Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Jamani Mnaona Watoto Wa Wakukubwa Wanvyo Rithi Ufisadi,
Hebu Anagalia Ubungo Terminals Ya Mabasi Ilivyochakaaa , Harafu Cha Kushangangaza Ni Kwamaba Kinje Anakula Kuku Tu, Mbabe Yeye Ukimwambia Kitu Bunduki Mkononi Anatashia Kuku Ditopile

Kinje Fichio La Ufisadi
 
Jamani Bunge sindilo lenye mamlaka ya kutunga sheria, Kwanini wasipige kuondoa immunity ya Mkapa from prosecution...

Kwanza, tofauti na sheria za kawaida, ni vigumu sana kubadilisha Katiba.

Pili, Mkapa anaweza asiguswe na hilo badiliko la katiba kwa sababu mara nyingi kuna utamaduni kwamba sheria mpya inaanza kutumika kwa kuangalia mbele kutoka siku ile inapopitishwa (presumption of prospectivity), isipokuwa kama Bunge litasema tutashitaki hata matendo ya nyuma. Sasa, inaweza kupitishwa kwa kuangalia nyuma (retrospective application) lakini ikionekana kama ni sheria ya kumtafuta Mkapa, italeta maswali mengine ya haki zake za kikatiba kwa sababu umem-target yeye mmoja.

Tatu, ni Mkapa ndio ame abuse hicho kipengele cha katiba, lakini kina sababu ya kuwepo. Kuna vitu ambavyo Rais anatakiwa awe na nguvu ya kuvifanya ambavyo wewe na mimi hatustahili. Kwa mfano kuagiza dola itulize machafuko, ikiwemo kupiga watu risasi. Kwa mfano, wapo wanaoamini kwamba mauaji ya Zanzibar yaliagizwa kutoka Ikulu. Iwapo haya ya Zanzibar yalikuwa justified au hapana, ni majadiliano mengine, lakini kuna wakati hizo nguvu ziko justified. Kwa hiyo Rais anatakiwa atende kazi bila kuogopa kushtakiwa.

Hata hivyo, kuna tafsiri ya kile kipengele cha ulizi wa Rais ambayo inaweza kuruhusu Rais asishtakiwe iwapo aliyo yafanya ni mbali kabisa na kazi yake. Kwa mfano, kujiuzia migodi. Inawezekana ikawa vigumu kushinda kwa sababu majaji wataona ina defeat the spirit of the law ( Marais watakuwa wanaogopa hata katika maeneo ambayo ni kazi yao.) Lakini kama kungekuwa na kesi nyingi zinaletwa, labda kuna jaji angekubali angalau kuisikiliza.

Baada ya kesi kama hizo kusikilizwa, hata kama zisingeshinda, kina Mkapa wa siku za mbele wangetiwa jamba jamba na wangetia akili kabla ya kujipa mikopo bila rehani au kujiuzia migodi.
 
1. MBUNGE wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM), amewatuhumu Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, mkewe Mama Anna Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona, kuwa walinunua mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira, wilayani Rungwe, Mbeya kwa kificho.

2. Mbunge huyo alidai bungeni jana kuwa mwaka 2004, Mkapa kwa kushirikiana na mkewe pamoja na Yona, walianzisha Kampuni ya TanPower Resources Ltd na mwaka mmoja baadaye wakauziwa machimbo ya Kiwira kimya kimya.

3. Alidai kuwa katika mauziano hayo ya siri, Kampuni ya TanPower Resources Limited, ilikuwa iilipe serikali Sh700milioni katika mradi huo uliogharimu, zaidi ya Sh4bilioni, lakini kampuni hiyo ilifanya malipo ya awali ya Sh70milioni tu.

4. "Waliuziwa kwa Sh700milioni bila kutangazwa na wao wakalipa down payment (malipo ya awali) Sh70 milioni," alisema Kimaro.

5. Aliendelea kudai kuwa mwaka 2006, Mkapa, Anna na Yona, waliingia mkataba na Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kwa ajili ya kufua umeme kwa makubaliano ya kulipwa Gharama za uwekezaji ('capacity charge') Sh146 milioni kila siku, bila kujali kwamba wamefua umeme au la.

