Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

baadhi yetu humu baada ya kusikia hizi accusations tulijua tu kwamba hakuna ukweli wowote ndani yake, hivyo sitoshangaa kuona "wanaomuandama mzee mkapa" wakiondoka patupu !

hizi accusations ni part ya ile take over campaign inayofanywa na akina nanihii wakitaka kupaka mavi kila sehemu. but ooh my goooshhh its not working for them.

..jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza tororo!
 
Hivi kwa nini sasa Mkapa na wenzake wanaanza kuongea baada ya kuona kuna tume itaundwa kuchunguza huo uozo wa kiwira ? Nadhani ili ni swali muhimu kujiuliza!

.."ukitaka kumtoa nyoka pangoni..........."
 
Huu ni ujinga, hivi wanafikiri watu wote ni wajinga, wanashindwa kujua kuwa watu wanweza kusoma sheria ya makampuni na kujua kuwa mabadiliko hayawezi kuwa effective mpaka yasajiriwe kwa msajili wa makampuni, ina maana wao walifanya mabadiliko halafu hawakuyasajiri, je katibu wao wa kampuni anafanya nini?

Mkapa watanzania sio wajinga tafuta sababu nyingine as long as tunaona ANNABEN kwenye articles of association wewe ni mmiliki halali kulingana na sheria za nchi na lazima tukusurubu utueleze ukweli kwanini umeiba mgodi wa wananchi.

Kamati itaundwa tu hata kama ukijaribu kuzuia there is no way to turn us back till you return what you owe to tanzanians.

Kada naanza kuquestion credibility yako, nilijua unatetea chama lakini katika hili wewe na sam mmenisikitisha sana au mnalipwa na fisadi mkapa, chama sio watu watu wanaweza kuoza lakini chama kikabaki imara ndo maana nilikuwa na kueshimu sana kwa maana nilikuwa naiona unatetea CCM, lakini within these two weeks umeanza kutetea majina kitu ambacho sio sahihi kwa mawazo yangu.

Mkuu naomba utwambie Cap 212 insemaje kuusiana na kubadilisha article kwenye AOA na mabadiliko yanakuwa effective wakati gani?
 
Jamani alichosema sumaye ni sahihi, serikali ya kikwete haiitaji tathimini kuijua kuwa ni mbovu, karamagi anatembea na mihuri ya serikali mpaka nje ya nchi, RD haipo lakini imepewa tenda ya kuzalisha umeme wakati kazi ya kwanza waliyopewa walishindwa kufanya hata kidogo, mafisadi hawezi kufikishwa mahakamani e.t.c halafu mseme mnataka tathimini, hapa na mimi naungana na Sumaye hamna haja ya kufanya tathimini.
 
Tujue kilichomo na kwa undani ndani ya ripoti ya Bomani maana nasikia imegusiaa..kiwanda hicho......
 
Huu ni ujinga, hivi wanafikiri watu wote ni wajinga, wanashindwa kujua kuwa watu wanweza kusoma sheria ya makampuni na kujua kuwa mabadiliko hayawezi kuwa effective mpaka yasajiriwe kwa msajili wa makampuni, ina maana wao walifanya mabadiliko halafu hawakuyasajiri, je katibu wao wa kampuni anafanya nini?

Mkapa watanzania sio wajinga tafuta sababu nyingine as long as tunaona ANNABEN kwenye articles of association wewe ni mmiliki halali kulingana na sheria za nchi na lazima tukusurubu utueleze ukweli kwanini umeiba mgodi wa wananchi.

Kamati itaundwa tu hata kama ukijaribu kuzuia there is no way to turn us back till you return what you owe to tanzanians.

Kada naanza kuquestion credibility yako, nilijua unatetea chama lakini katika hili wewe na sam mmenisikitisha sana au mnalipwa na fisadi mkapa, chama sio watu watu wanaweza kuoza lakini chama kikabaki imara ndo maana nilikuwa na kueshimu sana kwa maana nilikuwa naiona unatetea CCM, lakini within these two weeks umeanza kutetea majina kitu ambacho sio sahihi kwa mawazo yangu.

