Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Napenda kusema ukweli daima!

Inawezekana unachosema ni cha kweli lakini hakina misingi ya kisheria. Huwezi kujitetea kuwa uliiba kwa sababu mtu mwingine aliiba.

Na vilevile huwezi kujitetea kuwa uliiba kwa sababu ulifanya mambo mazuri.
 
hayo yote uliyoyaandika hayakufanyika katika utawala wa mwinyi?hayakuwa zaidi katika awamu ya pili?
Kama tunataka kweli haki itendeke hakyanani hatobaki kiongozi yeyote tanzania!

naomba unitajie aliyoyafanya mwinyi? kwa sababu ni kidogo sanaa kulinganisha na Mkkapa, halafu bangalia Mama Mwwinyi na Mama Mkapa, unaweza kuliaa. Ingawa najua umeona kichwa cha habari kinasemaje? hapa anaongelewa Mkapa.
 
Hivi kama unazungumzia rushwa katika tawala za Tanzania ni awamu ipi haikuwa na rushwa?Ni awamu ipi ilikuwa na rushwa iliyokithiri na hata kutishia mustakabali wa taifa?Hivi unaikumbuka rushwa ya utawala wa Mwinyi ilivyokuwa?Unakumbuka kiasi cha kodi kilichokuwa kinakusanywa na serikali ya Mwinyi kwa mwezi?Sasa kwanini rushwa muione wakati wa Mkapa tu?Je utawala wa Mwinyi haukuingia mkataba wowote ule,haukufanya magendo?Sasa kwa nini kila siku haya hamyaoni na badala yake ni Mkapa,Mkapa tu?
Tuache unafiki wabongo.

Maafa aliyo fanya Mkapa ni ya kua nchi kiuchumi au kuturudisha kwenye utumwa, angalia ATC, TANESCO sasa hivi etc, angalia hizo report mbali mbali za loss iliyopata nchi kutokana na ubinafsi wa huyo Mkapa tax exemption kwa makampuni ya madini, etc licha ya kujidai kwamba alikusanya kodi nyingi kuliko wengine. Huo wizi wa Mama Sitti ulikuwa mdogo saana versus wa Mkapa na Marafiki zake, hivyo tunaangalia huu ungonjwa aliyo leta huyu Mtoto Mkapa kwa sasa, ingekuwa Mkapa hakufanya hayo madudu labda tungeangalia hayo Matatizo ya Sitti. Hivyo kwa kufuata Ranking tunaanza na haya Maafa makubwa yalio wahi kulikumba Taifa Letu.
 
Wengine wenu mtadai turudi nyuma kwa Mzeee Mwinyi hata kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, mimi nasema hapana, tunaanzia na Mkapa wala si kulitafakari Azimio la Zanzibar bali ni utendaji kazi wa Serikali ya Mkapa na uongozi wake Serikalini, Chama cha Mapinduzi na Taifa zima..

Tukiambiwa Watanzania mara ingine hatusomi na kuwa makini kuelewa jambo tunalalamika.
Nimetoa tahadhari mapema kuw ahii hoja ni kuhusu Mkapa na utawala wake, si kuhusu Mwinyi au Nyerere.

Nikaendelea kutahadharisha kuhusu madai ya mafanikio ya Mkapa

Pamoja na yale machache tuliyoyashuhudia ambayo tunayaona kuwa ni chanya, kama kufutiwa madeni yetu na harakati za kuendeleza Mkukuta na Mkurubita, lakini ukweli wa mambo unabakia kuwa kama kweli Mkapa aliacha misingi imara, basi pamoja na Kikwete kujenga baraka la mawaziri kubwa na la kifahari, uchumi na pato la Taifa lisingeporomoka jinsi lilivyoporomoka kwa haraka.

Hivyo kama mnataka kuleta wasifu aliyoyafanya Mkapa au kumchambua mwinyi, narudia tena, anzisheni thread zenu mjengee hoja.

Sina maana msichangie, lakini msijaribu kuteka hoja kwa kupandikiza kisichotakikana? kama ni kesi dhidi ya Mkapa, kwa nin kama nyinyi ni mawakili wa utetezi, msijibu vipengele nilivyotaja ninavyosema kuwa Mkapa awajibike?

