Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

This is unbeliavable,
Sielewi baadhi yetu tuna agenda gani ya kuficha maswala yaliyo wazi?
Kwanini,hivi ni kwanini nyinyi mnakubaliana na wizi huu na kusema kirahisi eti..amwoni kosa?kweli amwoni kosa.
Je kipindikile Bwn.Ruksa akitoa misamaha ya kodi kwa Wahindi na kurusu wanae kufanya nchi hii mali yao binafsi nadhani mapaka leo baadhi yenu mnaandika uozo ule kama umetokea jana.
Na leo uozo huo huo unatokea na mnafumba macho na kusema hamna kosa? How? Aaah.. jamani..!
Baadae Mumwangwana nae anawapa bail na kuwabeba washikaji zake yale yale aliyokua anayafanya mtu wenu Ben lakini mnamshikia bango hata miaka miwili hajafika ofisini mnaona hafai..
Tuwe wakweli,yale ya haki tuyaseme bila kificho
 
Kuanzisha kampuni akiwa bado rais (ikulu) sidhani kama ni kosa. Lakini kosa ni pale kampuni/biashara inapoanza "operation" wakati mtukufu rais bado yupo madarakani/ikulu.

Iwapo kampuni/biashara ingeanza "operation" baada ya muda wa urais kupita/kwisha kusingekuwa na kosa.
 
Sanda Matuta,

Ndio ubinafsi huo huo tunaousema kila siku. Watu kama wanafaidika na huo
uozo utaona sababu wanazo kuja nazo. Hawaoni tatizo kwasababu ni sehemu
ya hilo tatizo.

Sasa wanaanza kulilaumu gazeti, mara muungwana. Kwanini uhangaike kutafuta source badala ya kujadili hoja iliyomo kwenye huo ujumbe?

So longer huo ubinafsi umejaa kwenye roho na mioyo ya Watanzania wengi sidhani kama haya mambo yataisha.
 
Kuanzisha kampuni akiwa bado rais (ikulu) sidhani kama ni kosa. Lakini kosa ni pale kampuni/biashara inapoanza "operation" wakati mtukufu rais bado yupo madarakani/ikulu.

Iwapo kampuni/biashara ingeanza "operation" baada ya muda wa urais kupita/kwisha kusingekuwa na kosa.

And you still dare!
Please,embu jitahidi kusoma posts za mwanzoni na related thread amboyo ili anza kabla ya hii ili ujue biashara ilianza lini.
Tusikurupuke tu na kuanza kutetea vitu ambavyo uhalali wake auwezi kuaproved.
 
Sanda Matuta,

Ndio ubinafsi huo huo tunaousema kila siku. Watu kama wanafaidika na huo
uozo utaona sababu wanazo kuja nazo. Hawaoni tatizo kwasababu ni sehemu
ya hilo tatizo.

Sasa wanaanza kulilaumu gazeti, mara muungwana. Kwanini uhangaike kutafuta source badala ya kujadili hoja iliyomo kwenye huo ujumbe?

So longer huo ubinafsi umejaa kwenye roho na mioyo ya Watanzania wengi sidhani kama haya mambo yataisha.

Nakusoma Mzee MTZ,
Sisi kama wana JF hatupo kwa ajiri ya maslai ya watu furani ila kwa Tanzania bora yenye viongozi bora pia.
Sasa baadhi yetu wana taka tushare views zao hata kama sisi tunona vinginevye bora na nyinyi mfungue milango kwa mawazo yetu ya mabadiliko tumesha choka na utawala mbovu wa viongozi walele na hesabu zao za bei rahisi.
 
Kuna haja ya kuwafanya watanzania sasa waanze kuyaona haya na kuyaweka kwenye tafsiri ya matatizo yao kwni hili jambo limeandikwa kwenye gazeti l kiingereza yafaa magazeti ya kiswahili wakaandika .

Pia shigongo kama analitakia mema taifa hili aanze sasa kuandika mambo haya kwani kuna kinamama wengi ambao ni wapiga kura huwa hawalali hadi waone hayo magazeti aanzishe column ya kujadili issue kama hizi kwa manufaa ya taifa letu.
 
Kuanzisha kampuni akiwa bado rais (ikulu) sidhani kama ni kosa. Lakini kosa ni pale kampuni/biashara inapoanza "operation" wakati mtukufu rais bado yupo madarakani/ikulu.

Iwapo kampuni/biashara ingeanza "operation" baada ya muda wa urais kupita/kwisha kusingekuwa na kosa.

Kwa mujibu wa kifungu kipi cha sheria?
 
