Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Mimi pia sina mengi ya kuandika mkuu!Lakini niweke angalizo tu.Wakuu nyinyi endeleeni na mchakato wa kumburuza mkapa mahakamani na endeleeni kumshawishi Kikwete ili abadili msimamo wake.Lakini yote hayo yakikamilika basi mjiandae na kusambaratika kwa taifa la tanzania.

Mtarajiwa,

Taifa litasambaratishwa na Kikwete kutofanyia kazi tuhuma dhidi ya Mkapa na siyo Kikwete kumburuza Mkapa Mahakamani!!!

I'm still around
 
Ukifuatwa utaratibu na sheria, basi kila kitu kitakuwa shwari tu. Na ni hii tabia ya kuogopa "kusambaratika ndio imeleta "impunity kwa baadhi ya wanaokuwa "Mafisadi leo" Hivyo ni vyema kuangalia kabla mambo hayajachacha.
 
Hatuwezi kuacha kupambana na wala rushwa wakubwa kama wakina mkapa kisa eti taifa litasambaratika. huo ni ujinga. ni bora tuwapeleke mbele ya sheria na wakithibitika wafungwe ili watu wajue kuwa sheria zipo na zinafanya kazi kwa mkubwa na mdogo. ili tuweze kufika pale tunapohitaji inatubidi tupite njia ngumu moja wapo ndio hizo za kupambana na maharamia wa nchi yetu.
 

Mkuu Kichuguu,

baadhi yetu hii sentensi hatukuelewa... tafadhari tunaomba ufafanuzi

Baba Enock,

Maneno ya watoto wa mjini,unadhani ni kwanini Ditto alimpiga Risasi yule kijana ?maneno ya dharau na matusi na kwa utu uzima
 
Je tunahitaji kumshitaki JK na Pinda wake baada ya dakika 90 kwa huu uhuni?! Bado hatujui hatma ya Richmond, Buzwagi, ATCl etc zote hizi zikiwa ni JK creation. Tutahitaji kuwashitakia hawa after their tenure?

ndo maana yake
 


Sheria haimzuii kufanya biashara kama mwananchi wa kawaida, lakini inamzuia kupora mali za wananchi akiwa rais, hivi wananchi wengine mnakuwa mmerogwa nini?

hakuna cha kurogwa wala nini. zaid zaid kuna sababu zingine

inabid jamaa akajitetee kulekule. ikiwezekana aturudishie alichochukua isivyo halali

muda ndio huu. it is our best chance. tukimwachia na wengine baadae watakuwa wanaingia, wanajikombea, wanatimka.
wengine watakuwa wanaenda benk, wanakopa wanaendesha kampen kwa hizo hela na wakishinda wanakomba, wanarudisha hela benk au hawarudishi kabisa.
wengine watakuwa wanashirikiana na wafanyabiashara za kulevya na zingine za kitapeli. wakiingia ikulu watakuwa wanawalinda wazwaz. kisa? kurudisha fadhila. na wabiashara za kitapeli taifa litakuwa linaingia nao mikataba isiyo na manufaa kwa taifa.
watakao kuwa wanagombea upresidaa wataongezeka sana maana ndo itakuwa sehemu ya kwenda kukwiba bila kushtakiwa (mawaziri tumeshaona wanashtakiwa).
wagombea upresidaa wenye nia ya kweli ya kutumikia watu watakata tamaa maana hawataona haja hasa ya kutumbukiza mapesa mengi kwenye kampeni. na amini usiamin watu wenye strong financial support kwenye kugombea nafas ndo wana nafas kubwa ya kushinda.
 
Suala "ni nani mwenye guts za kumshitaki Rais baada ya Katiba iliyopo kumpa kinga"? Ukweli ni kwamba, kesi hiyo (labda iwe ya madai) haitapelekwa mahakamani. Maana kuipeleka kwa Katiba iliyopo ni kujihakikishia kushindwa kesi na madai makubwa ya udhalilishaji kufunguliwa baadae. Kesi hiyo haitakuwa na maslahi kwa TAIFA hata kidogo. Itakuwa ni usumbufu tu kwa mtuhumiwa.
 
