Mji wa Arusha unakuzwa(overrated)

Mji wa Arusha unakuzwa(overrated)

Arusha ni mji mzuri ila ni wa kawaida sana.Nimekuwa nikisikia sifa inazopewa Arusha,lakini nilichokishuhudia ni tofauti na nilichokuwa nakisikia.

Nimekaa Arusha Kwa zaidi ya wiki 4 nimefanikiwa kuzunguka maeneo yote ya muhimu sijaona kitu cha ajabu.

Nimeona hata mji wa Moshi ni mzuri sana zaidi ya Arusha,ni sifa tu zisizo na miguu inapewa Arusha.

Hitimisho: Arusha ni mji mzuri Ila wa kawaida sana isipewe sifa zilizopitiliza.Moshi licha ya udogo wa eneo ni mji mzuri zaidi ya Arusha.
Fafanua hicho kitu cha ajabu ambacho hukukiona na huo ukawaida sana uliouona huko Arusha,labda ntakuelewa unaongea nini..!
 
Mkuu nakubali Arusha iko juu kiuchumi kuliko moshi ila kwenye suala la mpangilio wa mji Arusha kamwe huwezi ilinganisha na moshi, master plan ya mji wa moshi ni bora zaidi kuliko Arusha.
Jingine umekosea kwenye ubora wa makazi hapo moshi nayo inaikimbiza sana Arusha mkuu, tatizo la moshi town centre haijajengeka sana ila pembezoni mwa mji hada kwenye ubora wa makazi kwa kweli wachaga wako mbele mno.
Atakaye kataa ukweli ulioandika, akapimwe ubongo
 
Fafanua hicho kitu cha ajabu ambacho hukukiona na huo ukawaida sana uliouona huko Arusha,labda ntakuelewa unaongea nini..!
Pitia tu post zote,mengi tu yameshaandikwa
 
tetehee tehhee ,eti pembeni kidogo mamigomba ,kweli arusha bado.
Migomba ni chakula kikuu cha wakazi wa Arusha kama ilivyo Moshi, Bukoba, Mbeya. Kama unashangaa migomba mbona hushangai minazi kila kona Dar? Au Mikorosho Kibaha?
 
Migomba ni uchafu
 
Hizo ndiyo sifa za kijinga kuiita Arusha Geneva
Kwako wewe zinaweza kuwa sifa za kijinga,lakini ndio zinazoipaisha mji huo,Kama Bill Clinton katoa sifa za kijinga,we utakuwa Genius
 
Mimi siyo gineus ,wewe wasema
 
Kwa sasahivi hoteli gani zina viwango vya nyota nne na tano Arusha?
Kitu kinachonyanyua Arusha ni kuwa mlango wa vivutio maarufu vya utalii duniani
Ni kweli kabisa
 
Ulikuja na hela au ndo kuomba nauli kwa shemeji chuga hakna kitu cha ndogo kiatu cha kununua 20 mikoani hapa Jamaa linakwambia laki na 50 afu linaendelea kuchanja gomba
Arusha ni mji mzuri ila ni wa kawaida sana.Nimekuwa nikisikia sifa inazopewa Arusha,lakini nilichokishuhudia ni tofauti na nilichokuwa nakisikia.

Nimekaa Arusha Kwa zaidi ya wiki 4 nimefanikiwa kuzunguka maeneo yote ya muhimu sijaona kitu cha ajabu.

Nimeona hata mji wa Moshi ni mzuri sana zaidi ya Arusha,ni sifa tu zisizo na miguu inapewa Arusha.

Hitimisho: Arusha ni mji mzuri Ila wa kawaida sana isipewe sifa zilizopitiliza.Moshi licha ya udogo wa eneo ni mji mzuri zaidi ya Arusha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom