Tatizo la Makocha wazawa Timu ya Taifa ni Malezi yao Mabaya

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,319
12,622
Malezi anayopewa mtu utotoni kwenye mambo na matukio mbalimbali ndani ya familia, jamii na taasisi mbalimbali kama za kidini, shule na mpira vina uhusiano mkubwa na tabia na ufanisi wa mtu huyo wakati wa utu uzima.

Kama utotoni ulipigwa sana kuna uwezekano mkubwa na wewe kuwa mpigaji wa watoto, wanafunzi, wachezaji au hata watu wa rika lako. Kama utotoni ulikuwa ulinyanyaswa sana (abused) kuna uwezekano mkubwa sana na wewe kuwa mnyanyasaji (abuser).

Kama wewe ulikuwa mtu wa mabifu au ulifundindishwa na mzazi/mwalimu/kocha/mchungaji mwenye bifu kwenye malezi yako basi ni rahisi na wewe kupenda mabifu kwa watoto wako, wanafunzi au wachezaji wako.

Kabla ya kumpa mzawa kazi kubwa kama ya kuwa kocha mkuu wa timu lazima upate historia yake ya malezi, makuzi, mafunzo na uzoefu wake utotoni, ujanani na kwenye kazi zake za awali alizozifanya.

Kuwa kocha mkuu kunahitaji mtu ambae yuko vizuri sana kwenye malezi ya wachezaji wenye tabia, makuzi, ujuzi, umri, dini, maumbile na vipato tofauti. Lazima atambue individual differences za wachezaji kitabia, uwezo uwanjani na uharaka wa kushika mambo.


Kocha wa timu ya Taifa lazima aonyeshe maturity ya hali ya juu katika kulea wachezaji wenye tabia na vipaji tofauti. Kuonyesha maturity ni pamoja na kushirikisha wachezaji na wadau wengine kwenye maamuzi, kusamehe, kuvumilia na kukubali kushauriwa na kukosolewa hata na wachezaji.

Makocha wetu wazawa wengi wao wanakosa software hizi kwenye makuzi yao, wamekulia kwenye familia, jamii na taasisi ambazo kuna one way communication; kutoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto tu, kutoka kwa mwalimu kwenda kwa mwanafunzi tu, kutoka kwa kocha kwenda kwa mchezaji tu kuruhusu wala kukubali kuulizwa swali, kuhojiwa wala kukosolewa ("do what I say"), na kama atatokea mtoto, mwanafunzi au mchezaji kuhoji, kushauri au kukosoa atawekewa bifu, kupewa adhabu au kufukuzwa kaziba nyumbani, shuleni au kikosini kabisa.

Makocha wa hivi hawaoni tabu kuacha kumpanga acheze mechi mchezaji mzuri kwakuwa siku moja alichelewa kutoa pass kwa mwingine au alimkosoa.

Makocha wazawa ni bora lakini wachukuliwe vijana wanaofundishika hizi software za uongozi na wasichukiliwe wazee anbao ni vigumu kuwaambia jambo jipya. Vinginevyo wachukuliwe watu wazima lakini waliopitia malezi sahihi na mafunzo sahihi ya mpira tangu utotoni.

Kambi itasambaratika kwa hasira na chuki za benchi la ufundi kwa wachezaji.
 
Yaani huu uzi wote lengo ni kumtetea mtovu wa nidhamu dickson job na ukae ukijua mtoto umleavyo ndio akuavyo

Sasa ulitaka kocha aendekeze utovu wa nidhamu wa mchezaji mmoja mwisho wa siku wachezaji wote wasimheshimu?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Yaani huu uzi wote lengo ni kumtetea mtovu wa nidhamu dickson job na ukae ukijua mtoto umleavyo ndio akuavyo

Sasa ulitaka kocha aendekeze utovu wa nidhamu wa mchezaji mmoja mwisho wa siku wachezaji wote wasimheshimu?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Sitetei mchezaji mmoja hapa, bali nimeangali makocha kama Kibaden, Mkwasa, Morocco, Mecky, Julio, Minziro na wazawa wengine waliofundisha timu ya taifa na timu za ligi kuu utagundua kuwa mahusiano yao na wachezaji ni yaleyale mahusiano ya mzazi wa kiafrika na wanawe, mwalimu na wanafunzi, mwajili wa kiafrika na mfanyakazi. uhusiano
 
Back
Top Bottom