Mjadala wa DOWANS ITV waibua mapya!

Mjadala wa DOWANS ITV waibua mapya!

Nilkuwa na tazama mjadala wa Chadema kuhusu Dowans, hakuna lolote, pumba tupu, highly biased and highly contradictory. Wanabwabwaja bila mpango.

Mkinga ni CDM? Alipogombea dhidi ya Nchimbi alikuwa CDM? Hata siku moja hawezi kuwa CDM. Wewe unasemaje kuhusu Dowans??
 
Huyo Mzee ana ushahidi kwa anayo yaongea, ajuwe wenzake aliowataja wana vichwa kuliko yeye, asije akaomba msamaha kama Mtikila!
 
Kwani Richmond kampuni ya Costa Rica? mijitu mingine huwa inajisemea tu, hata haina mpango wala haijuwi inaongea nini.

hivi watu kama wewe mnalipwa sh ngapi kuuza utu wenu namna hii

kwenye dowans wamekuahidi sh ngapi??
 
KAMA UMEANGALIA ITV, MKINGA ANATOJA MAJINA YA WATU BILA YA KUWA NA EVIDENCE
je kwanini ITV wanamualika MKinga mchochezi? kwanini anawachonganisha viongozi na wananchi?
Ndio maana kuna mahakama...Waige mfano wa Membe.
 
God have mercy on us!

Kweli waTZ tumeshaonekana mazuzu. Nimegundua Kikwete si Zuzu kama tunavyofikiria. Yeye keshatuona sisi ndio mazuzu, na anajua hatuwezi kufanya lolote
Umesema vyema, MAFISADI wanajua kabisa tutapiga kelele and at the end of the day tutakaa kimya. Watanzania wengi si wazalendo.
 
Huyo Mzee ana ushahidi kwa anayo yaongea, ajuwe wenzake aliowataja wana vichwa kuliko yeye, asije akaomba msamaha kama Mtikila!

Wewe shida yako ni kulamba miguu ya hao mafisadi , huna uchingu wowote na haya mambo yote yanayotekea. AMKA.
 
Huyo Mzee ana ushahidi kwa anayo yaongea, ajuwe wenzake aliowataja wana vichwa kuliko yeye, asije akaomba msamaha kama Mtikila!

Wewe shida yako ni kulamba miguu ya hao mafisadi , huna uchingu wowote na haya mambo yote yanayotekea. AMKA. Kwani mara ngapi wametajwa hadharani lakini hawashtaki?? LIST OF SHAME???
 
katika siku nilizotizama tv nikafurahi today is one of them. Hivi kweli rais wa tanzania yupo? na anawashauri?
 
Mkinga alisema kuwa mkwere ametoa ahadi 70 something zenye thamani ya zaidi ya tsh trilion 9 (something like that). Hivi mkwere anatuchukuliaje sisi? Anajua kuwa hatuwezi ku act? This time mkwere kwisha habari yako
 
Baada ya kufuatilia mjadala huu wa ITV yafuatayo ni machache niliyoyang'amua....

Ni wazi mjadala ulikuwa wa kichochezi zaidi kuliko elimishi.

Rugemeleza amejaribu kuwa mkweli zaidi na kuepuka siasa nyingi lakini pia hulka yake ya hamasa tele imemfanya kuwa anajichanganya mambo mengi. Mojawapo ni hili suala la mikataba kwenda bungeni huku akitambua kuwa mkataba unaongelewa hapa ni wa Dowans Vs Tanesco na sio wa nchi na nchi. Lakini zaidi ameshindwa kuonyesha ni jinsi gani serikali inaweza kuingia katika kesi hii. Vile vile Rugemeleza amejichanganya katika suala la mikataba kuingia bungeni kwa hoja ya kuwa hiyo itasaidia kuepuka mikataba mibovu wakati ambapo katika maelezo yake anakiri kuwa mkataba huo hauna tatizo katika vipengele vyake isiopokuwa uhalali wake na pia makosa ya serikali kukubali suala hilo kupelekwa katika mfumo wa sheria wa nje ambao ukweli ni kuwa unakiuka hata vipengele vya mkataba huo.

Hata hivyo ni wazi kuwa wakati wenzake walishadadia sana katika upande wa kisiasa wa suala hilo, ni yeye pekee aliyeweza kutuelimisha upande wa kisheria ambao ndio muhumu zaidi wakati huu tunajitahidi ujinusuru na janga hili.

Mkinga was just being Mkinga lakini ni wazi kuwa ushabiki wake katika siasa za makundi ya MTANDAO umemfanya ajichanganye kupita kiasi hivyo kufanikiwa kuhemusha hisia za watu wa kawaida na washabiki wa kisiasa lakini kushindwa kuwaelimisha wale wenye weledi na busara.

Kibamba ameendelea kujikuta akitumia kauli mbiu na ajenda za chama chake huku akijinasabisha na uanaharakati. Ukweli ni kuwa wakati hawa wote wamejitambulisha kuwa ni wanaharakati lakini maoni yao yameonyesha wazi jinsi gani mitizamo yao ilivyoathiriwa na uanachama, ufuasi na ushabiki wa vyama vyao zaidi ya maslahi ya Tanzania.

Kibamba ni mwanachama hai wa Chadema na pia Michael Dalali ambae naambiwa ni mdogo wa damu wa mbunge wa Chadema Mheshimiwa John Mnyika wakati Mkinga ni kada mfu wa CCM ambaye maslahi yake yameegemea katika kundi za Membe na Samweli Sitta dhidi ya Lowassa na Rostam Azizi.

