Kafara,
Nilvyosikia mimi enzi hizooo. kuwa aliyemuua Karume ni shemeji yake au mtu katika familia ambaye alikuwa analipa kisasi..Hakuuawa on the spot kama sikosei, na Kisiasa mauaji yale yalifikiriwa yamepangwa na kundi la Umma party kina Abraham babu..ndio maana walikuwa wanted Zanzibar.
1. Alisema baadhi ya wasomi nchini wameanza kupotosha jamii kuwa Mkapa hawezi kushtakiwa mpaka bunge limwondolee kinga. Dk Slaa alisema Mkapa anaweza kushtakiwa bila ya kuondolewa kinga yake.
2. Alisema anashangaa wasomi nchini kuendelea kuipotosha jamii juu ya suala la kufunguliwa mashitaka Rais mstahafu, na anakusudia kuliweka bayana suala hilo tena katika bunge lijalo.
3. "Katika bunge lililopita katika hotuba ya Waziri Mkuu, niliwahi kulisema hili kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria na lazima tutofautishe mamlaka ya rais na mtu binafsi na hili nitalieleza tena bunge,"alisema Dk Slaa ambaye kitaaluma ni mwanasheria.
4. Alisema matendo ambayo Rais hawezi kufunguliwa kesi mpaka aondolewe kinga ni yale tu ambayo aliyafanyaka kama Rais, katika madaraka yake kisheria kama kuwaachia huru wafungwa, kuidhinisha sheria na masuala mengine yaliyoanishwa kwenye katiba ya nchi. Dk Slaa alisema masuala kama ya Rais Mkapa kufanya biashara akiwa Ikulu hayahitaji kuwa na kinga ili ashitakiwe kwani ameyafanya nje ya mamlaka ya rais aliyopewa.
5. "Watu wengi hawapendi kusoma, ni wavivu. Jambo hili lipo wazi kabisa na nashangaa wasomi wetu ikiwamo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (Takukuru) kudai eti kumshitaki mkapa ni kuvunja katiba,"alisema Dk Slaa.
6. Alisema kinachoendelea hivi sasa hapa nchini ni kukosekana kwa usimamizi mzuri wa sheria na viongozi wenye kauli ya mwisho juu ya masuala yenye maslahi ya Taifa. "Ni aibu Waziri Mkuu anazungumza kuwa hakuna aliye juu ya sheria, Takukuru wanadai hawamchunguzi Mkapa kwani mpaka aondolewe kinga, haya ni mambo ya ajabu,"alisema Dk Slaa. Akizungumzia vita dhidi ya ufisadi, alisema Chadema itaendelea kushinikiza watuhumiwa wote kufikishwa mahakamani hadi wamalizike.
7. "Sisi ndio tumeanzisha huu mjadala hakuna wa kuufunga sio Makamba (Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf) wala Chiligati (Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, John) na tutapiga kelele hadi watuhumiwa wote wakamatwe,"alisema Dk Slaa. Dk Slaa aliwataka Watanzania kwa ujumla wao kusimama kidete na kuliombea Taifa lao kwani wasipoamka na kutetea rasilimali zao nchi yao itamalizwa na mafisadi na siku zijazo hali itakuwa mbaya zaidi.
8. Akizungumzia kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda hivi karibuni kuhusu kuzuia magari ya kifahari, alisema jambo hili ni kuwadanyanga wananchi kwani serikali haina nia ya dhati kuacha kutumia magari hayo. "Anasema wanazuia wakati kuna magari 700 wamenunua kweli hapa kuna umakini na thamani ya gari moja ni zaidi ya Sh100 milioni na tunaendelea kudai nchi ni masikini,"alisema Dk Slaa.
- Ndio maana nilisema kwamba huyu Shujaa wangu Dr. Slaaa apewe nafasi ya kugombea urais huko Chadema, hata asiposhinda ataaamsha sana wanachi walioko usingizini,
Dr. Slaaa heshima mbelee shujaaa, hapa tupo ukurasa mmoja.