MKUU WA MEDANI TUSAIDIE KTK HAYA UNAYOYAHUBIRI HAPA KTK UWANJA WA SHERIA ZAIDI, MAANA NINAONA MSUKUMO WA MHEMUKO WA ROHO TUPU HAPA, TUAMBIENI HAPA JAMVINI, KUWA SHERIA NA... NA ADHABU NI FULANI DHIDI YA MUHUSIKA......, KASHESHE NA GEMBE WAMETHUBUTU KUWA WAKWELI NA KUMWAGA FACT HADHARANI, NIMEJITAHIDI SANA KUWATAKA NINYI NDUGU ZANGU HUMU KUIANGALIA SHERIA ZAIDI NA TUONE ANABANWA NA SHERIA IPI? HAKUNA MAJIBU WALA VIAMBATANISHO HUMU, IKULU NI OFISI NA MAKAZI YA RAIS, KAMA MTUMISHI ANARUHUSIWA KUKOPA BENKI KWA SABABU ZA BIASHARA WHY NOT RAIS AMBAYE NAYE NI MTUMISHI?!!! KWA HIYO MLITAKA YEYE AWATAJIRISHE NINYI TU NA YEYE ATEGEMEE PENSHENI YA URAIS, JE YEYE HANA FAMILIA NA NDUGU?

- Mkuu FDR kwanza nashangaa sana kwamba umekua kimya sana na huyu mtu wako Mkapa na Lowassa, hivi mkuu unafahamu mahali popote Tanzania ambapo zabuni ya kuuzwa kwa Kiwira ilipowahi kutolewa kabla ya kuporwa na Mkapa na Yona kama sheria yetu inavyosema tuanze na hilo kwanza kabla ya kufika kwenye majibu ya maswali yako mengine.

NAO WAKO ENTITTLED KTK PENSHENI YA RAIS MPAKA KUFA KWAKE? HAYA NI YA KUJIULIZA KIUBINADAMU TU NAYO HAYAHITAJI pHD YA FALSAFA. MLICHOTAKA JAMII IJUE NA KUFANYA VIA IPP MEDIA SASA KINAENDA MWISHO WAKUU, SILAA ANAJUA MCHEZO ANAOUCHEZA DHIDI YA CCM NA SI UCHUNGU WAKE KWA TZ, NDANI YETU WANA CCM TUNAJUA UDHAIFU WETU, VIONGOZI WETU NAO PIA WANAJUA MAPUNGUFU YAO ILA JF NI MAHALA PA KUPUMZISHA HISIA NA KUONGEA KWELI, NASHAURI SANA WAKUU TUNAOWAHESHIMU MSIJIINGIZE KTK HEKAYA ZA ABUNUWASI NA HADITHI ZA ALFU ULELAULELA.

- Kama Dr. Slaa kwa kulilia sheria ichukue mkondo wake kuna kamchezo anakacheza basi ni kamchezo kazuri sana kwa taifa na tunakahitaji sana kujifunza hako kamchezo. Familia ya Mkapa ni tatizo lake sio letu taifa, kwani Mwalimu hana au hakuwa na familia? Mwalimu hakupora mali zetu wananchi je kuna familia yeyote wa Mwalimu sasa hivi anayelala njaaa?

- Mapungufu ya viongozi wetu kama bin-adam hayana uhusiano wowote na sheria za jamhuri, infact ziliwekwa kwa sababu ya ku-deal na mapungufu ya wananchi in the first place, mshahara wa dhambi ni mauti na sio anything else, Mkapa amefanya madhambi na sasa tumeyagundua ni wakati wa yeye kujibu kuhusu uhalali wa aliyoyafanya, sio kujifanya kukimbilia jimboni mwake na kubweka bweka kwa wasioelewa kitu, aende Kisutu akatoe maelezo kama anayo,

- Hadithi za alfe lela u-lela ni yeye Mkapa kujidanganya kwamba hatafanywa kitu kwa sababu aliwapa urais Mtandao, that was a biggest mistake of his life, wewe rais wa jamhuri unaweza kuwaamini kina NChimbi na Rostam kwamba watakufichia siri zako za ufisadi? Unajua ina-raise hata some serious questions on the thinking capacity level ya Mkapa na kama kweli alikua na uwezo wa kufikiri kwa a presidential level, no wonder yuko kwenye hot water,

Mkuu wangu FDR, kuwafikisha kwenye sheria Mramba, Yona, na Mgonja bila Mkapa ni waste of our national time na pia taxpayer's money, na ni kuwaonea bure hao wengine maana walikuwa wanachukua orders kutoka kwa Mkapa.


