Utofauti wa Kanisa, Hekalu na Sinagogi

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,720
10,218
Hivi karibuni kuna mtu mmoja aliuliza swali sehemu kuwa kuna utofauti gani kani ya Kanisa, Sinagogi na Hekalu? Nikagundua kuwa wengi wanasumbuliwa na swali hili, hivyo leo nimekuandalia majibu kwa ufupi tu Mungu akitupatia neema siku nyingine tutaona kwa kina, karibu.

HEKALU
Hekalu ni jengo lililojengwa kwa ajili ya kumuabudia Mungu na kufanya upatanisho, na lilikuwa limegawanyika katika sehemu tatu, Hema ya kukutania (watu wote) Patakatifu (kuhani wa zamu mara moja kila wiki) na Patakatifu pa Patakatifu (kuhani mkuu mara moja kwa mwaka) ambapo ndani yake kulikuwa na sanduku la agano. Ambapo Hekalu lilijengwa na Mfalme Sulemani mwaka 957KK. Na lilibomolewa na Mfalme Nebukadneza wa Babeli na kuwaamisha Wayahudi wote na vyombo vyote ndani ya hekalu mpaka Babeli. Lilibomolewa mwaka wa 586 KK

Baada ya uhamisho Wayahudi wakayarudia makazi yao na kuamua kulijenga tena Hekalu kwa mara ya pili chini ya Zerubabel, Ezra kuhani, pamoja na kina Hagai nabii. Walifanikiwa kulijenga mwaka 516 KK. Na Hekalu hilo pia likabomolewa tena mwaka wa 70 BK na dola ya Kirumi ambapo tangu mwaka huo Hekalu halikuwai kujengwa tena mpaka leo hii, ni karibu miaka 2000 iliyopita. Ingawa Wayahudi wapo katika mipango ya kulirejesha hekalu hilo. (Nilishawahi kuandika masomo kuhusu Hekalu takatifu, na somo Je ni sahihi Israel kulirejesha hekalu lao? Humo nimechambua kwa kina)

Kwa sasa Hekalu ni mwili wa muumini na Roho hukaa ndani yake. Miili yetu sisi Kristo amenipa heshima ya kuwa hekalu takatifu la Mungu. Ikiwa mtu atauchezea Mwili wa mtu wa Mungu basi Mungu atamuharibu mtu huyo, hekalu la Mungu ni takatifu ambalo ndilo nyinyi. 1Kr 3:16

SINAGOGI
Sinagogi ni nyumba ya kufundishia sheria, hii wengi hujua ni Msikiti lakini si Msikiti, ila misikiti imechukua utamaduni wa masinagogi kwa Wayahudi. Baada ya kutoka utumwani Babeli Wayahudi wakaona waanze kuhimizana kushika sheria ya Mungu ili wasije abudu tena sanamu wakatupwa utumwani tena, ndo wakaanzisha masinagogi. Ila watafsiri wa Biblia wa Kiswahili walipokosa maana katika lugha yetu wakaamua kuita Msikiti.

Kumbuka baada ya kutoka Babeli moyo wa Wayahudi wengi waliamua kurejea kwa Mungu sasa Walipofika Yerusalemu hakukuwa na hekalu tena hivyo Ezra kuhani akaamua kuanzisha utaratibu wa ibada ili watu wajifunze sheria na ibada hizo walizijengea majengo wakayaita masinagogi. Hivyo Sinagogi zilikuwepo sehemu nyingi katika jamii ya Kiyahudi na mara baada ya Hekalu la pili kukamilika bado utaratibu wa masinagogi uliendelea na mpaka leo Wayahudi wanaishi bila hekalu huabudu katika masinagogi. Sinagogi lilijengwa kwa mfumo wa majengo ya kibabeli.

Hivyo Sinagogi si hekalu bali ni majengo ya kufanyia ibada na kujifunza sheria na walikuwa wakiyatumia hasa siku za sabato. Na Sinagogi halikuwa nyumba ya Mungu bali Hekalu ndilo lilikuwa nyumba ya Mungu. Hivyo hekalu Duniani kote lilokuwa ni moja tu, ila masinagogi hata yawe mengi kiasi gani aina shida. Hiyo ni tofauti ya Sinagogi na Hekalu.

KANISA
Kanisa ni mkusanyiko wa watu walioitwa pamoja. Zamani hata mikutano ya kisiasa watu wanakusanyika ilikuwa inabeba tafsiri ya kanisa. Hivyo neno Kanisa kwa Kiyunani huitwa Ekklesia ambalo ndo mkusanyiko, hivyo sisi ambao tumeitwa na Mungu na kukutana pamoja kwa ajili ya Kristo tunaitwa Kanisa. Maana nyingine ya kanisa ni mwili wa Kristo aliye kichwa, na pia ni bibi harusi aliye safi. Kanisa aina maana ya jengo au majengo tunayoyajenga ndo maana hata tukiabudia chini ya mti, au mtoni au darasani au kando ya njia bado litakuwa kanisa tu. Majengo tunayoyajenga hayana uzito wa kuitwa kanisa bali ni majengo ya kanisa.

