Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

PM..waandishi wangejuaje, wakati viongozi wetu hawana culture ya transparency? na ungetegemea reparcussions gani kwa watumishi ambao wangeleak hii info. Mbona watu mnakuwa kama nchi yetu hamuijui vyema? unless umekaa ughaibuni for ages. You will be excused for that!
 
Wanabodi,

Transparency inahusiana nini na USHENZI!...nitarudia kusema kuwa ukitembea na mke wangu iwe wazi ama kwa maficho - watu wazungumzie au wasi zungumzie bado haiondoi uzito wa KOSA la ZINAA!...transparency inafanya kazi ikiwa vitendo ni vizuri! - Haramu ni haramu haina afadhali!
Kiongozi kama Mkapa alitakiwa kuelewa toka mwanzo kwamba hizo fedha alizochukua zingeweza kuwasaidia Wajarisiamali 1000. Hii ndio kazi yake aliyokabisdhiwa na wananchi na kuaminiwa na hata benki za nje ktk mikopo. He is a President - for Christ sake!
Kama alivyosema Ibrah hapo juu, jamani ni wakati umefika kwa Wadanganyika kuweza kutambua mitume (viongozi) wa Uongo na kuwawajibisha!
hakuna kitu too late hapa, sheria waliitunga wenyewe hao viongozi kwa maslahi yao na bila ridhaa ya wananchi kwa hiyo tunaweza kabisa kulipinga swala hili. Hata tulipokuwa tukitawaliwa kulikuwa na sheria zimetungwa kwa maslahi ya Wakoloni, haikuwa late wakati ule na haiwezi kuwa late leo hii... Mapambano dhidi ya Unyonyaji hauna kipimo wala mipaka....
Ikiwa wanawake wameweza kubadilisha sheria zilizotungwa na wanaume itashindikana vipi taifa zima likisimama na kusema hatutaki mitume wa Uongo!...
Wayahudi hadi leo hii wanawasaka hao ma NAZI tena baada ya miaka 60 toka matukio ya genocide, itakuwa sisi na viongozi ambao hadi leo hii wamelimbikiza mali mbele ya macho yetu!

Lakini hata hivyo sina wasiwasi sana na matendo haya maovu ya viongozi wetu. Wanachosahahu ni kuuelewa Utamaduni wa mwafrika.. Watakapo kufa wataondoka na ufalme wao kaburini, mali wataiacha juu na mafisi wengine wataimaliza familia yake. Tumeyaona haya mkiwafanyia wazee waliokwisha kufa!... mmeweza kuwafukuza ktk majumba ya serikali, mkachukua mali zao na kuwaacha wajane maskini... same will happen to you.
Mkapa siku atakayo ondoka basi akumbuke kwamba mkewe, watoto wake na familia yake watakuwa matatani.. wataachiwa kibanda kimoja tu kwani Mdanganyika hucheka na wewe ukiwa hai bado...Mifisi hawa husubiri mauti tu, watakula hata tumbo za mama zao!
 
halisi na mkandara et all nakubaliana na nyie baadhi ya mambo ..especially hii habari kujulikana leo ..inaonyesha tusimlaumu mkapa tuwalaumu waandishi..kwani wako busy kutuletea habari za udaku na za utafiti kama hizi zinawashinda....kama mtu hakuficha jina iliwashinda nini kugundua miaka hiyo..ndio maana akawaanawaona hamnazo...UANDISHI NI KAMA KIOO CHA JAMII KUTUSAIDIA KUJIREKEBISHA ...KUCHELEWESHA HABARI NI SAWA NA KULETA MAJUNGU KUTULETEA HII HABARI LEO AMBAPO HATUWEZI KUMPIGIA KELEELE MKAPA ...Laiti ingekuja mapema habari hii tungeweza kuzuia au kumrekebisha ...kwa ajili imechelewa ..na pia kwa kuwa haikuwa imefichwa ..bali ilihitaji tu mwandishi mchunguzi kupitia makabrasha ya msajili wa biashara mara kwa mara BRELA tena naona hata wana mtandao...angeshagundua vigogo wooote wenye makampuni....ni kwa sababu tu imechelewa na imekuja kipindi ambacho THERES LESS WE CAN HELP NOW ...naamua kuiita MAJUNGU ..na inaonekana ni habari yenye nia iliyokusudiwa kwa sassa....
mbona pia hamuongelei wanasiasa wenye mapesa nje ..na hao tunawafanyaje??????

