Mchungaji apigwa na wananchi wa Kigoma kwa kuzuia waganga wa kienyeji "Kamchape" wasiingie eneo la kanisa kutafuta uchawi

MELEKAHE

JF-Expert Member
Nov 19, 2023
434
1,966
Mchungaji avamiwa na wananchi na kupigwa vikali baada ya kugoma kukubali watu wenye imani potofu kuingia kwenye viwanja vya kanisa kutoa uchawi.

waganga hao wa kienyeji wanakusanya 5,000/ kwa kila nyumba, kama malipo ya kuwatoa wachawi wote. Mchungaji aligoma kuwapa hela na aligoma kuwaruhusu kuingia kwenye maeneo ya kanisa.

Najiuliza kwanini watu Wa tanzania tunanaamini sana kwenye uchawi, Elimu itolewe ili Watanzania Tuache Imani za ushirikina. Imagine kwenye zama hizi za teknolojia bado kila nyumba inalipishwa 5000 na waganga wa kienyeji ili watoe wachawi

mchungaji avamiwa na wananchi na kupigwa vikali baada ya kugoma kukubali watu wenye imani potofu kuingia kwenye viwanja vya kanisa kutoa uchawi.

waganga hao wa kienyeji wanakusanya 5,000/ kwa kila nyumba, kama malipo ya kuwatoa wachawi wote. Mchungaji aligoma kuwapa hela na aligoma kuwaruhusu kuingia kwenye maeneo ya kanisa.

Najiuliza kwanini watu Wa tanzania tunanaamini sana kwenye uchawi, Elimu itolewe ili Watanzania Tuache Imani za ushirikina. Imagine kwenye zama hizi za teknolojia bado kila nyumba inalipishwa 5000 na waganga wa kienyeji ili watoe wachawi

View attachment 2932691
Hivi huo mkoa hauna serikali? Mkuu wa mkoa anafanya nini na kuachia huu ujinga? Ni siku nyingi tumesikia hizi habari mbona hachukui hatua? Rais anafanya nini kumfukuza kazi mkuu wa mkoa?
 
Hawa wajinga sijui kamchape wanawalea mpaka lini huko?

Wajinga sio watu wa kuwachekea kabisa.
Kigoma Kigoma Kigoma.
Tatizo kubwa linalosumbua Ni wivu miongoni mwa wananchi. Huwasingizia wenzao Ni wachawi Kwa kuwa wana maenseleo kuwazidi hivyo hula njama Na kuwaleta Kamchape ili wawadhalilishe wenzao.

Kamchape Kwa kuelewa udhaifu huo Wa wanachi huwaibia wanachi pesa mifugo n.k Kwa ajili ya shughuli hiyo ya kipumbavu kabisa.

Hakika inasikitisha Sana namna wanachi waliojawa Na wivu Wa kipumbavu huwatumia Kamchape ili wawadhalilishe wenzao simply wamewazidi kinaendelea au tu kutaka wadhalilike wenzao.

Kuna sehemu Kamchape hutonza Hadi 1500000 au 200000 Kwa kazi hiyo ya kijinga kabisa.

Wananchi Wa KIGOMA huona wivu uliopindukia aonapo mwenzake ameinuka. Hakika inasikitisha sana
 
Walikuja shuleni kutoa uchawi, wanakijiji waliwaleta, baadhi ya walimu tuliwagomea lakini wanakijiji wakashinikiza waingie wakatoe uchawi. Mara wakaingia ofisi ya mkuu wa shule na kudai wametoa uchawi wa mkuu wa shule na mwingine wakaufukua mbele ya shule. Walimu tusioamini uchawi tuliwaambia hatutaki ujinga wao na tutaripoti kwa mkurugenzi wa halmashauri kuwa tumevamiwa shuleni. Mchungaji hawezi kukubali upuuzi huo kwa mujibu wa imani ya kanisa lake. Huo ni uvamizi na hao wavamizi wanatakiwa washitakiwe kwa uchochezi
 
Mungu hafananishwi na chochote.
Funguka acha kukariri, Kila Jamii ina mungu wake, wachina Wana mungu wao, wahindi, waarabu, wazungu etc wana wa kwao pia, hata waafrica kabla ya ukoloni tulikuwa tuna mungu wetu, sasa Leo mmeletewa mungu na hao wazungu na waarabu mnaona hakuna mwingine, inabidi kutuma akili sana haya mambo ya Imani la sivyo utaonekana chizi tuu, Jamii nyingi sana zimeanza kushtukia huu usanii na hata hao wazungu waliowaletea huyo mungu wameanza kushtukia na kuachana na hayo mambo ya kufikirika na hadithi za watu wa kale
 
...Kwa hiyo Kamchape ndio mungu Wetu ??..
 
Back
Top Bottom