Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Akitaka asitake kuna siku ataongea tu. Au hamjuwi Mkwere nini?
 
Mkapa asilipwe mafao - Kiula
2008-02-27 08:54:20
Na Joseph Mwendapole

Waziri wa zamani wa Ujenzi wa Serikali ya Awamu ya Pili, Bw. Nalaila Kiula, ameishauri serikali kusitisha mafao na marupurupu ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa, kwa madai kuwa alikiuka maadili ya uongozi kwa kufanya biashara akiwa Ikulu.

Pia amemtuhumu kiongozi huyo kuwa alichokifanya wakati wa utawala wake, ni uroho wa mali na kwamba hakuwa na sababu ya kufanya hivyo.

Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu ufisadi na rushwa serikalini.

Alisema hakuna sababu ya kuendelea kumpa mafao kiongozi ambaye hakuwa mwadilifu na aliyekiuka maadili ya dhamana aliyopewa.

Bw. Kiula ambaye alikuwa Waziri wakati wa awamu ya Rais Ali Hassan Mwinyi, alisema anamwonea huruma Bw. Mkapa kutokana na tuhuma nyingi anazokabiliwa nazo wakati wa uongozi wake.

``Hata Ibara ya 17 ya Katiba ya CCM inasema kiongozi atosheke na asiwe na tamaa ya mali,`` alikumbusha Bw. Kiula ambaye alikuwa Mbunge wa Iramba Singida kwa miaka 20.

Alisema anashangaa kuona rais huyo anafanya biashara akiwa madarakani wakati analipiwa kila kitu na kupewa huku akihudumiwa na serikali hadi mwisho wa maisha yake.

Bw. Kiula ambaye alikuwa Waziri wa Ujenzi kati ya mwaka 1991 hadi 1995, alisema: ``(Mkapa) aliingia kwa mbwembwe kuwa hatakuwa na suluhu na rushwa lakini akaishia kuwa mfanyabiashara? Rais ana mafao mengi lakini inashangaza kuona mtu kama Rais anakuwa na tamaa,`` alidai.

Bw. Kiula aliwaambia waandishi wa habari kuwa kuna haja kwa Bw. Mkapa kutoa maelezo dhidi ya tuhuma zinazoelekezwa kwake badala ya kusingizia kuwa anapumzika na amestaafu.

Waziri huyo wa zamani alisema ana uhakika tuhuma kuwa Rais mstaafu alikopa Dola 500,000 za Marekani ili afanyie biashara ni za kweli.

Aidha, alisema inashangaza kuona yeye (Kiula) alipokopa Sh. milioni 12 ikawa nongwa na kufunguliwa mashitaka ya rushwa.

``Mimi nilikopa Sh. milioni 12 nikapatwa na msukosuko mkubwa sana lakini huyo aliyekopa dola 500,000 hakuguswa,`` alihoji.

Alisema Bw. Mkapa alifanya hivyo kwa kuwa hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere hakuwepo wakati huo na kwamba angekuwa hai asingethubutu.

Akizungumzia kesi ya tuhuma za rushwa dhidi yake, alidai ilipandikizwa kwa chuki binafsi za Rais Mkapa kutokana na umaarufu aliokuwa nao wakati huo.

``Wakati Mzee Mwinyi ananiteua kuwa Waziri wa Ujenzi alinisifu sana kuwa ni kijana mchapakazi na mwadilifu na alikuwa akinisifu mara kwa mara sasa naona hapo ikawa nongwa na gere,`` alidai Bw. Kiula ambaye mpaka mwaka 2000 alikuwa Mbunge wa Iramba.

Aliongeza kuwa hata Mzee Rashid Kawawa alikuwa akimsifu kwa utendaji wake na kwamba hali hiyo huenda ndiyo ilimfanya achukiwe.

Waziri huyo wa zamani pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. George Mlingwa, walikuwa watuhumiwa wa kwanza kufikishwa mahakamani kwa rushwa.

Kesi yao ilifuatia ripoti ya kamati ya Jaji Warioba ya kuchunguza na kubainisha mianya ya rushwa iliyotolewa mwaka 1996.