SUBIRINI HUKO BUNGENI JANUARI-FEBRUARI 2009, WENYE MASIKIO NA WASIKIE NA WENYE KUONA WAONE. FEBRUARI 2008 ILIVUNJA BARAZA LA MAWAZIRI NA KUMPOTEZA THE PREMIER EDWARD LOWASA, JE FEBRUARI 2009 INA NINI KWA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA? TUPO TUNASUBIRI KUONA JEURI YA SAMWEL SITTA, KIMARO, ZAMBI, SLAA NA WENGINEO....

- Wakati tunaendelea kusubiri ni wajibu wetu wananchi kuendelea ku-press hard mpaka kieleweke, wananchi wa Tanzania huwa hatuna haraka na sio wajinga tena kama zamani, kama huamini muulize Msabaha, Karamagi na Lowassa.

MKUU WA MEDANI NAKUSAHIHISHA KUWA TBL ILIUZWA AWAMU YA PILI NA SI YA TATU

- Ahsante kwa marekebisho mkuu, unajua sometimes tunakua emotional mpaka tunasahau ukweli, maana inatia uchungu sana kuona mwizi akitetewa kwa maneno ya kusambaratisha taifa, unajua hayo ni matusi makubwa sana kwetu sisi wananchi, yaani huyu Mkapa ni bora sana kwamba akiguswa tu na sheria alizoapa kuzisimamia akiwa rais, lakini akazivunja kwa makusudi kwa sababu ya tamaa za fisi basi taifa litaangamia never before kusikia wa-Tanzania tukitukanwa namna hii, ninataka kuamini kwamba you guys are damn right, kwamba hataguswa ili kulinusuru taifa!
 
-, maana inatia uchungu sana kuona mwizi akitetewa kwa maneno ya kusambaratisha taifa, unajua hayo ni matusi makubwa sana kwetu sisi wananchi, yaani huyu Mkapa ni bora sana kwamba akiguswa tu na sheria alizoapa kuzisimamia akiwa rais, lakini akazivunja kwa makusudi kwa sababu ya tamaa za fisi basi taifa litaangamia never before kusikia wa-Tanzania tukitukanwa namna hii, ninataka kuamini kwamba you guys are damn right, kwamba hataguswa ili kulinusuru taifa!

Naona kuna watu wameshageuzwa kuwa miungu watu (Kwamba hawaguswi) nani alijua kwamba hao Mawaziri wa zamani wataguswa. Mkapa sio Raisi wa nchi sasa hivi ni raia, na hakuna cha Taifa kuangamia wala nini.
 
-
- Hadithi za alfe lela u-lela ni yeye Mkapa kujidanganya kwamba hatafanywa kitu kwa sababu aliwapa urais Mtandao, that was a biggest mistake of his life, wewe rais wa jamhuri unaweza kuwaamini kina NChimbi na Rostam kwamba watakufichia siri zako za ufisadi? Unajua ina-raise hata some serious questions on the thinking capacity level ya Mkapa na kama kweli alikua na uwezo wa kufikiri kwa a presidential level, no wonder yuko kwenye hot water,



Yaani hata kama huyu jamaa alikumaliza kivyakovyako kwa namna yoyote ile huwezi kuandika kitu kama hiki hapa juu watu wasome na wakuelewe! Jf kuna watu wengi sana walimpigia kura, tena mara mbili. Kwa kusema namna hivi unataka ku-disqualify akili za hao waliompigia kura......! duh! Hata siwezi amini kama hapa kuna mtu za aina hii. Hamna. Hamna kitu kizuri hata kimoja unaweza sema kuhusu Mkapa?!!!!!!!!!!

Sasa, hivi wewe ndugu, hizi habari kama hivi hapa chini ukikaa na kuzisoma kwa makini sana bila vurugu vurugu kama unazozifanya hapa kuhusu Mkapa,, unapata picha gani hasa.......? Be fair kabisa kwenye analysis, usiingize unazi wowote.

Dar reduces foreign debts by 25 per cent
DAILY NEWS Reporter
Daily News; Tuesday,December 30, 2008 @21:15

The government succeeded to curtail the country’s total foreign debts by almost 25 per cent over the past three years. A report issued yesterday by the Ministry of Finance and Economic Affairs, said the country’s total debts was reduced from $49,383.9 million down to $7,041.3 million between December 2005 and December last year.

