Mkakati wa Kuingiza Nchi Kwenye Machafuko

Mkakati wa Kuingiza Nchi Kwenye Machafuko

Nchi yetu hii kuna kigenge wanajiona wao ni wazalendo zaidi kuliko wengine, wakati kiuhalisia ni matapeli tu
 
Jambo hili sio jepesi kulisema lakini hakuna budi lisemwe bila kupindisha maneno. Viongozi wa CHADEMA wanataka vurugu na machafuko yaliyotokea Kenya na maeneo mengine duniani yatokee nchini kwetu kama njia ya kuzuia au kuvuruga uchaguzi.

Baada ya Fr Kitima, Katibu wa Baraza la Maaskofu (TEC) kujeruhiwa, jana Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Ndugu Godbless Lema, ameandika kuwataka Maaskofu watoe tamko ili waumini wao wasusie uchaguzi.

Pia, Ndugu Godlisen Malisa ambaye ni mwanachama wa CHADEMA ameandika kwenye ukurasa wake wa instagram akimtaka Askofu Mkuu wa KKKT atoe tamko. Wafuasi wake wamemshambulia sana Askofu Malasusa kwa kila aina ya matusi bila yeye kuchukua hatua zozote.

Naye Bi. Maria Sarungi, shabiki na mshirika wa karibu wa Tundu Lissu aliyeko nchini Kenya akiratibu na kuhamasisha matukio haya kwa msaada wa mataifa ambayo hayana nia njema na nchi yetu, ameandika kwamba aliyekamatwa na Polisi hausiki!! Amejuaje hausiki? Aliyepigwa yuko hospitalini. Je anamjua aliyempiga? Alimuona na kumtambua usiku saa nne?

Maria anasema aliyekamatwa alikuwa anakula tu Kanteen ya TEC. Sasa mtu akiwa anakula hawezi kuwa mshirika wa tukio? Maria anajuaje mtu huyo hakuwa anakula kama sehemu ya mpango wa kutekeleza uhalifu? Anajuaje hakuwa pale akiwaambia aliopanga nao muda Fr Kitima akinyanyuka wakae tayari kumshambulia?

Hii sio bahati mbaya hata kidogo. Ni mkakati maalumu wa kuchochea vurugu za kisiasa kwa kutumia dini.

Suala la kupigwa na kujeruhiwa kwa Fr Kitima ni muendelezo wa mpango wa makusudi kuigombanisha Serikali na wananchi, haswa wa dini ya kikristo.

Ni lazima watanzania tuwe makini sana. Amani na utulivu wa nchi yetu ni lazima tuvilinde. Niwahakikishie, hapa kinachotafutwa na CHADEMA ni ‘trigger point’ (jambo litakalosababisha chuki isiyomithilika kwa kundi fulani aidha vijana au waumini wa dini) ili kuanzisha vurugu na machafuko kuzuia uchaguzi.

Viongozi wa CHADEMA wanatafuta kila namna nchi yetu ionekane inakiuka haki za binadamu iwekewe vikwazo! Wanawaaminisha wafuasi wao kwamba wanakubalika ila wanaonewa na sasa wanaumizwa!

Hii ndio nia yao! Hakuna namna wataweza kushinda uchaguzi sasa wameamua kutekeleza mkakati huu ovu. Wanachi wenzangu, tusikubali kuingizwa mtegoni. TUSIKUBALI. Tuilinde nchi yetu. Tuelimishane. Tuhimizane upendo na kuthaminiana. Tupingane kwa hoja. Tuhakikishe hakugawanyiki 🙏🏿
Akili ndogo sana . Unatakiwa kusema Mkakati wa kuharibu maslahi ya watawala

Usihusishe nchi na upumbavu wa CCM
 
Mimi mkristo mkatoliki Samia ni muislam mwenyeji wa kizimkazi Zanzibar, hatuna uhusiano wowote.
SAWA, ndiyo maana ukajipachika hilo jina 'Steven' ili uje hapa JF kwa ulaghai.

Huna chochote unachopenda kuhusu kazi anayofanya Samia, mbali ya kutupiwa makombo ili uje hapa kutetea maovu anayofanya kwa waTanzania
Sina siasa za chuki wala siwezi kukubali kuongozwa na chuki nasimamia ukweli mtupu. Samia anafanya mengi sana tatizo mashujaa wa nyuma ya keyboard hawana uwezo wa kuyaona kwa sababu dunia yao ni ndogo sana.
Lugha zile zile, kama za mama yenu; ni kama mlizaliwa mapacha, au watu wa familia moja. Ndiyo maana nasema tamaduni hizi mnazorithi kwa wajomba ni tofauti kabisa na hizi za huku.

Sijui unazungumzia jambo gani na huyo Heche, lakini ametokea kuwa mwiba mkali zaidi kwenu hata kuliko Tundu Lissu.
 
Kuna uwezekano mkubwa ulikuwa mpango wa CHADEMA kumpiga Padri Kitima na kitu butu. Pia Malasusa anashambuliwa na kina Lema kwa sababu kakataa KKKT kuwa tawi la CHADEMA. Dola isiwachekee hawa wahuni.
Nikiangalia wanachadema wa sasa walivyopinda na kuidharau serikali,na mashabiki wa yanga walivyo tayari kwa lolote wakiwemo mawaziri,ninaona nia mbaya ya kuleta vurugu Kali sana hususan kabla ya uchaguzi.
Hii ni dalili tosha mama anadharauliwa.Lakini mimi naamini Rais ni taasisi na bado unaweza kufanya lolote kwa usalama wa nchi
 
SAWA, ndiyo maana ukajipachika hilo jina 'Steven' ili uje hapa JF kwa ulaghai.

Huna chochote unachopenda kuhusu kazi anayofanya Samia, mbali ya kutupiwa makombo ili uje hapa kutetea maovu anayofanya kwa waTanzania

Lugha zile zile, kama za mama yenu; ni kama mlizaliwa mapacha, au watu wa familia moja. Ndiyo maana nasema tamaduni hizi mnazorithi kwa wajomba ni tofauti kabisa na hizi za huku.

Sijui unazungumzia jambo gani na huyo Heche, lakini ametokea kuwa mwiba mkali zaidi kwenu hata kuliko Tundu Lissu.
Hunijui wewe, na hizo hasira zako zisikufanye ukazidi kuwa na picha tofauti na uhalisia wangu. Mitano tena kwa Samia mpaka 2030.
 
Lugha hiyo ndiyo inayo ondoa watu kutekwa, kuumizwa na kuuawa?
Sasa mnajiandaa kumwaga damu ya waTanzania ili Samia aendelee kushika madaraka?
Hakuna anayeteka mtu, mara nyingi ni michezo ya wanasiasa wenyewe. Rais anakuwa na kazi nyingi sana hana muda wa kuwazia kutesa watu. Ili apate faida gani anapomteka na kumuua mtu!?.
 
Nikiangalia wanachadema wa sasa walivyopinda na kuidharau serikali,na mashabiki wa yanga walivyo tayari kwa lolote wakiwemo mawaziri,ninaona nia mbaya ya kuleta vurugu Kali sana hususan kabla ya uchaguzi.
Hii ni dalili tosha mama anadharauliwa.Lakini mimi naamini Rais ni taasisi na bado unaweza kufanya lolote kwa usalama wa nchi
Khatari sana
 
Back
Top Bottom