Katika kesi hiyo, Bw. Kiula alionekana hana hatia lakini mahakama ilimuona Bw. Mlingwa akiwa na hatia. Mlingwa alikata rufaa.

SOURCE: Nipashe
 
Nafikiri ni busara kwa mkapa kuongea lipi ni kweli na lipi si kweli? viginevyo alazimishwe kuongea mahakamani wa jameni?
 
Nafikiri ni busara kwa mkapa kuongea lipi ni kweli na lipi si kweli? viginevyo alazimishwe kuongea mahakamani wa jameni?

nnaona na yy inabidi atafute ajenda zero kama lowassa kwa ajenda 21 ili kujisafisha.

mwaka huu shetani aliusema na sijui kakimbilia wapi shwetani yule!!
 
Kiula naye bwana! Why now?? ana agenda gani? Na siku zote alikuwepo wapi hajaongea?

Au naye alitumika tu kama Bunguliso?

Mzee Bunguliso uko hapo?
 
Nipo nipo, naona anataka akumbukwe, bilion 1 ilishamuishia. Lakini kasema kweli sema tatizo tuu ni fisadi
 
kiula nakushauri ukae kimya tu.Ulikoswakoswa kufunga kaa chini mshukuru Mungu.Unafikiri sisi wananchi wa Singida tunafurahi ulichotufanyia?? Tunavikumbuka sana vile vidaraja vyako vilivyosombwa na mvua moja tu.Songera zigizigi kijiweni
 
Habari za Kitaifa Habari zaidi!
Mkapa hawezi kuchukuliwa hatua-Tume
Mwandishi Wetu
Daily News; Wednesday,February 27, 2008

SEKRETARIETI ya Maadili ya Utumishi wa Umma imesema Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, hawezi kuchukuliwa hatua zozote za maadili kutokana na kukosekana kwa walalamikaji waliofika katika sekretarieti hiyo kutoa malalamiko yanayoeleweka.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Ofisa Habari wa Sekretarieti hiyo, Augustus Kiria, alisema tuhuma dhidi ya Mkapa kuwa alijihusisha na biashara akiwa Rais hivyo kutumia madaraka yake vibaya kipindi cha utawala wake, hayatekelezeki katika maadili.

Kiria alisema kwa mujibu wa sheria ya maadili namba 13 ya mwaka 1995 iliyofanyiwa marekebisho mbalimbali hadi Machi 2002, Rais huyo mstaafu hawezi kuchukuliwa hatua bila malalamiko yenye vielelezo.

“Hakuna hatua yoyote dhidi ya Mkapa itakayoweza kutekelezwa na ofisi hii kwa sababu hakuna mlalamikaji kuhusu suala hilo aliyekuja hapa, hivyo wengi wanaweza kuzungumza lakini sisi tunaangalia vielelezo,” alisema Kiria.

Sehemu ya tatu ya Sheria hiyo ya maadili yanayotumika kwa viongozi wote wa umma kifungu cha nane, kimebainisha kuwa masharti katika sehemu hiyo yatakuwa ni sehemu ya maadili ya viongozi wa umma kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano na ikikiukwa hatua zinazoweza kuchukuliwa ni pamoja na kuonywa na kupewa tahadhari.
 
Bubu tunashukuru sana kwa article hii ya Padre Karugendo!! Nimeikuta hii artcle wakati nasaka posts zinazomzungumzia Mkapa. Nimeanza huu msako baada ya kutafakari sana jinsi Ndugu Benjamin William Mkapa alivyoingia madarakani mwaka 1995 kama mtu mnyenyekevu mwenye nia nzuri na kale kafumbo kake ka "MTAJI WA MASIKINI NI NGUVU ZAKE MWENYEWE"!! Sasa ndio nimeanza kupata akili kuwa masikini aliyekuwa anaimbwa ni Mkapa mwenyewe... na nguvu zake zimekuwa mtaji wa ujasiriamali ikulu.

Nakumbuka wakati anaingia madarakani kulikuwa na vuguvugu la viongozi kutaja mali walizonazo. Sijui kwa nini Mkapa hakuona sababu ya kufanya tena zoezi hilo la kutaja mali wakati anatoka madarakani.

