Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Ni wazi kabisa kwamba baad ya kuvunjwa kwa baraza la mawaziri na kuteuliwa kwa baraza jipya kufuatia ripoti ya Dr.Mwakembe kamati ya kuchunguza ubadhirifu wa BOT ivunjwe nayo kwani tayari kuna watuhumiwa wawili mule ambao watavuruga mchakato mzima na kutuletea taarifa kuwa "utapeli wa BOT haukuwa na madhara kwa taifa" kama walivyofanya kwa Richmond. Hawa watu wawili Hosea na Mwanyika ni wazi wanapaswa kuondolewa kwenye ile kamati ili sio tu kuonekana haki imefanyika bali watu tuione kuwa inatendeka.
Wakuu mnaonaje wazo hilo la Dr. Slaa mie naliunga mguu kabisaaa

Augustoons,

I could be wrong but nafikiri watu hawa wawili wapo kwenye kamati kwa nyadhifa zao, na kama watalazimishwa kujiuzulu automatically wanaondoka kwenye hii tume.

To think kwamba Kikwete alishupalia sana kuwa AG na Hosea watashikia bango issue ya BOT would be comical if it wasn't so tragic.

Tatizo langu tumepata Waziri Mkuu mtu wa Usalama wa Taifa (usalama wa Taifa hawastaafu really) na issue ya BOT inahusisha usalama wa taifa, kuna uwezekano mkubwa wa cover ups hapo.
 
2008-02-09 08:39:47
Na Mary Edward, Dodoma

Kambi ya upinzani, imependekeza kuwa, Rais mstaafu Bw. Benjamin Mkapa achukuliwe hatua kwa madai ya kushiriki ufisadi na kujimilikisha mradi wa makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya.

Walimtaka Rais Jakaya Kikwete, aache kumtetea kwa kauli za `mwacheni Mkapa apumzike amestaafu` kwa kuwa hakuna sheria inayomlinda Rais aliyestaafu kushtakiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Naibu Kiongozi wa Upinzani, Dk. Wilbroad Slaa, alisema Bw. Mkapa amejimilikisha asilimia 85 za mradi wa Kiwira, ujasiri alioupata akiwa Ikulu.

``Tutamshtaki Mkapa na sheria ya kumshtaki ipo, hana kinga kisheria,`` alisema kiongozi huyo.

Alisema baadhi ya taarifa alizoandika kwenye Ofisi ya Msajili wa Kampuni (BRELLA) zinaonyesha kuwa, alijisajili kama Ben Mkapa, mjasiriamali. ``Tutamshtaki kama mjasiriamali, si kama Rais,`` alisema.

Katika hatua nyingine, kambi hiyo ya upinzani imetaka maamuzi ya Baraza la Mawaziri yasifanywe kwa siri.

Kiongozi wa kambi hiyo, Bw. Hamad Rashid Mohamed, alisema katika mkutano huo kuwa, wakati umefika yanayoamuliwa katika baraza hilo, yakafahamika kwa wabunge na wananchi walioiweka serikali madarakani.

Alisema taarifa ya kamati ya Richmond imebainisha kuwa, maamuzi ya baraza hilo, yalivunjwa na kulisababishia taifa hasara, lakini kama yangekuwa yanafahamika kwa wabunge, suala hilo lisingekubalika kwani kila hatua ingekosolewa.

``Katika kikao cha Baraza la Mawaziri, iliamuliwa kuwa, TANESCO itafute mzabuni wa kuzalisha umeme wa dharura, lakini Wizara ya Nishati na Madini, ikapuuza agizo hilo kwa shinikizo la Waziri Mkuu aliyejiuzulu na kuvunja agizo la baraza hilo ambalo Rais wa nchi ni kiongozi.``

Akizungumzia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), alisema Watanzania hawana imani nayo kwa vile msimamizi wa hazina ya Taifa, amevunja imani ya wananchi kwa kuandika barua na kufungua akaunti ya Richmond licha ya benki za nje kama Citi Bank kukataa kwa vile Richmond ni matapeli.

Alisema miswada ya nishati inayoletwa bungeni, haikubaliki kwa vile imelenga kuwahalalisha vigogo kuendelea kuinyonya TANESCO kwa staili ya Richmond ambayo inalipwa Sh. milioni 152 kwa siku.

``Kampuni ya uzalishaji umeme ya Aggreco, IPTL, Songas na Alstrom huchota kutoka TANESCO jumla ya Sh. bilioni 244 kwa mwaka,`` alisema Bw. Mohamed.