Mkuu naomba utwambie Cap 212 insemaje kuusiana na kubadilisha article kwenye AOA na mabadiliko yanakuwa effective wakati gani?

nimekupata, lakini mkuu lazima tuelewe kwamba hadi hivi sasa watu humu wanachonga sana kiasi naona wanataka kuchafua hewa, wanasema mkapa kaoza ufisadi na hafai, lakini cha kushangaza mbona hadi leo sijaona case yoyote pending juu ya mkapa ? au ndio wanataka watujengee imani ili wengi wafuate mkondo ? je kama hawakuwa na facts za uhakika, walishindwa nini kusubiri hadi hapo watakapokuwa na facts kamili then ndio waje na hizo accusations ? maana kinachofanyika hapa sasa hivi ni maneno tu na kila mtu anajifanya anajua yaani wanamtumia mkapa kama product placement ya vyama vyao.

Wakileta data kamili, na facts za uhakika, na tukiona case inafunguliwa then i'll be much willing kuangalia na maybe kuafiki kwamba kweli mkapa ni fisadi na yanayosemwa juu yake ni kweli, but for the mean time AM NOT BUYING IT, NOT EVEN A TINY PIECE OF IT !
 
Ni sahihisho tu la kichwa cha habari... jadili

Kiwira yamsafisha Mkapa
Mwandishi Wetu
Daily News; Sunday,June 01, 2008 @19:01

Uongozi wa Kampuni ya Kiwira Coal and Power Ltd (KCP) inayomiliki mgodi wa Kiwira, umekanusha madai kuwa Rais mstaafu Benjamin Mkapa na mkewe Anna ni miongoni mwa wamiliki wa mgodi huo.

Badala yake, mgodi huo umesema Kampuni ya ANBEN inayomilikiwa na Mkapa na mkewe, ambayo awali ilikuwa sehemu ya Kampuni ya Tanpower, ilijitoa baada ya baadhi ya wanahisa wenzake kuwa na mpango wa kununua mgodi huo.

Mtendaji Mkuu wa KCP, Francis Tabaro, alisema ingawa katika hati za umiliki (Articles of Association) inaonyesha kuwa Mkapa ni sehemu ya Tanpower, lakini baadaye alijitoa.

"Ni kweli ANBEN ilikuwa sehemu ya Tanpower lakini baada ya wazo la kununua Kiwira kuingizwa na wadau wenzake, yeye aligoma akaona aitoe kampuni yake katika Tanpower," alisema Tabaro.

Tabaro pia alikanusha madai kuwa Anna Mkapa aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwira na akaeleza kuwa madai hayo hayana ukweli wowote, kwani kampuni hiyo haihusiani na kiongozi huyo.

Tabaro aliwataja wakurugenzi wa KCP kuwa ni Joseph Mbuna ambaye ni Mwenyekiti, Mafuru M. Mafuru, Wilfred Malkia na Evans Mapundi wakati serikali yenye hisa 15 katika mgodi huo inawakilishwa na Omari Chambo ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Asumpta Ndimbo.

Tabaro alisema upotoshaji unaofanywa na vyombo vya habari kuwa Rais mstaafu Mkapa ni sehemu ya wamiliki wa mgodi huo, hazina ukweli, bali zinalenga kuharibu jina la kampuni ambayo imechukua hatua ya kuendesha mgodi huo.

"Mkapa, mkewe au familia yake si sehemu ya wamiliki wa mgodi huu," alisisitiza huku akionyesha kukerwa na namna alivyodai kuna upotoshaji wa makusudi unaofanywa na vyombo vya habari.

Alisema lengo la kuripoti habari hizo ni kutaka serikali iwe na mtazamo hasi juu ya mgodi huo, hali ambayo inaweza kuzorotesha uzalishaji wa makaa ya mawe. Tabaro pia alisema kitendo cha baadhi ya maofisa wa serikali kutoa maelezo kuwa mgodi huo unachunguzwa kuhusiana na madai kuwa ulichukuliwa isivyo halali na Kampuni ya KCP, kunaweza kukaifanya kampuni hiyo kushindwa kupata fedha za kuendesha mradi huo.