Bravo mzee,

Uliyosema ni sahihi kabisa. Msingi wa yote haya ni kuwa hakuna sheria iliyovunjwa na Mkapa. Hayo ya why tumejua leo and not then.. pia sio hoja hata kama tungejua 1999 the fact still stands tall.... hakuna sheria iliyovunjwa.

On the other side kama tunaona morally is wrong huu ndio wakati wa kurekebisha hilo tuwe na sheria rasmi inayozuia hayo
 
Kanda2,
Wakati wakoloni wakiendeleza kututawala unafikiri pia haikuwa kosa la kutawaliwa kwa sababu tu sheria iliwaruhusu? Hata wale ma NAZI sheria iliwaruhusu kuua Jews...kwanini leo mnawakumu?
kama ndio mpango wenyewe ndio huu basi hao akina Gandhi, MLK, Che na wengine wengi sana wasingekuwa role model wetu...
Ama kwa sababu mkoloni leo ni mwafrika mwenzetu!
 
Kanda2,
Wakati wakoloni wakiendeleza kututawala unafikiri pia haikuwa kosa la kutawaliwa kwa sababu tu sheria iliwaruhusu? Hata wale ma NAZI sheria iliwaruhusu kuua Jews...kwanini leo mnawakumu?
kama ndio mpango wenyewe ndio huu basi hao akina Gandhi, MLK, Che na wengine wengi sana wasingekuwa role model wetu...
Ama kwa sababu mkoloni leo ni mwafrika mwenzetu!

Great!

Kwa mtaji huo solution ni kubadilisha sheria au tuwang'oe hao waliotuletea sheria hii (CCM) preferably ktk ballot box if not... other means... lakini mie simo! ( kwenye option 2)

Kuendelea kumsakama Mkapa ni sawa na kulaumu tulikoangukia na kusahau tulikojikwaa....
 
Kanda2,
Kuendelea kumsakama Mkapa ni sawa na kulaumu tulikoangukia na kusahau tulikojikwaa....

Kiswahili lugha yangu na napenda sana mazungumzo kama haya!...Hapo hapo naunganisha hivi:-

1. Unafikiri Wazimbabwe leo hii kumsakama Mugabe ni kosa kwa sababu walijikwaa wenyewe, hivyo muhimu kwao kutazama wapi walipojikwaa badala ya pale walipoangukia?
2. Ni wakati gani muafaka wa kutangaza maumivu huwa kabla kujajikwaa ama baada ya kujikwaa na kuanguka!.. Je, ni kisiki kinachotazamwa ama ulipodondokea pia.
3. Kisiki kilichowekwa na City kama alama kinaweza kuondolewa na mwananchi wa kawaida kwa sababu ni hatari kwao?....
4. Mkapa ni mmoja wa waanzilishi wa hiyo sheria ya viongozi kuwa ruksa kwao kufanya biashara!...tena kwa ubaya zaidi katumia Ujariamali kuchukua fedha za wanyonge!...

Bob, sidhani kama waafrika watakuwa na kosa kumlaani Ian Smith na Botha ati kwa sababu wao hawakuanzisha utawala wa mkoloni ila waliukuta tayari...

Tupo mjini hoja hii ni muhimu tupate kuilelewa vizuri na kutafuta ufumbuzi!..
 
Mzee Bob,

Heshima mbele, maneno mazito hayo hakuna la kuongeza,


Isipokuwa tu kwa mzee Admin, ni kwamba hiii tabia ya watu kuingia na majina mengi, ukweli ni kwamba inatia kichefu chefu na ndio maana ninasema kuwa usanii wa viongozi wetu unaanzia humu humu kwenye hii forum, I mean ninaelewa hii excuse kwamba ati watu wanaweza kuwa wanatumia compyuta moja, lakini please yaani tumegeuka kama watoto wadogo, yaani kweli jaama one minute anasema one thing kwa jina moja, halafu tena anageuka na jina lingine na kujidai kuwa ni hoja tofauti, hivi huu ujinga wabongo tutaondokana nao lini?

Yes, ujinga ujinga ujinga tuuuu, hamna la maana ni nani mwenye nguvu za serikali atatuchukulia kuwa tuko serious? I mean kuna watu ninaona wanatumia angalau majina mawili, lakini hawaandiki na kujijibu, yaani kweli bwana Admin hili tatizo haliwezi kutatuliwa?

