Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Babu,
Si mama peke yake. Mzee pale Geneva alikusanyiwa dola millioni karibu sita na Sharon Stone kwa ajili ya viandarua. Sikusikia amezikabidhi kwa taasisi gani. Hawa viongozi walioondoa hiyo miiko walijua wanachokifanya. Nasikia Azimio la Zanzibar lilipitishwa baada ya Mwinyi kumteua kiongozi fulani akaambiwa huyo hawezi kuchukua uongozi serikalini kwa sababu tayari ana madole yake katika kampuni za binafsi. Mzee Ruksa akasema hiyo sheria iondolewe. Ndiyo Tanzania yetu hiyo. Amri ya mtu mmoja inafuta kanuni zinazohusu wengi.
 
Najua nikisema nitaonekana kama Mkapa apologist lakini kama huyu mheshimiwa amekopa hizi "senti" milioni 750 tu ili atekeleze kile anachohubiri yaani ujasiri wa mali sidhani kama ni dhambi kubwa ambayo inahitaji kuumiza vichwa vyetu. Ni kweli atakuwa ametumia madaraka yake kinyume cha maadili lakini ni kweli vilevile kuwa tangia tufakamie huu unyang'au tunaouita soko huria ama ubepari, kitendo hiko sio dhambi tena kisiasa na maadili ya uongozi yanaishia pale katika kulinda siri za tabaka tawala tu na si vinginevyo.

Tanzaninjema
 
Hapa JF iliwahi kuwepo thread ya mali za viongozi, sijui iliishaje. Mi naona bora ifufuliwa tuanze kuanika hizi mali zao; tunaweza kuwa tunazungumzia BM hapa kumbe waliopo sasa, EL na wenzake wako busy kujikusanyia; miaka mitao ijayo tutakuwa bado tunashangaa hapa na mali zao, by then watakuwa wamemaliza walalahoi kwa ulafi wao.

EL si ndio alikuwa amejaza viwanja Mbezi na kawe yote? na bila kusahau lile Jumba lake la Masaki alilokuwa amepangisha ubalozi wa SA na walikuwa wanamlipa kwa dollar..sasa by the time ana maliza term yake sijui atakuwa amekula nini...na kuacha nini?
 
Adam Lusekelo
Daily News; Wednesday,May 23, 2007


'ETI' the government has failed to account for 273 billion shillings it spent for the financial year 2005-2006. They blew the money just like that.

Of course, no one got arrested or something. That’s our culture. Mega thieves are praised, mediocrity is rewarded. Honesty and steadfastness is heavily frowned upon.

According to the report by the Controller and Auditor General (CAG), the dosh was pinched by smart alecs -- blown away by ministries, departments and government agencies.

Some guys must be getting filthily rich. Of course a lot of mistresses and concubines and 'hawaras' must also be in the gravy train. You can see from the conspicuous consumption going on.

I mean, 273 billion bob is a lot of moola. Okay, even if you change that into real money – dollars-- it still is a lot of money to steal from the people of the United Republic of Tanzania. That is a cool bloody 273 million dollars!

Now the entire budget of Tanzania is barely a billion dollars. So a quarter of that has been blown by the people who know how to steal. They can be quite tasteless in their personal tastes. But, by God, they can steal. Do you know what you can do with such money? Plenty. You can abolish our school kiddies from sitting on floors while in class in our entire country.

According to Hakielimu Executive Director, Rakesh Rajani, with that dosh you can easily pay 180,000 primary school teachers. Or you can buy 100 million books for our kids to read. But that is not top priority. Stealing is.

Rajani adds more. He says with such moola you can buy 2 million laptop computers for our kiddies. Must be a madman this guy! Laptops? Who does he think he is – Colonel Muammar Gadaffi of Libya? The colonel has ordered a laptop for every Libyan school kid.

For us, laptops are for the sons and daughters of the oligarchs. The rest of the people can deal with no books, no teachers, no hospitals. Heavens ! hat do we need laptops for our kids for? Rajani said there should be a Treasury Memorandum ‘ as is done in Kenya and Uganda. That will explain the systematic actions the government will take to prevent problems noted in the CAG report and the memorandum should be made public.

I mean, what are we running here? A minister tells the Bunge it cannot question how taxpayers' money is being spent?!

Some greedy government people commission the buying of silly stuff without following competitive bidding procedures. They buy things without the blessing of tender boards, unsupported issue of stores. They overpay (hewa) contractors and on purchases for the ‘Shangingis’.

