Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Hizo tetesi pia zina sikika na kule kwenye kiwanda cha sukari turiani. ila yeye na sumaye wana mashamba makubwa sana ya miwa tuna yako barabarani kabisa kama unaelekea turiani (hii ya mashamba si tetesi)
Mengi tutayajua. Tena kafanya vema kufungua kinywa!
 
Chenge-nasingiziwa,

karamagi- sio hivyo nasingiziwa,

Lowassa- magazeti ya udaku, mnanisingizia, I will grant your wish

Msabaha-mnanisingizia, mi ni bangusilo

Yona- olewake mtu atakayenipeleka mahakamani

Mkapa-uongo …uongo ….uongo ….uongo …uongo….uongo….uongo

Meghji-Nimegundua kuwa Balali alinidanganya

Mramba.............................

kazi kweli......
 
Kwanza tunatakiwa kufahamu neno kusingiziwa alipoliongea Mheshimiwa Rais Mstaafu Mjasiliamali alikuwa anamaanisha nini! Wataalamu wa Kiswahili tunaomba mtupe ufahamu.

Tanzania tumekithiri kwa kuwa na viongozi ambao mara wawapo madarakani wanaamua kuwekeza katika 'illiteracy' level ya Watanzania kwa ujumla wakisahau kwamba sasa tumefumbuka macho.

Hivi ni lini tutaanza kuwafunga hawa na kuwaadhibu kama inavyotakiwa?
 
Kwanza tunatakiwa kufahamu neno kusingiziwa alipoliongea Mheshimiwa Rais Mstaafu Mjasiliamali alikuwa anamaanisha nini!

Kiswahili ni lugha pana sana.....Hasa ikichanganywa na siasa....Sawa muheshimiwa mjasirimali kasingiziwa.....Yeye ni raia huru hivi sasa. Angetumia masaa yake mawili matatu kutoka katika ratiba yake tight na kukaa pale ukumbi wa habari, na kumwaga data. Nina imani anasikia "Shutuma" zinazomkabili. Apinge moja baada ya jingine, kwa sharti moja lakini, akubali kuulizwa maswali na ayajibu, mbona nitakuwepo!!
 
Swali ambalo najiuliza mpaka ni kwa nini huyu Tuni Tuni aanze kuongea BAADA ya kifo cha Balali?Pili nianasema akuwa anasingiziwa,je ile kampuni ya ANBEM & Kiwira ni nani wanaimiliki?

Sasa kila mtu kasingiziwa kuanzia Chenge,marehemu Balali,Lowassa,Karamagi,Rostam,Mramba,Mgonja,etc...basi watuambie kina nani wanaowasingizia au watueleze ni kina nani basi walisababisha hasara ya mabilioni ya shilingi zetu...na pia huyu Tuni Tuni anasema watu ambao hakuwapa upendeleo ndio wanomchafua ni kina nani sasa?

Huyu bwana nilifikiri angeongea sense kumbe utumbo mtupu,ndo maana ameamua kunyamaza.
 
Mimi naweza kumuunga mkono kwamba kasingiziwa, maana hivyo vyote ni vijisenti na yeye hakumlazimisha mtu kumpa nyumba wala kumjengea na hako kabiashara alikuwa anawasaidia Kiwira maana walikwisha kukwama hata kulipana mishahara, maana Kiwira ilikua ikimhitaji Mkapa kuliko yeye alivyokua akiihitaji!!!! Kwanza munamsingizia maana yeye ni Mzalendo, mbona hamuwasemi wale Wahindi wanaotajrika na kuchukua mali zetu?

Nahisi Mkapa anasema haya:
"Yaani mimi niliyewekwa na MWalimu akafa nikaona nijichukulie japo vijisenti vya kujipatia ulabu na kucheza kamari munaniona tajiri!!! Sasa mukiona mali anazomiliki mama watoto!! Si mutazimia!!! Je, mukiona jinsi kijana wetu yule niliyemrithi kwa mzee wa Mlimani (BPM-Mzee wa kulam nyasi) anavyojiuzia mali za TTCL si mungelia machozi!???"
 
Naombeni msaada, hivi hii habari ya kiwira imeshaundiwa tume au ndo itakuwepo ndani ya repoet ya madini?? au ndo itachunguzwa toka tamko la Pinda alililitoa kuwa hizo shutma zote zitachunguzwa???
 
Sijui na huyu Kikwete naye anfanya nini hapo Ikulu grrrrrrrrrrrrr!!!!!

watu wazima wanaiba Ikulu mchana kweupe halafu yanaenda yakitamba mitaani kuwa yanasingiziwa
grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr!!!
 
Naombeni msaada, hivi hii habari ya kiwira imeshaundiwa tume au ndo itakuwepo ndani ya repoet ya madini?? au ndo itachunguzwa toka tamko la Pinda alililitoa kuwa hizo shutma zote zitachunguzwa???

Tuandamane,

Hii issue ya Kiwira ni skandali nyingine inapikwa taratibu na itakuwa inajitegemea. Linakuja moja baada ya jingine mpaka wananchi wachoke kabisa na kinachoendelea huko serikalini.
 
Tume ya nini? Suala la Kiwira linaweza kuwekwa wazi bila ya kuwa na tume. Kinachihitajika ni hiki:
1. Kwenda Brela/Wizara ya Nishati na Madini kuangalia nyaraka za umiliki wa mgodi huu.
2. Kama ni kweli Mkapa ndio mmiliki, Je, alifanya hivyo akiwa madarakani? Muda aliokaa madarakani tunaujua.
3. Je taratibu za manunuzi zilifuatwa?

