Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Makanisa na Misikiti vinatuangusha sana kwenye suala la ufisadi na rushwa. Ukatoliki wa siku hizi hata muumini wa kawaida anapewa nafasi kuhutubia kanisani kwenye ibada!!

Sasa ulitaka makanisa na misikiti wafanyeje wakati unajua kabisa kuna amri ya kumsamehe aliyekukosea hata mara saba sabini
 
Waumini wote kataeni makanisa yanayokumbatia mafisadi acha waende kwenye makanisa yao wenyewe watubu warudishe mali zetu.
 
ni bora kuwasamehe halafu tukae chini tuanze upya kuijenga nchi yetu mkuu.no way maana hata tukisema tuwabague haitupi faida
 
Hiyo sisi hauituhusu whether una dini, huna hiyo ni ya kwako .... la kwetu sisi ni malizetu ulizotuibia RUDISHA!!!!! WENYEWE TUNAZITAKA
 
Sasa ulitaka makanisa na misikiti wafanyeje wakati unajua kabisa kuna amri ya kumsamehe aliyekukosea hata mara saba sabini

Anasemehewa aliyekiri na KUTUBU. Mkapa, pamoja na yote yanayosemwa, hajakiri wala kukanusha hadharani.
 
makanisa wamegeuka vichaka vya mafisadi hapa nnchini. tuwe makini na kauli zao
 
Imeandikwa "huwezi kusema unampenda Mungu usiyemuona huku humpendi binadamu unayemuona."

Huyu fisadi Mkapa leo anasema sasa ni yeye na dini tu na anaongea kwa kunukuu vifungu vya biblia vinavyohusu upendo!! Acha unafiki wewe na usitumie dini kama kichaka. HIVI WEWE UNAELEWA NINI KUHUSU UPENDO?Tubu kwanza kwa watanzania kwa maumivu uliyotusababishia.

Sisi turudishie KIWIRA yetu, Meremeta na rasilimali zetu zingine ulizoIBA then wewe uendelee na hiyo dini yako
 
Anasemehewa aliyekiri na KUTUBU. Mkapa, pamoja na yote yanayosemwa, hajakiri wala kukanusha hadharani.
Wild, unataka mpaka aje kutubu kwako ndio uamini ametubu,Mungu akisha msamehe mtu hakuna mwanadamu wa kupinga. Maana kwenye Biblia anasema hivi HAYA NJOONI TUSEMEZANE ASEMA BWANA DHAMBI ZENU ZIJAPO KUWA NYEKUNDU KAMA BENDERA ZITAKUWA NYEUPE KAMA SUFU, ZIJAPOKUWA NYEKUNDU KAMA DAMU ZITAKUWA NYEUPE KAMA THELUJI.How far are u sure kwamba Che Nkapa haja tubu kwa Mungu wake. Sasa asiye na dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe!!!!!
 
Atubu kwa Mungu wetu, ATUOMBE RADHI Watanzania. Naamini akijitokeza hadharani bila ulinzi mawe atakayotupiwa hayana IDADI!
 
Wild, unataka mpaka aje kutubu kwako ndio uamini ametubu,Mungu akisha msamehe mtu hakuna mwanadamu wa kupinga. Maana kwenye Biblia anasema hivi HAYA NJOONI TUSEMEZANE ASEMA BWANA DHAMBI ZENU ZIJAPO KUWA NYEKUNDU KAMA BENDERA ZITAKUWA NYEUPE KAMA SUFU, ZIJAPOKUWA NYEKUNDU KAMA DAMU ZITAKUWA NYEUPE KAMA THELUJI.How far are u sure kwamba Che Nkapa haja tubu kwa Mungu wake. Sasa asiye na dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe!!!!!

Excellent intervention! suala la ibada ni baina M/mungu na mja wake kama katubu huko whether toba yake imekubaliwa au laa its none of our business...
 
Anasemehewa aliyekiri na KUTUBU. Mkapa, pamoja na yote yanayosemwa, hajakiri wala kukanusha hadharani.

Kweli kabisa.
Inafurahisha kuwa Roho Mtakatifu amemshukia Mkapa. Huu ni wakjati wa yeye kukiri makosa na kutubu. Watanzania ni wema sana, watamwelewa na kumsamehe. nadhini hii itatusaidia kuachana na jambo hili once and for all. Mkapa anatakiwa kuwa na courage ya kukiri hadharani makosa yake na kuomba msamaha. haitakuwa kazi kusamehemwa kwa sababu mema mengi aliyoyafanya yanazidi uzito wa mabaya machache aliyoyatenda, awaombe radhi watanzania
 
Afanye kama Zakayo alivyotubu kwa kurudisha kile alichodulumu kwanza ndiyo amfuate Mungu wake.
 