But they could be right, you know. Pomp and conspicuous consumption is very important to them. As I always say – nothing is going to happen. It is in our culture.

Cheers! 'Kwa niaba yenu wananchi' (Burp) and they clink their glasses.

mbwene2@yahoo.com
 
Jamaa wanaendelea na Mkapa leo:

More on ANBEM Limited dealings: NBC loaned Mkapa company $500,000

  • Subject of a heated debate over pros and cons of privatisation.
  • Right in the midst of a heated national debate on NBC privatization process
  • CRDB Bank also chipped in with 250m/-
  • Legal company documents describe State House couple as ’entrepreneurs’
THISDAY REPORTERS
Dar es Salaam

JUST three years after starting their own private company ANBEM Limited while still at State House, former president Benjamin Mkapa and first lady Anna Mkapa applied for and received a loan of $500,000 (approx. 630m/-) from the National Bank of Commerce (NBC) Limited in the name of this company, it has been learnt.

According to our latest findings, the huge credit from the country’s oldest and most well-established bank was granted in July 2002 to ANBEM Ltd, a company that was officially registered in 1999 with Mr and Mrs Mkapa named as sole directors.

The loan came on the heels of a heated national debate over the April 2000 privatization of the previously state-owned bank, which was fiercely opposed, amongst others, by the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, until his death in 1999.

A good number of members of parliament from both sides of the political divide ruling and opposition parties - were also strongly against the bank’s privatization, arguing that the once-giant national institution was being sold off far too cheaply.

But as eventually transpired, the privatization of the then NBC (1997) Ltd still went ahead as scheduled with the formation of NBC Ltd in April 2000 and acquisition by South Africa’s ABSA Group of 70 per cent of the bank’s shares - for a reported total price of just 15bn/-.

Records also show that Mr Mkapa, as sitting president, was always a vocal supporter of the privatization process which resulted in the bank being taken over by ABSA Group, whose direct association with NBC actually began in August 1999 when the South African firm effectively started managing the bank at the request of the government of the day.

Further investigations by THISDAY have now revealed that in December 2002 - five months after securing the NBC Ltd loan ANBEM Ltd landed another big credit-line in the form of a 250m/- loan granted by CRDB Bank Limited.

And it has been confirmed that by the time Mr and Mrs Mkapa were departing State House at the end of his second and final term as president in December 2005, ANBEM Ltd had total registered debts amounting to 750m/-.

The couple started the company in their own names while still at Ikulu, registering themselves as directors with a listed share capital of 500m/-.

It has also been verified that in the legal documents for setting up the company prepared by Dar es Salaam-based lawyers Kapinga & Company, Mr and Mrs Mkapa described themselves as ’’entrepreneurs.’’

The company was awarded certificate of incorporation number 36547, with Mr and Mrs Mkapa being allotted one nominal share each and listed as directors.

Among other things, the stated objectives of ANBEM Ltd include: ’’To carry on business and to act as merchants, general traders, warehouse, stockists, shopkeepers and operators of supermarkets, commission agents and carriers.’’

The revelations about the former president and first lady registering their own company and starting to do business while at Ikulu followed reports by THISDAY that the Mkapa family owns an office building in Dar es Salaam where a new bank with some big-name local businessmen as shareholders is to be located.

Records show that ANBEM Ltd bought the building, registered under certificate of title number 6809 at Number 8 Ocean Road in the city’s upmarket Sea View area, from a company called Tanzania Building Works in 2002.

Situated right next to Mr and Mrs Mkapa's official residence after retirement, it is understood that the two-storey building will be the official headquarters of the upcoming Bank M (Tanzania) Limited, now in the final stages of being launched after a fast-track registration process that started only in February this year.

THISDAY has sent written questions to Mr Mkapa’s office in Dar es Salaam regarding the nature of the business transactions conducted by himself and Mrs Mkapa while at Ikulu. No response has been forthcoming so far.
 
Yebo Yebo,

Unafurahisha kweli, CCM kama chama sio tatizo. CCM ni nini? CCM sio majengo wala sio yale maazimio yaliyomo ambayo kwa jinsi yanavyochafuliwa hayana thamani yoyote.

CCM ni hao viongozi bomu. CCM ni jina tu na CCM ya mwalimu sio hii CCM ya kwenu sasa. CCM haiwezi kujisafisha kama ambavyo vyama vya kikomunisti vilishindwa. CCM inatakiwa ife ili baadhi ya wanachama wa CCM waje upya, wanaweza kuja na CCM hiyo hiyo lakini itakuwa imebadilika.

