Mjumbe wa kamati kuu ya CCM amuomba Askofu Mwamakula kumfikishia ujumbe wake kwa Wananchi kuhusu mkataba wa bandari Ili asifukuzwe uanachama

Usimwamini Mwanasiasa yoyote anayeongelea kwamba anapinga mkataba wa DP World huku akiogopa kuvuliwa uanachama na chama chake

Wanasiasa ni Watu Waongo na Wanafiki sana

Mbarikiwe sana!
 
Usimwamini Mwanasiasa yoyote anayeongelea kwamba anapinga mkataba wa DP World huku akiogopa kuvuliwa uanachama na chama chake

Wanasiasa ni Watu Waongo na Wanafiki sana

Mbarikiwe sana!
Na wengine post kama hizo ni spinners tu, mimi naamini hakuna mwanasiasa yeyote aliyeongea hayo.
 
Usimwamini Mwanasiasa yoyote anayeongelea kwamba anapinga mkataba wa DP World huku akiogopa kuvuliwa uanachama na chama chake

Wanasiasa ni Watu Waongo na Wanafiki sana

Mbarikiwe sana!
ccm tuijuayo kwenye jambo la mwenyekiti wao, na slogani yao ya zidumu fikra za mwenyekiti, na jambo hili lingekuwa lina maslai mapana kwa taifa ungeona vibration na amshaamsha nchi nzima na maandamano juu kupongeza juhudi za mama, lakini nafsi zinawauma, zinawauma, kusaliti rasilimali za nchi, utaifa umekuwa mkubwa mioyoni mwao. na wameonyesha kwa vitendo kuwa hili jambo halina baraka, na wana hofu ya dhambi ya usaliti, binafsi nawaelewa

ni wachache sana wanaoongea lakini sura na mioyo yao inapishana.
 
Madini yalienda,
Gesi ikaenda ,
Mbuga za wanyama zinaondoka ivo,
Bandari plus bahari na ndio hiyo inaenda,
Ardhi soon inaenda baada ya bunge kuridhia.
HII SAFISHA SAFISHA MALI ZA WATANZANIA sijui tutajikuta tumebaki na nini..
Na tukiendelea kuwachekea na mlima kiliimanjaro utawekwa sokoni....
Hizi zote ni mali zao. Sisi wametuazima gu Oxygen tuweze kuishi.

Na wakiamua wataizima na yenyewe.

Wanakwambia Nchi hii ni yao ccm na ccm ina wenyewe
 
Mimi ninatumaini waTanzania wamepata funzo la kutosha hapa, kama bado walikuwa na matumaini juu ya hiki chama cha CCM.

Kwenda kupiga kura kuchagua yeyote ndani ya CCM ni kuliumiza taifa letu.

Ni wakati sasa watu watambue kwamba CCM ipo si kwa maslahi ya nchi na wananchi wake, bali ni kwa hawa viongozi na wanachama wanaofaidika na uwepo wa chama hiki.
100% perfect
 
Madini yalienda,
Gesi ikaenda ,
Mbuga za wanyama zinaondoka ivo,
Bandari plus bahari na ndio hiyo inaenda,
Ardhi soon inaenda baada ya bunge kuridhia.
HII SAFISHA SAFISHA MALI ZA WATANZANIA sijui tutajikuta tumebaki na nini..
Na tukiendelea kuwachekea na mlima kiliimanjaro utawekwa sokoni....

Hiyoo imeenda hiyo imeendaaa
 
Ujumbe ufuatao umetoka kwa mwanachama wa CCM ambaye amekuwa Mteule wa Rais wa muda mrefu. Kwa kuogopa kufukuzwa CCM, ameomba afikishe ujumbe kupitia kwa Askofu.

Mpendwa Baba Askofu Mwamakula!

Kwenye vikao vilivyoisha (Kamati Kuu ya CCM na Halmashauru Kuu ya CCM) imeelezwa kuwa Wajumbe wamebariki mkataba tata wa Bandari. Ninajiuliza maswali kadhaa: Je, ni Wajumbe wangapi katika vikao hivyo ni wanasheria au wachumi walioweza kuingia katika vikao na nakala ya mkataba na kuanza kujenga hoja ya kujadili kifungu kwa kifungu kuwa kifungu hiki hakiko sawa na hiki kiko sawa?

Je, Mwenyekiti wa kikao alitangaza maslahi yake katika jambo husika kuona busara kuwa jambo hilo lijadiliwa kwa uwazi bila yeye kuwa Mwenyekiti wa kikao kwa kuwa limepigiwa kelele sana na hivyo kujenga neutrality kwake? Je, isingekuwa ni busara kumuachia Makamu Mwenyekiti ili asimamie vikao husika?

Mpendwa Baba Askofu! Unajua kwenye Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ili mtu aweze kuingia katika Political Committee ama Kamati ya Siasa na ngazi zingine kubwa za maamuzi ni lazima awe na uelewa wa mambo hususani katika masuala ya fedha, sheria, mazingira na pia lazima awe na elimu au uwezo wa kuweza kujenga hoja.

Je, ni Wajumbe wangapi katika vikao vyetu ambao ni wanasheria na wachumi walio na uwezo wa kujenga hoja katika vikao ambavyo tumeambiwa kuwa wameridhia kwa kishindo?

Ninaomba ikikupendeza Baba Askofu unisaidie kuyafikisha haya kwa Watanzania kwani sio wote ndani ya CCM tunaounga mkono mkataba huo wa Bandari. Mazingira yetu ni magumu na hivyo tunaogopa kufukuzwa uanachama ndio maana hatutoki hadharani kupinga au kukosoa.

Ndimi .....
Dar es Salaam, 10 Julai 2023
If this information is real and stands it is real, the crack is growing. Nyufa ni kubwa sana.
 
Back
Top Bottom