Alisema upinzani utashangaa kama mafisadi watateuliwa katika baraza jipya.

``Hatutamuelewa Rais endapo waliotajwa na kamati kwa namna moja au nyingine kuhusika na Richmond watateuliwa,`` alisema mbunge huyo wa Karatu (CHADEMA).

Walionya kutocheleweshwa kufikishwa Bungeni taarifa ya Ernst & Young inayohusu ufisadi wa BoT na kwamba itakuwa jinamizi kwa serikali na kusisitiza baraza jipya liiwasilishe ripoti hiyo na uchunguzi ufanyike kikamilifu.

``Kwa kilichotokea BoT, hatuna imani na kamati ya uchunguzi, hivyo Rais atafute wataalam wengine hata ikiwezekana kutoka nje na wanaoteuliwa watajwe kwa majina ili tujue namna ya kuwawajibisha,`` alisema.

Mwanasheria Mkuu ndiye Mwenyekiti wa Tume inayochunguza ufisadi wa BoT, na wajumbe ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali na Jeshi la Polisi.
SOURCE: Nipashe

..my take!

..ukishakula nyama ya mtu lazima utatafuta minofu mingine!

..kazi ipo!
 
"Muacheni Mzee apumzike."Jakaya kikwete
Mie nadhani imetosha.muacheni Mkpa apumzike na mdili na uchaguzi wa kiteto.Msipoangalia mtasindwa vibaya.na hili suala la kumng'oa Lowassa limewasaidia sana Chama tawal katika Kampeni zao.Wapinzania hawatashinda tena.

Tatizo wapinzani wamekosa sear nzuri na wanatumia makosa ya viongzoi wa CCM kama seara ya kuwapandisha juu,hii haitawasaidia sababu CCM wameshagundua hili.,wakiona mnang;angania jambo wanafanya kama mnavyotaka na wataendelea kupeta.

angalia sula la kumpa zitto kamati ya MAdini,ni kumpoza tu.na analipwa posho kubwa sana
 
Gembe you are an agent of who? Unamtetea Mkapa kwamba yaishie hapa ? Are you serious ? Sera za wapinzani wewe umesha soma vitabu vyao na kuona hawana sera ? Kuna sera inaweza kuwa na maana kwenye ufisadi ?What made you feel for Mkapa ?Nimeshangaa sana . Wapinzani wana sera za wazi na nyingi zimetumiwa na CCM na hata zinatumika .So kwa maandiko yako ulitaka hata issue madini na Buzwagu watu wakae kimya waanze kuelezea Uchimi ambao hata wakachukua Nchi kutakuwa hakuna kitu Bank ?Yaani wapinzani wache kushughulikia kuisafisha serikali unasema nini ? Umenishangaza sana .

Kushinda na kushindwa ni kawaida penye ushindani .Watanzania wanapaswa kuwapa wapinzani kura kwa kazi nzuri .Kama si wao leo hii nani angaliweza kumgusa Lowasa ? Si Mbowe na Zitto walipita huko mikoani na kusema wazomeeni wakija na uongo wao ? Unadhani kule kuzomea hadi Tarime watu kupiga ndege kwa jiwe JK kuacha kushangiliwa na kupewa mabango hakujasaidia ? Sera ipi unayo ongelea ambayo Vyama havina ? Kuna watu kama wewe wenye mawazo ya aina hiyo ndiyo wanaishia kusema sera hakuna .Are you sure Upinzani hauna sera ?Umenishangaza sana .Unajua kabisa kwamba pesa za BOT waligawana hadi kuwapa wabunge kwa kulingana na umuhimu wa jimbo ili washinde kwa kuhonga nk nao unasema ushindi ama kununua haki ambayo baadaye walio uza inawatokea puani ?Nimeshangaa sana na nitaendelea kushanga . Ama kweli mswahili ni ngozi ya .......
 
********JF--USHINDI LAZIMA**********
NA KWA NGUVU ZA MWENYEZI MUNGU ATACHUNGUZWA NA HIYO KINGA ATKUWA WA KWANZA KUONA BUNGE LIKISALITI KINGA YAKE KUPATA HAKI ZA WATANZANIA..WANA JF--TUPIGE MAOMBI USHINDI LAZIMA,,,,,TUPENI MUDA

Kambi ya upinzani, imependekeza kuwa, Rais mstaafu Bw. Benjamin Mkapa achukuliwe hatua kwa madai ya kushiriki ufisadi na kujimilikisha mradi wa makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya.

