BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,283
Ya Mkapa, David Martin na Kiwira
Johnson Mbwambo Aprili 9, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Kitendo
JUMATANO ya wiki iliyopita Rais Mstaafu Benjamin Mkapa (Bwana Msafi) alifanya mahojiano na BBC (Network Africa) kuhusu masuala mbalimbali yanayoihusu nchi yetu.
Kwa kuwa katika kipindi chake cha urais Mkapa alishawaponda waandishi wa habari wa hapa nchini kwamba hawajui kuuliza maswali kama wafanyavyo kina Riz Khan, nilishawishika kuyasikiliza mahojiano hayo na BBC mwanzo hadi mwisho.
Nilijisogeza kwenye redio nikitarajia kwamba huyo bwana angeulizwa maswali mazito na BBC ambayo waandishi wa habari wa hapa nyumbani wasingeweza kumuuliza kwa sababu, kwa mtazamo wake yeye Mkapa, hawana uwezo huo.
Nilishangaa kwamba mahojiano hayo yalimalizika bila mama yule kumuuliza Mkapa japo swali moja tu kati ya mengi ambayo Watanzania wanasubiri kwa hamu kupata majibu kutoka kwake.
Hayo ni pamoja na skandali ya ufisadi ya EPA ambayo ilishamiri wakati yeye ni Rais na kuhusika kwake na waziri wake, Daniel Yona katika kununua kampuni ya umma ya mgodi wa makaa ya mawe ya Kiwira.
Mengine ni mauzo ya nyumba za serikali na ununuzi wa rada hususan zilikopotelea dola milioni mbili ambazo asasi ya uchunguzi wa ufisadi ya Uingereza iitwayo SFO ilidai zilipelekwa kwenye benki moja ya Uswisi kwa ajili ya rushwa kwa maofisa wa serikali yake waliohusika na ununuzi wa rada hiyo.
Nilijiuliza ni kwa nini mwandishi yule wa BBC hakumwuliza Mkapa japo swali moja tu kati ya hayo; angalau lile la ufisadi wa pesa za EPA ambalo limeziudhi hata nchi wahisani zinazochangia, kila mwaka, kiasi kikubwa cha pesa katika bajeti ya Tanzania.
Hisia zangu ni kwamba labda hilo lilikuwa ni sharti kubwa la kufanya mahojiano hayo. Kwamba mwandishi amuulize maswali yote ya uchumi, biashara, huduma za jamii na demokrasia lakini asimuulize hayo ya tuhuma za ufisadi yanayomgusa moja kwa moja katika kipindi alichokuwa yeye rais.
Kwa hiyo, mwisho wa mahojiano, nilibaki na kiu yangu ile ile ya kutaka kumsikia Mkapa akifungua mdomo wake, kwa mara ya kwanza, kujitetea kuhusu tuhuma hizo nzito za ufisadi zinazomwandama; kiu ambayo pia naamini Watanzania wengi wanayo.
Nitaendelea kumlaumu mama huyo wa BBC kwa kutomuuliza Mkapa maswali hayo, kama ambavyo nitaendelea kumlaumu David Martin (Mungu amlaze pema peponi), kwa kutokufanya mahojiano ya pili na Mkapa baada ya kuwa amemaliza kipindi chake cha miaka kumi cha urais.
Wenye kumbukumbu nzuri watakumbuka kwamba mahojiano ya kwanza ya Mkapa mara baada ya kushinda urais, mwaka 1995, hayakuwa na mwandishi wa Tanzania; bali na Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti na Hifadhi ya Nyaraka Kusini mwa Afrika (SADRC), David Martin ambaye pia alikuwa rafiki yake wa miaka mingi.
Mahojiano hayo ya kwanza kabisa akiwa rais, yaliyofanyika Novemba 1995, yalichora picha ya Mkapa ambayo ni tofauti kabisa na picha tuliyoiona miaka 10 alipokuwa Ikulu.
Kuelewa hiki ninachotaka kukizungumza; ngoja nikukumbushe maswali mawili tu kati ya mengi aliyoulizwa na David Martin na majibu aliyoyatoa.
SWALI: Nimewasikia waandishi wa habari wakitumia maneno kadha wa kadha kukuelezea wewe. Lakini wewe mwenyewe unaweza kujieleza vipi?
JIBU: Sijui, kwa kweli sijui. Mimi ni mzalendo, mimi ni mtu wa kimataifa, mimi ni mwanademokrasia wa kijamaa, napendelea utawala safi na upanuzi wa uwajibikaji na dhamana ya majukumu ya jumuiya, kitaifa na kimataifa. Mimi ndimi.
SWALI: Hatimaye tukiangalia miaka mitano au kumi ijayo utakayokaa Ikulu, utapenda ukumbukwe vipi katika historia?
JIBU: Ningependa nikumbukwe kuwa nimeongoza serikali ambayo imepambana na rushwa na kuimarisha aina ya uongozi, utumishi wa umma, maadili na majukumu yanayojenga uongozi bora. Kwamba nimeongoza jitihada katika utawala wangu kuboresha nidhamu kwa maana ya sheria, kanuni na taratibu, lakini zinazoendana na uhuru wa msingi. Kwamba nimeendesha agenda ya vyama vingi bila madhara kwa taifa bali katika kukuza hisia za utaifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Natumaini itajasemwa kuwa nimejitahidi kupata mafanikio hayo bila ya majivuno ambayo kwa kawaida huambatana na madaraka makuu nchini, ila kinyume, kwa uadilifu na unyenyekevu wa hali ya juu.