Mkiambiwa andika insha ya maneno 100, nyinyi mnacharaza maneno 500, mkipewa F kwa kushindwa kufuatilia maelekezo mnalalamika!
 
Kudhani kwamba makala yako haikusomwa yote kwavile watanzania ni wavivu wa kusoma si sahihi.
Habari za Mkapa zimekuwa zinazungumzwa hapa JF kwa muda mrefu na hoja zimekuwa ni zilezile.Ndiyo mana nikasema zinachosha na zimeegemea upande mmoja.Kwavile kila kukicha zimekuwa ni zilezile sasa zimeshapoteza radha na kuwafanya wengine waliokuwa wanapenda kumuona akitinga mahakamani kuwa na sympathy nae.
Kwahiyo mkuu tuanze ubunifu mwingine!
 
Hizi habari zinaendelea kuzungumzwa sababu bado hajachukuliwa hatua. Na hizi habari hazijachosha mpaka hapo hatua stahili itakapo chukuliwa, kuhusu kegemea upande moja huo ni muono wako, kwa sababu tumekuelezea kwamba kutokana na ranking ya madhambi yake tunataka tuanze nae, Aliye na sympathy nae hiyo hatuwezi ku-quantify , lakini mimi na wengi wanao changia hapa specifically kwenye hii article hawana hiyo sympathy, ukipenda kumtetea mtete kwa facts.
Kuhusu huo ubunifu ni kuziba matobo aliyo weka huyu mtoto, maana bila kufanya hivyo chochote tutakacho fanya sisi watanzania kitapotea kwenye hayo matobo.
 
Sikiza wewe,hii ni forum moja.Kokote utakoweka thread itafikiwa na kusomwa na kuchangiwa if it is wirth it.Kwanini ung'ang'ane kubanana hapahapa kwenye thread hii tu?Ushauri uliopewa ni mwafaka kabisa.Anzisha thread nyingine ili huo upande mwingine wa Ben ujadiliwe kwa kina na mapana stahiki.

Pili,unamtaka mwinyi na siti wake:fine.Hakuna akuzuiaye kuwataka hao kortini,weka thread nyingine.Jenga hoja.

Kinachokutia woga kufanya hivyo ni nini?Au hujiamnini?Unadhani members hawatapita huko?Is that why unadandia dandia thread maalum kwa malengo kinyume na ya mwanzisha thread?Wewe vipi wewe?Ala!

- Hakuna la kuongeza ubarikiwe tu!
 
Kudhani kwamba makala yako haikusomwa yote kwavile watanzania ni wavivu wa kusoma si sahihi.
Habari za Mkapa zimekuwa zinazungumzwa hapa JF kwa muda mrefu na hoja zimekuwa ni zilezile.Ndiyo mana nikasema zinachosha na zimeegemea upande mmoja.Kwavile kila kukicha zimekuwa ni zilezile sasa zimeshapoteza radha na kuwafanya wengine waliokuwa wanapenda kumuona akitinga mahakamani kuwa na sympathy nae.
Kwahiyo mkuu tuanze ubunifu mwingine!

Na wewe vilevile unatakiwa kuanza kuwa mbunifu. Ukiona posti yenye kumlenga Mkapa, inabidi usibonyeze.
 
maovu ni maovu tu. yawe makubwa ama madogo yote hayafai. kwahiyo wanaweza jadiliwa waliotangulia nyuma yake pia - lakini isiwe hapa maana tutashindwa kumjadili bwana BM kwa kina. mengi kafanya na sifa lukuki kapata kimataifa lakin hilo pia sio mada kuu kwa sasa hapa.

sisi kama watanzania hatusongi mbele kwa sababu kadhaa - zingine tunazisababisha sisi wenyewe zingine zi nje ya uwezo wetu.
yaliyo hapa chini kwamfano yalikuwa ndani ya uwezo wetu lakini yametokea na yanatuumiza kama taifa;