Sasa maswali haya matatu yanahitaji tume kweli au ni njia nyingine za ubadhirifu wa fedha za umma?

Mkuu Dotori upo sahihi kabisa nakuunga mkono LAKINI ni nani atakaye tekeleza hilo? maafisa wanaohusika hawapo tayari na Watawala wetu hawapo tayari. Ni kheri Bunge likaendeleza agenda iliyoanzishwa na Mhe. Kimaro.
 
Tunaenda Mbele hatua mbili tunarudi nyuma hatua tatu... Tume tumeeee tumeeee za nini? Nini hakiko wazi hapo
 
Tuandamane,

Hii issue ya Kiwira ni skandali nyingine inapikwa taratibu na itakuwa inajitegemea. Linakuja moja baada ya jingine mpaka wananchi wachoke kabisa na kinachoendelea huko serikalini.

Halafu mwisho kabisa hata baada ya kuichoka serikali yao bado ni CCm ndo inashinda uchaguzi, sijui nini kifanywe hapa
 
Nimefurahi sana kwa huyu bwana kuanza kusema. Sasa hana kisingizio tena cha kukataa kusema eti amestaafu. Ameamua kusema na sasa ajibu hoja zote zilizo mbele yake.
1. Kampuni anazomiliki hati zake ziko kwa msajili - hilo halina ubishi
2. Kwamba kampuni alizianzisha wakati akiwa ikulu, halina ubishi maana tarehe alizoingia ikulu na kutoka na tarehe alipoadikisha hizo kampuni zinajulikana.
Sasa hapa anakanusha vipi.
Kuna maswali ya kujiuliza hapa
a. Kwa nini ametafuta soft target ya kujitakasia. Wanakijiji yawezekana hawajui hizo kampuni zake - si angewaita waadishi wa habari ili nao wamuulize maswali?
b. Kwa nini amesubiri mpaka Balali amekufa ndipo naye anajitokeza kusema?
 
Unajua siku zote ss ni wadanganyika tu tume zinaundwa hakuna hatua zinazochukuliwa sasa hivi kama kiongozi kala mihela amekula rushwa migodini huko ni kumrestisha in peace tu...saizi nikufanya ka China watu hawa nikupoteza kabisa duniani,,,,hii ndio dawa sasa hivi.
 
Nimefurahi sana kwa huyu bwana kuanza kusema. Sasa hana kisingizio tena cha kukataa kusema eti amestaafu. Ameamua kusema na sasa ajibu hoja zote zilizo mbele yake.
1. Kampuni anazomiliki hati zake ziko kwa msajili - hilo halina ubishi
2. Kwamba kampuni alizianzisha wakati akiwa ikulu, halina ubishi maana tarehe alizoingia ikulu na kutoka na tarehe alipoadikisha hizo kampuni zinajulikana.
Sasa hapa anakanusha vipi.
Kuna maswali ya kujiuliza hapa
a. Kwa nini ametafuta soft target ya kujitakasia. Wanakijiji yawezekana hawajui hizo kampuni zake - si angewaita waadishi wa habari ili nao wamuulize maswali?
b. Kwa nini amesubiri mpaka Balali amekufa ndipo naye anajitokeza kusema?


Sasa ndo nimesikia Andrew Mkapa yuko Brela hizo, hati zitakuwa bado ziko salama kweli???
 
kwa nn kaongelea kwa wanakijiji wasio jua kuhoji maswali???na kwa nn ajibu tuhuma akiwa BUsh.........

Mkapa ataitoa nishai vibaya mno hiyo Press yenu ya Bongo wakikutana mjini.

Hizi shutuma hazikuanza juzi wakati Mkapa kawa Bubu. Mkapa amewahi kukutuna na Press mara kibao, mbona hawajaweza kum-bana? Wana habari Bongo simply hawana kende za kumuuliza Mkapa probing questions.

Unless, Press waje na mawakili kusaidia kuuliza maswali. Hapo sasa, na yeye atakuja na Mkono.

Mkapa aongee asiongee haileti tofauti yoyote, aidha kwenye press conference Da-es-Salaam mjini au uani kwa Mama yake mzazi "Bushi" kwao huko.

Hatutaki maelezo!
 
Tuandamane,

kuna mafile ya baadhi ya makampuni kwa sasa hutayakuta BRELA kwani yamechukuliwa na taasisi mbali mbali kwa "uchunguzi" ikiwemo PCCB,Ijumaa iliyopita nilikwenda pale kukagua (wao huita "official search") kampuni fulani (jina kapuni) kwa ajili ya kufanya mambo ya kibiashara, sasa nilipopeleka jina la kampuni hiyo nikaambiwa PCCB walikwisha lichukua muda kitambo...yawezekana huu ukawa upenyo pia wa "kupoteza" baadhi ya mafile kwa kisingizo cha kufanyiwa uchunguzi...tuvute subira tu tuone mwisho wa filamu hii...
 
Jamani hivi kama tunaweza kuchangia harusi Tshs.32million tunashindwa kuchangia Tshs.70million alizolipa mkapa na yona kwa kiwira?
 
its not about kuchangia milioni 70.
kama mkapa na yona walijiuzia mgodi kwa pesa hizo na wao wanalipwa kila siku milioni kadhaa, basi wao ndio wanapaswa kuturudishia sisi wananchi pesa na riba!
haiwezikani kiongozi avunje maadili ya uongozi 100 ya 100 ikisha tuambiwe tuchange tumrudishie!
 
Back
Top Bottom