Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Ukimsikia mtu analia namna hii si bure .Basi mwenye data aanze kutumwagia hapa ili tumjue huyu Sofia Simba ni nani na uwezo wake wa akili ya kawaida ni upi na katokea wapi hadi kuukwaa ukubwa huu .Huyu mama nadhani hajui kwamba tuna haki ya kujua lolote hadi siku aachia madaraka ya Nchi yetu .
 
Dhahiri huyu Mama kaonyesha ujinga wake..yaani unakuja sema maneno kama hayo kwenye matanga?.. as if Mkapa anahusiana na kifo cha Ditopile..jamani heshima ziko wapi siku hizi siasa hadi matangani!
Viongozi wetu jamani ama kweli vichaa watupu!..
Anapotaka watu waje na ushahidi yeye anao ushahidi gani kama sio mambo ya jikoni kuyaleta mahala sipo..UPUMBAVU mtupu, huyu mama nilifikiria zimelala kube naye yale yale...
 
Mama ni hawara wa Kitwana Kondo, ambaye ni rafiki wa karibu sana na muungwana, amesoma Mlimani alishindwa ubunge kwa vitimaalum, halafu akagombea UWT kote alikosa, lakini muungwana akampa ubunge wa bure na uwaziri juu, alichofanya kikubwa ni kwamba zamani alikuwa mshikaji wa karibu sana wa Mama Kilango, kwa hiyo deal zote za kampeni za uchaguzi wa rais alikuwa anazijua kwa karibu sana na kuziuza kwa mtandao, uwaziri ndio malipo yake, lakini pia ni mshikaji wangu wa karibu!

Kuna wakati anakuwa sawa na ansema sense, lakini sio hapa kwenye hili amekosea sana na ndio maana wanakaribisha maneno zaidi wanapojibu namna hii!
 
Huyu Mama naye ni fisadi. Maana yuko mstari wa mbele kuwatetea mafisadi kila kukicha. Hana ushahidi wowote wa kuthibitisha kwamba tuhuma dhidi ya fisadi Mkapa ni uzushi mtupu. Kuna ushahidi chungu nzima ikiwamo bank account ya fisadi Mkapa pale Switzerland. Nyumba Washington, New York, London, Dubai, J'burg na Ottawa. Kujimilikisha KCM katika mazingira ya kifisadi. Kuhusika na ufisadi katika ununuzi wa rada, ndege ya Rais, magari na helicopters za jeshi. Kumiliki nyumba nyingi Dar na sasa Mbeya katika mazingira ya kifisadi. Kwanini huyu fisadi Mkapa asiitishe news conference ili ahojiwe mambo mbali mbali dhidi ya tuhuma za ufisadi alioufanya akiwa Rais? Anajifichaficha migongoni mwa watu. Fisadi Mkapa unajua kuongea, wewe si bubu. Tokeza hadharani ujibu tuhuma dhidi yako badala ya kuwatuma watu wengine waongee kwa niaba yako.
 
Huyu atajuta kusema haya .Nadhani alikuwa hajui JF ni kitu gani .Amuulize Anna Kilango anajua kwamba JF ni namba moja na sasa wacha tule naye .Enhe Mkuu Es unasema huyu si mke wa Iddi Simba ama ni majina tu ? Kuna upwani pia kutumika kumpa uwaziri haya lazia yote yaangaliwe ila JK anasema yeye anawapa nafasi wanawake kama nafasi zenyewe ndiyo hizi basi waache wajifunze kwanza .
 
Naona wadhifa wake kuanzia sasa ujulikane kama Waziri mtetezi wa mafisadi na kazi yake kubwa ni kila kukicha kuwatetea mafisadi kwamba tuhuma dhidi yao ni uzushi mtupu.
 
Kinachosikitisha ni kwamba huyu ni waziri wa usalama wa taifa! Hapana mkuu huyu sio mke wa Simba, na pia ana mtoto wake mmoja ni jambazi la hatari sana amefungwa US longtime, na hatakuja kutoka karibuni!
 