The report attributed the success to the government’s relentless and deliberate endeavour to manage its indebtedness and to the recent debt cancellations by the country’s development partners – for which Tanzania qualified for being among countries commonly known as Highly Indebted Poor Countries (HIPCs).

Beneficiaries of the debt relief initiative included Africa, Latin America and Asian countries. In December, 2006 highly indebted poor countries whose debts the Group of Eight (G8) countries agreed to cancel by 100 per cent. According to the World Bank, Tanzania alone received 3 billion US Dollars in debt relief.

Following such debt cancellation, the government has now focused the money saved from debt cancellation on improving health, water, road infrastructure and also increasing education spending and eliminating school fees in primary education. The report also revealed that the country has for the past three years witnessed a substantial increase in development partners’ financial support from 1,712.4bn/- in 2005/2006 financial year to 2,429.5bn/- for this financial year.

The funds, says the government, has had been used for intended purposes, particularly to supporting development projects which are geared to improve welfare of the ordinary people. The report also indicated a conspicuous success in revenue collections by the Tanzania Revenue Authority (TRA), which contributes 90 per cent of internal revenue. The collections have jumped from 1,757.4 bn/-. in 2005 to 3,802.2 bn/- this year.

The increase in revenue collections has exceeded intended target by 116.4 per cent. Meanwhile, the government is in the final preparation to employ 617 new internal auditors and accountants who will be deployed to various parts of the country. The move is intended to grapple with the shortage of accountants and auditors in various government ministries and departments. The report also shows other 937 accountants and auditors have already been employed for the past three years.
 
Acheni ulofa, huyo Slaa kama ni jeuri asingesubiri kwenda kulia huko Bungeni. Kwa nini asiende moja kwa moja mahakamani. Adui wa Magabachori huwa asubiri bunge kufungua madai yake na kama huyo Slaa ana madai dhidi ya Rais Mstaafu Mkapa nini kinamzuia kwenda Mahakamani?....Huu ni Ujuha tu!


Utakufa nacho, kijiba cha roho!
 
Mkuu Kichuguu,

baadhi yetu hii sentensi hatukuelewa... tafadhari tunaomba ufafanuzi


  • मैं क्यों कुछ लोगों को लगता है कि बॉक्स के बाहर नहीं करना चाहता हूँ पता नहीं है.
  • Tôi không biết lý do tại sao một số người không muốn nghĩ rằng ở bên ngoài hộp.
  • 왜 어떤 사람들은 상자 밖에서 생각하고 싶지 않아 모르겠다.
  • Sijui kwa nini baadhi yetu hatutaki kufikiria nje ya utamaduni wa woga
 
Kumfungulia mashitaka Rais mstaafu kwa makosa aliyofanya akiwa Rais, bila kujali kama aliyafanya kwa manufaa binafsi ni kuvunja Katiba (Sheria Mama). Ushauri wangu kwa Mpiganaji Dr. Slaa ni kuhakikisha Katiba inaruhusu kushitakiwa kwa Rais baada ya kutoka madarkani. Vinginevyo, ni sawa na kutaka kujizolea utajiri wa kisiasa tu kutoka kwa wananchi kwa kuchochea yasiyoweza kutekelezwa.

Imani yangu ni kuwa, wale wanaotaka Rais mstaafu ashitakiwe bila kubadili Katiba, wanajua kuwa wanajenga misingi ya kuitoa serikali iliyopo madarakani. Kwani Bunge linaweza kum-impeach Rais kwa kuivunja Katiba. Watakaofaidika na hilo ni wapinzani, ambao kwa makusudi kabisa wanataka Katiba ivunjwe kwa kushitaki Rais mstaafu bila kuibadilisha.

Taifa haliwezi kufaidika kwa namna yoyote kama Mkapa atashitakiwa. Na uhakika uliopo ni kwamba, akishitakiwa na akashinda kesi, Taifa litalipa gharama kubwa sana. Kwa maana naamini atadai fidia ya kuvunjiwa heshima. Mawakili na wanasheria wengi wanasubiri kosa hilo la kiufundi lifanyike, ili wajizolee sifa kubwa na pesa nyingi.
 