  • Benki Kuu na kashfa zote; Meremeta, Epa, CIS, Tangold, Minara na menginewe.
  • Miundombinu na Nishati: ATC, TRL, Rada, IPTL, Richmond, Kiwira, Ndege ya Rais, Helikopta za Jeshi na mengine.
  • Demokrasia butu: uonevu kwa vyama vya siasa na wafuasi wa vyama ambavyo si CCM, kwa kutumia nguvu ya dola kama kule Pemba, mauaji ya Mwembechai, kufilisi au kutoza ushuru na kodi ya kukomoa kwa mwenye kuipinga CCM na Serikali ya Mkapa na mengineyo.
  • Uwekezaji: Mikataba mibovu, sheria mbovu ambazo zinawapendelea wawekezaji na kulipunguzia Taifa mapato.
  • Sheria na Katiba: kuendelea kuwepo kwa sheria na mambo mabovu katika sheria na katiba ambayo yameondoa kabisa mihimili ya Bunge na Mahakama kuwa na nguvu za kikatiba na mamlaka kuihakiki Serikali kuu.
  • Uchumi wa nchi, kudorora kwa uchumi kwa hali halisi ya uzalishaji mali, kudumaa kwa kilimo na kukimbilia utegemezi wa kuagiza chakula, kupungua uzalishaji mali kutokana na kosekana kwa umeme, maji, barabara nzuri.
  • Elimu na Afya: kushuka kwa kiwango cha elimu Tanzania kwa kuruhusu matakwa binafsi ya watu wachache waamue kubadili mfumo wa Elimu bila kupata ushauri wa wataalamu wa Elimu. Afya kuendelea kudorora huku kukiwa na uhaba mkubwawa vifaa, madawa na wataalamu wa afya.
  • Uongozi mbovu; kukosekana kabisa kwa uwajibikaji ndani ya serikali ambako kumezaa tabaka la viongozi wa Serikali na Mashirika ambao wanajiona ni Miungu wasio na makosa (Mattaka, Chenge n.k). Kukosekana na Sauti ya kuheshimiwa kuliongoza Taifa.

yote hayo na mengine mengi yamezidi kumdidimiza mtanzania na impact yake haiishi leo wala kesho. ni zigo letu forever: mimi, wewe, watoto wetu, wajukuu zetu na vitukuu vyetu.

tufanyeje? tuanzie wapi? tuanze na nani? tuanzie lini?

kilichoharibika kimeharibika. kurekebika kazi ya zege lisilo la kulala.

lakini tunaweza fanya kitu cha kutusaidia leo na baadae. kutuma MESEJI.

suppose huyo bwana amefunguliwa mashtaka. atapona au atapatikana na hatia. akipona au la itakuwa meseji kwa wengine waliopo na watakaofuata. nani anapenda adha ya kutinga kortin au kwenda keko hata kama kumekaa kiVIP? pia hadhi yake ktk jamii itakuwa imeshuka na historia itakuwa umejiandika.

naamini kikubwa itakuwa kutuma meseji tu maana tunaambiwa wakubwa hawapatikani na hatia.
 
Hivi kama unazungumzia rushwa katika tawala za Tanzania ni awamu ipi haikuwa na rushwa?Ni awamu ipi ilikuwa na rushwa iliyokithiri na hata kutishia mustakabali wa taifa?Hivi unaikumbuka rushwa ya utawala wa Mwinyi ilivyokuwa?Unakumbuka kiasi cha kodi kilichokuwa kinakusanywa na serikali ya Mwinyi kwa mwezi?Sasa kwanini rushwa muione wakati wa Mkapa tu?Je utawala wa Mwinyi haukuingia mkataba wowote ule,haukufanya magendo?Sasa kwa nini kila siku haya hamyaoni na badala yake ni Mkapa,Mkapa tu?
Tuache unafiki wabongo.

ok, tukubali kwamba mwinyi alikuwa na makosa, pia tukubali kuwa mkapa kuna mazuri alifanya. Je hali hii itahalalisha ufisadi wa kutisha na udikteta wa Mkapa?

Mkapa ana dhambi kubwa kuliko viongozi wote katika historia ya nchi hii kwa sababu alikuwa na uwezo mkubwa wa kujenga nchi. alikuwa pia na uwezo mkubwa wa kushawishi na kujenga hoja za kusaidia nchi. lakini yeye na kundi la majambazi wenzake wakatumia uwezo huo huo kuifilisi nchi.

Huyu mtu asiachwe tafadhali. akamatwe na kufikishwa kisutu mara moja.
 