Mama ni hawara wa Kitwana Kondo, ambaye ni rafiki wa karibu sana na muungwana, amesoma Mlimani alishindwa ubunge kwa vitimaalum, halafu akagombea UWT kote alikosa, lakini muungwana akampa ubunge wa bure na uwaziri juu, alichofanya kikubwa ni kwamba zamani alikuwa mshikaji wa karibu sana wa Mama Kilango, kwa hiyo deal zote za kampeni za uchaguzi wa rais alikuwa anazijua kwa karibu sana na kuziuza kwa mtandao, uwaziri ndio malipo yake, lakini pia ni mshikaji wangu wa karibu!

Kuna wakati anakuwa sawa na ansema sense, lakini sio hapa kwenye hili amekosea sana na ndio maana wanakaribisha maneno zaidi wanapojibu namna hii!

Hapa umemaliza kila kitu huyu ni mbumbumbu tu. Fadhilaka udaka.
 
Posted Date::5/31/2008
Kashfa zaanza kumtikisa Rais wa zamani Benjamin Mkapa

Na Mwandishi Wetu
Mwananchi

KITENDO cha Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa kusimama hadharani kuzungumzia kashfa zinazomkabali za kufanya biashara akiwa Ikulu, ni wazi sasa zimeyeyusha ujasiri wake na kuanza kumtingisha.

Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa, kuibuka upya kwa kashfa hizo sasa kumeanza kumsumbua Mkapa kiasi kwamba, ameamua kuanza jitihada za kujisafisha.

Hata hivyo, wachunguzi wa masuala ya siasa wanasema, hatua hiyo ya Mkapa haitaweza kumsaidia na kwamba, alitakiwa kujisafisha mapema akiwa Ikulu.

Wanasema kuwa, kushindwa kujisafisha mapema wakati akiwa madarakani ilikuwa ni dalili kuwa alikuwa akiwadharau wananchi na sasa kuibuka na kujibu tuhuma hizo, kunaonyesha kwamba, hana uhakika wa kubaki salama kutokana na tuhuma hizo.

Hata hivyo, wachambuzi wanakiona kitendo cha Mkapa kuhudhuria hitima ya Mkuu wa zamani wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzururi katika Ukumbi wa Dimond Jubilee wiki hii kama ishara kwamba, sasa huenda ameaanza kujichanganya na wananchi, baada ya kukaa kando kwa muda kusubiri huruma yao.

Tangu kuibuka upya kwa kashfa za ufisadi, alikuwa haonekani katika shughuli mbalimbali za kitaifa, hali ambayo ilitafsiriwa na wananchi kwamba, alikuwa akijificha kutokana na kashfa hizo.

Ingawa alivunja ukimya wake wiki hii kwa kujibu tuhuma hizo, huko nyuma aliwahi kuulizwa na kukataa kuzijibu akidai kwamba, amestaafu siasa hivyo hawezi tena kuzungumza.

Mkapa hakuonekana kijijini Butiama, mkoani Mara wakati wa vikao vya Kamati KUU (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Machi 20 hadi 30 na pia hakuonekana wakati wa Sherehe za Muungano zilizofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Pia hakuwepo katika Sherehe za Uhuru, Desemba mwaka jana.

Ukweli wa jambo hilo unathibitishwa na utetezi alioutoa, ambao umepokelewa na jamii kuwa ni dhaifu, kwamba tuhuma dhidi yake ni za uongo.

Hoja kwamba, wanaoshabikia au kukuza tuhuma dhidi yake ni watu ambao alikataa kuwapendelea katika utawala wake kwa kuwapatia vyeo ni dhaifu, ambayo bado haijawapa wananchi majibu ya kuridhisha.

Wananchi wanataka kujua ilikuwaje Mkapa na mkewe mwaka 1999 wakaanzisha Kampuni ya ANBEN akiwa Ikulu, ambayo anadaiwa kuitumia kukopea dola za Marekani nusu milioni kutoka benki wakati huo akiwa Ikulu na akaweza kuzirejesha katika kipindi cha mwaka mmoja.