Huyu muheshimiwa hakupenda kabisa watu kuongea chochote kuhusu serikali yake. Alitumia redio zetu na TV zetu wenyewe kutukaripia kila mwisho wa mwezi na kututukana kwa maneno ya kihuni kuwa watanzania ni wavivu wa kufikiri.

Sijui Mkapa aliingia madarakani kama rais akiwa na mtaji wa shilingi ngapi? Sijui alikuwa na makampuni mangapi? Sijui alikuwa na nyumba ngapi? Sijui alikuwa na magari mangapi?

Labda wana JF mtanisaidia hapa. Tusaidiane pia kutaja mali alizokuwa nazo wakati anatoka madarakani. Ni vizuri kuwa na uhakika na hili. Ni kama stori lakini najua siku fulani mahali fulani hizi nondo zitakuja kusaidia ukomboaji wa mali zetu. Yeye mwenyewe ndio atachambua zipi za halali na zipi za ufisadi.

Matukio kama haya yanakufanya mtu una-feel kabisa kuwa kuna watu wanaamini wao ni watanzania zaidi na wana haki kuliko wazalendo wengine. Nilipatwa mshtuko sana siku ya kwanza niliposikia kuwa Kiwira coal mine ni mali yake na waziri wake Dan Yona. Hii biashara hakututangazia mwenyewe kama anaifanya isipokuwa ni taarifa zilizovuja tu. Huenda kuna biashara nyingi alizofanya mjasiriamali.(lidumu azimio la mafisadi la Zanzibar)

Kwa kuanzia tu list ya nyumba zinazojulikana alizokuwa nazo mpaka anatoka ikulu ni hizi: (japo najua akiona hizi atasema tuna wivu wa kijinga)

  • Seaview (moja ya zile nyumba zetu za serikali walizogawana).
  • Nyumba aliyojengewa na Serikali Kule kijijini kwake Lupaso Masasi.
  • Nyumba ya Masasi mjini (inasemekana na hii amejengewa na serikali japo hii taarifa sina hakika nayo).
  • Nyumba aliyojenga huko Lushoto mkoani Tanga.[/
 
Green 29, Shukrani.
 
Pale seaview nyumba zake ziko mbili. Moja ni ile unayoisema ambayo ilitengenezwa kwa mabilioni na kisha kupewa yeye na nyingine ni ile ambayo sasa kama sikosei ni makao makuu ya Bank M

Kuna watu wanasema ana nyumba pia South Afrika ila hilo mimi sina uhakika kwahiyo naona tuiache mpaka tupate ushahidi.
 
Jamaa atakuwa aliingia ikulu na mtaji wa kutosha...
 
Ndugu zangu Watanzania Raisi Mkapa anatakiwa atoe speech kuelezea je ni kwa nini hii mikataba yote mibaya imetokea machoni kwake. Raisi kama kweli unapenda Watanzania huu ni wakati wa kujieleza au kuomba msamaha ili tuamini ulikuwa na nia nzuri na nchi yetu. Watanzania wengi walifurahishwa na kipaji chako cha elimu na kukuamini lakini badaya yake umebadilisha sheria za bunge 1995 na kufanya mikataba isainiwe na mawaziri badala ya kupitishwa bungeni. Vilevile inasemekana umejiuzia mradi wa makaa ya mawe. Tunakuoma ujieleza kable hatuja kuita mfisadi. Raisi mkapa tutakupa miezi michache uweze kutoa speech na kama hautafanya hivyo tutaandika mambo yote kama ni kweli na ulifanya kwa nia ya wizi.
 
Hili mbona liko wazi,unasubiri mpaka lini BWM kuitwa fisadi,BWM ni miongoni mwa vigogo wa ufisadi wakisaiidiana na Sumai wake.Mkapu anamiliki share kubwa sana ktk mradi wa makaa ya mawe Kiwira.Na kisingizio ni kwamba BWM eti ni mjasiliamali ndio alikua anaonyesha mfano wa kuigwa kwa watanzania.

