Mkuu Zanaki,
Heshima mbele, dataz zako ni nzito sana isipokuwa tu marekebisho kidogo,
1.
Na wale wanaosema Mkapa alikuwa ni chaguo la Nyerere,pia hio sio sawa! Chaguo lake lilikuwa Salim,na Salim aligoma akitoa sababu kuwa anataka kumalizia kazi zake OAU kwanza,na atagombea baada ya hapo,ofcoz yeye akijua Nyerere angekuwa bado yuko hai.
Mwalimu alijaribu kumpitisha Salim, wajumbe wa Visiwani wakamgomea kata kata, akaamua kutumia plan B yaani Mkapa!
2.
Waliomshinikiza Mkapa agombee ni Warioba,Salim,Butiku na jamaa mmoja anaitwa Adam Marwa,na hao ndio waliomfuata Nyerere ili amuendorse Mkapa.
Nyerere asingeweza kumu-endorse kiongozi yoyote asiyemtaka yeye, na siku zote alikuwa akimdharau sana Butiku, kiasi kwamba asingeweza kumsikilza, Warioba alikuwa anagombea ni yeye Mwalimu aliyemtoa na kumuweka kwenye kuhesabu kura za urais, siku Mkapa anatangaza kuchukua fomu, alikuwa na Salim na Warioba pembeni kwenye meza na waandishi wa habari, wakitegemea mkapa kuwapa unga, na he did kwa kutumia hela nyingi sana za taifa kumsaidia Salim kushinda tena OAU, na kumpa Warioba ile tume na pia kumsaidia kwenye kupata uhakimu wa law of the sea wa dunia, kote huku mkapa alitumia hela zetu walipa kodi kuwapitisha marafikiza ke, Warioba na Salim, ikiwa ni pamoja na shinikizo la Mwalimu, ambaye alikuwepo!
Ni Mwalimu aliyehangaika usiku kucha kwenye guest house za wajumbe wa CCM ili wampitishe Mkapa, na ni mwalimu aliyekata deal na Salmin la kumpitisha Mkapa, kwa kuwashinikiza wajumbe wote wa Visiwani kumpigia Mkapa, baada ya Mkapa kushindwa na Kikwete mara mbili za kwanza, in return Salmini aliruhusiwa kuiba uchaguzi wa kule Visiwani, na ndio maana alijiamini sana kutaka term ya tatu na kumpitisha mtu wake Bilali, ni maadui wa mkapa ndio walimkata panga Salmin, ambaye aliamini kuwa mkapa hawezi kumzuia, na pia alimshawishi sana mkapa naye adai term ya tatu, kitu ambacho mkapa alijaribu kwenye kikao kimoja cha mawaziri lakini Sumaye na Mwandosya wakam-shut down, akasingizia kuwa ana simu ya Bush na kukimbia kikao, hakurudia tena, lakini akaja kuwalipa Sumaye na Mwandosya kwenye urais!
3.
Ndio maana Salim mpaka leo amesema hawezi kamwe kumsamehe Mkapa kwa vitendo alivyofanyia Dodoma siku ya uchaguzi wa kutafuta mgombea wa CCM.Hana kinyongo na JK kabisa.
Salim hakuwa malaika kwenye ule uchaguzi na yeye alihusika sana kujaribu kuwachafua wenziwe, lakini alizidiwa kete na Muungwana, Mkapa alikuwa hamtaki period kwa sababu ya uarabu wake na kulikuwa na wajumbe wengi sana ndani ya CCm waliokuwa na hiyo thinking, ndio maana mkapa alikuwa amemuonya Ndejembi mapema kuwa aache kumpigia debe Salim, alisema "..mwarabu hawezi kutawala nchi hiii..."
Yes, Salim anamchukia sana Mkapa kuliko anything, lakini pia ana the same chuki na muungwana, the matter of fact kama sio JM kumtuliza, Salim alitaka kufanya mambo mengi ya ajabu baada ya kujifungia wiki nzima ndani analia, yeye na mkewe, aliamua kususia CCM ikiwa ni pamoja na kujitoa kila nafasi aliyokuwa nayo, na aliapa kuwa hatazungumza nao tena na kutojihusisha tena na siasa za bongo, lakini ni JM ndiye aliyewa-calm down yeye na Sumaye, ambao hawakuamini what Mkapa did to them,
Mkapa na Mugandas, wana uhusiano wa siku nyingi unaotokana na Mkapa kujikomba sana zamani kwa Butiku na Mwalimu, na pia watoto wa mkapa wametunzwa na kusomeshwa maisha yao yote na mke wa zamani wa Butiku kule NY infact yule mama ni mzazi zaidi kwa watoto wa mkapa kuliko hata mkapa na mkewe, lakini mkapa alipopata urais tu akamtelekeza yule mama, lakini ni mama Anna tu ambaye amekuwa akimkumbuka mara kwa mara,
Butiku alikuwa na tabia moja nzuri sana akiwa kwenye power, nayo ni kusaidia watu wengi mahali pa kukaa, nyumba yake siku zote ilikuwa imejaa watu, mmoja wapo alikuwa Museveni, maisha yake yote Dar, mpaka akiwa anasoma Mlimani, alikuwa akikaa kwa Butiku na hata kusaidiwa hela na mahitaji yake yote na Butiku, Museveni ndiye peke yake anayemhifadhi sasa hivi ama sivyo Butiku, angeshakuwa kichekesho mjini!
Otherwsie Mkulu Zanaki, dataz zako bado ni nzito!