Bila shaka hao maaskofu walifurahi sana na vigelegele chungu nzima juu yake mkuu 'Steven'.Leo kanisani asubuhi Dr Mpango kakabidhi shilingi milioni 20 kule Bagamoyo kwa ajili ya mafuta ya gari la Baba Askofu Msomba.
Ni pesa aliyotumwa na Dr Samia aikabidhi kwa kanisa. Serikali yenye mbinu za hadharani pia inazo chafu za gizani.
Hata hivyo inashangaza kidogo kwamba unasahau kuwa hongo hii siyo ya kwanza kwa hawa viongozi wa dini, au hukumbuki?
Lakini hilo tuliache pembeni, mkuu wangu. Lakini nashangaa sana kwa mtu kama wewe kuandika hayo hapo juu. Yaani hilo limekugusa sana hadi ukaona ni muhimu ulilete humu? Hiyo milioni 20 inaweza kufuta maumivu ya aliyeumizwa. Hiyo milioni 20 unaamini ndiyo bei halisi ya hawa watu kuwanyamazisha?
Sikumbuki kilitolewa kiasi gani kule kwa Marehemu Mzee Kibao. umepata mrejesho wowote kuwa kiasi hicho ndicho kimewafuta machozi ya uchungu waliompoteza mzee wao?
Lakini hata huwezi kutambua 'implications' za maswala kama haya kwa taifa zima! Yaani nyinyi mmekuwa ni viongozi wa kununua utu wa waTanzania, kweli? Mna hakika hii ndiyo njia sahihi na ya kibinaadam ya kumaliza matatizo makubwa yanayolikabiri taifa hili kwa sasa? Huu ndio uongozi mnaoujuwa?
Haya, nasubiri kusikia kule kwa Mdude Nyagali kitatolewa kiasi gani; na kwa hao wengine wote wanaoendelea kuvunjiwa HAKI zao zitanunuliwa kwa kiasi gani.
Hizi hela zinatoka wapi, ni za walipa kodi, au ni zile toka kwa wajomba Oman na kwingineko?
Mkuu 'Stene', ulipo anza humu JF kidogo ulikuwa tofauti, sasa naona hali imekuwa nyingine kabisa!