Sasa tutaendelea kuwa kichekesho mpaka lini, na watu wote ahpa ni watu wazima? Inatia kinyaaaa jamani!
 
hizi mada ziunganishwe ....

jamani watanzania MIIKO YA UONGOZI ILIFUTWA TANGU MIAKA YA 1990....na wala hatukuweka miiko inayoendana na karne hii ili kuchukua nafasi ya iliyofutwa..
kwa mantiki hiyo hakuna kipengele kinachomzuia rais au mwanasiasa kuwa na hisa au kuwa mkurugenzi wa makampuni....labda kama itadhibitika hiyo mikopo alichukua bila kuweka collateral..justify that!...tena kwa mr and mrs mkapa by using there own names and not hiding anything withregard to that ,whatsoever ..it has vividly shown that they had no BAD INTENT ,opening the compony And so nothing to hide ...

I DONT SEE ANYTHING BAD....unajua mara nyingine sisi watanzania tusifanye viongozi wawe wanafiki waweke mapesa ULAYA..kama mtu havunji sheria afungue kampuni au makampuni MCHANA KWEUPE ili kama kuna foul play watu waone..kama hivi mnavyoona kampuni hiyo na wakurugenzi mmewaona..hakuna siri...endeleeni tu kufuatilia kama mkopo amepata kihalali...kodi analipa..nssf kama ipo analipa..kodi za majengo ,,..ets ..

kunao viongozi tuanawafahamu walifanya kazi na mwalimu kina ms... wamejaza makampuni canada na japan huku walikuwa wakiimba UJAMAA naomba warudiushe hayo madola hapa yalete ajiara..zaidi wakingoja WAFE watadhulumiwa kama MOBUTU,,

Ama kwa hakika Wadanganyika tumekwisha. Lazima watetezi wa Mkapa kwenye hili watakuwa ni watu wanaofaidi sehemu ya uhuni huu. Hakuna njia mnaweza kuhalalisha ujinga huu, hakuna.
PM na Kanda2 hebu tuchukulie tu kwa sababu hakuna sheria inayomkataza kiongozi (mtawala) kuwa na kampuni au kuwa mjasiria mali (whatever that means), Barnabas Samata (Ndio yule Jaji Mkuu wa Tanzania) akaamua kuwa mjasiriamali na kuanzisha Samata Advocates and Co. itakuwaje? Si havunji sheria yeyote? Na majaji wengine nao wakaamua kuiga mfano kwani sheria haikatazi watu kuwa wajasiriamali.
 
Tabasamu, wengine na waungwana akina Mkandara tumeyapigia kelele mno haya mambo...ila inaonekana wananchi wenzetu hawalioni hili! We acha tuu..inasikitisha. Harafu tunakemea ufisadi? Unafiki mkubwa!
 
Point ambayo PM na Kanda2 hawaielewi ni kwamba Mkapa asingekuwa rais angeweza kupata huo mkopo wa NBC kirahisi hivyo? Na kama jibu ni ndiyo, mbona hawakufanya hivyo mpaka walipoingia Ikulu? Mnajua Marekani ni taifa la kibepari. Lakini wana sheria kabambe zinazowashika viongozi wao. Kama umeamua kuwa kiongozi wa Marekani achana kabisa na biashara. Cheney ilibidi ajivue uhusiano na Halibutron. Hivi leo ikifahamika Cheney alipia simu Halibutron kuulizia hisa zake anaweza kuachishwa kazi. Lakini baada ya uongozi anaweza kuendelea na miradi yake. Lakini Mkapa na mkewe waliipata hiyo mikopo kutokana na cheo chake rais, na si vinginevyo. Na hii kwangu ni haramu. Inapaswa kuwa hivyo kwa kila Mtanzania.
 
Hivi ni kiongozi gani wa serikali ya bongo leo, au aliyestaafu ambaye utajiri wake hauanzii na mikopo?

Ukweli ni kwamba wote huchukua mikopo, sasa kama mkopo ni justification ya utajiri wa viongozi wa bongo basi hakuna kiongozi aliyewahi kutuibia wananchi, wote ni wasafi ila utakiri wao unaanzia kwenye mikopo, je akiwa waziri kwa nini Mkapa alishindwa kuchukua hii mikopo?

Yaanai katika miaka 10 tu ya urais, Mkapa amechukua mikopo yakumuwezesha kuwa na hizi mali zote alizonazo sasa? I mean huuu ndio moja ya uozo ninaousema kila wakati ndani ya ccm, mali za huyu mzee ni nyingi kupatikana kwa mikopo in ten years, I have no beef na wanaomtetea, lakini please waje na another excuse ya mkopo hapana!
 
Naungana na Mzee Es lwa hili . Sitaki kusema sana maana inatia uchungu .watetezi wa mkapa waje na hoja mpya . Je hakuna ukweli wa hili jambo na JK akaanza kuangalia namna ya kutafuta haki hata kwa kutumia PCB nk wakasema uongo kama Richmond na mengine ambayo tunayategemea kusemewa na PCB ?
 
Mzee Jasusi.... Mr Cheney bado anapata mafao kutoka Halliburton... fuatilia Tax return yake ya mwaka jana ilivyowekwa public!
Ila hiyo ni kutokana na position yake kipindi hichooooo alipokuwa Halliburton wakati wa Clinton!
 
Brutus,
Ni kweli Chenney ANAPATA mafao yake Halliburton sawa na mimi hapa Mkandara nayefuatilia mafao yangu ndani ya Halliburton. Chenney ana nafasi sawa na mimi hapa ndani ya Halliburton kama mwenye hisa..
Ni ruksa kununua hisa kama vile Mkapa angenunua hisa kampuni zetu za DSE, haikatazwi. Kinachokatazwa ni kufungua biashara yako chini ya kofia uliyokabidhiwa na wananchi!... vitu viwili tofauti kabisa na nadhani Kichuguu kasema vizuri sana kuhusu jaji mkuu. Mkapa & co ni owner wa Halliburton za kibongo!
Kama viongozi wetu wangekuwa na nia ya kuliendeleza taifa toka mwanzo makampuni yote makubwa yangekwenda sokoni kuwapa wananchi nafasi ya kununua hisa!lakini yaliyauza wao na kupata 10% ambazo wengi wao wamewekesha tena ktk makampuni hayo hayo. Mtaji wa hisa zao ni nguvu ya wananchi.
Sawa na majumba yote ya NHC na Msajili wanayomiliki wameyachukua kwa kodi waliyoipanga wao mathlan 200,000 lakini wao wanayapangisha majumba hayo kwa 2,000,000 (wazungu) na hawalipi kodi serikalini kama wapangishaji.... biashara nyingine hiyo!

Nitarudia kusema Mkapa hawezi kuwa wala kuwekwa ktk kundi la wajiriamali, nitafurahi sana kumwona ktk ofisi zetu za Saccos maanake ndiko walalahoi wengi tumerundikwa kama kaa wanaosubiri mafuta ya moto.
 
Lakini Mkapa hajawahi kuwa ceo wa Halliburton, mafao anayopata kwa kuwa ex-rais ni shillingi millioni moja kwa mwezi kwa mujibu wa sheria, zetu sasa haya majengo yote mpaka Lushoto, hapa mjini ndo kabisaaa yametapakaa kila kona, yaani ni mikopo tu katika miaka kumi ya urais?

Chenney, alilipwa dola millioni 45, alipoacha huko Halliburton, je Mkapa alilipwa ngapi alipoacha uwaziri wa elimu ya juu na sayansi? Au ni kabila ya mke wake ndio inampa uhalali wa utajiri wake kuwa ni wa mikopo katika hii forum?
 
Alichofanya Mh Rais ni Unethical!
Mwl Nyerere alisema wanaokimbilia ikulu kuna biashara gani???... labda ndio hizi!
 
tabasamu...majaji bado wanayo code of conduct...tena juzi tena wamekutana nawakajadiliana kwa kina namna ya kuzilinda ETHICS zao..kwa mfano..mwenendo wa jaji unathibitiwa kimttazamo na kimatendo kuanzia ofisini,nyumbani ,hadi matendo yake ni lazima yawe ya kiungwana na yatoe tumaini la haki kwa raia...na wana commission yao kuangalia haya...wengi hapa mnawajua majaji kuanzia kina georges,nyalali hadi sammatta...mfano jaji hawezi tu kwenda kila mahali mfano mkanywa nae pale magomeni au brake point mpaka saa kumi usiku na kesho mkakutana mahakama kuu na ukampa heshima ileile..lazima hata sehemu anayikaa na kustarehe iwe na staha..mfano leaders club[enzi hizo]..police mess ,au hoteli zenye hadhi...sasa siku hizi hata serikali inashindwa kuwapa nyumba grade A ..ets

