Mchungaji Ezekiel Odero wa Mombasa aliyekuwa aje Tanzania ,Dodoma adakwa na Polisi kenya na kanisa lake kufungwa sa vifo kibao vya waliokufa wakifunga

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,904
Mchungaji Ezekiel Odero wa Mombasa aliyekuwa aje Tanzania ,Dodoma adakwa na Polisi kenya kuhusiana na vifo kibao vya waliokufa wakifunga

Mchungaji Ezekiel Odero ni mmojawapo wa watuhumiwa Kenya wasababisha vifo vya mamia ya watu ambao rafiki yake Mchungaji. MAKENZIE aliwazika shambani kwake porini liliko kanisa lake waliambiwa wafunge hadi wafe iki wakutane na Yesu walioambiwa na Rafiki yake Mchungaji Makenzie ambaye ni kidole na Pete na Mchungaji Ezekiel Odero wote wakuwa waliweka kambi Mombasa kwenye mapori walikonunua maeneo mama ya ekari

Alitarajia kuondoka Mombasa kuja Tanzania kuendesha mkutano wa injili Dodoma polisi wa Kenya wamemdaka leo Asubuhi na kufunga kanisa lake

Kwa Tanzania vyombo vya usalama viwe makini asije weka kambi huku hata akishinda kesi

Lakini pia niviombe vyombo vya usalama kuna Mchungaji mmo anaitwa Mbarikiwe Mwakipesile wa Kanisa linaitwa Kikosi cha Injili liko mbeya na limo online ana dalili zote za kuleta maafa kwa waumini

Huwavalisha waumini wake wote uniform akiwemo yeye uniform za rangi ya damu nyekundu.Wote huvaa nguo nyekundu

Kanisa lake liko eneo la Isyesye Mbeya Prevention is better than cure serikali imuwahi kabla hajafanya tukio.baya

Waumini wake ni kama misukule fulani hivi wako tayari kwa lolote analowaambia

Kuna clip kibao YouTube ana kesi nzito tu mahakamani serikali itumie hiyo kesi lumfungia huduma na kanisa wakimuacha kikitokea mbele wasije sema hawajastuliwa

Ana mwelekeo kabisa wa akina Kivwetere na wa huyo pastor Makenzie wa Kenya
 
Yeah watu kama Akina Mbarikiwa ni hatari kupita maelezo na wizara ya mambo ya ndani imwangalie kwa ukaribu sana Kuna wakati alikuwa analitukana sana kanisa la Assemblies of God
 
Jeshi la Polisi nchini Kenya limemkamata Mchungaji mashuhuri nchini humo, Ezekiel Ombok Odero wa kanisa la New Life Prayer Centre lililopo mtaa wa Mavueni mjini Kilifi kwa tuhuma za mauaji. Ofisi ya DCI imeeleza kuwa Pastor Ezekiel ametajwa kuhusika na vifo vya watu 98 vilivyotokea katika kanisa la Good News International Ministry la Mchungaji Paul Mackenzie.

Pia anatuhumiwa kwa vifo vingine vilivyotokea katika kanisa lake kwa kushawishi waumini wake kutorosha ndugu zao wagonjwa hospitalini na kwenda kuwaombea.

Katika tuhuma za kwanza, Pastor Ezekiel ametajwa kuwa mshirika wa Mchungaji Paul Mackenzie kwa kufanya mahubiri potofu ya kushawishi watu kufunga hadi kufa. Hapo jana mmoja wa wachungaji wasaidizi wa Ezekiel alisema kuwa Mchungaji Mackenzie alikua anafadhiliwa na Pastor Ezekiel na kwamba walikua na ushirika.

Akitoa maelezo yake mbele ya ofisi ya DCI, Mchungaji huyo ambaye polisi wamezuia kutaja jina lake, amesema Mchungaji Mackenzie alikua akilazimisha watu kufunga hadi kufa, na walipokufa Pastor Ezekiel alienda usiku wa manane kuchukua baadhi ya viungo vyao kabla ya kuzikwa usiku huohuo. Baadhi ya maiti zilizofukuliwa zimekutwa bila viungo kama sehemu za siri, ulimi, figo, ini, moyo etc.

Akaunti za benki za Mchungaji Mackenzie zimekutwa na ukwasi wa KSH Milioni 315, sawa na TZS Bilioni 5.5 ambazo ofisi ya DCI inashuku kwamba huenda zimetokana na biashara haramu ya viungo vya binadamu.!
 
😅😅😄😅😅😄
ninavyopenda kuslay mtu anivalishe sare kanisani??
kikosi_kazi.tv-20230427-0001.jpg
 
Back
Top Bottom