Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 949
- 2,865
Ujumbe ufuatao umetoka kwa mwanachama wa CCM ambaye amekuwa Mteule wa Rais wa muda mrefu. Kwa kuogopa kufukuzwa CCM, ameomba afikishe ujumbe kupitia kwa Askofu.
Mpendwa Baba Askofu Mwamakula!
Kwenye vikao vilivyoisha (Kamati Kuu ya CCM na Halmashauru Kuu ya CCM) imeelezwa kuwa Wajumbe wamebariki mkataba tata wa Bandari. Ninajiuliza maswali kadhaa: Je, ni Wajumbe wangapi katika vikao hivyo ni wanasheria au wachumi walioweza kuingia katika vikao na nakala ya mkataba na kuanza kujenga hoja ya kujadili kifungu kwa kifungu kuwa kifungu hiki hakiko sawa na hiki kiko sawa?
Je, Mwenyekiti wa kikao alitangaza maslahi yake katika jambo husika kuona busara kuwa jambo hilo lijadiliwa kwa uwazi bila yeye kuwa Mwenyekiti wa kikao kwa kuwa limepigiwa kelele sana na hivyo kujenga neutrality kwake? Je, isingekuwa ni busara kumuachia Makamu Mwenyekiti ili asimamie vikao husika?
Mpendwa Baba Askofu! Unajua kwenye Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ili mtu aweze kuingia katika Political Committee ama Kamati ya Siasa na ngazi zingine kubwa za maamuzi ni lazima awe na uelewa wa mambo hususani katika masuala ya fedha, sheria, mazingira na pia lazima awe na elimu au uwezo wa kuweza kujenga hoja.
Je, ni Wajumbe wangapi katika vikao vyetu ambao ni wanasheria na wachumi walio na uwezo wa kujenga hoja katika vikao ambavyo tumeambiwa kuwa wameridhia kwa kishindo?
Ninaomba ikikupendeza Baba Askofu unisaidie kuyafikisha haya kwa Watanzania kwani sio wote ndani ya CCM tunaounga mkono mkataba huo wa Bandari. Mazingira yetu ni magumu na hivyo tunaogopa kufukuzwa uanachama ndio maana hatutoki hadharani kupinga au kukosoa.
Ndimi .....
Dar es Salaam, 10 Julai 2023