Jamani hawa viongozi wetu hawali pekee yao..na beneficiries wengine wako humu humu JF! wengine wako ulaya na Amerika kwa wizi huu huu..kwa hiyo tusishangae kupata maoni tofauti katika hili swala la wizi wa mali ya umma.....Mi hapo ndo nachoka..hawa watu tunaotegemea kwamba wameiona dunia ya wenzetu wanajua vyema concept ya uwajibikaji ndo wanakuja kuparade baseless justification kuwatetea hawa mafedhuli! Kaisari alisema..mke wa mfalme hata kutuhumiwa ni kosa!!!!

Wewe kweli kiongozi wa nchi anaanzisha kampuni ya sepermarkets..na mengineyo! amekosa nini? yet is living on gazillion of pension from poor peasants in TZ after retirement.....unategemea "aombe" mkopo anyimwe? please JF members I bet we ought to be bigger persons than some of our arguments dipicts us to be! Unategemea hawa watu wa namna hii wanaotetea uozo hata wakija na PhD za Oxford na Harvard..zitatusaidia nini watanzania wa kawaida..maana mafanikio yao..yametokana na haya haya tunayoyapigia kelele...we are doomed!!!!!

Its a shame as Sanda above noted....Tanzanians we are the greatest enemy of our own...I guess we are always happy to see our compatriots..bleeding in abject poverty..watu mkitoka ulaya....mnaleta vizawadi vya mitumba...na wenzenu mliowaacha hapa nyumbani wanakuwa wapambe wenu..buying them beers and giving them a ride!..The president should be bigger person..ohhhh..its not the presidency..its the way one wears that title! That matters! Once a leopard, always will be..... JF...naombeni tuwe serious kukata issue za manufaa kwa taifa letu...Iam sure kansa ya ubinafsi, unafiki na ufisadi nk bado haijasambaa katika miili yetu.....at least for now, we not yet there..Atleast for now!
 
Mikuki,

Maneno mazito hayo mzee wangu! mazito na naomba Mungu wengi wetu tuupate mwanga zaidi kuelewa na kuyazingatia vifuani mwetu!.. it' s shame kuona sisi Watanzania tunazidi kujigubika ktk blanketi la Udanganyika!.. hatutaki kuona mwanga wa mchana kwa sababu tumo ktk stage za kuwa Mumiani ( Vampire)....
Yanatakiwa maji ya zam zam (maji ya Uzima)....
 
Mkandara inasikitisha sana. Worse unapokuja kuyakuta sehemu yenye heshima kama JF! Watu wenye kisomo cha hali ya juu wakitetea uozo wa namna hii. Mimi na wewe we might have crossed the wrath of poverty....but think of 80% of our compatriots..who have been denied even the right to exist as human beings! Just because of few people stealing what they dont need. At all! Mkapa anahitaji supermarket au kuwa enterprenuer aweze kuishi maisha ya starehe, Warioba anahitaji kampuni ya madini, Sumaye anahitaji mkopo wa PPF aweze kumake ends meet..do they? I resoundingly say, they dont! They have laws passed on their watches to ensure that they will live forever like kings. So why not leave the little remaining for the rest? Hii ni dhambi kubwa sana kuliko hata ya Adamu na Eva!
 
Hivi jamani mwee lini mtaweza kutazama issue kwa undani zaidi?

Soko huria lipi linalosema kiongozi anaruhusiwa kuwa mjasiriamali...Ama ni katiba yetu ambayo ilitengenezwa na hawa hawa viongozi katika kutazama maslahi yao. Nimewauliza swali moja la msingi sana. Ikiwa Mkapa alikuwa Mjasiriamali, je ni wakati gani alikuwa rais? na sheria inasema nini kuhusu rais anayejishughulisha na biashara kwa kirefu na wazim kwenu! Je,anapoomba kibali ni hatua gani anatakiwa kuzifanya akiwa kama rais wa nchi. majibu yote nadhani hatuna wala bunge hawana!....
Kisha hili neno Wajasiriamali limetokana na linatumika kwa watu wenye biashara ndogondogo ambazo zinahitaji boost ya serikali ktk mkakati wa kupunguza Umaskini. Kwa hiyo budi mfahamu source yakitu kabla hamjakipa support yenu.
Huyu Mkapa alikuwa na umaskini gani kama rais wa taifa?... acheni jamani kutetea vitu ambavyo vipo wazi kabisa.
Mtanisamehe kwa lugha kali lakini kama ndio mchezo wenyewe ndio huu basi tuna safari ndefu sana na vigumu kupata ufumbuzi maanake tunapoteza muda mrefu kusubiri mwezi uandame!... yaani ishara za Mungu.
Kubadilisha kwa mfumo wa kiuchumi ulikuwa unalenga Taifa sio viongozi na soko huria halina kabisa tafsiri inayowahusisha viongozi kumiliki makampuni ya biashara.
Tafsiri hiyo imetengenezwa na viongozi walafi wasiokuwa na uzalendo wala sifa za kuwa viongozi.....
 