Utawala bora ni lazima siku zote udumishwe na yeyote yule anayejipatia utajiri kwa kutumia wadhifa wake kwa nija za haramu ni lazima aadhibiwe bila kujali kwamna tunatoka naye mkoa mmoja, chama kimoja au dini moja. Hili litasaidia sana katika kuleta utawala bora nchini na pia wanasiasa waheshimu nyadhifa wanazopewa na kuwa na maadili meme ya uongozi mara Watanzania tunapowapa nafasi ya kutuongoza.
 
Date::12/31/2008
Wabunge, kusini wamtetea Mkapa

Na Abdallah Bakara, Mtwara
Mwananchi

"DAMU ni nzito kuliko maji"

Ndivyo unavyoweza kufupisha kitendo cha baadhi ya wabunge na wananchi wa mkoani Mtwara kujitokeza hadharani na kumtetea rais wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa.

Wakati shinikizao la kutaka Mkapa aondolewe kinga na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za makosa anayodaiwa kufanya akiwa Ikulu, wabunge na wananchi wa mkoani Mtwara na wananchi kuibuka na kumtetea.

Tayari mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa ameahidi kuwasilisha hoja ya kutaka Mkapa, aliyeongoza nchi kwa vipindi viwili (1995-2005), apandishwe kizimbani kujibu tuhuma za kufanya makosa wakati akiwa Ikulu, huku kiongozi wa upinzani Bungeni, Hamad Rashid, akiahidi kuwasilisha hoja ya kutaka kiongozi huyo aondolewe kinga ili aweze kupandishwe kizimbani.

Miongoni mwa tuhuma za Mkapa, ambaye anasifika kwa kuinua uchumi baada ya kuukuta kwenye hali mbaya, ni kujiuzia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya kwa bei nafuu akitumia kampuni ya Tan Power Resources anayoimulika pamoja na waziri wa zamani wa nishati na madini, Daniel Yona wakati akiwa rais.

Lakini wabunge hao na wananchi wa Mtwara wanaona kuwa tuhuma hizo dhidi ya Mkapa, ambaye alikuwa mbunge wa Nanyumbu wilayani Masasi kabla ya kuchaguliwa kuwa rais, hazitoshi kumuondolea mazuri yote aliyofanya wakati akiwa rais, kwa kuamua kumpandisha kizimbani kiongozi huyo aliyedumu miaka yote kumi ya urais wake akitumia sera ya "Uwazi na Ukweli".

"Huo ni upuuzi na nitaupinga kokote," alisema mbunge wa jimbo la Masasi, Raynald Mrope. "Siasa za sasa ni za kuchafuana... watu wanafikiri wakimchafua wenzao ndio wao watapata umaarufu.

"Jamani Mkapa amelitumikia taifa hili na kuliacha katika hali nzuri. Hata huyo Dk. Slaa tukisema tuchunguze upadre wake tutakuta makosa; binadamu hakosi kasoro ila muhimu tusiangalie alipoteleza tu, pale alipoweza mbona hatupasemi?"

Mbunge wa jimbo la Mtwara, Mohamed Sinani alizungumzia suala hilo kidiplomasia zaidi, lakini akashindwa kuficha msimamo wake kwa Rais Mkapa, ambaye aliteuliwa na CCM kuwania urais baada ya kumshinda Rais Jakaya Kikwete katika marudio ya kura za maoni.

"Sisi Wabunge tupo kwa ajili ya kuifanyia marekebisho katiba, kutunga sera na sheria," alisema Sinani na akaongeza kusema: "(Suala la hoja binafsi) Likiletwa tutalijadili, lakini pamoja na majukumu hayo sidhani kama ni busara kuifanyia marekebisho katiba kila kukicha, hasa pale unapomlenga mtu fulani."

Mbunge wa Tandahimba, Juma Njwayo aliamua kutoweka bayana msimamo wake na akazungumzia suala hilo kiufundi zaidi, akisema ni mapema mno kulizungumzia na kwamba anasubiri kwanza liwasilishwe kama hoja binafsi Bungeni.

"Ndugu yangu hili suala ni la Kikatiba, tusubiri walete hoja na vielelezo vya ushahidi, tutalijadili kuona uzito wake.Wakati huo ukinipigia (simu) nitakuwa katika nafasi nzuri ya kutoa maoni yangu, kwa sasa ni mapema mono," alisema Njwayo aliyehojiwa kwa njia ya simu.

