Kinumbo

JF-Expert Member
Dec 8, 2019
2,742
4,931

Maana ya Ndoa​

Ndoa ni muunganiko kati ya mwanamume na mwanamke, walio amua kwa ridhaa yao wenyewe kuishi pamoja kama mke na mume mpaka mwisho wa maisha yao ya ndoa.

Aina za ndoa kwa mujibu wa sheria
Kuna aina mbili tu za ndoa zinazotambulika na sheria ya ndoa Tanzania
  • Ndoa ya mke mmoja na mume mmoja tu.
  • Ndoa ya wake wengi.
Ndoa hizo zinaweza kusheherekewa kufuatana na misingi na taratibu za kidini, kimila au kiserekali, kushuhudiwa na watu wasiopungua wawili na kusajiliwa kwa mujibu wa sheria.

Hatua za kuchukua kabla ya ndoa kufungwa
  • Lazima taarifa ya nia ya kufunga ndoa itolewe siku 21 kabla ya ndoa kufungwa, kama kutakuwa na mwenye pingamizi budi litolewe itoe kabla ya ndoa kufungwa
  • Majina ya wale wanaotarajia kufunga ndoa, umri, majina ya wazazi wao na mahali wanapoishi yatajwe.
  • Tamko kwamba wanaotarajia kufunga ndoa hawana uhusiano unaokatazwa kisheria kufunga ndoa
KUSAJILI NDOA
Ndoa inaweza kufungwa Kiserikali au kwa madhehebu ya Kikristo au Kiislam au kufuatana na mila na desturi za wale wanaofunga ndoa.

Msajili wa ndoa atatoa cheti cha ndoa. Kila Ndoa inapofungwa lazima iwe na mashahidi wawili

Mambo ambayo sheria ya ndoa inakataza katika suala zima la kuoa au kuolewa
  • Mwanamke na au mwanaume kuolewa/kuoa bila ridhaa yake mwenyewe
  • Mwanamke na mwanaume wenye undugu wa damu kuoana
  • Mwanamke na mwanaume kuoana kabla ya kutimiza umri unaoruhusiwa kisheria (kwa mwanaume miaka 18 na kwa mwanamke miaka 18 au 15 kwa idhini ya wazazi/mlezi wake)
  • Kuoana watu wa jinsia moja
  • Mwanamke na mwanaume kutaka kuoana kwa mkataba wa kipindi maalum.
Haki za mume na mke katika ndoa
  • Wote wana haki ya kumiliki mali kama nyumba, shamba n.k. kwa majina yao binafsi;
  • Wote wana haki ya kutoa idhini katika uuzaji au kwa pamoja kuweka dhamana mali yoyote ya familia;
  • Wote wana haki ya kuishi katika nyumba ya familia iwapo mume/mke amemkimbia;
  • Mke ana haki ya kupewa matunzo yake na ya watoto wakati wa ndoa au iwapo mume amemkimbia, wameachana kwa amri ya mahakama. Na mume ana haki ya kupewa matunzo iwapo ana ulemavu hawezi kujiingizia kipato kutokana na ulemavu au ugonjwa wake;
  • Wote wana haki ya kutokupigwa na au kufanyiwa ukatili wa aina yoyote;
  • Wote wana haki ya kupeana unyumba;
  • Wote wana haki ya kutumia mali ya ndoa;
  • Wote wana haki kuomba amri ya talaka.
Ukomo wa ndoa Ukomo wa ndoa uko wa aina mbili:
  • Kifo cha mwanandoa mmoja wapo
  • Talaka ambayo imetolewa na Mahakama pekee pale inapojiridhisha kwamba kuna sababu ya msingi kufanya hivyo.
Baraza la usuluhishi la Ndoa
Baraza la usuluhishi la Ndoa, ni baraza lililoanzisha na kifungu 102 cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, sura ya 29 kama sheria zilizopitiwa mwaka 2002, kwa madhumuni ya kusuluhisha wanandoa ambao wanaingia kwenye migogoro ya Ndoa. Kazi za Baraza la Usuluhishi la Ndoa:-
  • Kusuluhisha Wanandoa walioko kwenye Ndoa baada ya kupokea lalamiko toka kwa mmoja wapo wa Wanandoa
  • Kutoa hati maalum kuthibitisha kuwa suluhu imeshindikana na kuelekeza wanandoa kwenda Mahakamani kwa amri zaidi.
MUHIMU: Mahakama peke yake ndiyo ina mamlaka ya kutoa amri ya kutengana au talaka
Sababu zinazopelekea au kuishawishi mahakama kuvunja ndoa:-
  • Uzinzi kati ya wanandoa
  • Ukatili kati ya wanandoa au watoto wa ndoa
  • Dharau au kupuuza kulikokidhiri dhidi ya mwenzi
  • Kumtelekeza mwenzi kwa zaidi ya miaka mitatu Pale mwenzi anapofungwa kifungo cha maisha au kwa kipindi kisicho pungua miaka miaka mitano
  • Ikiwa mwenzi ameugua ugonjwa wa akili na imedhibitishwa na daktari kwamba hakuna uwezekano wa kupona.
  • Kubadili dini baada ya ndoa kufungwa pale wanandoa wote walikuwa wakifuata imani ya dini moja.
Haki za wanandoa zinazoambatana na amri ya talaka
  • Mgawanyo wa mali za ndoa /familia
  • Matunzo ya mke Hifadhi na matunzo ya watoto
  • Kizuizi cha kutobugudhiwa
  • Kuoa/Kuolewa tena
  • Fidia ya uzinzi
  • Gharama za kuendesha Shauri la Talaka
Haki ya Mgawanyo wa mali za familia/ ndoa Mali yoyote ambayo imepatikana wakati wa uhai wa ndoa na kwa nguvu na au machango wa pamoja wa wanandoa.