Walimtaka Rais Jakaya Kikwete, aache kumtetea kwa kauli za `mwacheni Mkapa apumzike amestaafu` kwa kuwa hakuna sheria inayomlinda Rais aliyestaafu kushtakiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Naibu Kiongozi wa Upinzani, Dk. Wilbroad Slaa, alisema Bw. Mkapa amejimilikisha asilimia 85 za mradi wa Kiwira, ujasiri alioupata akiwa Ikulu.

``Tutamshtaki Mkapa na sheria ya kumshtaki ipo, hana kinga kisheria,`` alisema kiongozi huyo.

Alisema baadhi ya taarifa alizoandika kwenye Ofisi ya Msajili wa Kampuni (BRELLA) zinaonyesha kuwa, alijisajili kama Ben Mkapa, mjasiriamali. ``Tutamshtaki kama mjasiriamali, si kama Rais,`` alisema.

Katika hatua nyingine, kambi hiyo ya upinzani imetaka maamuzi ya Baraza la Mawaziri yasifanywe kwa siri.

Kiongozi wa kambi hiyo, Bw. Hamad Rashid Mohamed, alisema katika mkutano huo kuwa, wakati umefika yanayoamuliwa katika baraza hilo, yakafahamika kwa wabunge na wananchi walioiweka serikali madarakani.

Alisema taarifa ya kamati ya Richmond imebainisha kuwa, maamuzi ya baraza hilo, yalivunjwa na kulisababishia taifa hasara, lakini kama yangekuwa yanafahamika kwa wabunge, suala hilo lisingekubalika kwani kila hatua ingekosolewa.

``Katika kikao cha Baraza la Mawaziri, iliamuliwa kuwa, TANESCO itafute mzabuni wa kuzalisha umeme wa dharura, lakini Wizara ya Nishati na Madini, ikapuuza agizo hilo kwa shinikizo la Waziri Mkuu aliyejiuzulu na kuvunja agizo la baraza hilo ambalo Rais wa nchi ni kiongozi.``

Akizungumzia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), alisema Watanzania hawana imani nayo kwa vile msimamizi wa hazina ya Taifa, amevunja imani ya wananchi kwa kuandika barua na kufungua akaunti ya Richmond licha ya benki za nje kama Citi Bank kukataa kwa vile Richmond ni matapeli.

Alisema miswada ya nishati inayoletwa bungeni, haikubaliki kwa vile imelenga kuwahalalisha vigogo kuendelea kuinyonya TANESCO kwa staili ya Richmond ambayo inalipwa Sh. milioni 152 kwa siku.

``Kampuni ya uzalishaji umeme ya Aggreco, IPTL, Songas na Alstrom huchota kutoka TANESCO jumla ya Sh. bilioni 244 kwa mwaka,`` alisema Bw. Mohamed.

Alisema upinzani utashangaa kama mafisadi watateuliwa katika baraza jipya.

``Hatutamuelewa Rais endapo waliotajwa na kamati kwa namna moja au nyingine kuhusika na Richmond watateuliwa,`` alisema mbunge huyo wa Karatu (CHADEMA).

Walionya kutocheleweshwa kufikishwa Bungeni taarifa ya Ernst & Young inayohusu ufisadi wa BoT na kwamba itakuwa jinamizi kwa serikali na kusisitiza baraza jipya liiwasilishe ripoti hiyo na uchunguzi ufanyike kikamilifu.

``Kwa kilichotokea BoT, hatuna imani na kamati ya uchunguzi, hivyo Rais atafute wataalam wengine hata ikiwezekana kutoka nje na wanaoteuliwa watajwe kwa majina ili tujue namna ya kuwawajibisha,`` alisema.

Mwanasheria Mkuu ndiye Mwenyekiti wa Tume inayochunguza ufisadi wa BoT, na wajumbe ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali na Jeshi la Polisi.
SOURCE: Nipashe

*******USHINDI ------LAZIMA***********
 
Ni suala la muda tu, hii kashfa ya Mkapa na Yona kujibinafshia mradi wa makaa utafichuka tu. Ngoja kamati ya akina Zitto imalize kazi.
 
..lets take stock,hivi mpaka sasa hizi kashfa ziko ngapi?

..moja ishazaa matunda[ndo imevunda sijui],nyingine tunasubiri.
 
PCCB walisema kuwa hawana ubavu wa kumchunguza Mkapa; Waoa hao hao wakasema kuwa utoaji wa mkataba wa Richmond haukuvunja sheria. Nasubiri wakati utapowadia tukianza kumrarua Mkapa kwa ujasiriamali.
 