Mkandara,

Unafikiri hawaelewi? Wanaelewa vizuri ila wapo kutetea maslahi ya chama chao.

Kwa wengine chama ni muhimu zaidi ya nchi ndio maana hata wahubiriwe na Yesu au Mtume bado hawataelewa.

Si ndio hao hao walikuwa wanasema Mbowe anapata wapi muda wa kuchanganya shule na siasa? Sasa rais anayechanganya kuwa director
wa kampuni, anapata wapi huo muda?

Tuendelee na sio lazima wote wajiunge na bandwagon, tuendelee kuelemishana.
 
Wajameni ninaweza nisieleweke Lakini Nafikiri hawa vijana wanapoteza Golden chance ya kujilipua ili wapate mahitaji yao ya Muhimu ikiwemo hili kubwa la Elimu tena si bora elimu bali Elimu iliyo bora,Kwani hata kama watasaidiwa sidhani kama watapata karo yao kwa wakati muafaka. imekuwa ni kawaida ya serikali kuchelewesha malipo ya karo kwa wanafunzi wa ulaya mashariki.Uchunguzi umebaini hilo kwenye Nchi mbali mbali za ulaya mashariki ambazo serikali imepeleka wanafunzi Lakini pamoja na kuchelewesha na kukumbana na matatizo ya kufukuzwa madarasani ,mabwenini Lakini serikali inapojisikia huwatumia na vyuo vinatuliza mpira.Sasa Kama kuna nafasi kama hii ya kuitumia angalau uwe na uhakika wa kusoma bila ya bugudha za karo na mengine Kwanini wasiitumie kama wanafikiri upo uwezekano.Kupanga ni Kuchagua.
 
hizi mada ziunganishwe ....

jamani watanzania MIIKO YA UONGOZI ILIFUTWA TANGU MIAKA YA 1990....na wala hatukuweka miiko inayoendana na karne hii ili kuchukua nafasi ya iliyofutwa..
kwa mantiki hiyo hakuna kipengele kinachomzuia rais au mwanasiasa kuwa na hisa au kuwa mkurugenzi wa makampuni....labda kama itadhibitika hiyo mikopo alichukua bila kuweka collateral..justify that!...tena kwa mr and mrs mkapa by using there own names and not hiding anything withregard to that ,whatsoever ..it has vividly shown that they had no BAD INTENT ,opening the compony And so nothing to hide ...

I DONT SEE ANYTHING BAD....unajua mara nyingine sisi watanzania tusifanye viongozi wawe wanafiki waweke mapesa ULAYA..kama mtu havunji sheria afungue kampuni au makampuni MCHANA KWEUPE ili kama kuna foul play watu waone..kama hivi mnavyoona kampuni hiyo na wakurugenzi mmewaona..hakuna siri...endeleeni tu kufuatilia kama mkopo amepata kihalali...kodi analipa..nssf kama ipo analipa..kodi za majengo ,,..ets ..

kunao viongozi tuanawafahamu walifanya kazi na mwalimu kina ms... wamejaza makampuni canada na japan huku walikuwa wakiimba UJAMAA naomba warudiushe hayo madola hapa yalete ajiara..zaidi wakingoja WAFE watadhulumiwa kama MOBUTU,,
 
Well if worse comes to worse!...guess that is the last option.

Mikuki,
Inasikitisha sana bob, hawa jamaa wasomi!.... watu ambao tunawategemea kesho
Tena basi unajua hawa viongozi wetu wanachukua mikopo ambayo imeletwa kwa sababu ya kuondoa Umaskini nchini! just imagine IMF na World bank inatupa fedha kuinua wafanya biashara ndogo ndogo, rais anaingia kati na kufungua biashara zake na ku qualify ati ni mjasiriamali!..Hata vyandarua anatia ndani jamani?
Damn... Ama kweli Firaun (Pharaoh) alikuwa na afadhali kuwapenda wananchi wake kwanza.
 
