Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Haya Waziri Mtetezi wa mafisadi Mama Simba inabidi uzungumze tena kwamba maneno aliyoyasema aliyekuwa Waziri Mkuu katika sirikali ya fisadi Mkapa nayo ni uzushi mtupu.
 
JK, Mkapa atakutesa
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

VYOVYOTE iwavyo, kwa namna kashfa zinazomwandama sasa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, zinavyomchafua, ndivyo pia zinavyomchafua Rais Jakaya Kikwete.

Historia ya kashfa za Mkapa ndiyo inayotufanya tuamini hivyo. Historia hiyo inaonyesha kwamba, Rais Kikwete amekuwa akifuatilia kwa karibu sana tuhuma anazoelekezewa Mkapa, baada ya kauli yake ya kutotaka Mkapa achunguzwe kupingwa na baadhi ya wananchi, wakiwamo wanasiasa wa kambi ya upinzani.

Ukweli ulio dhahiri ni kwamba Kikwete hakuwa na nia ya kumchunguza Mkapa kama alivyokwisha kutamka hapo awali. Lakini amebadilisha msimamo wake kupitia kwa Waziri Mkuu wake, Mizengo Pinda, baada ya kusoma alama za nyakati zinazoonyesha kuwa Watanzania wanataka kujua ukweli kuhusu tuhuma zinazoelekezwa kwa Mkapa.

Pamoja na historia ya kashfa zinazomwandama Mkapa kutusadikisha hivyo, matukio ya hivi karibuni ya Edward Lowassa kujiuzulu, yanaonyesha kuwa Rais Kikwete sasa ametambua kuwa bila kukubaliana na matakwa ya wengi, serikali inaweza kuendelea kuyumba kwa muda mrefu.

Tunaamini kwamba baada ya kamati teule ya Bunge kutangaza ripoti yake iliyokuwa ikimtaja Lowassa pamoja na mawaziri wengine wawili kuhusika katika kashfa ya Richmond, na kufuatiwa na kitendo cha Lowassa kutangaza kuachia ngazi, jambo lililoshangiliwa sana na Watanzania, ni wazi Rais Kikwete sasa amebaini kuwa Watanzania wengi wanamchekea mdomoni na si moyoni.

Tunaamini kuwa kitendo cha Rais Kikwete kujitokeza hadharani mbele ya wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuanza kummwagia sifa Lowassa kuhusu utendaji kazi wake na kumuita shujaa, mtu ambaye kuanguka kwake kulitokana na kashfa ya Richmond, inayoligharimu taifa sh milioni 152 kila siku, ni kitendo ambacho sasa anakijutia.

Zaidi ni kwamba, tunaamini kuwa Rais Kikwete ametambua kuwa katika mazingira ambayo kila mtu anajadili ufisadi, katika mazingira ambayo wananchi wanashangilia kuanguka kwa waziri mkuu wao kwa kashfa ya upotevu wa fedha za umma, Rais anajitokeza na kumtaja mtu huyo kama kiongozi mwadilifu, mzalendo, mwaminifu na mchapa kazi, kumewafanya Watanzania waamini kuwa kilichomwangusha Lowassa alikuwa akikijua.

Kwa sababu hiyo, tunadhani Rais Kikwete amekwisha kutambua jinsi upepo unavyovuma sasa, hivyo atatumia ushawishi wake kumshawishi mtangulizi wake, Mkapa, kuacha kujibu tuhuma zinazomkabiri kwa mkato, jambo linalozidisha hisia mbaya kwa Watanzania.

Tunamwomba Rais Kikwete atambue kuwa ahadi yake kwa Watanzania ya kupambana na rushwa na ufisadi, inafuatiliwa na Watanzania na wataitumia kumhukumu mwaka 2010.

Kwa sababu hiyo, ana kila sababu ya kumshawishi Mkapa kutoa ufafanuzi wa kauli yake aliyoitoa hivi karibuni kijijini kwao Lupaso, ili kuondoa hisia mbaya kwa wananchi kuwa anatoa majibu ya mkato kwa sababu serikali yake inamlinda dhidi ya tuhuma anazoelekezewa.
 