Iwapo mali iliyopatikana na mwanandoa mmoja wapo kabla ya ndoa au kwa nguvu zake mwenyewe lakini imeboresha/imetunzwa na mwanandoa mwingine mali hiyo itatambulika kama mali ya ndoa.

Lakini kama kuna mali yoyote ambayo mwanandoa mmoja amempa mwanandoa mwenzake kama zawadi, mali hiyo itakuwa ya yule aliyepewa pekee.

Aina za mchango
Kutekeleza kazi nyumbani hasa kutunza familia; mfano kuosha vyombo, kupika, kufua nguo, kubeba maji na kazi zingine zinazofanana na hizo kwa maslahi ya familia.

Kutunza mali za ndoa: mfano kufyeka, kulima, kuvuna shamba, kufanya marekebisho ya mali za ndoa kwa maslahi ya familia.

Mchango wa fedha wa mwanandoa katika kununua mali.

Haki ya Matunzo ya mwanandoa
Jukumu la kutoa matunzo kwa mke na watoto ni la mume, jukumu hilo litatekelezwa wakati wa uhai wa ndoa na baada ya talaka.

Haki ya Hifadhi na matunzo ya watoto
Hifadhi ya watoto hutolewa kwa mume au mke au mtu baki (mlezi) hasa kwa kuzingatia ustawi na maslahi ya wale watoto. Zaidi ya hayo, mahakama pia inaweza kuzingatia yafuatayo:

Umri wa wale watoto, mfano, watoto walio chini ya miaka saba kipaumbele cha hifadhi hupewa mama mzazi; labda kama kutakuwa na sababu za msingi za kuto fanya hivyo. Mfano kama mama mzazi ana matatizo ya kiakili, anaishi katika mazingira hatarishi.

Mazingira ya mahali watakapoishi watoto, mfano, kama mazingira ya upande mmoja ni hatarishi kwa ustawi wa mtoto, basi haki ya hifadhi atapewa mzazi mwingine bila kujali umri.

Matakwa ya wazazi wa mtoto nani kati yao angependa kupewa hifadhi ya watoto. Mila na desturi za jamii ambayo wanandoa wametokea.

Kama mtoto anaumri zaidi ya miaka saba na ana uelewa wa kutoa mapendekezo yake, basi matakwa/maoni yake yatasikilizwa zaidi.

Haki ya hifadhi ya mtoto haimnyimi mzazi mwenza haki ya kumuona na au kumtembelea mtoto/watoto. Haki ya hifadhi ya mtoto haiondowi jukumu la baba kutoa matunzo.

images
--------

Baadhi ya hoja za wanaokubali ndoa
  • Ndoa ni heshima kwa binadamu
  • Ndoa husababisha malezi bora kwa watoto
  • Ndoa huonyesha ukomavu wa akali
  • Ndoa ndio chanzo cha Taifa imara
  • Ndoa chanzo cha maadili mema kwa Taifa
  • Ndoa hutunza mali za famili
=======
Nimeona kuna nyuzi nyingi sana hapa JF zikihamasisha vijana kupinga masuala ya ndoa. Mtu kakurupuka huko kaona familia moja ina matatizo yao basi moja kwa moja analeta uzi kuwa ndoa haifai. Ndoa zimekuwepo toka enzi na enzi na changamoto kwenye familia hazikosi lakini leo mtu anakwambia kirahisi tu eti kataa ndoa.

Ndoa ni muhimu sana kwa mwanamume na mwanamke, ile hali ya kukaa pamoja kama familia inakufanya ujihisi tofauti na kipindi kile ukiwa peke yako. Matatizo kwenye ndoa hayakosekani ila hiyo sio sababu ya kufanya kuepuka ndoa.

Hawa watu wanaopinga ndoa naona ni wakwepa majuku, vijana mnaogopa majuku ya kifamilia? Inasikitisha sana. Ewe kijana ingia kwenye ndoa ukiwa tayari umekoamaa kiakili haswa acha kupumbazwa na maneno ya watu.

Changamoto ama majukumu huwezi kuyakimbia kamwe, za kuambiwa changanya na zako.

Pia soma: Mjadala kwa wanaokataa Kuoa (Ndoa)
 
Daimond naye anaogopa Majukumu?
Vunja bei ? Je?

Ndoa ni mradi wa upigaji huwezi kuacha Legacy endapo ukioa mfano Ruge mtahaba akuwa na ndoa, kuoa ni kujiingiza katika mradi wa unyonyajii
Wengine ni masharti na maagano Ili kulinda fame.
Kama ukuishi maisha ya familia yaani baba na mama so ni rahisi kuwa negative kuhusu ndoa.
 
Wengine ni masharti na maagano Ili kulinda fame.
Kama ukuishi maisha ya familia yaani baba na mama so ni rahisi kuwa negative kuhusu ndoa.
Ni kweli aisee kama mtu umekulia kwenye mikono ya wazazi wote wawili Tena ndo Kama una wadogo zako,Kaka au dada zako Ile furaha ambavyo inatawala nyumbani Yale mapenzi kutoka kwenye familia yenu huwezi ukaacha kuoa Yani kunakuaga na hisia tofauti aisee kama mtu umepata mapenzi yote kutoka kwenye familia lazima utamani kuwa na familia yako
 
Katika uhuru wa kutoa maoni tunashuhudia kila aina ya michango kuhusiana na uzoefu juu ya maisha ikiwamo maisha ya ndoa, umuhimu wake kijamii na hata kiimani. Ni lazima watu wawe na mitazamo tofauti juu yake, kwa kuwa hata malezi hutofautiana sana.

Mtoto aliyekulia katika maisha ya uke wenza, "single parent" ama hata kukulia chini ya malezi ya ndugu wengine ambayo si ya baba na mama yake halisi, wengi wao huwa na hisia hasi juu ya umuhimu wa ndoa ama wanandoa kuishi pamoja.

Mtoto aliyekuzwa katika malezi mazuri, yaliyojaa hofu juu ya ukuu wa mamlaka ya Mungu, huiona thamani ya ndoa na umuhimu wa wanandoa kuishi kwa kicho mbele ya Mungu wao. Ndoa hii ya watu wawili kuishi pamoja kama mume na mke, kwa ajili ya kukuza familia yao.

Watu wengi huchanganya ndoa na harusi, kiasi kwamba hudhania kuwa ni kitu kimoja. Harusi ni tamasha kwa ajili ya kusherehesha ndoa. Lakini ndoa ni agano kati ya watu wawili kuishi pamoja kama familia ya mume na mke.

Hao wanaokwepa kuishi maisha kwa sababu ya gharama ni wakwepaji wa majukumu tu. Ndoa haina gharama zaidi ya mahari iendanayo na ridhaa ya kuishi na binti kutoka wazazi wake. Ni vyema ikaeleweka kuwa mahari wala siyo bei ya kumnunua mwanamke ili uweze kuishi naye.

Katika masuala ya imani, ndoa hukamilika pale mume anapopata ridhaa ya kuishi na mke kutoka kwa wazazi wa mke wake. Mambo mengine kuhusu kwenda kwenye nyumba za ibada, kutunukiwa shahada za ndoa, kufanya sherehe za harusi, zote ni mbwembwe za kibinadamu tu.
 
Mwanamke ni mzuri kwa matumizi ya muda tu (one night stand), mambo ya kugandana gandana karne hii?? Wanawake hawa hawa ambao ukishamuweka ndani anataka muwe Sawa!!!

Hit and run babake, huku ukiendelea kufukizia ndoto zako
 
Nimeona kuna nyuzi nyingi sana hapa JF zikihamasisha vijana kupinga masuala ya ndoa. Mtu kakurupuka huko kaona familia moja ina matatizo yao basi moja kwa moja analeta uzi kuwa ndoa haifai. Ndoa zimekuwepo toka enzi na enzi na changamoto kwenye familia hazikosi lakini leo mtu anakwambia kirahisi tu eti kataa ndoa.

Ndoa ni muhimu sana kwa mwanamume na mwanamke, ile hali ya kukaa pamoja kama familia inakufanya ujihisi tofauti na kipindi kile ukiwa peke yako. Matatizo kwenye ndoa hayakosekani ila hiyo sio sababu ya kufanya kuepuka ndoa.