Shutuma nyingine za Mkapa ambazo hakuweza kuzitolea majibu ni kashfa ya ununuzi wa rada ya kijeshi wenye utata, ambao unaendelea kuchunguzwa na Taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) ya Uingereza.

Wananchi wanataka kupata maelezo ya Mkapa, mazingira yaliyomfanya akafikia mahali akageuka mjasiriamali, akaanzisha kampuni yake na mkewe wakiwa bado ikulu na kashfa niyingine zilizofanyika ndani ya utawala wake.

Mkapa pia anadaiwa kuanzisha Kampuni ya Tanpower kwa kushirikiana na mkewe, Anna, mtoto wake Nicolas na mkwe wa mtoto wake pamoja na Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona na kujimilikisha mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, mkoani Mbeya.

Inadaiwa walimilikishwa mgodi huo kwa gharama ya Sh 700 milioni kinyume na thamani halisi ya zaidi ya Sh 4 bilioni bila zabuni kutangazwa na kuwashindanisha waombaji. Inadaiwa kuwa hadi sasa wamelipa kiasi kidogo cha Sh 70 milioni tu.

Wengi wanasema Mkapa katika maelezo yake alitakiwa kuwataja kwa majina, waliotaka awape vyeo au upendeleo wowote kama wa biashara au fadhila nyingine.

Licha ya Mkapa kujisafisha kwa kutumia kauli ya jumla jumla kuwa anapakaziwa na wabaya wake wa kisiasa, lakini wakati wa utawala wake, aliwajumuisha marafiki wake wa siku nyingi katika serikali yake na walikuwa na ushawishi mkubwa katika mambo nyeti ya kitaifa.

Miongoni mwao kwa kutaja wachache ni Frederick Sumaye, ambaye alishikilia uwaziri mkuu kwa mihula yote miwili; marehemu Abdallah Ngororo, aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais; Andrew Chenge, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Dk Hassy Kitine, aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora).

Washirika wengine wa Mkapa aliowajumuisha katika serikalini yake ni Mateo Qares, ambaye alishikilia nyadhifa za Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Baraza la Mawaziri), Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya; Profesa Simon Mbilinyi, aliyekuwa waziri wa Fedha; Hassan Ngwilizi, aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI); marehemu Daud Balali, aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na aliyekuwa Waziri wa Mipango na Ubinafsishaji, Dk Abdallah Kigoda.
 
Kabana mpaka mwisho kachomoa, lazima awaeleze watanzania mali alinazo amezipata vipi, mambo ya kuongelea kwenye misiba na makanisani hatutaki, haitishe mkutano na wana habari hawaruhusu waulize maswali. Nafikiri mojawapo ya maswali litakuwa la kwanini kaamua kuongea sasa baada ya balali kutangazwa kuwa amefariki na hakuongea wakati bado yuko hai?
 
Halafu baadhi wanadai eti hatuwezi kumfanya chochote fisadi Mkapa eti kwa kuwa katiba inamlinda!!!! Katiba ya Tanzania haikutungwa ili iwalinde wale viongozi mafisadi wanaoifisadi Tanzania na Watanzania. Na sasa hivi kuna kauli chungu nzima zilizotolewa na watu mbali mbali waliowahi kushika nyadhifa za juu Tanzania akiwemo aliyewahi kuwa Jaji Mkuu na Waziri Mkuu wa Tanzania Jaji Sinde Warioba. Taratibu tutawashinda tu mafisadi. Kwanini nchi yenye watu 40 millioni iwaogope mafisadi ambao idadi yao haifikii hata elfu moja.

