Mjerumani amchambua Lowassa, awashangaa Watanzania

Nilichokiona mtoa mada bado mtumwa akisema mzungu yeye hana chake muulize mzungu angemwambia yeye ndiye Baba yake angemkana aliyemzaa?
 
Ni raia wa nchi inayokusaidia wewe na familia yako ili uweze kuishi. Bila yeye huwezi hata kuwapeleka watoto wako shule. Bila yeye hata huyo fisadi Lowassa hawezi kupata fedha za kuiba!

labda anakusaidia wewe na hao wengine wanaopenda msaada. simuungi mkono Lowasa, lakini eti kusema mzungu ndo amesema, huo ni ufinyu wa fikra,yaani sie hatuwezi kuwahukumu wagombea mpaka tusemewe na wazungu????hata huko ni kutukanwa tena matusi mabaya.
 
Doesn't matter nani kaongea, ila ukweli ni kwamba sisi watz tu wasahaulifu sana. Mimi mwenyewe huwa najiuliza sana hayo maswali ila naamua ku-give time. Ukitokea ufisadi watu huzungumza sana ila it take a week watu kusahau kila kitu. Kifupi tz tunaishi kwa matukio. Mungu atusaidie
Kwa kweli Mzalendo mwenzangu mimi binafsi nimekuwa na wasiwasi sana na akili na tabia za Watanzania, Watanzania tu watu wa ajabu saana. Hatuipendi na kuijali nchi yetu, na ili ni kosa kubwa sana, hata Mungu atakuwa anatushangaa!!
Watu wameweka maslahi binaffsi mbele kuliko maslahi ya Taifa.....!!
 
Wewe maoni ya mzungu hapa kwa kwa ajili ya wtz toa ya moyoni au ya viongozi Wa tz
 
Huu ni mwaka wa kufanya tathmini kama watz tumeerevuka au la. Kama Lowassa akishinda watz wengi ni wajinga.
 
Ila huyo Mjerumani katika mazungumzo yenu mmeongelea ni kwa nini aliamua kuja Tanzania?
 
Hao wazungu sijui mnakakutana nao wapi na mnakutana kufanya nini? yaani nyie hata mzungu akiwa mwehu mnachekelea tu mawazo yake, sasa mbona kama mlikuwa mnatongozana tu hapa we ukiulizwa unajibu hata kama uhusiki eti hapana.

Anasema your amazing kutokana na aina ya watu anaokutana nao, na wewe ukaamini itatuchukua miaka mingi kupata mabadiliko alikuambia wao iliwachukua miaka mingapi? Ulimuuliza Adolf Hitra alikuwa mmatumbi wa wapi? Ulimkumbuka Water Rodney, Mkikutana nae tena mwambie siku hizi tunaamua wenyewe na hakuna kushobokea tena wazungu.

Katika hali ya kunishangaza, nilikuwa nabadilishana mawazo na mzungu mmoja raia wa Ujerumani kwenye N.G.O yake. Katamka maneno yaliyonistaajabisha.

Tumeongea mambo mengi lakini baadae tukaanza kuongelea siasa. Akasema kuna yule aliekuwa waziri mkuu anaitwa Lowasa, nimeona sasa mnampenda sana. Mimi nikamjibu inaonekana kuna Watanzania wanampenda awe Rais. Yule Mzungu akaniuliza, si yule aliejiuzuru kwa sababu ya Corruption?, nikamjibu ndie huyo. Akasema, wakati ule alionekana amekula Rushwa, sasa anataka kuwa Rais na watu wanamuunga mkono!, akaongezea kwa kusema how can you easily forget?, how can you easily change your mind?, yaani mnawezaje kuwa wasahaulifu namna hii, mnawezaje kubadili fikra zetu haraka hivi juu yake?, hapo mimi nikabaki na kigugumizi. Akaongeza, au Lowasa amewahi kuwaelezea uhusika wake na hizo corruption?, mimi nikamjibu hapana. Akasema tena, Or was he cleared by the court? yaani, je Mahakama iliona hana hatia?, nikamjibu kesi haijawahi kwenda Mahakamani. Akauliza, then which criteria do you use support him?, yaani mnatumia kigezo gani kumuunga Lowasa mkono? nikamjibu kwakweli sijui wananchi wanatumia kigezo gani.