Nimeanza kufarijika kusikia Dr. Slaa amelisemea hilo la Rais Mstaafu Mkapa kutohitajika kuondolewa kinga ili ashtakiwe. Ugumu unakuja, jee kuandikisha biashara ni kosa kisheria kwa Mkapa akiwa Ikulu. Hili halikuelezwa popote. Kuna baadhi ya makosa ni moral wrongs lakini sio legal wrongs.
Kama itathibitika hakuvunja sheria yoyote kusajili AnnBen, then kitendo cha kujiuzia Kiwira kimevunja sheria yoyote?. Hii inamaana mchakato wa uuzwaji wa Kiwira was it tranparency?. Ikithibitika nothing illegal, then he is off the hook.
Hata kama he is off the hook, amini usiamini dhamira yake inamsuta (if he has conscious) kwa baadhi ya madudu aliyoyafanya ikiwemo Radar na JetStrem. Wenye akili timamu wote tunajua kulikuwa na mkono wake tukijua haijui pesa, yaani ni Mr. Clean. Sasa baada ya kuthibitika kumbe kuoa Mchagga, kabadili na kabila sasa anaijua pesa vilivyo, them kwenye deal ya Rada na Ndege yake sii bure, vijisenti vyake vipo tena Uswisi, huko hakuna majina ni codes tu na password. No way to prove anything.
Heri ya X-mas na mwaka mpya wadau.
Pamoja na kwamba nakubaliana kabisa na Dr. Slaa kwamba Mh. Mkapa hana kinga... kulingana na kipengele cha katiba kwenye mambo aliyofanya binafsi...
Sikubaliani na Mtanzania yeyote yule ambaye anadhani kumshitaki Mkapa ni sawa na kumshitaki kiongozi mwingine...
Angalieni mbali wakuu... kwa ajili ya usalama na utengamano wa Taifa... naomba Mkapa asipelekwe Mahakamani hata kama ametenda makosa...
Over and Out
Kama huna cha kuandika si bora ukae kimya!
Kafara,
Shukran mkuu kwa taarifa hiyo, nimekusikia.. unajua tena habari za kusikia na usiri nchini ni vigumu kuwa na taarifa kamili..
Rev Kishoka,
Mkuu nadhani siku za nyuma tuliwahi kufikia hapo kuwa ni jukumu la Bunge letu kumsimamisha Mkapa badala ya kuwasubiri Hosea au Kikwete wapitishe uchunguzi, kulingana na Katiba...Lakini mpira umekuwa ukipigwa danadana muda wote hata hizi sahihi 20 za wabunge inakuwa kazi kuzipata.
Kila mtu akiogopa kurusha jiwe la kwanza na hata baadhi wabunge wa Upinzani wamekuwa Upande wa pili hivyo kufanya sheria hii kuwa ngumu kutumika kupitia Bunge kwa sababu nafikiri inatakiwa kitu kama 2/3 ya Wabunge kuelekea ushindi..
Na kibaya zaidi kuna watu wanaendeleza kampeni za kumwekea Kikwete na Hosea jukumu hili wakati ukweli umesimama kuwa hawa wawakilishi wetu ndio wenye matatizo. kwa mara ya kwanza nao wanasimamia maslahiu yao binafsi ndani ya Bunge...
Mwisho wakuu zangu ningeomba mwenye Kanuni za Uongozi na Maadili ya viongozi Kitaifa anirushie..
Sikubaliani na Mtanzania yeyote yule ambaye anadhani kumshitaki Mkapa ni sawa na kumshitaki kiongozi mwingine...Angalieni mbali wakuu... kwa ajili ya usalama na utengamano wa Taifa... naomba Mkapa asipelekwe Mahakamani hata kama ametenda makosa...Over and Out
FMES Kwa kweli Dk Slaa anastahili kupewa nafasi ya kugombea Urais huko CHADEMA amekuwa ni mwiba mkali dhidi ya mafisadi wote ndani ya chama na serikali pamoja na vitisho mbali vya kumfungulia mashtaka hata kuchukua uhai wake, lakini wakati mwingine nahofia kama hakupata nafasi hiyo basi Watanzania tutapoteza mtu muhimu sana ndani ya bunge letu. Kama kampeni zake zikiandaliwa vizuri katika kila kona ya nchi yetu na CCM haitatumia vyombo vya dola kumshinikiza na kumzuia kufanya kampeni zake basi ataibuka mshindi wa Urais.
- Mkuu Kasheshe, sometimes huwa sikuelewi sana, tunasema hivi Mkapa afikishwe Kisutu tena haraka sana, halafu in the process kama kuna rais mwingine wa zamani naye alipora mali za wananchi naye pia aburuzwe, kama hayupo basi familia yake iburuzwe, I mean taifa gani linasambaratishwa na wezi kufikishwa kwenye sheria?
- Hivi hivi vitisho mnavitoa wapi kwamba huyu Mkapa is so big kwamba akienda kwenye sheria kwa wizi wake wa kupora mali za taifa, basi taifa zima litasarambatika what a nonesense? Taifa linatakiwa kuwa imara kwa kusimamia sheria, sasa ukiona taifa linasambaratika kwa kusimamia sheria, maana yake ni moja tu halikuwa taifa anyways form the begining, sitaki kuamini kuwa that is the case na taifa letu!
Kuwapeleka Yona, Mramba, na Mgonja Kisutu, bila Mkapa ni waste of our national time na hasa our taxpayers money, Mkapa ni lazima aburuzwe Kisutu kama ni kusambaratika so be it itakuwa on our bloods!
Bubu, hizi stories za kumshtaki Mkapa ni porojo tu. Bahati mbaya sana hata wasomi hawagundui kuwa ni porojo. Kwa Rais wa nchi ile yetu, hakuna anayefanana na Mkapa so far. Watu wote wanaangalia kwenye ANBEN, KIWIRA na source ya UFISADI ila hawaangalii kuhusu uchuni ya nchi yetu na mabadiliko ya haraka sana Tanzania kipindi chake.
Binafsi, so far sijamuona rais kama Mkapa kwa Tanzania. Mkapa was the best president of TZ and and will remain so in records for many years. Hakuna kuchekacheka na very serious person. Of course bila kuwa kama vile tusingeweza hata kuc-chat hapa kwenye JF. Ali-open up kila kitu, vingine vinawafanya watu wajichanganye kwa vile wao wanataka. Mimi nashauri kuwa alitakiwa apewa another 10 years watu wajue uchumi imara maana ni nini!.
Zaidi ya hiyo, hizi politics za bei ya vitu kwa investors, by the way sijui kama watu wamewahi kujiuliza watu kama Abrahamovich na na mwenzake mwenye kampuni ya Yukos walinunua kwa bei gani zile kampuni kule Russia na kwanini?! How do we compare with Tanzania? Russia ni mfano mmoja, iko kibao, lakini Russia tunafanana kwa na uchumi wa aina moja (state controlled) kabla ya collapse ya USSR.
Mambo ya mafisadi, hata Kikwete akiondoka tutawaona wengi tu. Mbona enzi za mwinyi kulikuwa kuchafu zaidi lakini kwa kuwa press freedom ilikuwa ndogo hatukuweza kujua na kufanya kama sasa. Unakumbuka ambushi ya Mrema airport na yake majina? Umewahi uliza whose names were they?
Mimi nadhani tusiwe na jazba tu kuwa Mkapa aende mahakamani. Tujumuishe mambo kadhaa ambayo ni mazuri. Vinginevyo tunaweza jikuta tunashangilia tu kama soccer fans ambao kila wakati wanategemea team yao ishinde. Ikishindwa unafukuza coach!