Mh. Phillemon Mikael,

Nadhani uko right kwa mambo mengi uliyoyasama ikiwa ni pamoja na kuwa hakuna miiko ya viongozi. Lakini kusema kwamba kampuni iko wazi, naona hapo hujaweka wazi huo uwazi na ukweli ulikuwa wapi? Je, tokea mwaka 1999 alipoanzisha hiyo kampuni nani alijua kabla ya THISDAY kuandika? Je, alipokopa Benki nani alijua? Sumaye alipokopa milioni 50 mpaka leo ameandamwa Ben leo amekopa mamilioni kwa mamilioni (USD 500,000+ 250m/-), shamba la Sumaye la Mvomero na lile alilokodi ekari 7 Kibaigwa, limekua kelele na hakuna aliyewahi hata kuandika undani, leo Mkapa ana mashamba na kadhalika, tunasema ana haki. Jamani tujiulizeni, hawa walitangaza mali 1995, leo vipi? Wametangaza mali baada ya kuondoka? jamani hii kampuni ofisi zake zilikua wapi? Hebu tueleze kama wewe unajua unaposema hakufanya siri? alifanya siri na aliweka jina lake kwa kuwa alikua na kiburi na akijua hakuna wa kumgusa. (Hiyo ni mada mpya). Mkapa alifanya hivyo akijua Tanzana hakuna waandishi. Aliwahi kusema Waandishi wa Tanzania ni uchwara na hawajui kuandika wala kuchunguza. Alikua na haki kwani hakuna aliyeweza kupita anga zake. HAKUNA UHALALI WOWOTE NDIO MAANA COWI Counsult waliacha kupangisha kwa pale Sea View mara Mkapa alipoichukua nyumba. Wa Denish walisema hawawezi kumlipa Rais kodi ya nyumba. Walilipa kodi mara moja tu then wakahama
 
Phillemon Mikael,
ndugu yangu ndugu yangu wee unazungumza vitu gani hapa! samahani lakini.
Ebu nikuulize kitu ambacho kidogo kinaweza kuendana na maisha yako. Ikiwa Zinaa ni haramu, Je, mtu anayetembea na mathlan Mkeo (samahani) wazi wazi mchana kweupeeee! ina maana hana makosa ila yule anayejificha ndio mkosa?...
Mimi nadhani hakuna tofauti ya kosa hasa pale rais na viongozi wengine wamejitungia sheria kwa sababu ya maslahi yao. Hii sheria ya kuwaruhusu viongozi wa serikali wanaweza kufungua makampuni na kuendesha biashara imepitishwa na nani? kwa manufaa ya nani? na kwa nini wananchi wasihusishwe zaidi katika kutoa maamuzi yanayowahusu viongozi! Lini jaji akashika viti vya mshitakiwa, wakili wa pande zote mbili na mwisho kutoa hukumu yake mwenyewe?...Huoni kuwa it is wrong?
 
halisi na mkandara et all nakubaliana na nyie baadhi ya mambo ..especially hii habari kujulikana leo ..inaonyesha tusimlaumu mkapa tuwalaumu waandishi..kwani wako busy kutuletea habari za udaku na za utafiti kama hizi zinawashinda....kama mtu hakuficha jina iliwashinda nini kugundua miaka hiyo..ndio maana akawaanawaona hamnazo...UANDISHI NI KAMA KIOO CHA JAMII KUTUSAIDIA KUJIREKEBISHA ...KUCHELEWESHA HABARI NI SAWA NA KULETA MAJUNGU KUTULETEA HII HABARI LEO AMBAPO HATUWEZI KUMPIGIA KELEELE MKAPA ...Laiti ingekuja mapema habari hii tungeweza kuzuia au kumrekebisha ...kwa ajili imechelewa ..na pia kwa kuwa haikuwa imefichwa ..bali ilihitaji tu mwandishi mchunguzi kupitia makabrasha ya msajili wa biashara mara kwa mara BRELA tena naona hata wana mtandao...angeshagundua vigogo wooote wenye makampuni....ni kwa sababu tu imechelewa na imekuja kipindi ambacho THERES LESS WE CAN HELP NOW ...naamua kuiita MAJUNGU ..na inaonekana ni habari yenye nia iliyokusudiwa kwa sassa....
mbona pia hamuongelei wanasiasa wenye mapesa nje ..na hao tunawafanyaje??????
 
Unajuaje kama waandishi hawakufuatilia? Je, kama walifuatilia lakini msajili akawanyima hizo kumbukumbu? Na hata kama wangepewa taarifa hizo unadhani wangeweza kuzichapisha wakati BM yupo madarakani?
 
CCM kama chama sio tatizo...CCM wana sera nzuri lakini watendaji ni BOMU. Wananchi hawajui tofauti, kati ya chama na Watendaji,
Yebo yebo,

Inaonekana u mfurukutwa ambaye huoni hata ukweli ulio wazi!
Swali la 1: how can CCM or any political party fulfill his manifesto? Lazima kuwe na viongozi ambao ndiyo wakulaumiwa au kupongezwa. Unataka kutuambia CCM ni dudu tofauti na viongozi wake? Hizo sera nzuri zimeandaliwa na kuandikwa na nani, na zitatekelezwa na nani? Si viongozi wake hao hao?

Yesu alisema mtawatambua (manabii wa uongo) kwa matendo yao, na si maneno yao!

Hebu tuondoke kwenye ule upuuzi wa viongozi wengine wa dini ambao huwaambia wafuasi wao "fuateni maneno yangu na wala si matendo yangu"
 
Back
Top Bottom