kimsingitukubaliane kuondoa MIIKO YA VIONGOZI lilikuwa kosa ..hata mwalimu alisema."...viongozi wetu wamekutana zanzibar[1990] ..wameamua huko kimiya kimiya hawajatuambia wamerudi maneno yao MATENO yao ..wenye akili tukajua ..miiko ya viongozi ..azimio la arusha basi tena ...mimi huwa hadi leo natembea na vitabu viwili,,biblia na kitabu cha azimia la arusha..nakipitia kila siku sijaona kosa ..kinongelea usawa wa binadamu,,."

kwa hiyo wazee tunatibu je hili kosa tunatibu dalili au ugonjwa???
 
Hivi habari hizi pia ziko kwa KIswahili ili walalahoi wazijue ? Hivi kweli CCM wana la kutueleza hapa ? Maana haya yamefanywa na aliyekuwa Mwenyekiti ambaye pia alikuwa Rais wetu .
 
Mzee PM,

Azimio la Arusha, lilikuwa kwa ajili ya kina Mnauye na Sozigwa, huku the chosen kina Kahama, Bomani, Msuya, Rupia na the likes wakineemeka humo humo kwenye Azimio, ndio maana wakaamua kuwa kama ni kuneeemekea basi waneemeke wote, au wasineeemeke wote,

Mwalimu alijua wazi kuwa time was up ya mambo ya Aziimio, kufa kwa communism kumetufundisha kuwa itikadi ya siasa inayoweza kufanikiwa duniani ni ile tu inayojali matakwa binafsi ya wananchi wake,

I mean viongozi wa huko majuu ni matajiri wa kupindukia, lakini sio kwa mikopo wakiwa kazini yaani kwenye urais, infact watu kama Clinton, na Powell, ndio kwanza wanaanza kutajirika sasa baada ya kutoka madarakani, kutokana na kuandika vitabu na specch fees, hoja za Azimio na mikopo bado ni pungufu katika kuhalalisha utajiri wa Mkapa, ambao sasa umetapakaa mpaka kwa watoto na ndugu wa mke kina Joe Maro, ni aibu sana mbelele ya jamii na hata mbele ya Mungu, lazima kuwepo na hururma kidogo na hela za wananchi!
 
hivi watanzania kunaubaya gani kwa mfano wa watu wawili.....wote waadilifu tu
KADUMA..huyu alikuwa kijana mwadilifu wa mwalimu..waziri wa nje na mengine mengi...amelitumikia taifa vema mcha mungu....kajiwekea fedha zake za posho za safari ,vikao na vyanzo vingine halali..hadi leo anamiliki mashamba,shule ..na mali za kutosha kwa jasho lake ..hategemi kufa masikini tena.....je huyu si mfani wa kiongozi bora???..mwenye uwezo wakusave..hata kama pia alikopa..sifa ya mtu mwadilifu ni pamoja na kutumia vema mapato yake ..tuwatie moyo wafanye hivi wengi..

CHEDIEL MGONJA ..naye mtendaji ,.mjamaa mwadilifu tu..waziri wa nje,elimu..mkuu wa mkoa ets...mapato yake ya serikalini posho,ets kayatumia kwa njia mbadala...katika ule udhaifu binafsi wa kimwili..labada kampa huyu ..kamjengea huyu ..hakuwa na mali yake binafsi kwa pesa yake halali kwa kuogopa kuitwa bepari..hawa watu viongozi pesa wanayopata HATA BILA RUSHWA UNATOKA TU..[mfano mkapa wakati anaodakwa amalipwa mkupua wa arrears zake za safari,posho ets from consolidated fund alikuwa hachukuajgi in many hundreds of millions...bado kiinua mgongo unaongelea billioni moja au mbili....mlitaka azipeleke wapi ..ahonge????]..well come back..leo hii chedil mgonja anaishi maisha ya kukulima kijijini ....je huo ndio mfano bora kwa kiongozi ?
mimi naamini hakuna ubaya wa mtu kutumia kipato chochote halali..kama kuna kipato kisichokua halali kisheria na kikadhibitishwa hapo sawa! i will throw a towel..
 
Back
Top Bottom