Kwa nini mafisadi waendelee kuwa matajiri wakubwa kwa kutumia njia za haramu huku Watanzania chungu nzima wakiishi katika dhiki kubwa, mashule yetu hayana madarasa na madawati, mahospitali yetu hayana madawa, vitanda na vifaa vya kisasa, upatikanaji wa maji safi bado ni nadra kwa Watanzania walio wengi, umeme haujawafikia Watanzania walio wengi na wale uliowafikia wengi wanashindwa gharama kubwa za kutumia umeme huo jambo ambalo limesababisshwa na mikataba mibovu ya IPTL, RIchmond, Net group, songo songo. Tutapambana na mafisadi mpaka tuwashinde.
 
hivi huyu mama waziri mzima hana PR?

Huyu mama anachofanya ndio job description ya Minister of Propaganda!

Kikwete ndio amem recruit huko, akampa ubunge, akampa uwaziri, akampa kuwa Minister of Propaganda!

Mama Simba anasaidia kumuelewa zaidi Kikwete kuliko yeye Simba mwenyewe.

Kikwete ndio fisadi wa kwanza hapa, kwa sababu anateua Minister of Propaganda kutetea ufisadi!

Vingine hivi ni vinyampara tu!
 
jamani huyu mama mimi huwa ananichosha kabisa...

kama uwaziri ndio huu, basi, mimi lazima naweza kuwa president...

alisoma shule gani...? huo mwaka lazima mitihani ilibiwa...!

Atamfuata Chenge wakati wowote kuanzia sasa.!
 
Huyu Mama naye ni fisadi. Maana yuko mstari wa mbele kuwatetea mafisadi kila kukicha. Hana ushahidi wowote wa kuthibitisha kwamba tuhuma dhidi ya fisadi Mkapa ni uzushi mtupu. Kuna ushahidi chungu nzima ikiwamo bank account ya fisadi Mkapa pale Switzerland. Nyumba Washington, New York, London, Dubai, J'burg na Ottawa. Kujimilikisha KCM katika mazingira ya kifisadi. Kuhusika na ufisadi katika ununuzi wa rada, ndege ya Rais, magari na helicopters za jeshi. Kumiliki nyumba nyingi Dar na sasa Mbeya katika mazingira ya kifisadi. Kwanini huyu fisadi Mkapa asiitishe news conference ili ahojiwe mambo mbali mbali dhidi ya tuhuma za ufisadi alioufanya akiwa Rais? Anajifichaficha migongoni mwa watu. Fisadi Mkapa unajua kuongea, wewe si bubu. Tokeza hadharani ujibu tuhuma dhidi yako badala ya kuwatuma watu wengine waongee kwa niaba yako.

This makes me sad when I read this.
Hivi kama una proof, kwanini usimburuze mahakamani? Why cant people do that?
Kwanini aje mbele yako ajishitaki?
 
Kinachosikitisha ni kwamba huyu ni waziri wa usalama wa taifa! Hapana mkuu huyu sio mke wa Simba, na pia ana mtoto wake mmoja ni jambazi la hatari sana amefungwa US longtime, na hatakuja kutoka karibuni!

Mkuu Es mimi bado niko nawe ama tuseme kwa PM maana nyeti za huyu Mama na kuropoka kwake kunanifanya nichanganyikiwe .Huyu ndiye boss wale RO kweli kuna usalama tena ? Huyu si ndiye alikuwa kidogo apate kichaa lakini bado akawa anaomba kupata kura za NEC na kweli kapata, hivi huko CCM huwa wanapigaje kura ?
 
Hivi kama hizi shutuma si za kweli kwa nini Mkapa au huyo bi Sofi wasiitishe press conference wakatoa maelezo ya kina ya ni nini uzushi na wapi Mkapa anasingiziwa. Ushari kwa be Sofi " Better remmain silent and be thought you are a fool than opening your mouth and remove all doubt"

Kwa mwendo huu maisha bora kwa kila mtanzania hata baada ya miaka mia ni ndoto!!!!!!

Badala ya Waziri kumtaka mwenye ushahidi ampeleke Mkapa mahakamani, kwa nini hamshauri Mkapa kuwapeleka wanao mshutumu mahakamani, ikiwa anasingiziwa kama anavyodai?

