Kuhani
JF-Expert Member
- Apr 2, 2008
- 2,944
- 64
FMES, heshima mbele.
Nimetaabishwa kidogo madongo uliyo mtupia Butiku hapa. Nilitegemea busara yako iliyotuongoza kwenye mjadala mwingine unao husiana na kuwakejeli viongozo wanao dhaniwa 'wamechoka.'
Nisaidie kuoanisha mawazo yako hapa:
Na uongozi ulio uonyesha hapa:
Halafu, ukimaliza kunisaidia kuoanisha hayo mawazo, baadae tutajadili ukweli wa hili:
Kwa wanafunzi wa Nyerere, details za closest deputy wa Rais tumezifuatilia. Na sio rahisi 'kumiliki' facts kuhusu mtu kama Butiku. Kwa mfano, maisha pale kwa Butiku sio kweli kama picha uliyo ileta. Nyumba ya Butiku haiku jaa watu zaidi ya familia ya kawaida ya Kitanzania ambapo tuna familia kubwa zaidi ya Baba na Mama na watoto. Tena kwa kipindi kirefu kwa Butiku kulikuwa empty kwa sababu mji ulikuwa hauja kamilika. Mke wake na mtoto walitimua. Mke mwingine nae baadae wakatimuana kabla familia haijawa kubwa. Mara nyingi pale palikuwa empty. OK?
Kwa hiyo, tutakapo kuja kujadili hili la Nyerere kumdharau Butiku kumbuka humiliki hizi facts peke yako. Na kwamba japo mambo binafsi yanayo zunguka maisha ya Rais hakuna anae yajali Bongo kwa sababu aidha Wanahistoria wapo kama hawapo, au kwa sababu 'mwanamme mzima huwezi kuuliza mwanamme mwenzako Kikwete ana watoto wangapi' na 'kujua nani mke wa Kawawa hakuleti maji Kigoma' bado tupo wanafunzi wa Historia tunao fuatilia maisha ya hawa viongozi wetu.
Hata hivyo, nakushukuru kwa kujali hizi details. Hatuwezi kukaa tunashutumu Mkapa fisadi wakati hatutaki kujua anafanya nini na anaishi vipi nje ya ofisi. Madili ya kifisadi mara nyingi yanapikwa taa zikizimwa. Mchana wanatoa spichi kupinga wanayo yafanya kwenye kona usiku. Ni muhimu kujua hawa ma Rais wanaamkia wapi na wana lala kwa nani. Tupo tunao fuatilia haya.

...Butiku alikuwa na tabia moja nzuri sana akiwa kwenye power, nayo ni kusaidia watu wengi mahali pa kukaa, nyumba yake siku zote ilikuwa imejaa watu, mmoja wapo alikuwa Museveni, maisha yake yote Dar, mpaka akiwa anasoma Mlimani, alikuwa akikaa kwa Butiku na hata kusaidiwa hela na mahitaji yake yote na Butiku, Museveni ndiye peke yake anayemhifadhi sasa hivi ama sivyo Butiku, angeshakuwa kichekesho mjini...
Na uongozi ulio uonyesha hapa:
Huenda kwa sasa [Luhigo, Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa THA] physically amechoka kwa umri, sasa subiri huko mbele ya haki ndio utaelewa nani kati ya mkapa na huyu Luhigo atakayekuwa amechoka kwenye kila kiungo cha mwili, maana huko mkapa atapewa mihela yenye moto aibebe kichwani yeye si greedy na mingine aitafune huku ikiwa inawaka moto!
Bravo Mzee Luhigo, wazee hebu mtafuteni mawasiliano yake tuweze kujua anvyoendelea na ikiwezekana kumsaidia kwa chochote maana viongozi kama yeye ni adimu sana Tanzania!
Halafu, ukimaliza kunisaidia kuoanisha hayo mawazo, baadae tutajadili ukweli wa hili:
Nyerere... siku zote alikuwa akimdharau sana Butiku, kiasi kwamba asingeweza kumsikilza...