Uumini wa kweli ama si wakweli ni kati ya mungu na yeye , siyo bubu au mimi tunaoweza kumtenganisha na mungu

Huyu ndiye kiongozi aliyejidai kwamba yeye ni 'utawala bora' tu kumbe huku anafanya biashara ndani ya Ikulu na 'uwazi na ukweli' kumbe anatuficha wizi na ufisadi uliokuwa unaendelea ndani ya serikali ukiwamo wa Rada, EPA, Ndege ya Rais, Helicopters za jeshi na magari, Mgodi wa Kiwira n.k. Hatuwezi kumtenganisha na Mungu na hakuna popote pale nilipoandika hivyo lakini tunajua mtu mwenye dhambi kama yeye za kuwadhulumu mamilioni ya Watanzania utajiri wao kamwe sala zake ni za kifisadi ikiwa hadi hii leo amekataa hata kuongea hadharani chochote kile ambacho kilifanyika ndani ya awamu yake. Anajifanya mcha mungu ili Watanzania tusiendelee kumshinikiza kuhusu mali zetu, na hilo kamwe hatutaliaacha. Asituletee yale ya mapadri wanaojifanya wanamtumikia Mungu kumbe wanatumia nafasi zao za utumishi wa Mungu kulawiti watoto wadogo na kutembea na wake za watu.
 
JAMANI MAFISADI MSIGEUGE NYUMBA ZA IBADA KUWA KIMBILIO LENU TUBUNI KWANZA MADHAMBI YENU NA MRUDISHA MALI ZA WALALA HOI NDIPO MBISHE HODI NYUMBANI MWA BWANA!

......"Siye kila asemaye BWANA BWANA ataona UFALUME WA MBINGU"
 
Hiyo sisi hauituhusu whether una dini, huna hiyo ni ya kwako .... la kwetu sisi ni malizetu ulizotuibia RUDISHA!!!!! WENYEWE TUNAZITAKA

Haitoshi kusihi na kubembeleza kwa woga na kujificha fisadi hili lituridishie kilicho chetu!! Kurudisha hataki!!! Hiyo alishaweka wazi long time yeye pamoja na swahiba wake fisadi Daniel Yona!! SASA NI WAKATI MWAFAKA WENYE MALI WENYEWE WATANZANIA MILIONI 40 TUKAZICHUKUE MALI ZETU!!!
 
Fisadi Rostam Aziz alikimbilia kanisani na kujifanya anatoa msaada ili ajisafishe, huyu naye fisadi Mkapa anajifanya sasa ni mcha mungu baada ya ujambazi mkubwa alioufanya na kutuletea Watanzania wezi wa EPA shilingi bilioni 133, Meremeta shilingi bilioni 155, Rada bilioni 12, hatujui ni kiasi gani kwenye Ndege ya Rais na magari ya jeshi. Kiwira mgodi wetu wwenye thamani ya shilingi bilioni 4 kalipa shilingi 70 milioni tu. Hakuna kumcha mungu wakati hujatubu dhambi zako mbele ya Watanzania wote na kuturudishia mali zetu zote ulizozipata kwa njia ya haramu. Mungu hawezi kupokea maombi yako wakati Taifa la Watanzania milioni 40 linanung'unika kila kukicha kuhusu ufisadi wako
 
Mkapa hamuogopi hata Mungu?

Umekwiba mali za watanzania. Na kutokana wizi huo na ubabe mwingine, maisha ya watu kadhaa yamepotea chini ya dhamana yako.

Sidhani kama mungu wa mkapa ni huyu huyu tunayemwamini sisi. Pengine ana kamungu kake kanakoshabikia ufisadi pia. Maana hata shetani ana mungu wake.
 
Kanisa lipo kwa ajili ya mafisadi,wazinzi,waongo ,wauaji na wafanya mabaya yote.

Waovu ndio walengwa HASWA ,YESU ambaye ni MUNGU Mwana alikuja hapa duniani kwa ajili ya watu mafisadi kama Mkapa Na si kwa wema.

wewe kama unajihisi uko mwema basi KANISANI sio mahala pako subiri siku ya mwisho utapaishwa mbinguni.
 
Jamani mnataka ku monopolise mpaka dini mwenyewe kasema yeye na dini nyie hamtaki tu.. Its too much now
 
Jamani mnataka ku monopolise mpaka dini mwenyewe kasema yeye na dini nyie hamtaki tu.. Its too much now

Dini na mali ya Taifa wapi na wapi?

Mali ya Taifa aliipata akiwa serikalini....Na serikali haina dini.

Dini ya serikali ni sheria za nchi kwa kupitia mahakama.

Na ndio maana ukifunga ndoa ya kiserikali ni mahakamani.

Kweli alisema watanzania ni wajinga na EPA ni halali...Hata wananchi waliandamana kuifagilia hotuba ya Mh Rais.

Wacha washike dini na waendelee kula tu....Kwani ni wazi kuwa wamebarikiwa na Bwana.
 
Back
Top Bottom