Inasikitisha na kukasirisha kumsikia Waziri wa Utawala Bora anasema sema hovyo namna hii, tena hitimani.
 
Ukimsikia mtu analia namna hii si bure .Basi mwenye data aanze kutumwagia hapa ili tumjue huyu Sofia Simba ni nani na uwezo wake wa akili ya kawaida ni upi na katokea wapi hadi kuukwaa ukubwa huu .Huyu mama nadhani hajui kwamba tuna haki ya kujua lolote hadi siku aachia madaraka ya Nchi yetu .

EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
University of Zimbabwe Post Graduate Diploma in Women's Law 1996 1996 POSTGRADUATE
University of Dar es Salaam LLB 1987 1991 GRADUATE
MekanForbidant College-Sweden Information Studies 1982 1982 CERTIFICATE
University of Dar es Salaam Certificate in Law 1982 1983 CERTIFICATE
NBC Secretarial College Certificate in Secretarial Training 1970 1971 CERTIFICATE
Kibosho Secondary School O-Level Education 1968 1969 SECONDARY
Forest Hill Secondary School O-Level Education 1966 1968 SECONDARY
Ilonga Middle School Middle Education 1961 1964 PRIMARY
Kilakala Primary School Primary Education 1957 1960 PRIMARY

--------------------------------------------------------------------------------
CERTIFICATIONS
Certification Name or Type Certification No. Issued Expires
No items on list

--------------------------------------------------------------------------------
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From Date To Date
Ministry of Community Development, Gender & Children Minister 2006 2/8/2008
President's Office - Good Governance Minister 2/13/2008
Dar es Salaam City Council Councilor 1994 1996
Metal Engineering Industries Development Organization (MEIDA) Legal & Administrative Officer 1992 1997
Metal Engineering Industries Development Organization (MEIDA) Administrative Officer 1983 1992
TANTRUST Personal Secretary 1979
UWT-NDC Branch Chairman 1974 1979
National Development Coorporation (NDC) Personal Secretary 1971 1978

--------------------------------------------------------------------------------
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of Parliament of Tanzania 1995 Todate
Union of Women Tanzania - UWT Chairman(Upanga West branch)) 1994
Chama Cha Mapinduzi - CCM Councilor 1993 1996
Union of Women Tanzania - UWT Secretary (UWT-NDC branch) 1973
Chama Cha Mapinduzi - CCM Member of the board(NDC Branch-CCM) 1973

PUBLICATIONS
Description
Published Date
No items on list

--------------------------------------------------------------------------------
SPECIAL SKILLS
Skill Name or Description Years Experience Acquired Through Skill Level
No items on list

Source: http://www.parliament.go.tz/bunge/Mp...rname=GUEST")

KILICHONIFURAHISHA KWENYE CV YAKE NI KIPENGELE CHA SPECIAL SKILLS...IMEJAZWA NO ITEMS ON THE LIST. DA KWELI MAFISADI HAWATAISHA HAKI YA MAMA VILE NA NDIO YUPO OFISI YA RAISI JAMANI DUUU.
__________________
 
Dhahiri huyu Mama kaonyesha ujinga wake..yaani unakuja sema maneno kama hayo kwenye matanga?.. as if Mkapa anahusiana na kifo cha Ditopile..jamani heshima ziko wapi siku hizi siasa hadi matangani!
Viongozi wetu jamani ama kweli vichaa watupu!..

Media ya Bongo jamani haitutendei haki kabisa. Kama walikuwepo ukumbini ilibidi watuambie ishu za ufisadi wa Mkapa ziliibuka ibuka vipi msibani? Hii media gani jamani inashindwa hata kuripoti ilicho kiona?

Utetezi wa ufisadi wa Mkapa huyu Simba kauleta leta vipi msibani? Alitoa kispichi au aliulizwa swali, au Mkapa alitoa bakshishi ya Matanga ikabidi watu waanze kujikomba komba au ilikuwaje? Duuuh, Bongo sijapata ona!
 
Back
Top Bottom