Ndio maana nchi zile za Eastern Europe vile vyama vya Kikomunisti vimerudi madarakani lakini vimekuja na watu wapya na adabu mpya na sheria mpya.

CCM wala hata sio hao wanachama walioko vijijini. CCM ni genge la hao majambazi walioko NEC, Kamati kuu, baadhi ya wabunge wao na hao waliong'atuka ambao bado wanashirikiana nao.

Acha kutumia siasa za kikomunisti zilizopitwa na wakati kwamba eti CCM ni wanachama wote. Wanachama wana nguvu gani ndani ya CCM? Leo Mangula kasema kitu ambacho kila mtu anajua kipo, anaambiwa ajieleze NEC. Upuuzi mzima. Wabunge wenyewe hawawezi hata kusema mambo wanayoyaamini, kisa watachukuliwa hatua na CCM. HIcho chama kweli kinawakilisha wananchama.

Ndio maana nawashangaa watu wenye elimu zao Ulaya, wanapopoteza muda wao kufungua matawi ya CCM nje ya nchi.
 
Ulafi ni kitu kibaya sana..kuna mtu aliwahi kuweka 'vichwa vya dhambi' hapa naaamini atakuwa aliweka na ulafi.
Kwa wanajua rasilimali alizojilimbikizia mama BM na mumewe, jamani hadi inachekesha..lini watakula, watoto na ndugu za mama nao wameshachukua chao mapema, sasa hizi mali watazikwa nazo? ulafi, ulafi, ulafi..hadi nchi inakuwa maskini...watu wamekuwa malofa, na walioko madarakani walafi, walafi, duh, watakula hadi mchanga..chondechonde wasiuze na mchanga wetu wa bahari maana beach na visiwa ndo washauziana siku nyingi

On a more serious note: hebu tunyamazie hilo la nyumba za serikali maana kwa ulafi wao hata sisi walalahoi tulipatepo ..taratibu jamani na sie tupate kwenye migongo yao!
 
Ndio maana nawashangaa watu wenye elimu zao Ulaya, wanapopoteza muda wao kufungua matawi ya CCM nje ya nchi.

Hivi wewe MTZ,

Haufikiri hao mabwana wanao fungua hayo matawi tuseme tawi huko ulaya kama wana motives zaidi ya kua wanaCCM?
Ngoja nikuambie kitu,kama hapa Dar es salaam unakibanda chako cha biashara barabarani na unahisi unaweza kuja kukumbwa
na bomobomo ya jiji basi unaweka bendera ya chama cha mapinduzi (CCM),hii inawafanya wale mabwana wa jiji kufyata mkia.
Majirani zako wote wanaweza kubomolewa wewe ukaachwa.

Sasa nadhani unaweza kupata picha ya kwanini hilo tawi limefunguliwa huko?Vile vile kunaweza kua na sababu
nyingi zaidi kwa wanachama hao(tafadhali Ndg.wanachama mnisamehe..haya nia mawazo yangu tu...!)
Unafikiri watu ambao wamekaa tu huko na elimu zao wakija Bongo bila ya kua na contact za maana wanaweza
kupata kazi sawa na elimu zao kwenye serikali hii ya kujuana na ukada haupati kazi mpaka uletwe na furani au uje na kimemo.
Pia kuna watu huko wana vijibiashara vyao au wana represent maslai ya hao hao waungwana na lazima iwa husu kua
under mwamvuli wa utawala ambao ni CCM.
Alafu waBongo ni watu wenyeakiri sana,niamini nakuambia ilikupata assistance ya haraka kutoka huku lazima
wafungue tawi hata kama sio wanachama kweli we huoni ya kilichowatokea wale wa Ukrein?unafikiri wangekua
na umoja wao wa wana CCM nakuamabia nini serikali hata chama kingetoa msaada wa haraka.
 
"Bubu ataka kusema;37624:Miiko ya uongozi ni lazima irudishwe ili kurudisha heshima ya viongozi na pia kuondoa uwezekano wa viongozi kutumia nyadhifa zao walizokabidhiwa na Watanzania kujitajirisha wao wenyewe na familia yao."

Mzee Bubu heshima yako,

Kwani miiko ya uongozi iliondolewa lini? Kuna ahadi moja ya TANU (nadhani CCM bado wanayo) isemayo: sitatumia nafasi yangu kwa manufaa yangu, na kuna sehemu moja inasema cheo ni dhamana.