Hivyo basi kwa sababu kanisa ni kusanyiko yatupasa tusiache kukusanyika kama ilivyo desturi, maana kila walipo wawili watatu kwa ajili ya Kristo basi Mungu naye anakuwepo. Leo watu hawajumuiki na wenzao kwa kigezo cha kufanya ibada kwenye TV unaangalia Live ujue kuwa umekufa. Ni lazima tukusanyike, tuonyane, na kutiana moyo inapobidi, ni lazima tuwajibike chini ya, na siyo kukaa kutazama video za ibada Online ikiwa wenzako wapo kwenye kusanyiko, unajidanganya.

Kanisa ni mwili wa Kristo na sisi tu viungo, hivyo Kristo anao mwili mmoja tu, madhehebu haya hayana uzito wa kuwa Kanisa bali ni taasisi ila kanisa duniani kote ni moja tu ambalo ni mwili wake Kristo, ambalo limepambwa mfano wa Bibi arusi safi hasiye na waa kwa ajili ya karamu ya mwanakondoo. Madhehebu yanatugawa bali Kristo anatuunganisha, kila mtu aliyempokea Kristo kwa dhehebu lake huyu ni ndugu yetu katika Mungu bila kujali anapoabudu.

Mungu akubariki sana, ukibarikiwa unaweza kushea na kwa wengine pia.

Mwl: Vincent Mwakisyala Vincent
0753114222

#nitajitianguvukwaBwana
#yamefunuliwakwetu
 
Hekalu pia husimama kama mwili...

Neno linasema Mwili ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? ninyi si mali yenu wenyewe, kwakuwa mlinunuliwa kwa bei. Hivyo basi mtukuzeni Mungu katika miili yenu
1Wakorintho 6:19-20
 
Sisi dini zetu ni full matambiko haya mengine hayatuhusu bas tu ni viranga vimetujaa.
 
Hii sisi kama waafika hizi dini walitet wazungu inatusaidia nini
huu msemo wa kusema wazungu walituletea dini haituhusu ni msemo mfu. Wale walileta injili afrika wakitimiza ujumbe wa enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri injili kwa kila kiumbe. Watu wale waliokaa gizani mwanga uliwazukia
 
Makobazi wanakwambia Yesu alikua muislamu kisa alienda kwenye sinagogi kama ilivyo desturi yake( msikitini)

Wanakwambia bilblia imetaja swaum( ni kweli)

Lakini vile vile kitabu cha Isaya kimetaja neno mashekhe, na sikukuu ya IDDI

Takbiiiiiiiiiiiiiiirrrrrrrrttt!

Hapo kobazi wote wanaitika Alahu akbar
 
Hivi karibuni kuna mtu mmoja aliuliza swali sehemu kuwa kuna utofauti gani kani ya Kanisa, Sinagogi na Hekalu? Nikagundua kuwa wengi wanasumbuliwa na swali hili, hivyo leo nimekuandalia majibu kwa ufupi tu Mungu akitupatia neema siku nyingine tutaona kwa kina, karibu.

HEKALU
Hekalu ni jengo lililojengwa kwa ajili ya kumuabudia Mungu na kufanya upatanisho, na lilikuwa limegawanyika katika sehemu tatu, Hema ya kukutania (watu wote) Patakatifu (kuhani wa zamu mara moja kila wiki) na Patakatifu pa Patakatifu (kuhani mkuu mara moja kwa mwaka) ambapo ndani yake kulikuwa na sanduku la agano. Ambapo Hekalu lilijengwa na Mfalme Sulemani mwaka 957KK. Na lilibomolewa na Mfalme Nebukadneza wa Babeli na kuwaamisha Wayahudi wote na vyombo vyote ndani ya hekalu mpaka Babeli. Lilibomolewa mwaka wa 586 KK

Baada ya uhamisho Wayahudi wakayarudia makazi yao na kuamua kulijenga tena Hekalu kwa mara ya pili chini ya Zerubabel, Ezra kuhani, pamoja na kina Hagai nabii. Walifanikiwa kulijenga mwaka 516 KK. Na Hekalu hilo pia likabomolewa tena mwaka wa 70 BK na dola ya Kirumi ambapo tangu mwaka huo Hekalu halikuwai kujengwa tena mpaka leo hii, ni karibu miaka 2000 iliyopita. Ingawa Wayahudi wapo katika mipango ya kulirejesha hekalu hilo. (Nilishawahi kuandika masomo kuhusu Hekalu takatifu, na somo Je ni sahihi Israel kulirejesha hekalu lao? Humo nimechambua kwa kina)