Hayo ndiyo majibu ya Mkapa kuhusu maswali mawili tu kati ya mengi aliyoulizwa na David Martin wiki ya kwanza tu baada ya kuwa rais. Na hapa, wala sijaweka maelezo yale muhumu aliyoyatoa kuhusu rushwa kwamba mtu anakuwa waziri (na hana mali) lakini baada ya muda mfupi wa uwaziri anakuwa na mali na majumba kadhaa kiasi cha watu kujiuliza alipata wapi pesa kipindi hicho kifupi tu?
Narudia kusema kwamba nitaendelea kumlaumu David Martin kwamba hadi mauti yalipomkuta (mwaka jana) hakupata kufanya mahojiano mengine na Mkapa baada ya kuwa amemaliza hiyo miaka 10 ya kukaa Ikulu.
Miaka 13 iliyopita, Mkapa alimwambia David Martin kwamba anataka akumbukwe kama Rais aliyepambana na rushwa. Hivi kweli kama David Martin angefanya sehemu ya pili ya mahojiano na Mkapa baada ya kuondoka Ikulu, na akamuuliza, kwa namna tofauti, maswali hayo hayo aliyomuuliza miaka 10 iliyopita, angejibu nini kuhusu rushwa na ufisadi?
Baada ya mahojiano hayo na David Martin, Novemba 1995, Mkapa alikwenda mbali zaidi na kutangaza mali zake; lakini miaka 10 baadaye wakati anaondoka Ikulu akagoma kutangaza tena mali zake licha ya shinikizo la vyombo vya habari la kumtaka afanye hivyo.
Hebu fikiria. Alipoingia Ikulu alitangaza, kwa hiari yake mwenyewe, mali alizokuwanazo; lakini wakati wa kuondoka, miaka kumi baadaye, akagoma kufanya hivyo licha ya shinikizo la vyombo vya habari. Kwa nini agome? Jibu linaeleweka.
Miaka 13 iliyopita alimwambia David Martin kwamba angependa akumbukwe kama Rais aliyeongoza serikali iliyopambana na rushwa. Ni rushwa ipi aliyopambana nayo wakati yeye mwenyewe na waziri wake Daniel Yona, walijiuzia kampuni ya umma ya Kiwira Coal Mines Limited kwa bei poa ya Sh. milioni 700 wakati thamani halisi ya mgodi huo ilikuwa Sh. bilioni 4 ? (Kulikoni Aprili 2, 2008).
Rushwa ipi aliyopambana nayo wakati ufisadi uliendelea kila kona katika serikali yake ukiwemo huo wa mwisho mwisho wa EPA ambao ni wa aina yake katika historia ya Tanzania?
Ninachojaribu kueleza hapa ni kwamba picha ile ya Mkapa tuliyochorewa na David Martin mwaka 1995 si picha ya Mkapa tuliyemwona baadaye Ikulu.
Alitaka akumbukwe kama kiongozi aliyepambana na rushwa; lakini picha tuliyoiona ni ya Rais aliyeutamani utajiri wa haraka haraka kiasi cha kufanya biashara angali bado Ikulu; huku akinunua shirika la umma kwa bei poa.
Na naambiwa alikuwa pia akikimezea mate kiwanda cha sukari cha Mtibwa na mashamba yake makubwa ya miwa!
Kwa ufupi, ujumbe wangu ni kwamba wanasiasa hubadilika wakishaingia Ikulu; hivyo si jambo jema hata kidogo kuendelea na katiba ya nchi inayompa rais mstaafu kinga ya kushitakiwa kwa makosa aliyoyafanya akiwa madarakani.
Kinga ile ya kikatiba inakuwa na maana ukiwa na rais mwadilifu wa aina ya Mwalimu Nyerere, lakini nusu karne inaweza ikapita bila kumpata kiongozi mwingine wa aina ya Nyerere.
Kinga hiyo ya kikatiba haina maana hata kidogo unapokuwa na marais wa sampuli ya Mkapa wanaofanya biashara na mashirika ya umma wakishaingia Ikulu, na wakitoka Ikulu baada ya kumaliza muda wao bado wanaendelea kulipwa marupurupu yote ya Rais mstaafu!
Nionavyo; tukiliacha suala hili la kinga ya kushitakiwa ya rais mstaafu kuendelea kuwa open ended, tunaweza siku moja tukampata rais mwizi kupindukia wa aina ya Sani Abacha, na bado akimaliza kipindi chake cha urais tukashindwa kumfikisha mahakamani kwa kuwa tu ana kinga ya kikatiba.
Wakati umefika kwa Watanzania kuanza kulijadili suala hili. Wakati umefika kwa wabunge wetu kuliangalia hili; na ikibidi atokee jasiri mmoja awasilishe hoja binafsi bungeni juu ya suala hili ili mwishowe kinga ya rais mstaafu isiachwe open ended; hasa inapokuja kwenye kuhusishwa na ufisadi.
Ni lazima kinga hiyo iwe na mipaka kwa kuweka mazingira fulani fulani yanayoweza kuifanya kinga hiyo kuvuliwa ili kulinda fedha na mali za umma dhidi ya marais wa aina ya Abacha tunaoweza kuwachagua.
Tunaweza kumpigia kura mwanasiasa anayeonekana mwadilifu kweli kweli; lakini mwaka mmoja tu akiwa Ikulu akaanza kupora huku na kule kwa sababu tu anajua ana kinga ya kikatiba ya kutokushitakiwa.
Maana, kama nilivyosema mwanzo, wanasiasa hubadilika wanapoingia Ikulu. Na mfano mzuri ni Mkapa. Mkapa yule aliyehojiwa na David Martin Novemba 1995, si yule aliyetoka Ikulu miaka 10 baadaye.
Tafakari.
Email: mbwambojohnson@yahoo.com