Tanzania ikiwa ni mara yake Ya tatu kufanya mkutano na hiyo ni kwasababu ni taifa analolipenda na watu wake ni wakarimu sana wenye upendo na akikupenda amekupenda kweli na sio unafiki .

Alisema lengo ni kuja kuhubiri injili Ya Yesu kristo juu ya wokovu ,ukombozi , miujiza na ishara peke yake na huo ndio ujumbe wa yesu alioutoa.

Mchungaji Ezekiel aliwaomba wenye Dhambi waachwe waje kanisani ili wabadilike .kanisa langu wanakuja watu wengi sana wenye Dhambi.
 

Attachments

  • DSC_1169.JPG
    DSC_1169.JPG
    592.5 KB · Views: 3
Mkutano mkubwa wa Injili uliokuwa ukiendelea katika viwanja vya shule ya msingi Ngarenaro na Mhubiri maarufu toka Kenya Nabii Ezekiel Odero umepigwa marufuku na serikali mchana huu.
Wakiwa katikati ya mahubiri ghafla ilitangazwa kuwa ni marufuku kuendelea na maombi hayo jambo liloshtua idadi kubwa ya watu walio kuwa wakisikiliza mahubiri hayo.
Idadi kubwa ya watu waliokuwa wametoka mikoani Walipigwa na Butwaa wasijue cha kufanya.
Wewe mgen hamjachoka kuuwa watu huko? Mnataka na wengine tena?
 
Kwa hekima tu, wazuiaji wa huo mkutano wasingejitokeza wao kutoa zuo, mkutano utakuwa una mwenyeji ambaye ndiye angetangaza kuwa hakuna mkutano utakaoendelea. Watu wasiohusika na mkutano huo kuvamia na kutoa katazo ni uhuni na ni fujo, bora polisi wangevamia na kuutawanya mkutano huo kwa yale mabomu ya machozi hata kama hawana maelezo ingeeleweka mkutano umevunjwa na polisi labda hauna kibali cha kukusanyika. Hekima na busara ni bora sana katika kuamua mambo kwa amani na upendo
 
Wazee wamafuta wamesaidiwa,,,isijekuwa nimwamposa amemfiti nabii mwenzake
 
Back
Top Bottom