Yule mzungu akasema, anyway, you are such amazing country, with this style it may take you so many years to change. Yaani ninyi ni nchi ya ajabu, kwa style hii itawachukua miaka mingi kupata mabadiliko.
 
Hivi kile chama cha kikristo cha ejerumani chenye ushirikiano na chadema kishaleta pesa ya campaign? Mbona mapema mmeanza ...
 
Katika hali ya kunishangaza, nilikuwa nabadilishana mawazo na mzungu mmoja raia wa Ujerumani kwenye N.G.O yake. Katamka maneno yaliyonistaajabisha.
..................................Akasema, wakati ule alionekana amekula Rushwa, .............................

Haya mambo siyo kwamba hatuyajui ktk nchi hii. Tulio na akili tunachoweza kusema ni mfumo mbovu ndani ya CCM ambao umeruhusu wezi na wacheza dansi kuingia ikulu. CCM wanadai hii ni serikali yao na hivyo hivyo yabidi wadai upuuzi huu ni wa serkali yao.

Huwezi kuruhusu watu kama hawa akina Lowasa na akina Wasira ambao wote walishahusishwa na mambo ya rushwa. Wasira alishafungiwa kushiriki ktk siasa kwa sababu ya mambo ya rushwa, leo hii amezaliwa upya? Ndo maana mtu anakusanya watu kwa kutumia watu wa hovyo ktk jamii, halafu anapata wafuasi hadhalani. Lowasa anaishia kusema ajira ni bomu, ni bomu, ni bomu bila hata kusema iweje sasa!
 
Baada ya maongezi ukamuomba hela ya sigara akakupa mia tano.
 
upumbavu tuu,unaishi kwakunyeyekea wazungu wewe,fanye kila jitihada pindukeni kwakila style lakini hamuwezi kuuzima moto huu
 
Katika hali ya kunishangaza, nilikuwa nabadilishana mawazo na mzungu mmoja raia wa Ujerumani kwenye N.G.O yake. Katamka maneno yaliyonistaajabisha.

Tumeongea mambo mengi lakini baadae tukaanza kuongelea siasa. Akasema kuna yule aliekuwa waziri mkuu anaitwa Lowasa, nimeona sasa mnampenda sana. Mimi nikamjibu inaonekana kuna Watanzania wanampenda awe Rais. Yule Mzungu akaniuliza, si yule aliejiuzuru kwa sababu ya Corruption?, nikamjibu ndie huyo. Akasema, wakati ule alionekana amekula Rushwa, sasa anataka kuwa Rais na watu wanamuunga mkono!, akaongezea kwa kusema how can you easily forget?, how can you easily change your mind?, yaani mnawezaje kuwa wasahaulifu namna hii, mnawezaje kubadili fikra zetu haraka hivi juu yake?, hapo mimi nikabaki na kigugumizi. Akaongeza, au Lowasa amewahi kuwaelezea uhusika wake na hizo corruption?, mimi nikamjibu hapana. Akasema tena, Or was he cleared by the court? yaani, je Mahakama iliona hana hatia?, nikamjibu kesi haijawahi kwenda Mahakamani. Akauliza, then which criteria do you use support him?, yaani mnatumia kigezo gani kumuunga Lowasa mkono? nikamjibu kwakweli sijui wananchi wanatumia kigezo gani.

Yule mzungu akasema, anyway, you are such amazing country, with this style it may take you so many years to change. Yaani ninyi ni nchi ya ajabu, kwa style hii itawachukua miaka mingi kupata mabadiliko.

He he huyo mzungu alikuwa ni mimi.
 
Na ndiyo sababu hata huko kwao tukienda wanatuona mapoyoyo kweli.

Kwa hakika sisi ni nchi ya ajabu duniani. Na tuombe tuingizwe Guiness.
 
Sasa hapa nani anaonesha kujitambua kati yake na wewe? Kwa nini utegemee mwanaume mwenzio kula?

cc INGENJA
 
Back
Top Bottom