Ni wazi kutokana na mchanganyiko huo ukijumuishwa na hulka ya kugubikwa na hamasa zinazozidi busara za Rugemeleza zimesababisha kukosekana na hoja makini ambazo zinngeweza kuwaelimisha watanzania zaidi ya kuhemusha hisia zao tu. Mchanganyiko huo pamoja na tabia ya muongoza kipindi Chuwa ya kuwa mshiriki wa kipindi kama ile ya Mzee Mwakwaia wa Kuhenga wa Channel Ten umekosesha haki ya watanzania kujua ukweli wa ndani wa sakata hilo ingawa umefanikisha kuongeza nguvu hoja na maslahi ya kisiasa katika sakati hili huku watanzania wakiendelea kukosa umeme na uchumi kuendelea kuzama. Ni wazi kuwa hiyo ni dhumuni kuu la wengi wa wanasiasa wetu nchini lakini ni wazi si kwa faida ya watanzania katika mizania ya maslahi ya muda mrefu
 
HUyu Mzee Mkinga akikaa na Mtikila wataanzisha kanisa kubwa kuliko hata la Kakobe. Mzee anaongea kwa uhakika bila woga utadhani alikuwepo.... kweli huyu Mzee ni noma!
 
Wandugu,
Kama kawaida yake, Bw. Mkinga ametamka waziwazi bila woga kwenye Kipindi cha Kipima Joto ITV kuwa wamiliki wa Dowans watakaofaidi mabilioni ni Rostam, Karamagi, Msabaha Chenge.

Hii ya Msabaha na Chenge imekula kwake na pengine ITV....
 
1. Kwa nini Werema alisema ati ''nimeshaisoma hukumu na nimeufunga uu mjadala, DOWANS walipwe tu''?

2. Kwa nini JK haipeleki issue hii kwenye baraza la Mawaziri ili ijadiliwe na kutolewa maamuzi?

3. Kwanini wanaharakisha process ya kuwalipa DOWANS wakati hata suala lenyewe halijaandikishwa mahakama kuu?

4. Kwanini Ngeleja amekumbuka kuwatafuta ''wamiliki halali'' wa DOWANS kutoka BRELA juzi juzi tu? alikuwa wapi muda wote huu? au alikuwa anavuta time ili documents zitengenezwe?

5. Kwanini Werema hakuupita ushauri uliotolewa na REX Attorneys kwa TANESCO kuupiga chini mkataba?

6. Kwa nini JK yu KIMYA?? hivi aliigusia issue hii wakati akitoa salamu zake fake za kuufunga mwaka 2010??

7. .............

MY TAKE: Wadanganyika wote tulishaonekana mazuzu tu. Longolongo nyiiiiiiiiiiingi na hatuwezi kufanya lolote. JK analijua hili, Karamagi analijua hili, Lowasa, Chenge, Rostam, Werema, Msabaha etc wanajua kwamba watamlipa DOWANS (watajilipa wenyewe na kuwakatia 10% maswahiba walioshiriki kufanikisha mpango mzima) na issue itafukiwa kama kawaida na life litaendelea kama kawa.

Kuna mtu mmoja alishauri japo wadanganyika waonyeshwe picha za wamiliki hao - ili tujue wanaotudai ni akina nani!

God help us!
 
jk yupo kimya maana wote ni walewale tu-
 
Wandugu,
Kama kawaida yake, Bw. Mkinga ametamka waziwazi bila woga kwenye Kipindi cha Kipima Joto ITV kuwa wamiliki wa Dowans watakaofaidi mabilioni ni Rostam, Karamagi, Msabaha Chenge.

huyo mkinga ana hamu ya kuuza kibanda chake,ataburuzwa mahakamani ukoo wake nzima watachangishana,,,ha ha ha njaa kitu kibaya sana
 
Kibamba ni mwanachama hai wa Chadema na pia Michael Dalali ambae naambiwa ni mdogo wa damu wa mbunge wa Chadema Mheshimiwa John Mnyika wakati Mkinga ni kada mfu wa CCM ambaye maslahi yake yameegemea katika kundi za Membe na Samweli Sitta dhidi ya Lowassa na Rostam Azizi.
Upofu wa itikadi ni mbaya sana unaua uwezo wa kufikiri Mkinga nasikia ni juzi tu kagombea ubunge na Nchimbi kupitia CCM leo amekuwa mfu.
 
Hii ya Msabaha na Chenge imekula kwake na pengine ITV....
<br />
<br />
Ni suala la uelewa tu, ITV imemwalika kuchangia mada. Na yeye kachangia kwa kushutumu kwamba ni wahusika na wala hajahukumu. Sheria inamlinda ni kweli wakati huo walikuwepo madarakani. Hivyo walishiriki katika maamuzi.
 
Nimeshtuka ajabu,kumbe mahakama inaweza kuwa huko Paris lakini kesi ikasikilizwa hapa Dar na maamuzi ya kesi yakafanyika Moven Peak,so kule ni majengo tu????au kesi yenyewe haikuwepo???mbona sielewi.......................nimesikia tena wale wamiliki wote ni marehemu????:car::car::car::ban:

.
Huyu jamaa RA kwa kuwamilikisha marehem makampuni ni mtaalamu.
Ukikumbuka hata faili la kagoda kwa maelezo ya ofisi ya mwanasheria mkuu ilikuwa ina wamiliki wawili mmoja ni marehem na wapili hakuwahi kugundulika ni wa wapi japo walimpa jina. Labda tuseme huyo wa pili bado hajazaliwa na ikitokea akizaliwa tu tutajulishwa ili atakapokua na akili za kupambanua tumwajibishe kwa wizi wa pesa yetu dollar 40m.
.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom