Dkt Slaa atoa wito kwa Viongozi wa dini zote na madhehebu yote na wananchi wote kwa ujumla kuhudhuria mkutano mkubwa wa kujadili hatma ya bandari zetu

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,505
51,107
WITO WA KUHUDHURIA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA: BANDARI ZETU! URITHI WETU!

Kwa viongozi wa dini zote na Madhehebu yote nchini Tanzania!

Sisi Watanzania tulioko ndani na nje tumeamua kulinda rasilimali za nchi tulizopewa na Mungu sisi na vizazi vyetu kama ilivyoanishwa kwenye Ibara ya 27 (1) na (2) ya Katiba yetu. Tunaomba waumini wote wafike kwa wingi na kuwaalika wengine kufika Mkutano Mkubwa wa Hadhara kupata elimu kuhusu Mkataba wa Bandari wa DP World siku ya Jumamosi 22 Julai 2023.

Viongozi wa dini, wanasiasa, mawakili, vyama vya kiraia na wanaharakati mbalimbali nchini watashiriki kwenye mkutano huo.
Taarifa itatolewa kuhusu mahali lakini muda ni kuanzia Saa 4 asubuhi mpaka saa 12 Jioni.

Imetolewa na
Dr. Wilbroad Peter Slaa, kwa niaba ya Sauti ya Watanzania (SYW).
Dar es Salaam, 14 Julai 2023
 
Mbona ameibuka gafla kutoka mafichoni huyu babu Slaa, tena ni mkosoaji mkubwa ktk kipindi hiki cha mama, mbona huko nyuma alinyamaza kimya, au kipindi chote hicho hakukuwa na ajenda yeyote ambayo ingekinzana na maoni yake, sio kweli analo lake jambo, suala la bandari limekuwa kama ni kisingizio tu.
 
Kama hicho kisingizio kina mantiki lazima asikilizwe, hatuwezi kuacha bandari zetu zote Tanganyika apewe mwarabu milele, halafu badala ya kuzikomboa tuanze kutazama usoni nani ni nani, muhimu bandari zetu kwanza mengine baadae.

Wewe kama unamjua malaika wako asie na doa, tutajie nasi tumjue, ukishindwa kumtaja, nenda kamsikilize Dr. Slaa hiyo siku ikifika.
 
Mbona ameibuka gafla kutoka mafichoni huyu babu Slaa, tena ni mkosoaji mkubwa ktk kipindi hiki cha mama, mbona huko nyuma alinyamaza kimya, au kipindi chote hicho hakukuwa na ajenda yeyote ambayo ingekinzana na maoni yake, sio kweli analo lake jambo, suala la bandari limekuwa kama ni kisingizio tu.
Kwani vibaya,, Mbona Wengine wamemgeuka Magufuri.
 
Mbona ameibuka gafla kutoka mafichoni huyu babu Slaa, tena ni mkosoaji mkubwa ktk kipindi hiki cha mama, mbona huko nyuma alinyamaza kimya, au kipindi chote hicho hakukuwa na ajenda yeyote ambayo ingekinzana na maoni yake, sio kweli analo lake jambo, suala la bandari limekuwa kama ni kisingizio tu.
Jikite kwenye anayo zungumza. Ya kweli au uongo?
 
WITO WA KUHUDHURIA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA: BANDARI ZETU! URITHI WETU!

Kwa viongozi wa dini zote na Madhehebu yote nchini Tanzania!

Sisi Watanzania tulioko ndani na nje tumeamua kulinda rasilimali za nchi tulizopewa na Mungu sisi na vizazi vyetu kama ilivyoanishwa kwenye Ibara ya 27 (1) na (2) ya Katiba yetu. Tunaomba waumini wote wafike kwa wingi na kuwaalika wengine kufika Mkutano Mkubwa wa Hadhara kupata elimu kuhusu Mkataba wa Bandari wa DP World siku ya Jumamosi 22 Julai 2023.

Viongozi wa dini, wanasiasa, mawakili, vyama vya kiraia na wanaharakati mbalimbali nchini watashiriki kwenye mkutano huo.
Taarifa itatolewa kuhusu mahali lakini muda ni kuanzia Saa 4 asubuhi mpaka saa 12 Jioni.

Imetolewa na
Dr. Wilbroad Peter Slaa, kwa niaba ya Sauti ya Watanzania (SYW).
Dar es Salaam, 14 Julai 2023
Sawa mzalendo slaa
 
Mbona ameibuka gafla kutoka mafichoni huyu babu Slaa, tena ni mkosoaji mkubwa ktk kipindi hiki cha mama, mbona huko nyuma alinyamaza kimya, au kipindi chote hicho hakukuwa na ajenda yeyote ambayo ingekinzana na maoni yake, sio kweli analo lake jambo, suala la bandari limekuwa kama ni kisingizio tu.
Huko nyuma kulikuwa na hili la bandari?
 
Back
Top Bottom