Mkataba wa Taikon na Mchungaji Jonathan Kanjunju kuhusu ushirika wangu katika kanisa lake

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,894
MKATABA WA TAIKON NA MCHUNGAJI JONATHAN KANJUNJU KUHUSU USHIRIKA WANGU KATIKA KANISA LAKE

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Baada ya kukutana na Mchungaji Jonathan Kanjunju wa Kanisa la Cherubim of paradise "The Church of the Cherubim of Paradise" lililoko jijini Dar es salaam.

Huu ni mwaka sasa tangu nifahamiane naye akiwa jirani yangu hapa Mbezi Beach yalipo makazi yangu.

Kwenye Christmas ya Mwaka jana Apostle Kanjunju alikuja nyumbani kwangu akiwa na mualiko wa kipekee kuwa niende kwenye kanisa lake kama mgeni maalum,na angefurahi sana mimi kuwapo kwenye mkesha wa Christmas. Nilimkubalia ombi lake na mimi na familia yangu tulifika usiku wa kuamkia tarehe 25Dec2022.

Programu za mkesha zilifaana sana. Nilipewa utambulisho wa kipekee na familia yangu. Kisha Apostles watatu kutoka Nigeria na mmoja kutoka Afrika ya kusini wakaonyesha miujiza ambayo kwa kweli Taikon ilitaka kunizoazoa mzobemzobe, lakini kama mjuavyo Taikon sio mtu wa maamuzi ya haraka hasa akiwa katika kona kali ya kimihemko.

Usiku wa mkesha ulihusisha nyimbo kutoka kwa Kwaya mbalimbali pamoja na waimbaji binafsi ambao baadhi yao walitoka nje ya nchi. Hii ilizidisha uzuri wa mkesha ule ulionekana mfupi kwani masaa yalikuwa yakikimbia sana.

Hatimaye shughuli iliisha, Aposto Kanjunju akafunga Mkesha na ndipo aliponifuata na kuniambia anahitaji niwe sehemu ya Kanisa lake. Nilipohitaji kujua kwa nini anataka jambo hilo. Jibu lake lilikuwa "God has given me your blessings. God will do something great if you open your heart to Him"

Aliongea kingereza cha lafudhi ya Kinigeria. Sikutaka kumkatisha tamaa. Nikamuambia anipe muda wa kutafakari.

Basi akatabasamu kisha ananiambia; Sitaki kukaa na mibaraka yako Taikon. Usichelewe"
Kisha tukaachana, nikimuacha kwenye kanisa lake akiwa na watu wengine (baadhi ya waumini na wale wachungaji wageni).

Mwaka huu ulipoanza mara nyingi sishindi Mbezi beach. Hiyo ilimfanya anikose pale kwangu. Akapewa namba za simu. Mwezi wa kwanza mwishoni akanipigia simu. Tukawasiliana, huku akitaja kujua nimefikia wapi. Nikamwambia aendelee kuwania subira.

Mwezi wa nne mambo yangu yakachacha. Kila kitu kikaenda mrama. Uchumi ukitetereka kwenye jiji la DSM unaweza kufa kwa presha. Basi nikamkumbuka Apostle Kanjunju lakini sikutaka kimchezo kiharaka. Mwezi wa nane nikashindwa kuvumilia kwani kodi ya nyumba ya pale mbezi beach ilianza kunishinda na sikujua ni wapi nitapata pesa ya kulipa. Ukizingatia kodi pale unalipa kwa miezi 12. Milioni Nane nitatoa wapi mimi wakati biashara zote zimeyumba.

Nikajiuliza kwa nini tangu nifike kwenye kanisa la Cherubim of Paradise" mambo yangu yameyumba kwa kiwango cha kutisha hivi.

Septemba nikakutana naye. Nikamwambia nimekubali ombi lake lakini kwa sharti. Akaniuliza sharti gani. Nikamwambia nahitaji kuandikishana naye mkataba. Akaniambia nazungumzia jambo gani.

Nikamwambia, nataka tuingie mkataba wa kisheria wa mimi kuwa muumini wako katika kanisa lako na kuchukua hiyo mibaraka uliyosema umepewa na Mungu ili kama utanidanganya basi sheria za nchi zitachukulia shauri hili kama Jinai ya wizi wa kuaminika. Akacheka sana.

Kisha akasema kwa kujiamini. Haina shida. Niandae huyo mkataba kisha nimpelekee.
Nikamwambia huo mkataba nilishau-draft tangu juzi. Huu hapa mkononi. Hapo nikampa ile bahasha. Akaifungua na ndani yake akatoa karatasi zenye maandishi.

Na hivi ndivyo ulivyosomeka ule Mkataba.

MKATABA WA TAIKON MASTER NA APOSTLE JONATHAN KANJUNJU KUHUSU USHIRIKA WANGU KATIKA KANISA LAKE.

Makubaliano baina ya Taikon Master (Ambaye hapa ni Muumini) na Apostle Jonathan Kanjunju (ambaye hapa ni mchungaji wa kanisa la Cherubim of Paradise) ambapo kuanzia sasa 24 septemba 2023 na kuendelea kadiri ya muda wa mkataba huu ulivyo. Taikon Master atakuwa muumini halali na mwenye haki zote katika Kanisa la Cherubim of Paradise. Haki hizo kama zitakavyotajwa hapo chini.

Muda wa Mkataba ni miaka mitano tangu siku ya tarehe uliposainiwa mkataba huu. Hivyo mkataba huu utakuwa halali mpaka 24 septemba 2028.

APPENDIX 01
1. HAKI, WAJIBU NA MAJUKUMU.
i) Muumini ambaye hapa ni Taikon atakuwa na haki zote za kuabudu katika Kanisa la Cherubim of Paradise.
Kuabudu hapa itamaanisha shughuli zote za msingi za kiimani kama vile kuomba na kuombewa., kuimba, kutoa sadaka na zaka.

ii) Muumini atakuwa na haki ya kujua mapato na matumizi ya Zaka, sadaka na matoleo yote ya Kanisa.

iii) Muumini atakuwa na haki ya kuuliza maswali ikiwa kuna jambo anaona halielewi. Na haitakuwa ruhusu kumpeleka peleka au kumlazimishia jambo ambalo anaona halipatani na akili na uelewa wake.

iv) Muumini hatalazimika kuingia na familia yake katika Kanisa la Cherubim of Paradise.

v) Mchungaji ambaye hapa ni Jonathan Kanjunju atakuwa na Haki za kichungaji kama kutoa neno, kuombea na kutoa baraka, kupokea sadaka, zaka na matoleo.

vi) Mchungaji atakuwa na wajibu wa kuhakikisha ahadi zote alizozitoa kwa muumini wake katika haki zake za kichungaji anazitimiza pasipo kuacha ahadi hata moja.

vii) Mchungaji atakuwa huru kujibu maswali atakayoulizwa kulingana na vyanzo vya taarifa alivyonavyo, rejea, utashi na uelewa wake.

viii) Mchungaji atakuwa na wajibu wa kufuatilia maendeleo ya muumini wake na kuhakikisha ahadi zote alizoahidi kwa muumini zinatimia.

Ix) Muumini atakuwa na wajibu wa kumheshimu mchungaji kama kiongozi wake wa kiroho.

2. AHADI ZA MIBARAKA
Mchungaji Jonathan Kanjunju Kwa utashi na hiyari yake alimfuata Muumini Taikon Master na kusema kuwa anamibaraka yake kutoka kwa Mungu. Taikon Master alipoihitaji mibaraka hiyo alipewa sharti la kujiunga kwanza na Kanisa la Cherubim of Paradise kisha ndipo atapokea hizo baraka.
Zifuatazo ni baraka ambazo Mchungaji Jonathan Kanjunju atampa Taikon Master ndani ya miaka mitano tangu siku mkataba huu uliposainiwa;

i) Jumba kubwa la kifahari lenye thamani ya milioni mia tisa.
ii) Gari la kifahari lenye thamani isiyopungua bilioni moja.
iii) biashara na kampuni kubwa yenye mizizi iliyojichimbia na matawi marefu yaliyosambaa mpaka nchi jirani.

APPENDIX 02
1. KUKIUKA NA KUVUNJA MKATABA
i) mchungaji atalazimika kumlipa muumini wake shilingi bilioni 2 ikiwa baada ya miaka mitano ahadi zote hazitatekelezwa.

ii) Mchungaji akivunja mkataba kabla ya miaka mitatu atamlipa Muumini bilioni 1 kwa sababu miaka mitano itakuwa haijafika

iii) Ikiwa Muumini atakufa kabla ya hiyo miaka mitano. Mchungaji atalipa bilioni mbili kwa familia ya muumini kwa sababu ahadi hazikutimia kwa wakati na mungu wa Apostle Kanjunju hakuwa mwaminifu.

iv) Ikiwa Mchungaji atakufa kabla ya miaka mitano ya mkataba huu hiajafika na ahadi za mibaraka alizotoa hazijafikia. Basi kanisa lake litawajibika kumlipa Muumini bilioni mbili.

Mkataba huu umesaniwa mbele ya Mashahidi wafuatao:

Mashahidi wa upande wa Mchungaji Jonathan Kanjunju
1. Aposto Abe chinubu
2. Aposto Ziyabonga ShakaZulu
3. Adv Charless Kansi

Mashahidi wa upande wa muumini Taikon Master
1. Ryan Kasese
2. Binti Kimoso
3. Karah Samboki

Saini ya Mchungaji прывітанне
Saini ya Muumini. כן אניוהב
Tarehe 24 septemba 2023

Huo ndio mkataba wetu. Miaka mitano ijayo hapa tutazungumza lugha nyingine. Miujiza ndani ya mikataba ya kisheria. Bilioni mbili zangu kama naziona.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Hizi thread tunachoshana bure na kupotezeana muda. Pengine ingewekwa kwenye majukwaa ya hadithi na udaku. Why on earth do you put it here ambako kuna serious issues kwa great thinkers

Ungeanzisha hata kiblogu chako ili uweke na kujadili hayo mambo unayoyaona serious.

Kitendo cha wewe kuandika maoni yako kwenye jambo unaloliona halipo serious inaonyesha jinsi maisha yako jinsi yalivyo. Kujihusisha kwa mambo ambayo hayahusiani na wewe
 
Wewe unatuletea mambo binafsi ya maisha yako na imani yako, unatukosea sana JF. Ningekuwa MODERATOR hii ningeifuta tu
 
Hizi thread tunachoshana bure na kupotezeana muda. Pengine ingewekwa kwenye majukwaa ya hadithi na udaku. Why on earth do you put it here ambako kuna serious issues kwa great thinkers
mdau mbona sijaona la ajabu hapo kwenye uzi wa mwana ! Usiwe na chuki kihivyo .Uzi uko open sana na nimeelewa hizo terms na conditions za mkataba. Zama hizi sio za kupelekeshana kama maroboti hususan kwenye maswala nyeti kama ya kiimani. Sasa sijui kwanini umekuwa shocked na uzi wa mdau? Au wewe ni mchungaji ili tujue.
 
Yupo kwaajili ya mambo serious wakati anafuatilia mambo asiyohusiana nayo.

Kikawaida Watu wanaojifanyaga serious mara nyingi wengi huwa na maisha duni Sana. Fuatilia.
 
Hilo kanisa lako ni ushirikina mtupu, kwanza huyo Apostle kwa kutambua kinachokupa kiburi mpaka ukachelewa kumkubalia ombi lake ni kipato chako, akaamua kuzifunga njia zako, hapo mtoto wa watu akili zikakurudia.

Halafu baada ya hapo unaenda huko kanisani kwa Apostle kuvuna mapesa tu, sijaona popote jambo gani la maana kiroho unalotegemea kupokea kutokea hapo kanisani, ni mwendo wa bilioni moja mkataba ukivunjwa kabla ya wakati, na bilioni mbili kwa familia kama ukifa kabla ya mkataba kutamatika!.

Simply umeingia mkataba wa kujifunga kwenye nguvu za giza kwa miaka mitano.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Hilo kanisa lako ni ushirikina mtupu, kwanza huyo Apostle kwa kutambua kinachokupa kiburi mpaka ukachelewa kumkubalia ombi lake ni kipato chako, akaamua kuzifunga njia zako, hapo mtoto wa watu akili zikakurudia.

Halafu baada ya hapo unaenda huko kanisani kwa Apostle kuvuna mapesa tu, sijaona popote jambo gani la maana kiroho unalotegemea kupokea kutokea hapo kanisani, ni mwendo wa bilioni 2 mkataba ukivunjwa kabla ya wakati, na bilioni moja ukifa kabla ya mkataba kutamatika!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app

Ndio mibaraka aliyosema kapewa na Mungu.
Angesema ipo mingine ya kiroho ningeandika kwenye mkataba
 
Ndio mibaraka aliyosema kapewa na Mungu.
Angesema ipo mingine ya kiroho ningeandika kwenye mkataba
Next time ukienda hapo kanisani muulize "mungu" wake anaitwa nani, utuletee jibu hapa tafadhali.

Apostle ameona una nyota itakayomfaa kwenye kazi zake, amechukua ili akaitumie hiyo nyota kwa muda atakaoona unafaa, baada ya hapo unaweza kupata hasara ambayo utakuja kujijutia for the rest of your life.

Soma biblia myfriend ikuweke huru kiroho, huu wakati tuliopo ni wengi sana huchukuliwa na kwenda kuabudu kwenye madhabahu ya shetani bila kujua, miujiza ikiwa ndio mtego mkuu kwao.

Kwa bilioni 2 mkuu muache atatoka kapa
 
Sa
Ungeanzisha hata kiblogu chako ili uweke na kujadili hayo mambo unayoyaona serious.

Kitendo cha wewe kuandika maoni yako kwenye jambo unaloliona halipo serious inaonyesha jinsi maisha yako jinsi yalivyo. Kujihusisha kwa mambo ambayo hayahusiani na wewe
Safi kwa kumchana huyo vyeti feki
 
Back
Top Bottom