Hizi habari zinaendelea kuzungumzwa sababu bado hajachukuliwa hatua. Na hizi habari hazijachosha mpaka hapo hatua stahili itakapo chukuliwa, kuhusu kegemea upande moja huo ni muono wako, kwa sababu tumekuelezea kwamba kutokana na ranking ya madhambi yake tunataka tuanze nae, Aliye na sympathy nae hiyo hatuwezi ku-quantify , lakini mimi na wengi wanao changia hapa specifically kwenye hii article hawana hiyo sympathy, ukipenda kumtetea mtete kwa facts.
Kuhusu huo ubunifu ni kuziba matobo aliyo weka huyu mtoto, maana bila kufanya hivyo chochote tutakacho fanya sisi watanzania kitapotea kwenye hayo matobo.

Nakuelewa.Nina uwezo wa kumtetea na facts ninazo na ndiyo lilikuwa lengo langu.
Lakini kwavile hampendi watu wenye mawazo tofauti na yenu mkaanza kunisurubu kwa kuniamuru nianzishe thread yangu.
Kwahiyo nyie endeleeni kuchoshana akili lakini mjue kuwa Mkapa hatofikishwa mahakamani na hii serikali ya Kikwete.
 
Perfect !!!!!!!. Leta facts sasa. Lakini facts zisiwe kulinganisha ukwaju na mpera. Facts ziwe squarely kwanini yeye sio FISADI.
 
Nakuelewa.Nina uwezo wa kumtetea na facts ninazo na ndiyo lilikuwa lengo langu.
Lakini kwavile hampendi watu wenye mawazo tofauti na yenu mkaanza kunisurubu kwa kuniamuru nianzishe thread yangu.
Kwahiyo nyie endeleeni kuchoshana akili lakini mjue kuwa Mkapa hatofikishwa mahakamani na hii serikali ya Kikwete.

basi kwa kutumia hiyo akili yako, tena nzuri tu ungeanza ni hizo pwanti zako, otherwise fuata ushauri wa Zakumi? Kuhusu Mkapa kushughulikia au la hilo ni jambo lingine, lakini uelewe kuna njia nyingi za kumua Paka Shume, inaweza ikawa sindano, risasi, mawe kufuzwa kwa kuzomea mwishowe kukimbilia bahari ambako hajui kuogelea na akazama au kujiishia kwa Shinikizo etc kwa kwa kuwa huyu Mstaafu ana fana fana na PAKA SHUME basi nafikiri za reasonable action available for most tanzanians kama Kikwete hato mshughulika itakuwa kumzoe akimbilie Bahari akajifilie huko, na wakati huo atakuwa ametupa hizo shekheli alizo tuibia. kama vile Yuda wa Iskarioti alivyo tupa Shekeli 32 baada ya kubusu mesiah
 
Jinsi kila kitu kinavyosambaratika na kuangamia, uharamia, uzembe, ukosefu uadilifu, kukosa uungwana na utu, hujuma, wizi, ufisadi na dhuluma zikiongezeka, vifole vyote vinabidi vimnyokee mtu mmoja, Benjamin William Mkapa, Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ndiyo, Mchungaji kanena msilishangae. Ndiyo, Mchungaji kanena pamoja na kumshikia bango Rais wa Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kwa kuwa mgumu kufanya maamuzi mazito kuisafisha nchi yetu, lakini badala ya kuendelea kumwagia Kikwete lawama, Mchungaji anasema, turudi kwa yule aliyekuwa madarakani kabla ya Kikwete.

Wengine wenu mtadai turudi nyuma kwa Mzeee Mwinyi hata kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, mimi nasema hapana, tunaanzia na Mkapa wala si kulitafakari Azimio la Zanzibar bali ni utendaji kazi wa Serikali ya Mkapa na uongozi wake Serikalini, Chama cha Mapinduzi na Taifa zima.

Nilipoandika mada kuhusu Andrew, Omari, Cornell na Robert, niliwataja wakuu wa mambo ya sheria na dola, usalama wa Taifa na nchi, katiba na haki na kuwatuhumu kuwa wao katika nyadhifa zao na wakati wa uongozi wao, Tanzania iligeuka kuwa dangulo na handaki la kila aina ya uharamia kuliibia Taifa wazi wazi bila woga wala aibu.

Kikwete katuambia, tumuache "Mzee Mkapa" astaafu kwa amani, mimi nasema hapana, hatuwezi kuendelea mbele bila Mkapa kufikishwa kizimbani na kujibu mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka, kushindwa kulilinda Taifa kutoka maadui na uhalifu na mbaya zaidi kuliingizia Taifa hasara.