Najua Azimio la Arusha lilizikwa kule Zanzibar, ingawa Mzee wetu Nyerere hadi mauti yanamkuta alikuwa bado akilalama kuwa haoni ubaya wa Azimio la Arusha.

Shida ya CCM ni kutusadikisha uongo; ajabu ni kuwa Watanzania bado wanaamini uongo huo hadi leo. Sijui ndiyo ule Mwenge ambao Watanzania wanakesha usiku wote wakiuimbia nyimbo?

Hawa CCM hadi leo bado wanatudanganya kuwa Tanzania ni nchi ya Ujamaa na Kujitegemea, kwenye katiba yao na kwenye katiba yetu ya nchi!

Mzee Bubu washauri vijana wako waliojiunga katika umoja wa vyama vya upinzani wasiwe na agenda ya kuingia Ikulu bali wapiganie katiba mpya na tume huru ya Uchaguzi. Waonye kuwa kwa katiba hii feki ya ya Ujamaa na Kujitegemea na Tume hii feki ya Uchaguzi; Ikulu wataisikia na kuiota tu!

"Mtawatambua kwa matendo yao". Yesu

Wanatudanganya kuwa nchi yetu ni ya ujamaa na kujitegemea lakini wanatumia ofisi za umma kujilimbikizia mali, wakikiuka miiko waliojiwekea na ambayo walitulazimisha kuiamini na kuiimba mashuleni.
 
Bado sijaona kosa la Mkapa zaidi ya ufundi wa watu wa kumwaga porojo
 
Hata mimi kweli sijaona kosa unless wataalamu kutoka Norway waje watueleze kuwa ni kinyume na katiba au sheria ya nchi kuanzisha kampuni ukiwa Ikulu!!!!!

FD
 
Tanzania njema

Pokea Tano zingine...pesa yenyewe alikopa. Hebu tuaze kuangalia wale wanachukua kama vile ni za kwao.
 
Kanda 2,

Unataka kutuambia kuwa kufanya biashara akiwa Ikulu ni sawa? Maadili ya wapi hayo? Nadhani tusishangae siku moja mtu Rais akifungua duka ndani ya Ikulu maana katiba si inasema yuko juu ya sheria? Tena kwa mawazo yako si waona sawa kufanya biashara kutoka Ikulu.

This day wametoa nyingine leo.
 
Tatizo sio kwamba Mkapa ana kosa au hana kufanya biashara Ikulu. Tatizo kimaadili inakubalika kuwa na "mjasilimali" Ikulu?
 
www.thisday.co.tz

leo wameweka wazi tena suala la mkopo.

Kuna hoja kwamba huenda Muungwana ameamua kumrudi Ben na kwamba THISDAY wanaweza kuwa wametumiwa. No, sitaki kuamini yote hayo kwani kama ingekua hivyo leo Yusuf Manji angekua jela, Mahalu asingepata BAIL, Warioba na kampuni yake ya MWananchi Gold wangeshachukuliwa hatua, lakini wote hao wanapeta, hii ina maana Muungwana hafuati wala hahusiki kabisa na habari za THISDAY.

Lakini KAMA NI KWELI kwamba Muungwana anamrudi BEN thats GOOD, nadhani ni hatua nzuri kama itakua kama Zambia kwamba sheria ichukue mkondo wake, hakuna KULINDANA. Tusikwepe mada nyeti na nzito kwa kujaribu kutafta sababu ambazo hazina MASHIKO
 
Hakuna suala la kumuhusisha awaye yote kwenye hili suala. WaTZ inabidi muanze kujifunza kusoma habari na kuzichambua na kuangalia credibility ya habari bila ya kuangalia nani yupo nyuma ya hiyo habari.La sivyo hatutafika
 
Umesema kweli Mafuchila. Tukianza kuangaliana kwa sura nani kaleta nini badala ya kujadili hoja hatutafika
 
Hivi wale wapiga kura kule vijijini wangefahamu haya yanayotendwa na viongozi wanaowapa kura kwa KISHINDO hali ingekuwaje? maana huu ni usaliti mkubwa sana kwa kutumia kigezo cha elimu ndogo ya walio wengi kuwadhulumu.Hakika wangepigwa mawe! Na dalili zinaonyesha,hilo laja na sherehe zile za kufanya mwaka mzima kujipongeza kwa `kishindo' zitakoma.
 
Chakaza,
Tusiwaonee wananchi wa vijijini. Angalia matokeo ya kura maeneo ya kura mjini DAR ambako ndiko 'Mujini kwenyewe' kabla hatujawarukia watu wa kijijini.
 
Back
Top Bottom