Baadhi ya wananchi wa mikoa hiyo walihojiwa na Mwananchi walionekana kupinga hoja hiyo, wakitaka Mkapa aangaliwe pia kwa mazuri aliyofanya.

"Mkapa aliichukua nchi ikiwa katika hali ngumu… mfumuko wa bei ulifikia zaidi ya asilimia 10, lakini ameuacha ukiwa katika asilimia 4.5. Si hilo tu amefanya mengi ambayo anastahili kuheshimiwa na kuachwa apumzike. Watanzania wenzangu tusiwe na shukrani za Punda," alisema Ibrahim Mchopa mkazi wa mjini Mtwara.

Alisema kutoka na utendaji aliouita kuwa mahiri wa Mkapa wakati wa uongozi wake, umewafanya Watanzania wengi kumuunga mkono hadi sasa na kwamba kitendo cha kumshitaki ni udhalilishaji ambao unaweza kuleta mgawanyiko katika umoja wa kitaifa uliopo.

"Leo hii tukisema wangapi wanamuunga mkono Mkapa tutawapata wengi kuliko wachache wanavyofikiri. Tunapomfikisha mahakamani kwa tuhuma ambazo msingi wake ni kutafuta umaarufu wa kisiasa, sidhani kama tunalitakia mema taifa hili," alisisitiza Mchopa.

Mkazi mwingine Rashidi Athuman alisema kuondolewa kwa kinga kwa marais waliomaliza muda wao kutasababisha machafuko ya kisiasa na hatimaye kuvunjika kwa amani na utulivu.

"Tunamshangilia Dk. Slaa, lakini kesho tutakuja kujutia. Ni lazima watu wawe na mtazamo wa mbali. Nilifurahi kumsikia Rais Kikwete akisema hatamshitaki Mkapa, bila shaka aliona mbali. Kimsingi siungi mkono si tu kwa sababu Mkapa ni wa kusini bali alivyoliongoza taifa," alisema Athumani akimzungumzia Mkapa ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Lupaso wilayani Masasi.

Mkazi mwingine aliyetoa maoni alisema kwa kuwa sheria ni msumeno na kwamba ni matarajio yake kuwa kuondolewa kwa kinga hiyo haitakuwa kwa Mkapa, bali hata rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na kwamba vinginevyo madai hayo yatakuwa yamelenga kumchafua Mkapa kisiasa.

"Nilivyoelewa mimi ni kwamba kinga ikiondolewa ni kwa marais wote waliomaliza muda wao kwa kuwa katiba ni moja. Hivyo kama Mzee Mwinyi naye alitenda kosa wakati wa utawala wake, basi atachukuliwa hatua. Hali kadhalika kwa rais wetu atakapomaliza muda wake, kama alitenda kosa naye atashitakiwa," alisema Mohammed Omari.
 