Nitoe wito kwa watanzania wote kwamba kinachowapa jeuri marais wetu ni KATIBA,hii katiba tusipo fight mabadiliko kazi tunayoifanya hapa haitakua na maana.Japo sikumbuki ibara ya katiba lakini katiba imetamka wazi kwamba Rais hawezi kushitakiwa kwa kosa lolote alilolitenda akiwa madarakani,kwa misingi hiyo wanafanya wanavyoweza kufanya wakijua hawawezi kushitakiwa wala kufanywa lolote hata kama wataingia mikataba mibovu.

KATIBA JAMANI KATIBA,RAIS APUNGUZIWE MADARAKA.
 
Miaka kadhaa iliyopita niliwahi kupata barua pepe (Email) kwa mmoja Mtanzania kama mimi aki-solicit hizo emails I guess kwa watanzania kusaini petition ili Tanzania iruhusu DUAL CITIZENSHIP. Naamini watu wengi wali-support na mie mwenyewe nili-end up kwa kusaini. Hii issue ikawa kubwa na ya kitaifa na ninaamini ilianzwa kujadiliwa mpaka kwenye ngazi ya Bunge. Na hata JK mwenyewe aliwahi kuliongelea alipokuwa anajibu maswali ta watanzania wanaoishi nje ya Tanzania. Nikaona kuwa hiyo petition ilifanya serikali na Bunge kuwapa attention watanzania ambao walikuwa wanahitaji mabadiliko fulani. Nika-conclude kuwa petition nayo ina nguvu yake na hata kama serikali haitaki kusikiliza.

Sasa nirudi kwenye mada. Kumekuwa na tuhuma nyingi zimetajwa zinazomgusa Mfanyabiashara Ben W. Mkapa (sorry kwa kutotumia Rais Mstaafu kwa sababu alivunja miiko ya urais na alianza bizinee tangu akiwa Ikulu). Watanzania tena kwa wingi walimuomba Muungwana amfikishe huyo bizinesimani Mkapa mbele ya vyombo vya sheria ajibu jinsi alivyosimamia Utawala Bora. Lakini jibu linakuja "Tumuacheni Mzee wa Watu apumzike, alishastaafu siasa" Hili jibu uwa linanitia hasira sana. Najua alikuwa Mwenyekiti wa SISIEMU Taifa lakini linapokuja suala la Urais no siasa hapa. Mambo ya chama wanapaswa kumuuliza wanachama wenzake lakini linapokuja suala la Taifa, NO WAY SOME HAS GOT TO BE RESPONSIBLE. Tuhuma zimekuwa tuhuma, pesa inasafirishwa nje ya nchi a day before rais mpya anaingia madarakani, come on hapa lazima tupate majibu. JK kaombwa sana afikishe hili suala kwenye vyombo vya sheria lakini inaonekana kama anamkingia kifua. Najua kuna sheria ambazo zinamlinda kama Rais mstaafu na si kama Mhujumu maana anajua jinsi alivyocheza na Daniel Yona kutuibia. Sasa hizi sheria si zinapitia Bungeni kwanza na ndipo Rais ana saini?

Mie nafikiri tunaweza kutumia njia hiyo ya petition kwa kuwaelimisha wananchi wengi ambao hawana ideas na kile ambacho MAFISADI akiwemo Mkapa wamefanya. Baada ya hapo naamini wabunge wengi watajisikia kuwa pressured na Constituents wao na wakaikalia Bunge kooni wakapitisha huo muswada wa kumshughulikia Rais mstaafu hata yule aliyeko madarakani akionekana kavunja miiko ya kazi. Suala la Mkapa ni uhujumu Uchumi, hata kama hajafanya yeye personally lakini kwa njia moja au nyingine kashiriki. Sina zaidi cha kuelezea hapa maana tumesoma humu jinsi alivyoweza kujipatia hiyo kampuni yake toka serikalini.

