Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Waungwana linapokuja swala linarohusu maslahi ya taifa tuwe kitu kimoja. Thisday..irrespective wametumwa na nani..as long as they are exposing uozo tuwape support. Tatizo kubwa la waafrika ni ubinafsi ambao chanzo chake ni umaskini! Tumekulia katika mazingira ya suluba sana
!!!, labda generation ijayo ambayo imekulia katika mazingira mazuri (by the way na hawa ni wachache maana wengine wananyimwa elimu). Otherwise hata JK na EL wote wanaganga njaa ndo maana hata ungewapa mishahara na mafao billions by billions..wataiba tuu..maana uroho na ubinafsi ni hulka ya mwafrika. We unafikiri mtu Kama BM kuanzisha kampuni na kuchukua hela kibao za umma..amekosa nini? ni ubinafsi tuu-simple. Na hapa sijui dawa ni nini! (kuna msemo wa kiafrika which goes like......mtoto mtukutu akiamua kulia, atalia tuu.... hata kama akiwa na glass ya maziwa mkononi!)
 
In August 1999, Absa started managing NBC Ltd. at the request of government but at their cost, with the understanding that if they did not buy it, they would be compensated for the costs incurred.

If they bought it, all the costs would be for their own account. That was not a cheap exercise. The cost factor has since been pushed up by the fact that extensive training is required to boost skills levels and to replace the bank's hardware.

NBC Ltd. was formed on 1st April 2000 when NBC(1997)Ltd. was privatised and sold to ABSA Group Ltd. of South Africa. NBC(1997) Ltd. was itself born out of the nationalization of banks and financial institutions in Tanzania in 1967.Tanzania later deregulated banking in 1991. In 1997, a decision was taken to split NBC into three entities, namely NBC Holding Corporation, National Micro-finance Bank (NMB) and NBC (1997) Limited. This was the first step towards the privatization of NBC.

Source: http://www.nbctz.com/aboutus.htm
 
Its introduction to accounting BUSINESS & THE OWNER(s) OF THE BUSINESS ARE TWO DIFFERENT ENTITIES!
 
Mafuchila,
Nitarudi tu kama Dua atakubali kunisindikiza. Lakini ukweli mbali tunakoelekea si kuzuri hata kidogo.
 
Naapa hapa .Siku CCM wanashindwa kwa kura halali Nchi itapinduliwa maana hawtakuwa tayari kuona mali zao walizo iba zinachukuliwa wazi wazi . Ndiyo maana wana haha usiku na mchana kutaka kujikita madarakani . CCM hawana nia ya kumkomboa Mtanzania huu ndiyo ukweli . Mnashanaga ya BM nawaambie JK atakuwa na makubwa zaidi ya haya nyie kaeni hapa mngoje mtaona .
 
Mwisho wa Yote mtakuja kubaliana na mimi kuwa Azimio la Arusha lilikuwa ni Azimio la Ubinafsi na wote waliopiga kura kulipitisha sii viongozi tunaowahitaji!...Na waliopitisha sio CCM peke yao.
Kiongozi kukubaliwa kuwa mfanyabiashara kisha analipwa mshahara mkubwa na serikali yetu!.. Hivi kipi kitatangulia kati ya maslahi ya kampuni yake kama kiongozi mfanya biashara ama maslahi ya nchi ?...

Kisheria tatizo sio Mkapa na viongozi wengine ila tatizo ni sheria yenyewe - AZIMIO LA ARUSHA...
 
Mkandanra mbona mimi nalilia Azimio la Arusha kila siku mzee wangu ?
 
Mkandara,
Nadhani ulimaanisha kusema Azimio la Zanzibar, au siyo?
Aliwahi kunisimulia mjumbe mmoja aliyekuwepo katika kikao hicho kwamba yeyote aliyejaribu kutetea azimio la Arusha walim"shout down" kuwa amepitwa na wakati. Kwa hiyo hakukuwa na debate kabisa.
 