Kashfa hili neno linamaanisha kitu gani ? Ukweli au uongo au nini mbona sielewi au huwa Kashfa halafu ndio unafuata ukweli ? Embu angalieni hapa !

"...VYOVYOTE iwavyo, kwa namna kashfa zinazomwandama sasa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, zinavyomchafua, ndivyo pia zinavyomchafua Rais Jakaya Kikwete..."

Je matumizi ya neo Kashfa yanalingana na hiyoi habari hapo juu ? Nahisi kuna msamiati unaepukwa hapo au wataalam wa lugha mnasemaje , je magazeti yetu yanakosa wataalamu wa kuitumia lugha sanifu mahala pake ?
Pengine wanaona woga kutumia neno ubadhirifu ,au kuvunja sheria maana Mkapa atakuwa amevunja sheria ikiwa ni kosa la mwanzo ,sidhani kama anaweza kuelezwa kama ametumia madaraka yake vibaya labda akihusika na mauaji ya Pemba ambayo kesi yake ipo njiani,zaidi naomba ufafanuzi wa Kashfa na linavyotumika katika kuwakilisha hawa viongozi wanaotuhumiwa na kosa la uhujumu uchumi na wizi wa kuliibia Taifa la Tanzania .
 
Tumzomee Mkapa

Charles Mullinda
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

NINA kila sababu ya kutofautiana na mawazo na misimamo ya watawala wetu, nikiamini kuwa tofauti zetu zitaisadia Tanzania kufika pale ilikokusudia. Nisipotofautiana nao, mimi na wengine kadhaa naamini kwamba watawala wetu hawatatekeleza ahadi yao ya kutupatia maisha bora Watanzania wote.

Wanaweza kutudharau kwa sababu sote tutakuwa tumekubali kufuata kile wanachokitaka wao - hata kama kinadhalilisha utu wetu.

Wa kwanza ninayetofautiana naye ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliyetukataza tusimzomee Benjamin Mkapa, kiongozi wetu mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu, anayetuhumiwa kwa mambo lukuki.

Kisa, eti ana heshima yake katika jamii yetu na kwamba utu wake lazima ulindwe hata kama yeye mwenyewe (Mkapa) hataki kuheshimiwa na jamii wala heshima yake hataki ilindwe.

Sikubaliani na Pinda katika hili na kama atachukia, sitasikitika kwa sababu nadhani nitakuwa sifanyi kosa. Hataki tuendelee kumzomea Mkapa, lakini mimi nadhani tuendelee kumzomea kwa sababu anaonekana anapenda kuzomewa.

Na kama Pinda atazidi kutulazimisha kuacha kumzomea mzee wetu huyu, tugeuze kibao, tumzomee yeye. Najua akizomewa atakasirika (na yeye anajua kuwa hasira hasara), tumwache akasirike kwa sababu hasira hizo zitamfundisha kitu.

Lakini tusifike huko kwenye kumzomea Pinda – ni mapema mno – lakini hapo ni bila kusahau ule msemo anaoujua kaka Pinda kwamba ‘mwenzake mtu fulani akinyolewa, yule anayesubiri kando yake lazima atie maji kichwani ili asije akaja akalalama kuwa wembe unamuumiza'. Tumwache kwanza Pinda hadi atakapoanza kutukorofisha kwa kutuzuia kuonyesha hisia zetu kwa viongozi wetu akiwamo yeye.

Kwa wakati huu sisi tuendelee kumzomea Mkapa hadi siku atakapotueleza ukweli kuhusu madai ya yeye kujitajirisha wakati akiwa ndani ya nyumba yetu takatifu - Ikulu.

Na Mkapa asidhani kwamba tunavyomzomea hatumuheshimu au tunamuonea, la hasha. Tunamzomea kwa sababu sisi tunadhani yeye ndiyo asiyetuheshimu. (Kuna kosa gani baba akiwaheshimu watoto wake! Si kuwaheshimu tu…baba anaweza hata kutaniana na watoto wake; cha ajabu nini? Si anatudharau na hao aliowapisha kuishi katika nyumba yetu takatifu, wanampa kiburi kwamba pamoja na madudu anayodaiwa kuyafanya katika kipindi chake cha uongozi, hakuna atakayemgusa.