Wabunge wengi wa CCM wakishakubaliana na huo muswada sijui ni vipi JK akashindwa kusaini kuwa sheria etkumlinda Mkapa basi hata miswada mingine itapitaje kama atashindwa kushirikiana na wabunge wake!! Hatuwezi kuvumilia nchi inaliwa eti kwa sababu sheria zinamlinda. Ziwekwe sheria kali ambazo zitawafanya WAKAZI WOTE IKULU kujiheshimu pindi wawapo madarakani. Kwa mtindo huu kama ukiendelea basi hata JK naye anaweza kuvurunda mwishoni mwa kipindi chake (Sijui kama atapata cha pili) na kubeba anachopenda ili mradi sheria inamlinda rais hata anapoachia madaraka. Kama kweli kuna hiyo sheria ya kumlinda Rais mwizi basi iundwe sheria nyingine ya kulinda mali ya umma inayoporwa na Rais. Najua kuna wengine watadai kuwa nimewahi kumuhukumu kwa kumwita Rais mwizi, Ndiyo ni mwizi maana ukitolewa tuhuma juu yako na usipotoa ushahidi wako basi nina-assume u r guilty. Mpaka kesho Mkapa kagoma kuzungumzia tuhuma zake kisa ameshastaafu siasa. Yaani kweli hilo ni jibu la mtu ambaye amewahi kuwa Rais. Hili suala halihusu siasa bali ethics za kazi pamoja kutuhumiwa kuuibia umma na pesa hiyo ambayo anaifanyia biashara. Kama umestaafu siasa kilichokupeleka Kenya kilikuwa nini????? Au ni kuchangamkia dolali za UN. Sikatai kwenda kuwapatanisha majirani zetu wakaelewana na kukaa meza moja kuwahudumia wananchi. Sasa Mkapa kinakushinda nini kuwapatanisha watanzania ambao wengine wanasema umeuibia UMMA na wengine wanasema haujaiba. Njoo before Tanzanians tena under OATH ueleze ni nini unachokijua kuanzia hiyo SONGAS yako na madudu yote ya BOT na kile mlichofanya pale TRA.

JK akishindwa kumsadia huyu Mzee kujibu tuhuma kwa ustaarabu basi itumike Petition na kuwashinikiza wabunge kuwa kama huyu jamaa wanamuonea aibu basi nasi tutaonyesha the same aibu kwenye sanduku la KURA.
Naamini Mama Kilango anazidi kuonyesha ukomavu kwa kuikalia serikali shingoni. Sasa bila ya kuwa na Kinyongo alichofanyiwa J4 kwenye sakata ya kutafuta mgombea SISIEMU, Mama Kilango unatakiwa kuuliza maswali mengi kuhusu viongozi maana naamini wewe ndiyo umepewa jukumu la kuongoza kamati ya Bunge inayohusu maadili. Hawa watu waulizwe under oath kwa sababu hakuna mtu aliye juu ya sheria na JK anamuonea aibu Mkapa kwa kulipa fadhila aliyomfanyia Dodoma kwenye zoezi la kutafuta mgombea. Sasa ni nani atakaidi BUNGE??????

Ikishindikana PETITION INAKUJA.
 
You people are only jealous of people who have made it. If someone turns in his motorbike and buys a car, you say he is corrupt. If someone builds a house through hard work, you say he is corrupt...If someone is corrupt, then tell us about it and you are going to see. But you must have proof. Even the press- you must have both sides of the story. I was a journalist. I know. You don't just accuse people for corruption without proof!

Do you still want the proof to show you that you made it through illegal means and looting from fellow Tanzanians?
 
What kind of proof do you need, everybody knows Mr. Mkapa is a corrupt i*******************
 
What kind of proof do you need, everybody knows Mr. Mkapa is a corrupt i*******************

Kokolo,

Kwa jinsi ulivyoandika hapo juu, unaweza kujikuta wewe ndio unaanguka kwa BP. Umetumia hasira mno na manguvu bila haja. Hakuna haja ya kutukana na badala yake mlime Mkapa kwa hoja na wala sio matusi.

Unavyochukia hivyo unaweza jikuta unajiumiza wewe mwenyewe bure. Ukiona kuna jambo umechukia basi usiandike mpaka ukiwa umetulia. Ukiandika na mahasira, ni rahisi mno kukosea.
 
Back
Top Bottom