You are probably right - I was very confused. I think Mkandara must have meant " Azimio la Zanzibar ". And it must have been the most painful thing for Mwalimu to live thru.I can almost feel his pain.
 
Lunyungu,

CCM watashindwa kweli TZ? Kule vijijini mpaka waiangushe CCM, labda
itokee balaa. I am not optimistic at all.

Inabidi kutafuta njia zingine halali za kuikoa nchi. Tukitegemea CCM wataporomoka, tutasubiri miaka mingi sana. Tatizo ni moja, watu wengi vijijini mpaka kuja kuelewa sio kazi rahisi.
Tutaelewa sisi hapa JF lakini kule vijijini ambako wanatoa kura kwa pombe
ya shilingi 100, itakuwa kazi kubwa sana.

CCM walifanya kosa 1995 na laiti pale Mrema angelikuwa makini na kukubali
kushirikiana na wengine, naamini CCM wangekuwa wamepoteza. Labda wagombane tena.
 
Jasusi,
WanaCCM wanaolitetea azimio la Arusha wanajulikana kwa jina la Wanachama wa Ibara. Ambao kwa kifupi hawana nafasi ndani ya chama kwa sasa.
 
Tatio sio CCM bali ni watendaji ndani a ccm. Sasa wananchi wengi kule vijijini hawajui hilo. Wao wanaona CCM ndio kila kitu.

Ukiwachukua vinara wote wa ccm wote na kuwaweka Chadema unadhani chadema watashinda uchaguzi...sidhani. Hata kama CCM itabakiwa na watenda bomu kiasi gani bado watakuwa na nafasi kubwa sana ya kushinda uchaguzi...hapo ndio utagundua kuwa tatizo ni wananchi kwa kutokujua tofauti.

Katika hali iliyopo sasa hata madarakani waje malaika watakuwa kama ccm tu, maana hakuna jamii yenye uelewa wa siasa. Kusema hivyo, hao wapinzani wakiweza kushinda uchaguzi at the first place then mabadiliko yamewadia.
 
Mwisho wa Yote mtakuja kubaliana na mimi kuwa Azimio la Arusha lilikuwa ni Azimio la Ubinafsi na wote waliopiga kura kulipitisha sii viongozi tunaowahitaji!...Na waliopitisha sio CCM peke yao.
Kiongozi kukubaliwa kuwa mfanyabiashara kisha analipwa mshahara mkubwa na serikali yetu!.. Hivi kipi kitatangulia kati ya maslahi ya kampuni yake kama kiongozi mfanya biashara ama maslahi ya nchi ?...

Kisheria tatizo sio Mkapa na viongozi wengine ila tatizo ni sheria yenyewe - AZIMIO LA ARUSHA...
Mkandara!
wakati wa Azimio la Arusha hatukuwa nayo haya bali hili ni Azimio la Zanzibar!
 
Ama kweli Uzee kazi nzito, shukrani sana Jasusi maanake nimeweka chunvi ktk chai badala ya sukari....

Naomba ieleweke nilikuwa nataka kuandika Azimio la Zanzibar!..
 
Mafuchila,
Nitarudi tu kama Dua atakubali kunisindikiza. Lakini ukweli mbali tunakoelekea si kuzuri hata kidogo.


Tutakaporudi pale bongo patakuwa hapatoshi huu mchezo wanaoufanya itabidi tuukomeshe, kwa sababu huku ulaya ukiwa Mzee hakufai kwa mawazo yangu.
 
Yebo Yebo,
CCM ni tatizo, hata kama hupendi ndio ukweli wenyewe. Sisemi Wapinzani wakija ndio tutaokoka ila kwasasa CCM ni tatizo.

Angalia tu Eastern Europe, tatizo vilikuwa vyama vya Kikomunisti, vilivyoanguka mambo yakabadilika. Wananchi ni wale wale.