Alisema kampuni yao ina mpango wa kupata fedha kutoka taasisi za benki hivyo mtazamo hasi kutoka kwa maofisa wa serikali utaathiri namna ya upatikanaji wa fedha hizo na wakati mwingine taasisi hizo zinaweza kutoa mkopo kwa masharti magumu kutokana na wasiwasi wa kisiasa.

"Cha kushangaza ni kwamba serikali iko kimya kuhusiana na madai hayo, hali ambayo haionyeshi kutatua tatizo hilo," alisema Tabaro. Akieleza tuhuma za kununua mgodi huo kwa Sh milioni 700 wakati mgodi umejengwa kwa Sh bilioni nne, Tabaro alisema wakati kampuni inanunua mgodi huo ulikuwa chakavu na mashine zake zilikuwa hazifai kuendeleza uzalishaji.

Alisema ndiyo maana KCP imeamua kutumia Sh bilioni 48 kwa ajili ya kuweka mitambo ili angalau mgodi huo uweze kuwa na uwezo wa kuzalisha tani 300,000 kwa mwaka. Wakati KCP inatoa utetezi huo, hivi karibuni Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM), alidai bungeni kuwa mgodi huo ambao ulijengwa na serikali kwa Sh bilioni nne umeuzwa kwa Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona.

Hata hivyo, Tabaro alisema Waziri huyo wa zamani Yona pia si mmoja wa wamiliki wa mgodi huo kama ambavyo inaripotiwa katika vyombo vya habari. Wiki iliyopita, Rais Mstaafu Mkapa akiwa nyumbani kwake Kijiji cha Lupaso wilayani Masasi Mkoa wa Mtwara, alisema tuhuma zote za ufisadi zinazoelekezwa kwake ni za uongo na zinaenezwa na watu ambao walitegemea kupata upendeleo wakati wa utawala wake, lakini hawakupata.

Mkapa ambaye enzi za utawala wake alijulikana kwa falsafa yake ya Uwazi na Ukweli, pia alisema yeye si tajiri, bali anaishi kwa pensheni ya serikali kama mstaafu kama walivyo viongozi wengine.

UWONGO MTUPU NA PROPAGANDA ZA CCM NA SERIKALI!! NAHOJI KWANI NINI HABARI HII ITOLEWE NA GAZETI LA SERIKALI LA "DAILY NEWS" AMBALO MKAPA ALISHAWAHI KUFANYA KAZI NA AMBAKO WAMEJAA VIBARAKA WA MKAPA? MNATAKA KUTUFANYA WATANZANIA MABWEGE SIYO??

SIMPLY PUT: WE AIN'T BUYING ANYTHING FROM DAILY NEWS/UHURU UNLESS "THISDAY" CONFIRMS THESE REPORTS. AFTERALL, IT WAS "THISDAY" WHICH BROUGHT TO THE PUBLIC ATTENTION THESE AND OTHER ALLEGATIONS AGAINST MKAPA (AND NOT UHURU/DAILY NEWS), AND THEREFORE ONLY "THISDAY" SHOULD HAVE THE LAST WORD.
 
Hata mtoto wa chekechea anajua kabisa kwamba mkapa na Kiwira ni watoto wa baba mmoja. Kwa nini huo ungozi wa Kiwira haukukanusha mwaka 2006 huko wakati hii story imevuja? Jee huyu jamaa anaweza kutestify mbele ya bunge?
 
nimekupata, lakini mkuu lazima tuelewe kwamba hadi hivi sasa watu humu wanachonga sana kiasi naona wanataka kuchafua hewa, wanasema mkapa kaoza ufisadi na hafai, lakini cha kushangaza mbona hadi leo sijaona case yoyote pending juu ya mkapa ? au ndio wanataka watujengee imani ili wengi wafuate mkondo ? je kama hawakuwa na facts za uhakika, walishindwa nini kusubiri hadi hapo watakapokuwa na facts kamili then ndio waje na hizo accusations ? maana kinachofanyika hapa sasa hivi ni maneno tu na kila mtu anajifanya anajua yaani wanamtumia mkapa kama product placement ya vyama vyao.

Wakileta data kamili, na facts za uhakika, na tukiona case inafunguliwa then i'll be much willing kuangalia na maybe kuafiki kwamba kweli mkapa ni fisadi na yanayosemwa juu yake ni kweli, but for the mean time AM NOT BUYING IT, NOT EVEN A TINY PIECE OF IT !