Hakuna Mtanzania anayemchukia Mkapa, hivyo ndivyo ninavyoamini, wanachokichukia ni matendo yake yaliyochangia kuwafikisha katika wakati mgumu walio nao sasa.

Watanzania wanachukia wanapomuona Mkapa akionyesha ‘kiburi' cha wazi kwa kutojibu maswali anayopaswa kuyajibu kama kiongozi mstaafu na Mtanzania wa kawaida, anapotakiwa kufanya hivyo.

Wanachukia wanapowasikia watawala wa sasa wakisema Mkapa anapaswa aachwe apumzike, hawataki achunguzwe au ahojiwe kuhusu tuhuma zinazoelekezwa kwake.

Kwa sababu hawawezi kumfikia na kumlazimisha awaeleze kile wanachotaka kusikia kutoka kwake, kwa vile ana ulinzi usiopitika kirahisi, ndiyo maana wanamzomea ili akasirike, avunje ukimya wake, azungumze japo kidogo kuhusu utajiri anaodaiwa kuwa nao.

Kumzomea mtu ni njia mojawapo ya kumfanya azungumze, hivyo tusipomzomea Mkapa ataendelea na tabia yake ya kukimbilia kijijini kwao Lupaso kule wilayani Masasi, na kutoa kauli zisizoridhisha. Lakini kwa sababu anaowaambia ni jamaa zake na anakuwa amewapelekea ‘vijiwazadi' wanakubaliana naye na kumshangilia.

Sote tunakumbuka aliyoyasema hivi karibuni wakati akiwa huko kwao. Kwamba wanaomtuhumu wanafanya hivyo kwa vile aliwanyima vyeo wakati alipokuwa madarakani kwa kipindi cha miaka 10, na kwamba watu wote wanaomuita fisadi ni wa kupuuzwa kwa kuwa wana chuki binafsi naye.

Inawezekana ni kweli. Lakini Watanzania hawakuuliza kama alikuwa akifanya upendeleo kwa baadhi ya watu wakati akiwa Ikulu au la. Watanzania wanachohoji ni, je, Mkapa huyu aliyekingiwa kifua na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kuwa ni msafi na mkweli alifanya biashara wakati akiwa Ikulu? Hilo ndilo analopaswa kulitolea maelezo kinagaubaga kama hataki aendelee kuzomewa.

Na Pinda anapaswa kufahamu kuwa Mkapa anazomewa kwa mengi likiwamo la kumuaibisha Mwalimu Nyerere aliyetembea nchi nzima akimnadi Mkapa kama mtu safi, anayepaswa kuwa kiongozi wa Watanzania, lakini amekuwa kiongozi wa kwanza wa taifa hili kutajwa hadharani kama mtu aliyeichafua sifa ya Ikulu.

Ilielezwa na Mwalimu Nyerere kama Ikulu ni sehemu takatifu. Lakini yeye anadaiwa kuigeuza kuwa pango la walanguzi. Hapa anazomewa kwa kumwangusha Mwalimu.

Wanaomtuhumu Mkapa wanaeleza wazi ushahidi wa yeye kufanya biashara akiwa Ikulu kuwa upo Mamlaka ya Usajili wa Leseni na Biashara (BRELA), Tanesco na katika taasisi nyingine zinazohusika na mambo ya biashara.

Kikubwa anachopaswa kukitolea maelezo kwa Watanzania wote na si kijijini kwake tu ni iwapo yeye na rafiki yake, Daniel Yona, Desemba 2004 walipokuwa wanaitumikia Tanzania kwa nafasi za Rais na Waziri wa Nishati na Madini, walisajili kampuni ya Tanpower Resources, wakiwahusisha pia watoto, wake, wakwe na ndugu zao wengine wa karibu.