Simtuhumu Mkapa kwa wizi, bali nalisema wazi kuwa ndani ya utawala wa Mkapa wa miaka 10, makovu na majeraha tunayoyaona leo hii ya uhujumu na ufisadi, yalianzia nyakati hizo, michubuko na mikwaruzo ilifanyika nyakati hizo na tulichobakishiwa ni uozo ambao unatambaa kama algae na fungi.

  • Benki Kuu na kashfa zote; Meremeta, Epa, CIS, Tangold, Minara na menginewe.
  • Miundombinu na Nishati: ATC, TRL, Rada, IPTL, Richmond, Kiwira, Ndege ya Rais, Helikopta za Jeshi na mengine.
  • Demokrasia butu: uonevu kwa vyama vya siasa na wafuasi wa vyama ambavyo si CCM, kwa kutumia nguvu ya dola kama kule Pemba, mauaji ya Mwembechai, kufilisi au kutoza ushuru na kodi ya kukomoa kwa mwenye kuipinga CCM na Serikali ya Mkapa na mengineyo.
  • Uwekezaji: Mikataba mibovu, sheria mbovu ambazo zinawapendelea wawekezaji na kulipunguzia Taifa mapato.
  • Sheria na Katiba: kuendelea kuwepo kwa sheria na mambo mabovu katika sheria na katiba ambayo yameondoa kabisa mihimili ya Bunge na Mahakama kuwa na nguvu za kikatiba na mamlaka kuihakiki Serikali kuu.
  • Uchumi wa nchi, kudorora kwa uchumi kwa hali halisi ya uzalishaji mali, kudumaa kwa kilimo na kukimbilia utegemezi wa kuagiza chakula, kupungua uzalishaji mali kutokana na kosekana kwa umeme, maji, barabara nzuri.
  • Elimu na Afya: kushuka kwa kiwango cha elimu Tanzania kwa kuruhusu matakwa binafsi ya watu wachache waamue kubadili mfumo wa Elimu bila kupata ushauri wa wataalamu wa Elimu. Afya kuendelea kudorora huku kukiwa na uhaba mkubwawa vifaa, madawa na wataalamu wa afya.
  • Uongozi mbovu; kukosekana kabisa kwa uwajibikaji ndani ya serikali ambako kumezaa tabaka la viongozi wa Serikali na Mashirika ambao wanajiona ni Miungu wasio na makosa (Mattaka, Chenge n.k). Kukosekana na Sauti ya kuheshimiwa kuliongoza Taifa.
Pamoja na yale machache tuliyoyashuhudia ambayo tunayaona kuwa ni chanya, kama kufutiwa madeni yetu na harakati za kuendeleza Mkukuta na Mkurubita, lakini ukweli wa mambo unabakia kuwa kama kweli Mkapa aliacha misingi imara, basi pamoja na Kikwete kujenga baraka la mawaziri kubwa na la kifahari, uchumi na pato la Taifa lisingeporomoka jinsi lilivyoporomoka kwa haraka.

Ni wajibu wetu wote kama taifa kuwajibika na kuchapa kazi ili kulikwamua Taifa kiuchumi ili kuwepo na elimu na afya bora, ajira na tumaini la kuwa Taifa linalojitegema, lakini kinara, kiranja mkuu ambaye alitutukana kuwa tuna wivu wa kike na ni wavivu, matusi na lawama za Taifa kushindwa kusonga mbele zinarudi kwake na si mtu mwingine.

Ni haki yetu kama Wananchi, kutaka Mkapa awajibishwe kwa kuvurunda kazi. Hata pamoja na kuwa hawezi kupigiwa kura tena, lakini anapaswa afikishwe mahakamani kwa uzembe na matumizi mabaya ya madaraka yake.

Suala la Kinga ni la kitoto na linaendelea kulea uozo, ujuvi na ubabe wa kutishana na kulindana.

Atakapofikishwa Mkapa mahakamani, hata kina Rostam, Lowassa, Chenge na wengine watabaini kuwa Watanzania, hatutaki mchezo. Kila mwenye ndoto ya Ufisadi, Uzembe, utumiaji vibaya madaraka, uvivu na kukosa kuwajibika ama itabidi atafute nchi nyingine ahamie au anyooke na kuanza kuishi kama Mtanzania Mzalendo.