Kwa Afrika tatizo ni mabadiliko gani tunataka. Kama ni kubadilisha JK na kumweka Mbowe, hapo hakuna kitakachobadilika. Lakini kama watakaokuja wataamua kufanya mabadiliko ya katiba, sheria na mengineyo, basi kuna nafasi kubwa ya nchi kuwa tofauti na huu uongozi bomu wa CCM.

Wananchi hawaelewi ni kwasababu ya hao CCM wanaowadanganya kwamba
vikija vyama vingine watachinjana.

Mahali pengine popote duniani huyo Mkapa angekuwa anajiandaa kwenda mahakamani lakini kwa Afrika tunaishia mwacheni mzee wetu.
 
Yebo Yebo,
CCM ni tatizo, hata kama hupendi ndio ukweli wenyewe. Sisemi Wapinzani wakija ndio tutaokoka ila kwasasa CCM ni tatizo.

Angalia tu Eastern Europe, tatizo vilikuwa vyama vya Kikomunisti, vilivyoanguka mambo yakabadilika. Wananchi ni wale wale.

Kwa Afrika tatizo ni mabadiliko gani tunataka. Kama ni kubadilisha JK na kumweka Mbowe, hapo hakuna kitakachobadilika. Lakini kama watakaokuja wataamua kufanya mabadiliko ya katiba, sheria na mengineyo, basi kuna nafasi kubwa ya nchi kuwa tofauti na huu uongozi bomu wa CCM.

Wananchi hawaelewi ni kwasababu ya hao CCM wanaowadanganya kwamba
vikija vyama vingine watachinjana.

Mahali pengine popote duniani huyo Mkapa angekuwa anajiandaa kwenda mahakamani lakini kwa Afrika tunaishia mwacheni mzee wetu.


CCM kama chama sio tatizo...CCM wana sera nzuri lakini watendaji ni BOMU. Wananchi hawajui tofauti, kati ya chama na Watendaji, wananchi wanakipenda chama, chama kilichowaletea uhuru, chama kinachoongoza tawala, chama chetu cha mapinduzi kilichotuunganisha waTz. Hawaoni kama watendaji wa chama hawawajali na kuwathamini, wao mapenzi yao ni kwa chama...ndugu yangu Mtanzania ccm wakikuweka wewe kugombea uraisi hata leo utashinda tena kura nyingi tuu. Hiyo inaonyesha mapenzi ya wananchi wa chama kama ccm (ccm as brand) hata iweje hawawezi kukuona wewe utendaji wako bomu kwa sababu upo kwenye ccm. Kwa upande mwingine, hamwangalii mtu wanaangalia chama. Sasa niambie mwenye tatizo ni CCM au Wananchi.
 
Mimi nadhani hiyo stori ina ujumbe ulio wazi na uliofichika.Uljumbe ulio wazi ni ukweli kuhusu urais wa Ben.Ujumbe uliofichika unaweza kufahamika kwa kujiuliza: hivi hawa jamaa wa Thisday wanapata habari hizo from their ivenstigative journalists au kuna watu wanamjua Ben "kinyumenyume" ndio wanawa-feed info hizo.I go for the second.Binafsi I wasnt convinced na kauli za JK kuwa "mzee wa watu aachwe apumzike."Well,he had to say something kwa vile ishu ya rada ilikuwa inaihusu serikali nzima ya awamu ya tatu including muungwana,so he defended Ben to save his (muungwana) own skin.
Hypothesis yangu ni kwamba kuna watu wanawapatia Thisday habari za Ben.Na si ajabu Muungwana akawa amebariki zoezi hilo.Mchezo mchafu ndani ya CCM huwa hauchagui mtu.Muungwana anaweza kuwa amepata nafasi ya ku-revenge kwa Ben for lack of support during his (Muungwana's) campaign for nomination and presidency.
Ni mawazo yangu tu,lakini i can smell some fish,sio kwamba habari hizo sio za kweli (i'm not even surprised kuziskia),bali nadhani watu wameamua kumrudi Ben just kama kimbunga cha wanamtandao kilivyowakumba the likes of Salim,Sumaye,etc.It's the manifestation of the dirty games within CCM.Tutasikia mengi sana....
 