Awaeleze Watanzania kuhusu ukweli wa tuhuma hizi, wala asidharau kwa sababu anaweza kusababisha hata mke wake, Anna Mkapa, mtoto wake Nicholaus Mkapa, na baba mkwe wa mtoto wake anayetajwa kwa jina la Evans Mapunda, nao waanze kuzomewa kwa sababu ya kuficha ukweli.

Mkapa ambaye ametoa jibu la jumla kwamba si tajiri kama inavyoelezwa na anaodai kuwa wana kinyongo naye kwa sababu hakuwapendelea alipokuwa Ikulu, anapaswa awaeleze Watanzania kama kweli kampuni na washirika wake walitumia nyadhifa, majina au umaarufu wao kupata leseni ya kuchimba mkaa wa mawe, ili kufua umeme wa kuuza, transmita na vifaa vya kusambaza nishati na usimamizi wa miradi na ushauri wa miradi pia.

(Mimi nashindwa kuelewa mzee mstaafu anaposema hakuwapendelea viongozi fulani alipokuwa Ikulu - anataka ieleweke kuwa alipokuwa akitoa vyeo kwa mawaziri alikuwa anafanya hivyo kama mtu anavyogawa karanga, tena kwa watoto, bila kujali wana uwezo gani - wao bora warushe karanga tu mdomoni?) Tunajua viongozi wote waliopewa vyeo walikuwa watu makini waliostahili kuwa katika nafasi walizokuwa nazo.

Hapana bwana! Mzee wangu toa maelezo kuhusu tuhuma mbaya kabisa za kutumia wadhifa wako wa urais kubinafsisha mradi wa Kiwira Coal Mine na mwaka 2005 miezi michache baada ya kusajiliwa Tanpower Resouces, ikaingia ubia na serikali kununua asilimia 70 za hisa za Kiwira na baadaye kampuni hiyo ikaongeza hisa zake hadi kufikia asilimia 85, huku ikiiachia serikali asilimia 15 tu.

Pia Mkapa asiache kuzungumzia kampuni nyingine anayodaiwa kumiliki yeye na mkewe Anna ya ANBEN. Na bila kusahau atoe maelezo kuhusu madai kwamba waliokuwa wafanyakazi wa mgodi wa Kiwira hawakutendewa haki katika malipo ya mafao yao.

Akishamaliza kuzungumzia hayo, ageukie kwenye sakata la rada anakodaiwa kukataa ushauri wa wataalamu kuhusu ununuzi wa rada iliyogharimu mabilioni ya shilingi za walipa kodi, na ilipofikishwa nchini ikabainika kuwa haikuwa katika kiwango kinachotakiwa cha kufanya kazi.

Aeleze kama ni kweli au si kweli alishauriwa na viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani, viongozi wa taasisi mbalimbali na hata wale wa mataifa ya nje, kuwa Tanzania haikupaswa kununua rada hiyo kwa fedha nyingi kiasi hicho, lakini hakusikia.

Kwa makusudi au kwa sababu anazozijua akakubali kununuliwa rada hiyo na sasa imeibua kashfa kuanzia kwake hadi kwa wasaidizi wake, akiwamo Chenge. Wananchi mnajua kuwa mzee wetu Chenge naye anachunguzwa? Basi habari ndiyo hiyo.

Tuhuma hizo ni nzito kwa sababu ya maisha na ustawi wa Watanzania. Kama Mkapa alikosa aibu akaamua kufanya anayodaiwa kuyafanya, sidhani kama kuna kosa kwa Watanzania nao kukosa aibu na kumzomea, sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kumlazimisha aeleze ukweli anaoujua ili ahukumiwe kulingana na matendo yake.

Na akiwa mjanja, anaweza kuepukana na adha anazokumbana nazo sasa za kuzomewa na kulamizika kutoa maelezo yasiyolingana na upeo wake wa kuelewa mambo.

Aje Dar es Salaam ambako ndiko chimbuko la tuhuma zake, asema alivyohusika, kama hakufanya kabisa au alishawishiwa kufanya hivyo au ‘ibilisi alimpitia' kama binadamu wengine akajikuta anasahau kwamba yeye ni Rais, akafanya biashara akiwa Ikulu.

Na kisha akikubali kuhusika na kashfa hizo kwa namna yoyote ile, aombe radhi kwa matendo yake hayo na kurudisha mali zote alizochuma isivyo halali, wakati wa kipindi chake miaka kumi ya urais.

Akifanya hivyo atakuwa ameokoka kwa sababu Watanzania badala ya kumzomeoa wanaweza kumcheka na wengine kumshangaa kwa kutenda kinyume na walivyotarajia.

Wakishaona amerudisha kilicho chao, watamsamehe kwa sababu hiyo ndiyo jadi yao na ili awe na uhakika na hili aangalie jinsi mafisadi wa mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) wanavyorudisha fedha (kisirisiri) walizoiba kisha wanaendelea kudunda mitaani kama kawaida.

Vinginevyo ajue kuwa ‘kutosikia' kwake na kudharau kila ushauri anaopewa anazidi kujiharibia.

Na kama ataendeleza utamaduni ambao nadhani ameuiga kwa Andrew Chenge na Edward Lowassa wa kukimbilia katika vijiji walikotoka kujitetea, basi Watanzania wasiotoka kijijini kwake wataendelea kumzomea.
 
Kama Sumaye hawezi kutoa tathmini ya serikali hii kwa argument alizotoa kweli hata hiyo Havard anatuzuga tu! Arguments ni za ki - ziro ziro! Kama hataki kutoa tathmini angesema hivyo lakini sio kwa kujenga hoja inayom expose kuwa ni ziro! Otherwise ni vizuri kuwa bubu wameanza kusema! Wameanza kwa kigugumizi - with time watesema sentensi zilizonyooka tu! Na mwisho kabisa wata 'rap'.......and we will dance!
 
Amesema yeye si mtoto wa Mkapa

Frederick T. Sumaye, aliyekua Waziri Mkuu wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kwa miaka kumi, leo amemtolea uvivu bosi wake wa zamani, Ben Mkapa kwa kukataa kumtetea "kwa mambo binafsi" akisema kama ni utendaji wa serikali, anaamini kia mtu anajua serikali ya awamu ya tatu ilifanya kazi nzuri, lakini wapo watu binafsi mmoja mmoja waliofanya makosa na kwa kuwa wanachunguzwa watahukumiwa kwa makosa yao na si serikali nzima.... Akatoa mfano wa ununuzi wa rada, ujenzi wa barabara, ununuzi wa ndege, uwekezaji na mengineyo kuwa ni mambo ambayo yana manufaa kwa taifa, lakini kupitia maamuzi hayo mema wako watu ambao walifanya uhalifu kama vile kula rushwa na kuhujumu uchumi watu ambao alisema wanastahili kuhukumiwa kwa makosa yao binafsi baada ya kuchunguzwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Alipoulizwa kwanini hamtetei Mkapa alisema, "Kama angekua anatuhumiwa kama kiongozi wangu ningemsaidia kujibu, lakini jamani mambo binafsi mimi siwezi kumsemea, Kwani mimi ni mtoto wake?... Si alisema kule Lupaso? Naona hakumridhika,,, mbona hata Bush anaweza kwenda katika ranchi yake kuzungumzia mambo?"

Akasema yeye anajiamini kuwa ni safi mbali ya kuwapo maneno machafu dhidi yake, akirejea sababu ya kuzungumza na waandishi leo, ambako alikua mualikwa katika mkutano wa uongozi wa gazeti la Tanzania LEO (Limekufa) ambao ulifika kumuomba radhi kwa habari yao ya kwamba ana trilioni kumi nje ya nchi na akaunti zake zimezuiwa na JK.

Habari zaidi..... baadaye
Mtu mwingine huyo anawaambia hayo ni mambo binafsi na sio kwa manufaa ya umma. Pinda kasema hivyo, mama simba kasema hivyo na JK alisema asisumbuliwe. Na nyie waandishi wa habari acheni kutuzingua kwa miaka 10 hakuna hata mwandishi mmoja ambaye aliweza one-to-one na Mkapa na akawatukana vile vile hata leo akiwaita waandishi wa habari hakuna hata mmoja ambaye atamuweza.
 
