BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,283
na wakala wa manunuzi haya alikuwa ni yule yule muhindi wakala wa Rada aliyejipatia shilingi bilioni 12 na kuanza kuzisambaza kwenye bank accounts mbali mbali za vingunge akiwemo mzee wa vijisenti...sasa CAG anashauri ndege hiyo iuzwe
CAG: Ndege ya Rais iuzwe
na Tamali Vullu
Tanzania Daima
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Serikali (CAG), Ludovick Utouh, amesema iwapo ofisi yake ingeombwa kuifanyia ukaguzi ndege ya rais, wangeshauri iuzwe.
Utouh, alisema hayo mwishoni mwa wiki katika semina iliyoandaliwa na ofisi yake kwa wahariri wa vyombo vya habari, iliyofanyika mjini Bagamoyo ili kufahamu majukumu ya ofisi hiyo.
Kauli hiyo ya CAG, inatokana na swali la mmoja wa wahariri aliyetaka kujua kama ofisi hiyo ingepewa jukumu la kuifanyika ukaguzi ndege hiyo, ingetoa ushauri gani kwa serikali.
Alisema hivi sasa hakuna sababu ya msingi ya kuifanyia ukaguzi ndege hiyo kwa kuwa gharama zilizotumika kununulia ni halisi na ni uamuzi wa rais kuamua kuitumia anapokwenda safari za nje ya nchi au la.
"Kwa sasa hakuna msingi wa kuifanyia ukaguzi, kwani gharama iliyotumika kununua ni sahihi na hapa suala la thamani ya pesa halipo, kwa sababu ni uamuzi wake kuitumia ama la," alisema.
Wiki iliyopita, Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa (CCM), alidai ndege hiyo haina faida kwa taifa na kutaka iuzwe.
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo bungeni wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Fedha na Uchumi kwa mwaka wa fedha 2008/20009.
Alisema matumizi ya ndege hiyo kwa sasa, ambayo hivi karibuni iligongwa na gari la maofisa usalama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, hayakidhi mahitaji ya rais, kwani haitumiki anaposafiri nje ya nchi.
Alisema uwezo wa ndege hiyo iliyonunuliwa kwa bei kubwa hata kuibua malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na wabunge, ni kubeba watu 12 wakati rais anapokuwa na safari, huwa na ujumbe wa zaidi ya watu 18, hivyo haifai kwa matumizi yaliyolengwa licha ya kununuliwa kwa bei kubwa.
Katika hatua nyingine, Utouh, alisema wamekuwa wakikumbana na vitisho vya aina mbalimbali kwa kuwa kazi wanayofanya inaingilia masilahi binafsi ya watu.
"Kazi yetu haina tofauti na ya uandishi wa habari, ingawa tunafanya hivyo kwa masilahi ya taasisi husika na taifa kwa ujumla, lakini tunagusa masilahi ya watu, hivyo vitisho vipo, lakini wanasema ukishayavulia nguo maji, sharti uyaoge," alisema.
Aidha, alisema ofisi yake ipo katika mchakato wa kuandaa ripoti nne ambazo wanatarajia kuzikamilisha kabla ya Desemba mwaka huu.
Alizitaja ripoti hizo kuwa ni za ukaguzi kwa shule za sekondari katika masomo ya hesabu na sayansi, afya ya msingi kwa wananchi, taka ngumu na viwango vya barabara.
Alisema baada ya kukamilisha ripoti hiyo, huikabidhi kwa rais na baadaye kupelekwa bungeni.
Awali, akiwasilisha mada kuhusu ukaguzi wa mashirika ya umma, Jumaa Mshihiri, alisema ofisi hiyo inakabiliwa na upungufu wa wakaguzi katika mashirika hayo.
Alisema kutokana na hali hiyo, wakati mwingine wanalazimika kutafuta wakaguzi binafsi kwa ajili ya kufanya kazi hiyo na wakaguzi hao hupatikana baada ya kutangaza zabuni.