[
QUOTE=mwanjelwa;349831]kujibu kauli yako: Hivi wewe unadhania finance and support kubwa ambayo Lowassa and company waliyompatia Jk kwenda ikulu ilikuwa bure bure! Tatizo Lowassa ni kumba kumba na mrafi wa ghafla ghafla. Ile bond tungeishangaa after 10 years.
Mkuu Mwanjelwa hapo hakuna ubishi...Mimi binafsi siamini kama kuna siasa safi katika nchi yetu ya Tanzania, Tukianza kumchambua kila mwanasiasa hakuna msafi hata mmoja....lakini mahali tulipofikia ni itabidi tu tuanzie na wale wanaolitia hasara kubwa Taifa kabla ya kushuka chini...hakuna asiyejua kuwa Lowassa na timu yake waalikuwa walafi wakubwa wa mali za wananchi, sasa kama kamanda JK alikuwemo time will tell, lakini hivi sasa macho kwa muheshimiwa Ben.
Juzi juzi Jk and company wamekodisha TRC kwa wahindi kwa mkataba fake. Reason kubwa- ni kuwa wataalamu wa reli waliwadanyanga investors kuhusu halisi halisi ikiwemo uhai wa mabehewa/engines na kwahiyo wahindi hawakuandaa fungu la kutosha kwa kuendeleza hayo (very stupid)!. Matokeo yake Pinda kuepusha aibu anawabeba wahindi wazi wazi kwa kisingizio cha kuwasaidia wafanyakazi ambao ni wajibu wa RITES huku waalimu na wanafunzi vyuo vikuu wanaambia hakuna hela!. Je hizi hela za kuwapa wahindi wanazichukua wapi na kwa mpango upi? Je tunahitaji kumshitaki JK na Pinda wake baada ya dakika 90 kwa huu uhuni?! Bado hatujui hatma ya Richmond, Buzwagi, ATCl etc zote hizi zikiwa ni JK creation. Tutahitaji kuwashitakia hawa after their tenure?
Naona hapa umeorodhesha mambo meengi ambayo mengine yanapingana na hoja yako ya msingi...mengine yalikuwa ni uoza wa mheshimiwa Ben Mkapa mkuu. Again hakuna serikali safi hadi hivi sasa, lakini kwa kuanzia tu tuanze kusafisha yale mambo ambayo obviously yalikuwa ni uoza wa waziwazi...kama JK kahusika, time will tell...nani alijua kama mkuu Ben angekuwa katika wingu la hatia hizi kule 1995?
Kwa hiyo, Kuhusu huyu "Serious man, Ben", wabongo ni Jazba na wivu tu kama kawaida yetu. Sheria zote za TZ zinasema kila mtu hana kosa mpaka apatikane nalo. Sasa hili la kusema Ben kaiba nani katoa hukumu na wapi? Halafu ni nani kasema Mramba na Yona wameisababishia serikali hasara? Hakuna hata mmoja mpaka itakapoamuliwa na mahakama kuwa ni hivyo. Inaweza kula kwa serikali tukala hasara zaidi. Until then, let is shut up and work hard for our prosperity!
Nina imani mkuu mzee Ben amefanya ya maana sana kule Mwanjelwa, naona unampigia kifua cha hali ya juu. Lets be serious a bit....mzee kaharibu we all know that, then lets the law take its course.....wengine watafuatia tu....
 
[
Mkuu Mwanjelwa hapo hakuna ubishi...Mimi binafsi siamini kama kuna siasa safi katika nchi yetu ya Tanzania, Tukianza kumchambua kila mwanasiasa hakuna msafi hata mmoja....lakini mahali tulipofikia ni itabidi tu tuanzie na wale wanaolitia hasara kubwa Taifa kabla ya kushuka chini...hakuna asiyejua kuwa Lowassa na timu yake waalikuwa walafi wakubwa wa mali za wananchi, sasa kama kamanda JK alikuwemo time will tell, lakini hivi sasa macho kwa muheshimiwa Ben.

Naona hapa umeorodhesha mambo meengi ambayo mengine yanapingana na hoja yako ya msingi...mengine yalikuwa ni uoza wa mheshimiwa Ben Mkapa mkuu. Again hakuna serikali safi hadi hivi sasa, lakini kwa kuanzia tu tuanze kusafisha yale mambo ambayo obviously yalikuwa ni uoza wa waziwazi...kama JK kahusika, time will tell...nani alijua kama mkuu Ben angekuwa katika wingu la hatia hizi kule 1995?

Nina imani mkuu mzee Ben amefanya ya maana sana kule Mwanjelwa, naona unampigia kifua cha hali ya juu. Lets be serious a bit....mzee kaharibu we all know that, then lets the law take its course.....wengine watafuatia tu....

Sheria za nchi yetu hazina matabaka mawili ya walio viongozi na wasio viongozi. Mbele ya sheria wote tuko sawa kabisa bila kujali nyadhifa mbali mbali tulizowahi kushika ndani ya chama na serikali.

Pia sheria zetu hazina matabaka ya kumnusuru yule tunayetoka naye eneo moja, mkoa mmoja, kabila moja, dini moja au chama kimoja.

Tunapotenda losa lolote lile basi sheria za nchi ziachwe zifuate mkondo wake ili muhusika achunguzwe na kama anaonekana ana tuhuma za kujibu basi afunguliwe mashtaka.

Kuna ushahidi wa kutosha unaonyesha maamuzi mengi ya Mkapa yamelitia Taifa letu hasara kubwa ambazo zinaweza kuwa zilimnufaisha Mkapa kwa namna moja au nyingine ikiwemo ununuzi wa Rada, ndege ya Rais, magari na helicopters za jeshi, uuzwaji wa nyumba za serikali, kujimilikisha Kiwira na kuwaleta Net Group. Hivyo kuna kila sababu ya Mkapa kuchunguzwa ili kujua kashfa zote hizi kwa undani zaidi na pia kujua biashara aliyokuwa anaifanya Ikulu ilikuwa ni biashara gani na alikuwa anaifanya na nani. Kwa tamaa yake aliyokuwa nayo si ajabu alikuwa anaifanya na serikali ya Tanzania kwa kuiuzia vitu kwa bei ya kuruka.