Mtu mwingine huyo anawaambia hayo ni mambo binafsi na sio kwa manufaa ya umma. Pinda kasema hivyo, mama simba kasema hivyo na JK alisema asisumbuliwe. Na nyie waandishi wa habari acheni kutuzingua kwa miaka 10 hakuna hata mwandishi mmoja ambaye aliweza one-to-one na Mkapa na akawatukana vile vile hata leo akiwaita waandishi wa habari hakuna hata mmoja ambaye atamuweza.

Yaani wewe unafurahia fisadi Mkapa kuwatukana waandishi wa habari wa Tanzania!!!!!?
😕😕😕😕😕😕😕
 
huyu alisema anenda kusoma amerka awe uptodates, sasa kuna waliosema kuwa kule marekani alidata sijui kwa mama mmoja, sasa mtajiju
 
Yaani wewe unafurahia fisadi Mkapa kuwatukana waandishi wa habari wa Tanzania!!!!!?
😕😕😕😕😕😕😕

Kwa manasiasa kuwatukana waandishi wa habari ni kitendo cha ushujaa kwani waandishi wa habari wanaweza kukumaliza in a second.
Mimi namshauri Mkapa aitishi mkutano na waandishi wa habari nione mate yatakavyokuwa yanawatoka mdomoni. Wanamshindwa JK watamuweza Mkapa.
 
Kwa manasiasa kuwatukana waandishi wa habari ni kitendo cha ushujaa kwani waandishi wa habari wanaweza kukumaliza in a second.
Mimi namshauri Mkapa aitishi mkutano na waandishi wa habari nione mate yatakavyokuwa yanawatoka mdomoni. Wanamshindwa JK watamuweza Mkapa.

Son, you don't know what you're talking about. I have realized that I am wasting my time. Go back to reload for 2025 maybe you'll be ready by then, but I doubt it.
 
Kwa manasiasa kuwatukana waandishi wa habari ni kitendo cha ushujaa kwani waandishi wa habari wanaweza kukumaliza in a second.
Mimi namshauri Mkapa aitishi mkutano na waandishi wa habari nione mate yatakavyokuwa yanawatoka mdomoni. Wanamshindwa JK watamuweza Mkapa.

Lakini ni kweli ninyi waandishi wa ki tz mbona hamumshambulii JK kwa kumprotect BWM? mnatakiwa kumsema JK na kumsema na kumsema na kumsema mpaka atakapo riaresti hili fisadi. Kama hamna ujasiri wa kumsema huyu basi na mkapa muacheni apete maana ni kawaida ya wa tz
 
Last edited by a moderator:
Na nyie waandishi wa habari acheni kutuzingua kwa miaka 10 hakuna hata mwandishi mmoja ambaye aliweza one-to-one na Mkapa na akawatukana vile vile hata leo akiwaita waandishi wa habari hakuna hata mmoja ambaye atamuweza.

Ukitumia hekima, kwa uamuzi wa Mkapa kuwatukana waandishi, halafu uamuzi wa waandihi kutojibu matusi yake, na sasa Mkapa kushindwa kujiho hoja zilizoibuliwa na waandishi, utabaini nani mwenye busara kati yao
 
sam,
nakubali kuwa BWM akipewa platform ni vigumu kumu-overcome face to face, however u-smart wa kuongea mtu akipewa platform (for this case BWM) hakumfanyi a get away na UFISADI ulio obvious aliuokwisha ufanya.

Yes wakati wa Mwinyi mengi yalisemwa na sio kuwa yamefutika NO, ila information flow ya sasa iko mbele zaidi ya wakati wa Mwinyi.

Ni kweli hajapelekwa ktk vyombo vya sheria kutokana na JK kupiga stop.....everybody knows......."mwacheni mzee apumzike".............now while pple are putting record straight.....mengi yanatokea.....yakiwamo na kuzomewa......wakati wa Mwinyi hili lisingetokea kwani ndio tulikuwa tumetoka tu ktk lindi la siasa za "KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI".........na woga wa watu kutoka vyombo vya dola.