6. "Sasa mimi nauliza huu ni uadilifu kweli? Haya ni maadili kweli? Tufike mahala tuseme inatosha. Hivi tunawafundisha nini vijana hawa ambao ni mawaziri?," alihoji Kimaro na kuongeza:

"Rais Jakaya Kikwete alisema urais wake hauna ubia na mtu. Basi aseme huu ni mwisho kwa wanaotuhujumu, tuwaambie basi na washughulikiwe kwa mujibu wa sheria."

Finally, wabunge wa CCM wanaanza kuamka, kutoka kwenye usingizi mzito sana, hii ndio mijadala inayoweza kutuletea mabadiliko, ingawa kwa sasa wakubwa wameziba masikio, lakini ngoma ikiendelea kupigwa kama hivi mwisho kutakuwa hakuna alternative bali kubadili sheria, ili hawa wahujumu uchumi watinge kwenye mkondo wa sheria,

ila in the meantime, Mkapa na wenziwe warudishe mgodi wa wananchi, tena now!
 
sitoshangaa nikas8kia chadema hoja hii na kuibeba na kudai wao ndio wameibua bungeni
 
Rais mtaafu Mkapa, mkewe waumbuliwa bungeni kwa mgodi wa Kiwira
Na Muhibu Said, Dodoma

.............Naye Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela alimwangaliza Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kutambua aina ya wawekezaji wanaotarajiwa kuwekeza katika sekta ya umeme baada ya sheria mpya ya sekta hiyo kupitishwa, kwani ndiyo watakaomwangusha ama kumwinua.

"Nakupa angalizo Mheshimiwa Waziri, ujue kuwa aina ya wawekezaji watakaoingia katika sekta ya nishati ndiyo watakaokuangusha au kukuinua, wapo Watanzania wenzetu wanajiandaa kuingia katika biashara hiyo, wengine ni wale walionufaika na mikataba mibovu kama ule wa Richmond," alitahadharisha Mbunge huyo.

Alidai kuwa baadhi ya Watanzania, hususani walionufaika na mikataba inayolitia hasara Tanesco, wameanza kujiandaa kuwekeza kwenye sekta hiyo.........

Nami ningependa kukuongezea tu kidogo.. ndugu waziri kama ujuavyo kazi mliyonayo haina guarantee ni short career hivyo basi usifikirie kujaza vujisenti kwenye mabenki ya offshore bali wacha jina kuwa ulikuwa mzalendo....

Mkuu Lunyungu leo mkulu alionekana akipanda KLM baada ya kumsindikiza waziri mkuu wa Norway. Je ameenda tena ULAYA?
 
hawa ndio aina ya wabunge tunaowahitaji. haijalishi wanatoka chama gani.

hata iwapo tutashindwa kumshitaki moja kwa moja mkapa, mama mkapa na yona wanauwezo wa kushitakiw, and we are waitting for that
 
mbungekimaro.jpg



Name Aloyce Kimaro
Surname Kimaro
First Names Aloyce Bent

From 2005
Organisation

Position MP for Vunjo Constituency

Date of Birth 24 Jun 1953
Political Affiliation CCM


EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
Institute of Development Management- Mzumbe Advanced Diploma in Business Education 1980 1983 ADV DIPLOMA
Kleruu College of National Education Diploma in Education 1977 1978 DIPLOMA
Mkwawa High School A-Level Education 1973 1975 HIGH SCHOOL
OldMoshi Secondary School O-Level Education 1970 1973 SECONDARY
Lyasongoro Primary School Primary Education 1962 1969 PRIMARY
--------------------------------------------------------------------------------
CERTIFICATIONS
Certification Name or Type Certification No. Issued Expires
No items on list
--------------------------------------------------------------------------------
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From Date To Date
Ministry of Trade Business Officer 1984 1988
Ministry of Education - Azania Secondary School Teacher 1979 1980
Ministry of Education- Minaki Secondary School Teacher 1978 1979
Good guy lakini kama Agustino Mrema akiamua kugombea anaweza akamuondoa kwenye kiti chake.
 
mnakumbuka ni mbunge gani aliongoza hoja ya kukataa muswada wa TANESCO usijadiliwe kwenye Kamati hadi wapate nafasi ya kusikiliza ripoti ya Richmond na ikawa ndio mwanzo wa domino effect...?
 
