3) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais
kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufuku
kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la
kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya
kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye
kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais
kwa mujibu wa Katiba hii.
Apart from all contradiction, hakuna sub-section inayo ipa bunge uwezo wa kuondoa hiyo kinga either kwa rais aliyepo madarakani au aliye staafu?
Apart from all contradiction, hakuna sub-section inayo ipa bunge uwezo wa kuondoa hiyo kinga either kwa rais aliyepo madarakani au aliye staafu?
August,
Hapo juu kifungu kimeacha mwanya kumshitaki rais mstaafu aliyefanya makosa yaliyo nje ya capacity yake ya urais (kama kufungua kampuni dubious under the capacity of citizen Mkapa, not president Mkapa, which is exactly what Mkapa did)
Kuhani,Bunge likimtoa madarakani kwa mashitaka Bungeni, Rais atakuwa hana kinga ya mashitaka mahakamani.
Katiba ya Jamhuri
46.(3) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufuku kumshtaki...
46A(10) yasema:
Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bunge lilipopitisha azimio hilo.
Kama DPP na ofisi ya AG wameshindwa kumhusisha Yona na kashifa ya Kiwira unategemea akatafsiri hicho kifungu dhidi ya BWM? It'll be like walking while dreamNimekiona hicho kitundu, lakini wenzetu DPP na wenzake wanajifanya hawalioni hicho kifungu, hivyo wanataka tundu kubwa , ndio maana nikawa naangalia uwezekano wakuwaongezea hilo tundu la kumshtaki mstaafu wetu Che Nkapa
Je, katiba inasemaje kuhusu former President?
Zambia walitumia utaratibu gani kumfikisha Chiluba hatiani?
Kikatiba hakuna sheria ya kumshtaki Mkapa zaidi ya mtu mmoja katili na Dikteta ambaye kaamua kufanya yale yasiyowezekana ikiwa ni pamoja na kuibadikisha Katiba kwa nguvu ya dola yake!..
Ndio maana nikasema badala ya kumtazama Mkapa nadhani kisheria kwa Mkewe inawezekana na kama huyu ataingizwa mahakamani basi Mkapa ndio kesha..Kimaisha ni pigo kubwa kuliko yeye mwenyewe!
Azimio lile linahalalisha kiongozi kufanya biashara, lakini halihalalishi kiongozi kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu; kupata mali kwa njia ya udanganyifu ni kosa la jinai.Kichuguu,
Tazama Azimio la Zanzibar... maslahi binafsi kwa viongozi ni ruksa..
Nakubaliana na wewe isipokuwa unaweza kutupa ushahidi wa huo udanganyifu uliotumika!.. maanake hapa ndipo tunapokwama kisheria. Inawezekana kabisa kuwa Mkapa aliweza kujilimbikiza mali (udanganyifu) kwa kutumia kiti cha Ikulu, hili ni kosa nje ya kanuni za uongozi na sidhani kama sheria inamkinga...hakuna sheria inayoweka kinga dhidi ya Utawala bora - Kitu muhimu ni kuweza ku prove that na ipingane na Azimio la Zanzibar...Azimio lile linahalalisha kiongozi kufanya biashara, lakini halihalalishi kiongozi kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu; kupata mali kwa njia ya udanganyifu ni kosa la jinai.
Kichuguu,
Nakubaliana na wewe isipokuwa unaweza kutupa ushahidi wa huo udanganyifu uliotumika!.. maanake hapa ndipo tunapokwama kisheria. Inawezekana kabisa kuwa Mkapa aliweza kujilimbikiza mali (udanganyifu) kwa kutumia kiti cha Ikulu, hili ni kosa nje ya kanuni za uongozi na sidhani kama sheria inamkinga...hakuna sheria inayoweka kinga dhidi ya Utawala bora - Kitu muhimu ni kuweza ku prove that na ipingane na Azimio la Zanzibar...
Ndiyo maana tunataka achunguzwe kwa mujibu wa sheria, asikingweakingwe na kivuli cha katiba; tunataka tujue ukweli kuhusu alivyojipatia mradi ule na contract ya kulipwa na TANESCO kwa miaka 20.