Hivi sasa mpaka wastaafu, Mramba, na wengine wengi tu wananyambuliwa/wanachambuliwa kama karanga.....woga umeanza kuondoka.........na ndio maana leo tunao akina

1.Anna Kilango
2. Mwakyembe
3. Shelukindo na wengine kama hao......(within CCM)

sam,
mapambano ya mageuzi kwa ajili ya manufaa kwa wananchi....unless ni mapinduzi......hayaji kama usiku na mchana..........wananchi huelimishwa.....halafu will ikiwepo, ndipo utakapoona watu kama BWM au washiriki wake......hata wale akina Mama Sitti na dhahabu yetu hatujasahau...........watafika tu ktk mikono ya sheria.................iko siku.......but we have to start somewhere.......wanaosoma nyakati wanaliona hili na wanajiepusha na ZALI LINALOKUJA
 
Ukitumia hekima, kwa uamuzi wa Mkapa kuwatukana waandishi, halafu uamuzi wa waandihi kutojibu matusi yake, na sasa Mkapa kushindwa kujiho hoja zilizoibuliwa na waandishi, utabaini nani mwenye busara kati yao

hata kama mtu una hekima, lakini hiyo hekima haitokuwa active muda wote !
 
whaaaaaaat anasemaje huyu?...............yaani watu tuache kutathmini kwakuwa........eti....nini?.................yaani watu watuingize mikenge ktk mikataba ya hovyo......halafu tusiitathmini hali hiyo.........is this bi-polar dis-oder........or am i dreaming here.......damn!!,

Mtu kakimbilia kusaini mkataba Uingereza....hotelini.......halafu unatuambia niniiii!!!!!

Hii ni attempt ya kumparaphrase Mwinyi bila ya kuwa na uwezo wa Mwinyi katika lugha.
 
jamani eeh kuna watu kule wameanzisha thread ya kutoamini kifo cha ballali and i like the way wanavyoongea utumbo maana kila mtu anakuja na lake, basi naishia kucheka tu bila mpango ! nashauri wengine wakimbilie kwenye ile thread !
 
sam,
nakubali kuwa BWM akipewa platform ni vigumu kumu-overcome face to face, however u-smart wa kuongea mtu akipewa platform (for this case BWM) hakumfanyi a get away na UFISADI ulio obvious aliuokwisha ufanya.

Yes wakati wa Mwinyi mengi yalisemwa na sio kuwa yamefutika NO, ila information flow ya sasa iko mbele zaidi ya wakati wa Mwinyi.

Ni kweli hajapelekwa ktk vyombo vya sheria kutokana na JK kupiga stop.....everybody knows......."mwacheni mzee apumzike".............now while pple are putting record straight.....mengi yanatokea.....yakiwamo na kuzomewa......wakati wa Mwinyi hili lisingetokea kwani ndio tulikuwa tumetoka tu ktk lindi la siasa za "KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI".........na woga wa watu kutoka vyombo vya dola.

Hivi sasa mpaka wastaafu, Mramba, na wengine wengi tu wananyambuliwa/wanachambuliwa kama karanga.....woga umeanza kuondoka.........na ndio maana leo tunao akina

1.Anna Kilango
2. Mwakyembe
3. Shelukindo na wengine kama hao......(within CCM)

sam,
mapambano ya mageuzi kwa ajili ya manufaa kwa wananchi....unless ni mapinduzi......hayaji kama usiku na mchana..........wananchi huelimishwa.....halafu will ikiwepo, ndipo utakapoona watu kama BWM au washiriki wake......hata wale akina Mama Sitti na dhahabu yetu hatujasahau...........watafika tu ktk mikono ya sheria.................iko siku.......but we have to start somewhere.......wanaosoma nyakati wanaliona hili na wanajiepusha na ZALI LINALOKUJA
Una make sense ila nitakucheki kwenye PM.
 
Back
Top Bottom