Kura zile za Tsunami hazikuwa za kutuletea Ze Comedy! Bwana Kikwete nakuomba fanya kazi yako, ondoa magugu, visiki na viwavi jeshi walio ndani ya Serikali na Chama chako.

Jaruzelski, pamoja na yote aliyofanya kwa madai ya kutumia madaraka au kwa mujibu wa sheria, leo hii yuko mahakamani kujibu mashitaka. Kila kona dunia hii, kiongozi aliyebainika alifanya kosa anavuliwa kinga na kufikishwa mahakamani, kama rafiki yetu Chiluba alivyofanyiwa.

Hivyo basi, tupaze sauti zetu kwa nguvu tukimtaka Kikwete amfunge paka kengele.

Rais Kikwete, nakuomba usicheze nalenale, ushamfikisha Mramba, Yona na Mgonja, tunamtaka Lowassa, Rostam na zaidi ya yote, tunamtaka Mkapa.

La sivyo, unatupa kazi moja, nikinukuu maneno ya mmoja wa viongozi wa chama cha wafanya kazi Ugiriki walipofanya fujo kutokana na Polisi kuua mtoto mdogo "It is very simple, we want the government to fall". Sentenzo hiyo ilitolewa kwa ghadhabu kwa Serikali kushindwa kufanya kazi yake ipaswavyo.

Ukishindwa kufanya kweli, basi nasi kwetu itakua "it is very simple, we want the government to fall" na kweli kwa kiapo cha kilio cha machungu Serikali yako itashindwa na kuanguka yenyewe. Usitufikishe hapo kwenye mchanga tukakuchukia na kugotesha meli yetu na kutoa kauli hiyo ya kutakia maangamizo ya Serikali yako.

Ili tuendelee mbele, fungua kesi, Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya Benjamin William Mkapa.

Heshima yako mchungaji. Nilishaandika hapa kwamba kuwakamata akina Yona, Mramba na wengineo hakuleti maana kama Mkapa hatakamatwa, hiyo ni sawa na kumpiga nyoka mkiani badala ya kumpiga kichwani.

Watanzania tutazunguka huku na kule tukiimba nyimbo za ufisadi lakini majibu yote ni MKAPA. Huyu ndiye ALFA NA OMEGA katika ufisadi.

Bila kumkamata, kumyang'anya mali zetu na kumfunga Mkapa basi wote waliokamatwa kwa ufisadi waachiwe huru.
 
Mtarajiwa,

Mahakamani kesi ikifunguliwa na mashitaka kusomwa, upande wa utetezi kazi yake ni kupinga madai ya mashitaka na kuonyesha kuwa mtuhumiwa hakufanya hayo makosa anayotuhumiwa.

Sasa katika kesi hii ya Wananchi na Mkapa na makosa aliyotajiwa na mwendesha mashtaka, je wewe unaleta utetezi gani kujibu mashitaka ama kwa kupinga kwavitendea kazi kuwa mfano uhujumu Benki Kuu haukutokana na Uzembe wake yeye Mkapa kama Rais wa nchi kushindwa kuwajibika?
 
Nakuelewa.Nina uwezo wa kumtetea na facts ninazo na ndiyo lilikuwa lengo langu.
Lakini kwavile hampendi watu wenye mawazo tofauti na yenu mkaanza kunisurubu kwa kuniamuru nianzishe thread yangu.
Kwahiyo nyie endeleeni kuchoshana akili lakini mjue kuwa Mkapa hatofikishwa mahakamani na hii serikali ya Kikwete.

teh! teh!
punguza hasira.
mwaga mamboz.
tutakusoma.
tutakuelewa.

unajua ilikuwaje watu wakakuambia vile? walikuwa wanasema makosa yake hayawezi kutokuwa makosa kwa vile kuna mazuri aliyafanya. pia walisema kama yeye alikosea tusimwachie eti kwa vile kuna wengine waliomtangulia pia walikosea.

now, can you start? mwaga facts zitakazoonyesha kuwa yale si makosa
 
Mitandao ya wizi wa magari na wizi wa ngawira kwenye mabenki na maduka ya fedha iliyokuwa ikilindwa na polisi. Ujambazi mwingi ulitekelezwa na maafisa wa polisi na au wa Jeshi. Inaelekea IGP wa enzi hizo na wakubwa wote walijua. Mbona baada ya awamu ya nne kuanza kazi watu fulani walikamatwa na mambo hayo yakaisha?
 