Siku zote nawaambia Changes lazima zitatokea ndani ya CCM na sio huko kwenu wapinzani. Kwani wengi wa wapinzani (sio wote) ni CCM au waganga njaa!
 
FD... ndugu yangu si kila kitu kinachotokea CCM kinatokea hewani... kila effect has a cause..
 
Hadi sasa hivi jamaa waliotuibia hawana raha kabisa. Nawahakikishia Mkapa kwa sasa anaishi kama gerezani tu. Ina maana gani kama kiongozi mstaafu hawezi kuongea hadharani au kualikwa kwenye uzinduzi wa jambo lolote la kitaifa. Kwa sasa yuko kwenye mateso makali kwa ajili ya tamaa zake za kijinga kabisa
 
sitoshangaa nikas8kia chadema hoja hii na kuibeba na kudai wao ndio wameibua bungeni
Kama kawaida Yao Chadema wamekuwa wakirukia mambo ya CCM,ila kwa suala la List of Shame wao ndio walionlianzisha,mengine kama suala la Buzwagi yaliaanzia pale wizarani baada ya wale watu wa kamati ya ushauri madini ya wizara kudhalauliwa,ila ukiangalia bado na hawa wahtu aw madini kw akumchongea mwenzao ,miaka ya nyuma kwanini walikuwa wanapitisha hiyo mikataba,,,ni sula al kujiuliza??Je ni waadilifu..

Nadhani kuna haja ya jk kuanza na hawa makamshna ambao hawatusaidii.
 
Hadi sasa hivi jamaa waliotuibia hawana raha kabisa. Nawahakikishia Mkapa kwa sasa anaishi kama gerezani tu. Ina maana gani kama kiongozi mstaafu hawezi kuongea hadharani au kualikwa kwenye uzinduzi wa jambo lolote la kitaifa. Kwa sasa yuko kwenye mateso makali kwa ajili ya tamaa zake za kijinga kabisa

Pamoja na hayo something must be done to punish him as well as other mafisadis and show Tanzanians that corruption does not pay in our country no matter your position in the Government.
 
mnakumbuka ni mbunge gani aliongoza hoja ya kukataa muswada wa TANESCO usijadiliwe kwenye Kamati hadi wapate nafasi ya kusikiliza ripoti ya Richmond na ikawa ndio mwanzo wa domino effect...?
kipindi gani unachoongele a Mzee Mwanakijiji,Cha ngeleja ni huyu hapa mama Anne Kilango Malecela (CCM).na kipindi cha karamagi najitahidi kukumbuka..kama waligoma wote vile wakati wa kamati baada ya kumgomea Karamagi
 
Hapana.. kipindi cha kujiuzulu Lowassa. Kulikuwa na Semina kule Dodoma kuhusu muswada huo wa Nishati.. wabunge wakakataa kuujadili hadi wasikie ripoti ya Dr. Mwakyembe. Ni Mbunge gani aliyetoa hoja ya kutoendelea na ile semina..?
 
... Mkapa is a next victim simuoni kumaliza huu mwaka bila kuumbuliwa, let us wait and see.

Ila ninajiuliza usalama wa huyu Mbunge masikini, tumsaidieje jamani? Hawa mafisadi wa CCM watamuacha hivi hivi? Mungu amrinde AMEN


Mkapa is not a next VICTIM, but He is a CULPRIT! Njimba, Mkapa ndiye Baba wa Ufisadi hasa. Hata CCM wakimkingia kifua vipi, watachomea wenyewe! Tusibiri, bado kitambo kidogo.
 
Hapana.. kipindi cha kujiuzulu Lowassa. Kulikuwa na Semina kule Dodoma kuhusu muswada huo wa Nishati.. wabunge wakakataa kuujadili hadi wasikie ripoti ya Dr. Mwakyembe. Ni Mbunge gani aliyetoa hoja ya kutoendelea na ile semina..?

Mwanakijiji check PM yako...
 
Back
Top Bottom