Mlalahoi

Jibu la swali lako liko kwenye timu ya THISDAY angalia CV za waandishi wao walikopitia.
 
Miiko ya uongozi ni lazima irudishwe ili kurudisha heshima ya viongozi na pia kuondoa uwezekano wa viongozi kutumia nyadhifa zao walizokabidhiwa na Watanzania kujitajirisha wao wenyewe na familia yao.

Mkapa kama alijua kama kwamba anataka kuwa mfanya biashara basi asigombea urais ili ajishughulishe na biashara. Kamwe hili lisingezua mshangao kwa Watanzania, lakini kitendo cha kufungua biashara wakati yuko Ikulu kama Rais wa Tanzania kina utata wa hali ya juu. Kuna uwezekano mkubwa kwamba biashara zake zilihusika katika kutoa huduma ya aina moja au nyingine kwa Idara mbali mbali za serikali. Yeyote aliyekuwa anaamua nani ni mshindi wa tender zilizotangazwa, kamwe asingeweza kuamua kwamba kampuni ya Mkapa siyo mshindi, maana hii ingeweza kumwagiwa mchanga kitumbua chake.

Halafu inashangaza kwamba kuna watu eti wanaona Mkapa hakuvunja sheria yoyote!!!! Hili ni la kushangaza sana. Huyu analipwa mshahara mkubwa na marupurupu ili kuwahudumia Watanzania katika muda wake wote, kumbe wakati huo huo anatumia muda anaolipwa na Watanzania kufanya biashara zake, je ni masaa mangapi kwa siku alikuwa anawahudumia Watanzania na masaa mangapi alikuwa anafanya shughuli binafsi ambazo hakustahili kulipwa mshahara na Watanzania. Pia hata huo mkopo alioupata mimi naamini kabisa Mkapa hakuwa na Assets zozote ambazo angeweza kutumia kama collateral kupata mkopo mkubwa kiasi hicho, ni wadhifa mkubwa aliokuwa nao ndio ulimwezesha kupata mkopo huo. Kwa maana nyingine alitumia madaraka yake kujinufaisha yeye binafsi na familia yake.

Kuna sababu za msingi kabisa viongozi mbali mbali wa serikali kuanzia wakurugenzi wa idara mbali mbali za serikali mpaka Rais wa nchi kuwekewa sheria ambayo wao au familia zao wasiruhusiwe kujihusisha na biashara ya aina yoyote ile.

Huyu Mama Mkapa alipewa mabilioni ya pesa na Bill Gates ili kupambana na ukimwi Tanzania. Mapesa yale alipewa kama Mke wa Rais wa Tanzania (first lady...sidhani hata kidogo kama ana behave as a lady) na siyo kama Mrs Mkapa. Pesa hizi hazijulikani zimetumika vipi maana hakuna mtu yeyote aliyeweza kukagua matumizi ya pesa zile zimetumika kama alivyokusudia Bill Gates. Kwa maana nyingingine pesa hizi badala ya kuwanufaisha wagonjwa wa ukimwi, zimewanufaisha wajanja wachache.

Kuna kila sababu ya kurudisha miiko ya uongozi ili kuondoa mianya iliyopo ambayo viongozi wanaweza kuitumia kujitajirisha. Hizi NGO nazo zipigwe marufuku kwa viongozi wote na familia zao na tunamuomba mama Mkapa atupe mahesabu ya pesa alizopewa na Bill gates, je zilikuwa ni kiasi gani na zimetumika wapi na lini ili kuwasaidia wagonjwa wa ukimwi.
 
Back
Top Bottom