Niliwahi kuzungumza siku nyingi sana hapa kijiweni kuwa Mkapa ndiye aliyeharibu nchi yetu. Aliuza raslimali zetu zote kwa faida yake pamoja na jamaa na marafiki zake tu. Akajenga msingi wa aina maalum ya ufisadi kuzidi ule uliozoeleka wa Nigeria. Wafanyabiashara za halali waliofanya biashara zao kwa siku nyingi sana wakaachwa nyuma sana na wafanyabiashara walitoka kwenye siasa au walioingia kwenye siasa au waliokuwa na connection na wanasiasa.

Adhabu ya mtu aliyeaminiwa na kupewa madaraka makubwa sana akayatumia vibaya kwa kujinufaisha binafsi inatakiwa iwe ni kubwa sana, sawa na ile ya kuua kwa kukusudia!!!

Ndiye aliyeanzisha huduma za kulipia kama vile shule , hospitali n.k Kumbe nchi ilikuwa na fedha nyingi tuu ,wakazilamba na kuanza kulipisha wanafunzi , wagonjwa nk. Kwani enzi za mwalimu na Mwinyi mbona mambo yalikuwa safi tu shule bwereree, mahspitali bure tena dawa zilikuwepo . Leo ni ujinga mtupu.............
 
kwa nini usianzishe thread yako ukawajadili mwinyi na mama sitti? Au ukaanzisha thread kusifu aliyofanya mkapa? Kwa nini utulazimishe kuongea unalotaka na usilianzishie hoja?

mchungaji tafadhari linda heshima yako kwa kuwa mwepesi wa kupokea hoja zinazopingana nawe.

Sidhani kama huyu ndugu amekurupuka tu kukupinga bali ni kutokana na chokochoko ya hoja yako dhidi ya netanyahu, nakuomba usiingie ktk ulingo wa ngumi ukiwa umevalia taulo, vaa kama mpiganaji na pigana kadri utakavyoweza mwisho wa pambano tutamuona mshindi wa pambano.

Huyu bwana amekuja na hoja zake hata kama ni nyepesi, hiyo haikupi fursa wewe kumfukuza ktk mada uliyoianzisha. Si uungwana tena inapokuja suala la ukasisi mkuu.

Tuonyeshe ukomavu kwa kuhimili ngumi za uso
 
rev. Kishoka,

Swala la kumuondolea kinga Mkapa na kumpeleka mahakamani ni hoja finyu na hatari. Kama Mkapa alifanya makosa akiwa rais, basi rais aliyeko madarakani atengue maamuzi hayo na kuyarekebisha. Tuchukue mfano rahisi, wamarekani wamemchagua Obama kuwa rais wao katika kipindi kigumu kabisa. Rais Bush amefanya maamuzi mengi mabaya ambayo yameitumbukiza Marekani na dunia katika msukosuko mkubwa sana, lakini kamwe hautasikia wamarekani wakisema Bush aburuzwe mahakamani kama ambavyo wengi wetu hapa tunavyomshupalia Mkapa aburuzwe kisutu! na hautasikia kamwe Obama akisema 'amerithi' matatizo ya nchi kutoka kwa Bush, wamerekani watampima kwa uwezo wake wa kutatua matatizo yao na sio kwa kisingizio cho chote kile. Vile vile JK hatakiwi kutoa lawama zozote kwamba amerithi matatizo kwa Mkapa. kama kuna maamuzi yeyote mabaya aliyofanya Mkapa, basi atengue (reverse) na abadilishe.
Kumpeleka Mkapa mahakamani kuta -set precedence, ambapo baada ya Mkapa atafuata mzee ruksa, na wakati huo huo JK akijitayarisha kutia nywele zake maji maana baada tu ya kumaliza kipindi chake naye ataburuzwa mahakamani!
kinachotakiwa kufanyika kama nilivyosema ni kutengua maamuzi yote mabaya aliyofanya Mkapa akiwa madarakani tu!

nawasilisha.
 
Back
Top Bottom