Haya yote kuna haja ya Watanzania kuyajua. Hakuna yeyote ambaye ana chuki binafsi na Mkapa, bali ni kutaka kuhakikisha hakuna aliye juu ya sheria za Tanzania na utawala bora unaopigiwa debe kila kukicha unatimizwa bila dosari zozote.
 
Kweli bwana... kifungu gani cha sheria kilimzuia kufanya hivyo?
Mh. Ali Hassan Mwinyi alivyokuwa ikulu aliendelea na kuwa na mashamba yake...
Mh. Julius K. Nyerere Marehemu, alikuwa na mashamba yake hata alipokuwa ikulu... swali hizo hazikuwa kazi binafsi kwa kizungu business...
Mpaka sasa muda mwingi tunaongelea ana kinga, hana kinga... lakini anatakiwa ashitakiwe kwa lipi?
Pili; Kwani kesi lazima aipeleke Felesi, Huyo Dr. Slaa si anaweza peleka kesi mahakamani?
Kwa nini tunapenda kuongea sana?
Kwani mkuu Ben ali-own Kiwira kabla ya kufika Magogoni? Kama jibu ni ndio basi itakuwa ni biashara kama ulivyonukuu za mashamba ya marais waliomtangulia aliyoianza kabla ya kuwa Rais wa Jamhuri. Kama jibu ni hapana, na tujiulize ni muda gani muheshimiwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania alioupata wa kufanya biashara wakati alikuwa na full time job ya kuwa kiongozi wa nchi? Conflict of Interests ndio tutakalolipigia kelele hapo....as long as rada, Kiwira na nyinginezo zilikuwa legal businesses.
 
Wataka Mkapa anyang’anywe Kiwira

na Hellen Ngoromera
Tanzania Daima~Sauti ya watu

CHAMA cha Wafanyakazi wa Shughuli za Meli na Bandari (Dowuta) kimeishauri serikali kumnyang’anya Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, mgodi wa Kiwira anaodaiwa kuumiliki tangu akiwa madarakani.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Katibu Mkuu wa Dowuta, Abdallah Kibunda, alisema badala ya serikali kumnyang’anya kizuizi cha kumshtaki kama rais suala la kumshtaki liwe mikononi mwake.

“Kama kweli Rais Mkapa alichukua mgodi wa Kiwira kinyume cha sheria, anyang’anywe na ikiwa ataona ameonewa akashtaki yeye mahakamani”, alisema Kibunda.

Sambamba na hilo, katibu mkuu huyo alishauri pia hata waliouziwa nyumba za serikali wakiwemo viongozi mbalimbali kunyang’anywa kwa sababu walifanya hayo kinyume cha maadili ya uongozi.

“Pamoja na Rais Mkapa, waliouziwa nyumba za serikali ambao wengi wao ni viongozi, wanyang’anywe, wanalidanganya na kuliaibisha taifa, haiingii akilini kiongozi aliyekuwa madarakani kubariki suala kama hilo la wao kujiuzia nyumba.

“Katiba ya sasa inasema rais alindwe kutokana na yaliyotokea akiwa madarakani, Bunge litunge kanuni za uongozi bora ili inapotokea kuwa kiongozi ametajirika kwa kutumia vibaya madaraka yake itamkwe wazi kuwa atanyang’anywa mali na kushtakiwa kuliko ilivyo sasa.

Kuwepo kwa kanuni hizo hakutaleta utata kuhusu kiongozi anayekosa kushtakiwa au la, kama mtu ana tuhuma, tuhuma zake zichambuliwe hata kama akiwa madarakani na hatua kali zichukuliwe dhidi yake”, alibainisha.

Alibainisha kuwa kuwepo kwa kanuni hizo kutawezesha rais aliye madarakani kuongoza kwa maadili kutokana na kufahamu kuwa ikiwa atakwenda kinyume atabanwa na vipengele gani.
 
Back
Top Bottom