Hawa watu wanaopinga ndoa naona ni wakwepa majuku, vijana mnaogopa majuku ya kifamilia? Inasikitisha sana. Ewe kijana ingia kwenye ndoa ukiwa tayari umekoamaa kiakili haswa acha kupumbazwa na maneno ya watu.

Changamoto ama majukumu huwezi kuyakimbia kamwe, za kuambiwa changanya na zako.
Ndoa ni mpango wa Mungu. Je kataa ndoa ni mpangonwa nani?
 
Wengi wao ni watoto ambao hawajui baba zao nani

Sent using Jamii Forums mobile app
ili lina ukweli hawaoni umuhimu wa ndoa,ni ngumu sana mtoto amekulia familia yenye heshima zake alafu akakataa kuoa ni ngumu sana;though in some cases inaweza kuwepo
pia siku hizi kama mnavyoona hali halisi baadhi ya wanaume wamekuwa magasho sasa mtu wa hivyo hawezi kuonaumuhimu wa ndoa
 
Katika uhuru wa kutoa maoni tunashuhudia kila aina ya michango kuhusiana na uzoefu juu ya maisha ikiwamo maisha ya ndoa, umuhimu wake kijamii na hata kiimani. Ni lazima watu wawe na mitazamo tofauti juu yake, kwa kuwa hata malezi hutofautiana sana.

Mtoto aliyekulia katika maisha ya uke wenza, "single parent" ama hata kukulia chini ya malezi ya ndugu wengine ambayo si ya baba na mama yake halisi, wengi wao huwa na hisia hasi juu ya umuhimu wa ndoa ama wanandoa kuishi pamoja.

Mtoto aliyekuzwa katika malezi mazuri, yaliyojaa hofu juu ya ukuu wa mamlaka ya Mungu, huiona thamani ya ndoa na umuhimu wa wanandoa kuishi kwa kicho mbele ya Mungu wao. Ndoa hii ya watu wawili kuishi pamoja kama mume na mke, kwa ajili ya kukuza familia yao.

Watu wengi huchanganya ndoa na harusi, kiasi kwamba hudhania kuwa ni kitu kimoja. Harusi ni tamasha kwa ajili ya kusherehesha ndoa. Lakini ndoa ni agano kati ya watu wawili kuishi pamoja kama familia ya mume na mke.

Hao wanaokwepa kuishi maisha kwa sababu ya gharama ni wakwepaji wa majukumu tu. Ndoa haina gharama zaidi ya mahari iendanayo na ridhaa ya kuishi na binti kutoka wazazi wake. Ni vyema ikaeleweka kuwa mahari wala siyo bei ya kumnunua mwanamke ili uweze kuishi naye.

Katika masuala ya imani, ndoa hukamilika pale mume anapopata ridhaa ya kuishi na mke kutoka kwa wazazi wa mke wake. Mambo mengine kuhusu kwenda kwenye nyumba za ibada, kutunukiwa shahada za ndoa, kufanya sherehe za harusi, zote ni mbwembwe za kibinadamu tu.
umemaliza,mkuu wanaoendesha kampeni waendeshe kwa sababu tushakuwa na watu wenye mitazamo tofauti
 
Nimeona kuna nyuzi nyingi sana hapa JF zikihamasisha vijana kupinga masuala ya ndoa. Mtu kakurupuka huko kaona familia moja ina matatizo yao basi moja kwa moja analeta uzi kuwa ndoa haifai. Ndoa zimekuwepo toka enzi na enzi na changamoto kwenye familia hazikosi lakini leo mtu anakwambia kirahisi tu eti kataa ndoa.

Ndoa ni muhimu sana kwa mwanamume na mwanamke, ile hali ya kukaa pamoja kama familia inakufanya ujihisi tofauti na kipindi kile ukiwa peke yako. Matatizo kwenye ndoa hayakosekani ila hiyo sio sababu ya kufanya kuepuka ndoa.

Hawa watu wanaopinga ndoa naona ni wakwepa majuku, vijana mnaogopa majuku ya kifamilia? Inasikitisha sana. Ewe kijana ingia kwenye ndoa ukiwa tayari umekoamaa kiakili haswa acha kupumbazwa na maneno ya watu.

Changamoto ama majukumu huwezi kuyakimbia kamwe, za kuambiwa changanya na zako.
Hongera sana Kwa ujumbe kuoa sio tatizo tatizo kuoa virus au mchawi, anakutimua kama mfungwe Ile dhana ya upamoja na kuanzisha family haipo, mwanamke anaishi kama hajaondoka kwao, akiwa na wewe kama yuko Oman anachuma ili arudi kwao afanye mambo yake binafsi ya maendeleo.

Namalizia mtajijua wenyewe mi ntapangisha sitaoa
 
Back
Top Bottom