Kada ndugu yangu,
kwani Karamangi ni msafi? jee umeona kesi yoyote aginst Karamangi? Jee Rostam azizi? Umeona kesi yoyote against Rostam aziz?

Public judgement ni jambo la kawaida kwa binadamu, either iwe kuhusu Scott Peterson au OJ simposon wananchi watajaji kutokana na facts zao. Sawa na Tanzania ambao majority ya watu including mimi nina imani kabisa asilimi 100% kwamba Mkapa ni mwizi, na mkapa amecripple resources za Tanzania.

I have facts kusopport maamuzi yangu, kwani natazama mambo kama mgodi wa Billion 4 kuuzwa million 700. Japo kuwa mmnunuzi anadai machine zilikuwa chakavu, swala la kwanza jee kwenye swala la natural resources investements tuna analyze asset za aina gani (machine + makaa au)? Jee machine zilikuwa depriciate mpaka kuwa na salvage value ya sifuri? Jee ni muda gani hizo machine zilichukuwa kudepriciate? Jee huo muda ni sawa na time frame ya machine au? Jee serikali ilitumia credential gani kurun analysis zake ambazo zili conclude kwamba mgodi una worth ya 4B. sasa kama wewe unajua maswala ya Investments unaona kabisa maelezo ya KCM manajor haya make sense, then una derive decision kwamba Mkapa ni Jambazi.

Nafahamu mzee Kada unapenda upate data ili ufanya conclusion yako, laki hebu spend few minutes analyze ili swala la Kiwira then utaniambia.
 
Inayonikosha zaidi ni statement hii nyekundu:

Mtendaji Mkuu wa KCP, Francis Tabaro, alisema ingawa katika hati za umiliki (Articles of Association) inaonyesha kuwa Mkapa ni sehemu ya Tanpower, lakini baadaye alijitoa.

Utadhani kuwa Tanzania inajiendesha bila kufuata sheria zozote, hata zile ndogo kama hii ya uandikishaji wa makampuni ya biashara.
 
Hata BEN mwenyewe wakati anaongea kwa jaziba kule kijijini kwake hakutamka kuwa si mali yake badala yake alibakia kuongea uongox10 hivi. Angelikuwa anajua si kati ya wamiliki si ndo angepigilia msumali hapo hapo bila kumungunya maneno?

Anyway ameisha nusa halufu fulani. Ni katika kutafuta pa kushika hila masikini amechelewa saana. Hivyo ni halali yetu tu.
 
Baada ya kwenda Harvard sasa muheshimiwa anajiweka mbali kabisa na baba yake. Sumaye yeye aliona bora ajikatie mashamba ili alime zake. Ben ndio Jasusi au Mafia au KGB. Mwizi Ben
 
Naomba tusaiende mbele sana katika kujadili haya, turudi nyuma kidogo.
Kwa mujibu wa bwana Tabaro, ANBEN ilikuwa sehemu ya Tanpower, sawa. Kwa mujibu wa tabaro huyo huyo, ANBEN inamilikiwa na Mkapa na Mkewe, tumekubali.
Sasa, alipotoa majibu kuhusu TUHUMA zinazomkabili, Mkapa alisema KWA UJUMLA kuwa ni uongo, uongo, uongo, uongo, uogo. Sasa tuanzie hapo.
Kama Tabaro anaaminika, habari kwamba Mkapa na mkewe walianzisha kampuni wakiwa Ikulu zinapata mashiko. lakini Mkapa ameijumuisha tuhuma hii katika fungu la uongo.
Hapa ndipo ninapomtaka Mkapa arudi nyuma na kuanza kuchambua kila kitu. Inavyoonekana si kila kitu kilichosemwa dhidi yake ni uongo kama alivyojibu. Kama anataka kututendea watanzania haki, akae chini, azipitie tuhuma dhidi yake kwa makini, halafu aje atueleze, hata kwa ujumla wake, tuhuma ipi ni kweli na ipi si kweli. Aanze kwanza na hii ya kuanzisha kampuni akiwa Ikulu. najuwa wapo watakaosema kuwa sheria haikatazi, lakini maadili ya viongozi wa umma yametungiwa sheria kwa minajili ya kuzuia vitu kama hivyo.
 