Kwa sasa Hekalu ni mwili wa muumini na Roho hukaa ndani yake. Miili yetu sisi Kristo amenipa heshima ya kuwa hekalu takatifu la Mungu. Ikiwa mtu atauchezea Mwili wa mtu wa Mungu basi Mungu atamuharibu mtu huyo, hekalu la Mungu ni takatifu ambalo ndilo nyinyi. 1Kr 3:16

SINAGOGI
Sinagogi ni nyumba ya kufundishia sheria, hii wengi hujua ni Msikiti lakini si Msikiti, ila misikiti imechukua utamaduni wa masinagogi kwa Wayahudi. Baada ya kutoka utumwani Babeli Wayahudi wakaona waanze kuhimizana kushika sheria ya Mungu ili wasije abudu tena sanamu wakatupwa utumwani tena, ndo wakaanzisha masinagogi. Ila watafsiri wa Biblia wa Kiswahili walipokosa maana katika lugha yetu wakaamua kuita Msikiti.

Kumbuka baada ya kutoka Babeli moyo wa Wayahudi wengi waliamua kurejea kwa Mungu sasa Walipofika Yerusalemu hakukuwa na hekalu tena hivyo Ezra kuhani akaamua kuanzisha utaratibu wa ibada ili watu wajifunze sheria na ibada hizo walizijengea majengo wakayaita masinagogi. Hivyo Sinagogi zilikuwepo sehemu nyingi katika jamii ya Kiyahudi na mara baada ya Hekalu la pili kukamilika bado utaratibu wa masinagogi uliendelea na mpaka leo Wayahudi wanaishi bila hekalu huabudu katika masinagogi. Sinagogi lilijengwa kwa mfumo wa majengo ya kibabeli.

Hivyo Sinagogi si hekalu bali ni majengo ya kufanyia ibada na kujifunza sheria na walikuwa wakiyatumia hasa siku za sabato. Na Sinagogi halikuwa nyumba ya Mungu bali Hekalu ndilo lilikuwa nyumba ya Mungu. Hivyo hekalu Duniani kote lilokuwa ni moja tu, ila masinagogi hata yawe mengi kiasi gani aina shida. Hiyo ni tofauti ya Sinagogi na Hekalu.

KANISA
Kanisa ni mkusanyiko wa watu walioitwa pamoja. Zamani hata mikutano ya kisiasa watu wanakusanyika ilikuwa inabeba tafsiri ya kanisa. Hivyo neno Kanisa kwa Kiyunani huitwa Ekklesia ambalo ndo mkusanyiko, hivyo sisi ambao tumeitwa na Mungu na kukutana pamoja kwa ajili ya Kristo tunaitwa Kanisa. Maana nyingine ya kanisa ni mwili wa Kristo aliye kichwa, na pia ni bibi harusi aliye safi. Kanisa aina maana ya jengo au majengo tunayoyajenga ndo maana hata tukiabudia chini ya mti, au mtoni au darasani au kando ya njia bado litakuwa kanisa tu. Majengo tunayoyajenga hayana uzito wa kuitwa kanisa bali ni majengo ya kanisa.

Hivyo basi kwa sababu kanisa ni kusanyiko yatupasa tusiache kukusanyika kama ilivyo desturi, maana kila walipo wawili watatu kwa ajili ya Kristo basi Mungu naye anakuwepo. Leo watu hawajumuiki na wenzao kwa kigezo cha kufanya ibada kwenye TV unaangalia Live ujue kuwa umekufa. Ni lazima tukusanyike, tuonyane, na kutiana moyo inapobidi, ni lazima tuwajibike chini ya, na siyo kukaa kutazama video za ibada Online ikiwa wenzako wapo kwenye kusanyiko, unajidanganya.

Kanisa ni mwili wa Kristo na sisi tu viungo, hivyo Kristo anao mwili mmoja tu, madhehebu haya hayana uzito wa kuwa Kanisa bali ni taasisi ila kanisa duniani kote ni moja tu ambalo ni mwili wake Kristo, ambalo limepambwa mfano wa Bibi arusi safi hasiye na waa kwa ajili ya karamu ya mwanakondoo. Madhehebu yanatugawa bali Kristo anatuunganisha, kila mtu aliyempokea Kristo kwa dhehebu lake huyu ni ndugu yetu katika Mungu bila kujali anapoabudu.

Mungu akubariki sana, ukibarikiwa unaweza kushea na kwa wengine pia.

Mwl: Vincent Mwakisyala Vincent
0753114222

#nitajitianguvukwaBwana
#yamefunuliwakwetu
Umefafanua kwa usahihi kabisa
 
Back
Top Bottom