PCCB walisema kuwa hawana ubavu wa kumchunguza Mkapa; Waoa hao hao wakasema kuwa utoaji wa mkataba wa Richmond haukuvunja sheria. Nasubiri wakati utapowadia tukianza kumrarua Mkapa kwa ujasiriamali.

Siku Mkapa atakapofunguliwa mashtaka kwa ufisadi alioufanya alipokuwa madarakani ndio siku wanyonge wote Watanzania watashangilia kwa nguvu zote na kujua kwamba kwa kupitia nguvu ya umma tunaweza kabisa kuhakikisha hakuna yeyote Tanzania aliye juu ya sheria, kama akifanya madudu tu basi mkono wa sheria utalala naye mbele. Na kama ataonekana ana hatia basi afilisiwe, hili litawatia adabu mafisadi na kutouchangamkia ufisadi.

Ningependa pia kuona wanachunguza mkopo aliopewa Mzindakaya toka BoT. Alipewa katika mazingira gani hasa ukitilia maanani kwamba BoT haitoi mikopo ya kibiashara. Na yule Mkono ambae alilipwa shilingi bilioni 8 naye achunguzwe alifanya kazi ipi BoT hadi akastahili kulipwa pesa nyingi kiasi hicho, kama hakuna ushahidi basi naye afilisiwe na kufunguliwa mashtaka.
 
PCCB walisema kuwa hawana ubavu wa kumchunguza Mkapa; Waoa hao hao wakasema kuwa utoaji wa mkataba wa Richmond haukuvunja sheria. Nasubiri wakati utapowadia tukianza kumrarua Mkapa kwa ujasiriamali.

Na ndio huu usanii wa Hosea ambao inatakiwa tuondokane nao haraka sana. Mkapa lazima atapekuliwa tu, ndio maana nikasema ni suala la muda.
 
Kwenye suala la Mkapa, tusiende kichwa kichwa kwa ajili ya ushabiki au unazi kuwa "asulubishwe, auawe'.
  • Kiwira; hapa kama kuna hoja, ni suala la conflict of interest na kutumia ofisi (madaraka) kwa manufaa binafsi. Suali je kifungo chake ni nini? Je hata kama Mkapa na Yona wakichunguzwa na ikabainika walichofanya ni kununua shirika kwa kuua ushindani, watapelekwa jela au kupigwa faini na ama kunyang'anywa mradi mzima (be ready for another litigation kudai fidia za mtaji)?
  • BOT; Mkapa alihusika vipi katika kuidhinisha malipo makubwa kama haya? je yeye kama Rais, kwa nini alishindwa kuwa makini na kudhibiti matumizi mabovu ya Hazina ya Taifa? Je hakuwa na kiwango cha kuidhinisha katika malipo au kila kitu kiliishia kwa Gavana, Katibu Mkuu na Waziri Hazina? Je ni kifungu gani Mkapa atafungwa? Uhujumu, Uzembe, Udhaifu wa Kiutendaji au Ufisadi?
  • Rada, IPTL, Madini; Mkapa kama raisi, nafasi yake ilikuwa ipi? je kila kitu alikiacha kwa watendaji wa wizara husika bila idhini ya baraza la mawaziri? Je ni uongozi wa namna gani ambao alikuwa nao kuachia mikataba mikubwa kufanyika na yeye kutia sahihi bila kuhoji faida zote na umuhimu wa mikataba hiyo kwa Taifa? kosa ni Uzembe, Uhujumu, Udhaifu au Ufisadi?
Mengi ya haya ya Uhujumu na Ufisadi yanayohusisha viongozi wetu yataishia kuwa kashfa na aibu machoni pa Taifa na Jamii na si kifungo cha jela. Lowassa keshaanza kutumikia hiko kifungo, je swali ni hili, Bunge na Serikali itafanya nini ili kuzuia kutokea kwa Uhujumu, Uzembe, Udhaifu wa Kiutendaji na Ufisadi wa namna hii ambao huishia kuwa Aibu na si Uhalifu wa Jela?

Je Mheshimiwa Pinda na Kikwete wanaweza kutuhakikishia kuwa wataziba mianya yote ya Uhujumu kwa kupitia mitaa ya uzembe? Je CCM itafanya nini ili kuhakikisha inaondokana na tabaka hili la Ki-Lowassa au Ki-Mkapa ambapo hitimisho ni watu kuaibishwa eti walikuwa ni Wazembe, Dhaifu au si Makini sana na si Uadilifu kwa Uhujumu wa Kifisadi?

It is easy to say "amekula hela" lakini kuleta ushahidi ni shida, kumbuka Mkapa alishasema mwenye "ushahidi" aulete! Mbilinyi, Kitine na Simba wakawajibika kwa aibu na si kwenda jela!
 
Sisi ndo tunatengeneza histori ya Tanzania, magumu yapo mengi lakini lakini uzuri wake ni kwamba yana utatuzi.

Tulipoanza kuongelea kuhusu ufisadi na Wizi ndani ya serikali watu wengi walituona majuha wakubwa. tena walituita wakimbizi tumekimbia nchi na kuja kuishi Marekani.
Baada ya kuitwa mkimbizi bainafsi niliapa kwamba nitatawanya uchfau wa serikali yetu kwa kila mwananchi wa marekani mwenye kutaka kuusoma, pia mimi mwenyewe nitaendelea kupiga kelele mpka kieleweke.

Watanzania wenye nia ya kujenga nchi yao wapo kila kona, ila kwa sababu ya kuzidiwa nguvu kiuchumi kisiasa na kihali na Mafisadi uzalendo wao hauonekani hata kidogo. Ili mradi wapo mtu au kikundi kisijidanganye kwamba hakuna kitakacho fanyika, tutaishia kuwatazama tu.

Mtu mwongo siku zote huidanganya nafsi yake kwanza ndipo huondoka kwenda kudanganya nafsi nyingine.

Mtu asijidanganye, hakuna jiwe litakalo simama juu ya jiwe mpaka ukweli uanikwe juani na wnyewe kunyaushwa mmoja hadi mwingine.
Nikisema jiwe ni pamoja na kokoto. hakuna kokoto itakayo simama juu ya kokoto nyingine tutachambua kila kitu kama karanga za kuchoma.

Hilo bango la Umoja na Amani mnalijivunia siku zote ndiyo dila yetu wanyonge.Chini ya Umoja na Amni mtashitakiwa na kuchukuliwa hatua bila kelele wala mikwaruzo yeyote.

Hata kama itachukua miaka 10 Wahujumu wa uchumi wa Tanzania ni lazima washitakiwe, kitakacho wasevu ni kifo tu.

Hujuma walizo zifanya ni za makusudi kwa hiyo ni lazima washitakiwe popote pale watakapo kimbilia duniani.

Kama kuna maagent wa kuwatetea Mafisadi hapa JF tunawakaribisha kwa mikono miwili ila tu jueni moja ma client wenu ni lazima siku moja wata simama kizimbani kijibu hoja moja baada ya nyingine huku Watanzania wote wakiona tendo hilo Live katikaTV kwa mara ya kwanza tangu nchi ijipatie Uhuru.
 
Kama DITO aliyeua yuko huru itakuwa Che-Nkapa? Yote yanawezekana ni muda tu! Tukaze uzi.
 
Kwenye suala la Mkapa, tusiende kichwa kichwa kwa ajili ya ushabiki au unazi kuwa "asulubishwe, auawe'.

Mkuu, hakuna anayeenda kichwa kichwa. Mkapa kafanya ufisadi ndio maana hayuko tayari kuzungumzia ufisadi alioufanya. Kama utakumbuka yeye alituita Watanzania wavivu wakufikiri na tukimuona mtu amekuwa tajiri tu basi tunashabikia kwamba kachukua rushwa. Wakati ule aliposema haya tulikuwa hatujui kwamba the so called mr clean alikuwa si msafi chochote! alikuwa ni mchafu wa hali ya juu.

Mkapa ni mtu anayeelewa mambo kwa upeo mkubwa na alijua fika kwamba madaraka aliyokabidhiwa na Watanzania ya kutuongoza yalikuwa hayamruhusu kufanya biashara akiwa Rais wa nchi, lakini ama kwa dharau au uroho wa utajiri wa haraka haraka hakuliona hili kama ni pingamizi la hali ya juu.

Magazeti chungu nzima Tanzania yameandika jinsi yeye na Daniel Yona walivyojipatia KCM katika mazingira ya kutatanisha. Angekuwa mstaarabu angeshaomba ama kukutana na wanahabari au kuandika katika gazeti lolote lile jinsi walivyojipatia KCM, lakini kwa kutudharau Watanzania ameamua kukaa kimya.

Alidhani kwamba baada ya muda Watanzania tutasahau na yeye aendelee kufaidi utajiri wake alioupata kupitia ufisadi aliofanya akiwa Ikulu. Hakujua Watanzania wa leo siyo kama wale wa mwaka 47 wanalalamikia pembeni kwa unyonge halafu wanasahau na kuendelea na shughuli zao. Hili la ufisadi limemganda kama luba atajibaraguza anavyotaka lakini Watanzania tumesema mpaka kieleweke hawezi kujimilikisha rasilimali zetu kienyeji nasi tunyamaze kimya tu. Watanzania wote popote pale walipo duniani wanataka Mkapa atendewe haki lakini kama alinufaika kwa njia za haramu alipokuwa Ikulu lazima afunguliwe mashtaka na akionekana ana hatia lazima pia afilisiwe.
 
It is important that the opposition "strike while the iron is hot"

This is the best time to hold Kikwete to his oath and his presidential accountability. My only fear is Kikwete is toothless to prosecute Lowassa, let alone Mkapa, since he himself is implicated.

Swali la kujiuliza si Mkapa he is old news/the past.
Rais Kikwete anacho tuambia ni nini pamoja na taasisi zote za serikali alizonazo hakuwa anajua nini kinatokea kwenye serikali?? haya maskandali yote anajidai kuya-distance from himself. Ni sahihi kuwa alikuwa hajui??
Anakubali kuwa yeye ni zimamoto?? Na kuwa sio kiongozi??

Wajibu wake ni kuongoza njia kwa watanzania anatakiwa yeye ndiye anayejua kila kitu kinachotokea TZ na kuongoza (all initiatives should have his blessings) he is the "Initiator"

Maana yake ni kuwa yeye amechukua back-seat kwenye uongozi. Hakuchaguliwa ili awezimamoto bali aongoze maendeleo ya TZ

Katika hali hii tunasemaje "AMESHIDWA KAZI" He has to pull up his socks.

Asijidai kuwa his house will be in order before President Bush visit. Je anawajibika kwa Bush??
 
Mkuu, hakuna anayeenda kichwa kichwa. Mkapa kafanya ufisadi ndio maana hayuko tayari kuzungumzia ufisadi alioufanya. Kama utakumbuka yeye alituita Watanzania wavivu wakufikiri na tukimuona mtu amekuwa tajiri tu basi tunashabikia kwamba kachukua rushwa. Wakati ule aliposema haya tulikuwa hatujui kwamba the so called mr clean alikuwa si msafi chochote! alikuwa ni mchafu wa hali ya juu.
Bubu,

Suala si kuwa hatujui kuwa Mkapa ni fisadi, suala ni kuwa je kuna ushahidi wa kufungika na kufilisiwa mali?

Hili linanijia ukiangalia Tokomile alilocheza Lowassa na Muungwana kwenye Richmond. Lowassa kawajibika kisiasa na kupoteza kazi, lakini ripoti ya Mwakyembe haionyeshi kuwa kuna ushahidi wa wizi au yeye Lowassa kunufaika kifedhaau kimali.

Ndio maana nasema tusiende kichwa kichwa maana CCM na mafisadi wana turufu mpya ya Ubangusilo ambayo huishia kuaibishwa hadharani lakini kesi hamna, ushahidi hautoshi na hivyo MWafisadi kuendelea kupeta kula walivyochuma.

Trust me I would like to see every one of the mafisadi gets trivial time at Mahakama Kuu kivukoni, serve time in Ukonga and loose everything kwa kufilisiwa. Lakini compromises za kichama ambazo huwa ni adhabu kwa uzembe au kutokuwa makini hazina vifungo au kufilisiwa!

That is where I have a beef that kelele za "asulubiwe' zitaishia kuwa kelele na hakuna atakaye kwenda Golgota!
 
Maneno yako mazito na wa TZ wakae wafikirie tena hizi reports .Kwa kuwa hazikuonyesha wizi ndiyo maana Slaa kaomba polisi wapewe kazi na kujua ukweli zaidi ili twende Mahakamani .
 
Kuna mengi yameongewa yakimhushisha Mkapa na kashfa nyingi sana ambazo sisi kama watanzania wenye nchi tunahitaji majibu toka kwake. Mimi sikubaliani kabisa na hii sheria ya kinga ya rais mstaafu kutohojiwa au kufikishwa mahakamani hata kama kuna walakini katika utumishi wake. Naamini Mkapa anaringa kutokana na sheria hii kumlinda. Najiuliza mashwari,kashfa ya BOT na zingine zitakapoonyeha amehusika moja kwa moja,JE ITACHUKULIWA HATUA?
 
Back
Top Bottom