Amaa kweli saa ya kufa nyani miti yote huteleza.. Hata Mr. Zero leo anamkana bosi wake. Mimi nimeshasema kuwa Sala zetu zitashinda tuu. Hatuna majeshi, polisi, mahakama wala Usalama wa CCM, tunaye Mungu. Tutamuomba Mungu awaumbue mmoja mmoja mchana peupeeeee

tuko pamoja mtu wangu.
 
BWM na kiwira ni tako na chupi huwezi kuwatenganisha au tuseme hapo alipiga tiktaka akiwa na tauro
 
Haya Waziri Mtetezi wa mafisadi Mama Simba inabidi uzungumze tena kwamba maneno aliyoyasema aliyekuwa Waziri Mkuu katika sirikali ya fisadi Mkapa nayo ni uzushi mtupu.

huyu mama ni fisadi na mpenda sifa mkubwa kwa viongozi wenzake namjua sana ni mtu wa kujikomba komba sana na sijui anategemea nini kwao na sijui ni kwanini alipewa hiki cheo ila ni jukumu letu wana jf kumtangaza wazi kuwa ni KIONGOZI NA MLINZI WA MAFISADI ili popote akipita naye azomewe "kama ni kupona alipona jk bwana",asituletee uzuri hapa!! maana huyu anataka kukwamisha vita yetu.
 
baadhi yetu humu baada ya kusikia hizi accusations tulijua tu kwamba hakuna ukweli wowote ndani yake, hivyo sitoshangaa kuona "wanaomuandama mzee mkapa" wakiondoka patupu !

hizi accusations ni part ya ile take over campaign inayofanywa na akina nanihii wakitaka kupaka mavi kila sehemu. but ooh my goooshhh its not working for them.

UNAJUA WAKATI MWINGINE KADA MPINZANI HUWA ANAONGEA KINAFIKI. SIDHANI KAMA HUWA HAJUI. MIMI HUWA NAFIKIRI NI MTU WA USALAMA WA TAIFA ANAYETAKA KUPIMA JE WANANCHI WANAJUA UKWELI KWA KIASI GANI?

SASA KWA SISI TUNAOELEWA TUKUELEZE.

TAARIFA YA KAMPUNI YA KIWIRA INASHINDWA KUTOFAUTISHA NAHISI KWA MAKUSUDI KATI YA MWANAHISA NA WAKURUGENZI.

BWANA MBUNA NA WENZAKE NI WAKURUGENZI. BWANA MKAPA NA YONA NI WANAHISA (INGAWA KUNA TETESI KUWA TAYARI MBUNA AND CO. ADVOCATES (KAMPUNI AMBAYO INA UHUSIANO WA KIUKWE NA MKAPA) WAMESHABADILISHA DOCUMENT BRELLA NA KUIONDOA ANBEM NA TANPOWER (ILA TAARIFA NI KWAMBA WATU WA TISS TAYARI WANAZO OFFICIAL DOCUMENTS NDIO MAANA SERIKALI IKO KIMYA).

SASA SWALI KWA KADA MPINZANI NA WENGINE MNAOPINGA.

MZEE MBUNA ANA MTOTO WA KIKE AMEOLEWA NA MTOTO WA MKAPA. HIVI KWELI MZEE MBUNA NA UWAKILI WAKE WOTE HATAWEZA KUMSHAURI MZEE FISADI NAMNA YA KUFICHA SIRI?

SWALI LINGINE. KWA WALE WANAOMJUA HUYU MAFURU MAFURU. HIVI NI KWELI ANAWEZA KUWA DIRECTOR WA KAMPUNI KUBWA YA MABILIONI? (KAMA MNABISHA NENDENI OFISINI KWA MBUNA AU PALE MAHAKAMANI MUMUONE). HANA HATA UCHEMBE WA UDIRECTOR.

SINA LA ZIADA KWA SASA!!
 
Hapo sasa kila mtu atakuja na utetezi wake lakini hili swala la ndege ya rais na ununuzi wa rada mnalionaje wana JF alivyoongea?
 
Back
Top Bottom