Jambo hili sio jepesi kulisema lakini hakuna budi lisemwe bila kupindisha maneno. Viongozi wa CHADEMA wanataka vurugu na machafuko yaliyotokea Kenya na maeneo mengine duniani yatokee nchini kwetu kama njia ya kuzuia au kuvuruga uchaguzi.
Baada ya Fr Kitima, Katibu wa Baraza la Maaskofu (TEC) kujeruhiwa, jana Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Ndugu Godbless Lema, ameandika kuwataka Maaskofu watoe tamko ili waumini wao wasusie uchaguzi.
Pia, Ndugu Godlisen Malisa ambaye ni mwanachama wa CHADEMA ameandika kwenye ukurasa wake wa instagram akimtaka Askofu Mkuu wa KKKT atoe tamko. Wafuasi wake wamemshambulia sana Askofu Malasusa kwa kila aina ya matusi bila yeye kuchukua hatua zozote.
Naye Bi. Maria Sarungi, shabiki na mshirika wa karibu wa Tundu Lissu aliyeko nchini Kenya akiratibu na kuhamasisha matukio haya kwa msaada wa mataifa ambayo hayana nia njema na nchi yetu, ameandika kwamba aliyekamatwa na Polisi hausiki!! Amejuaje hausiki? Aliyepigwa yuko hospitalini. Je anamjua aliyempiga? Alimuona na kumtambua usiku saa nne?
Maria anasema aliyekamatwa alikuwa anakula tu Kanteen ya TEC. Sasa mtu akiwa anakula hawezi kuwa mshirika wa tukio? Maria anajuaje mtu huyo hakuwa anakula kama sehemu ya mpango wa kutekeleza uhalifu? Anajuaje hakuwa pale akiwaambia aliopanga nao muda Fr Kitima akinyanyuka wakae tayari kumshambulia?
Hii sio bahati mbaya hata kidogo. Ni mkakati maalumu wa kuchochea vurugu za kisiasa kwa kutumia dini.
Suala la kupigwa na kujeruhiwa kwa Fr Kitima ni muendelezo wa mpango wa makusudi kuigombanisha Serikali na wananchi, haswa wa dini ya kikristo.
Ni lazima watanzania tuwe makini sana. Amani na utulivu wa nchi yetu ni lazima tuvilinde. Niwahakikishie, hapa kinachotafutwa na CHADEMA ni ‘trigger point’ (jambo litakalosababisha chuki isiyomithilika kwa kundi fulani aidha vijana au waumini wa dini) ili kuanzisha vurugu na machafuko kuzuia uchaguzi.
Viongozi wa CHADEMA wanatafuta kila namna nchi yetu ionekane inakiuka haki za binadamu iwekewe vikwazo! Wanawaaminisha wafuasi wao kwamba wanakubalika ila wanaonewa na sasa wanaumizwa!
Hii ndio nia yao! Hakuna namna wataweza kushinda uchaguzi sasa wameamua kutekeleza mkakati huu ovu. Wanachi wenzangu, tusikubali kuingizwa mtegoni. TUSIKUBALI. Tuilinde nchi yetu. Tuelimishane. Tuhimizane upendo na kuthaminiana. Tupingane kwa hoja. Tuhakikishe hakugawanyiki 🙏🏿
Waloua Kule Zanzibar 2001 ni Chandema au SERIKALI ya CCM katika mkakati wake wa kutaka kukaa madarakani kwa nguvu ?
Waliopanga njama za kumfanyia ubaya Padri Kitima wanajulikana ?
Kwa nini hawakamatwi ?
Hiyo amani ya kuua wenzenu ili nyie mkae madarakani hatuitaki .
Vita halali ni kati ya wema na ubaya .
Tanzania wakati wa Nyerere tulishinda vita nyingi ikiwemo vita kubwa ya Uganda kwa sababu tulipigania Haki sio amani maana amani inaweza ikawepo kwa nchi ya upanga lakini haki ni hata wanyama wanahitaji haki yao ndio maana kuna haki za wanyama lakini hakuna amani ya wanyama .
Ukaingia porini na kuwanyima wanyama chakula na haki yao ya kuishi porini wataingia mitaani na kudhuru watu.
Hakuna kiongozi wa dini ya Kikristo anayemwamini Mungu na Kristo kama Masihi na mtawala wa kila kitu anayeweza kukubaliana na Suala la CCM kunyima watu haki zao za kisiasa na kuchagua na kuchaguliwa kwa haki .
Waislam wachache wa Bakwata mmefanikiwa kuwarubuni ili waunge mkono Dhulma na kuwatumia kutisha na kuua waslam wenzao wasiomuunga mkono Samia .
Lakini kwa Wakristo mjiandae tu kuwaua wote lakini kamwe hakuna Askofu atakayempigia magoti shetani kwa sababu ya fahari za kidunia .
CONSTANTINO mfalme aliyetawala karibu nusu ya dunia nzima alishindwa kuwamaliza Wakristo na adui zake akaamua kuungana nao na kuibatiza nchi nzima ili ashinde vita dhidi ya adui zake.
Tatizo ni moja kubwa Samia na akina Mwaipopo hawaamini kuwa ukristo ni dini . Hawaamini katika yale yanayohubiriwa na Viongozi wa dini ya Kikristo hata kama ni ya haki kwa hiyo wanaamini hata ukiwaua ni kama kuua mbu tu na hakuna dhambi kuua wakristo .
Sawa tumekubali kuwa ukristo sio dini na hauna haki ya kukataza mabaya isipokua Bakwata tu ndio wanye dini basi wekeni sheria za haki ili tupate viongozi tunaowataka wenyewe .
Wapeni basi hata viongozi wa dini Jukumu la kusimamia uchaguzi lakini sio kusimamiwa na wale wanaochaguliwa na mwenyekiti wa CCM.
Kwa nini Tume isichwgulowe kwa kushindanisha wetu kwa uadilifu wao na sio kwa wizi na historia ya kuharibu uchaguzi?
Eti Rwanda maaskofu walishiriki vita kwa nini hamsemi kuwa Serikali ya Wahutu iliwaua Watutsi zaidi ya laki 9 wakiwemo mapadri na maaskofu kwa sababu tu ya kutaka kuwanyamazisha na kuwaondoa kwenye mfumo mzima wa kiserikali kama tunavyoona juhudi kubwa ya political Curtailers ndani ya CCM kuwaua wale wasiomuunga mkono Rais Samia ili aendelee kutawala lengo ni kuja kumwachia Mkwe wake nchi .