MJADALA: Je, ni kwa namna gani YouTube humlipa mmiliki wa account?

srinavas

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
4,025
3,588


MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU MADA HII
Habari ndugu zangi ,
Kama kichwa kinavyouliza hapo , ningependa kujua ni kwa namna gani kupata subscribers wengi na viewers wengi kwenye you tube , kunaweza kukunufaisha mmiliki...

Tafadhali kama kuna mwenye majibu , ushuhuda, uzoefu au elimu yoyote kwenye hili anijuze na mchanganuo mzima.

Natanguliza shukran zangu za dhati kabisa.
---
---
Habari ndugu zangu mimi Nina channel ya YouTube lakini ninahitaji masaada mnielekeze au mnifundishe jinsi channel yangu kuwa online. Natanguliza shukurani

BAADHI YA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU
---
---
---
---
---
---
---
 
Mimi wananilipa kwa electronic transfer moja kwa moja kwenye account yangu. Kutegemea na nchi uliyopo wanasupport check, EFT, Western Union etc.
 
Mimi wananilipa kwa electronic transfer moja kwa moja kwenye account yangu. Kutegemea na nchi uliyopo wanasupport check, EFT, Western Union etc.
Na mchanganuo wake ndio upoje? Na wewe ni channel yako gani wanayokulipia? Unaweza nipatia link tafadhali nikaiona!?
 
wanalipa kutokana na views,advertisement(Pay-per-click (PPC),
ila ninavyojua ili uweze kulipwa lazima umonetize account yako kwanza,content zako ziwe original(video unazoweka,miziki,yote isiwe na copyright)
ikiwa na copyright nyingine zinafutwa,au earning zinakwenda kwa mwenye original content
..1000views=1.30$
 
Na mchanganuo wake ndio upoje? Na wewe ni channel yako gani wanayokulipia? Unaweza nipatia link tafadhali nikaiona!?

Kwa kifupi unachotaka ni views na "engagement".
Makampuni wanawalipa Youtube (Google) kuweka matangazo yao youtube na kila mtu akiangalia tangazo wakati yupo kwenye video yako basi na wewe unapewa vijisenti.

Ni vigumu sana kujua utapata kiasi gani maana inategemea mambo mengi sana, aina ya tangazo, alipo mwangaliaji etc. Pia anapo click tangazo unapata kiasi fulani.

Mtu anapofungua video yako na kuiangalia kwa angalau sekunde 30 hiyo ni view ila sio kila view itakupatia hela maana sio kila mara wanaonyesha tangazo.

Kuna hizi calculator online zinakupa kadirio la mapato kutokana na views
Estimated Youtube Money Calculator (By Social Blade)

Ushauri wa kawaida ni kufocus kwenye niche (sekta) moja kwenye channel yako ya youtube so kama ni games basi kila siku iwe games au vitu vinavyohusiana ili watu wajiunge na channel yako na wawe wanaangalia video kila unapotoa.

Jihadhari na kubandika kazi za watu za aina yoyote maana hii ina penalty zake ikiwemo kufungiwa account. Kumbuka kuwa hata game ni kazi za watu na watengeneza game wakikumind wanakubania.

Nisengependa kuweka channel yangu humu ila inadeal na mambo ya technolojia.
 
Na nikitaka kuweka muziki au video yangu Youtube ili kuiuza kwa viewers. Steps ni zipi
 
Wakuu, naomba msaada nimesumbuka na hili swali muda sasa. Hivi msanii anapoweka video YOUTUBE anipigia promo hili watu waitazame hivi anapataga faida gani?

Je, huwa anaingiza pesa?? kama anaingiza ni kwa jinsi gani?

Je, kama anaingiza nini kinaonesha kuwa anastahili kulipwa?

Je, kama analipwa analipwa na nani na kwa jinsi gani?

Kama zinamuinguzia hela kupitia Viewers je ni idadi gani inahitajika au wanamcalculateje?
WAKUU NAOMBA MSAADA KWA WANAO FAHAMU.
 
Wasanii au mtu yoyote mwenye channel iliyothibitishwa na Youtube anaweza kuingiza kipato kupitia matangazo yanayowekwa katika video mfano wa matangazo hayo ni matangazo ya video(Skippable Ads) ambayo huanza kuonekana kabla ya video husika kuanza kucheza pia kuna matangazo ya graphics(overlay) ambayo hutokea ndani ya video huwa yanaonekana zaidi chini ya video na mengine huonekana nje ya video pembeni.

Matangazo haya huwa yanatolewa kupitia mfumo wa matangazo kwenye mitandao unaojulikana kama adsense ambao unamilikiwa na google na hela inayopatikana kupitia haya matangazo hugawanywa kwa asilimia kati ya Youtube na mtu anayemiliki channel ya Youtube inayodisplay matangazo hayo mfano msanii au mtu yoyote anayemiliki channel ya youtube na malipo hufanyika kupitia Western Union,Cheque au Wire Transfer kwenda kwenye account ya Bank.

Watu wengi wamekuwa wakitumia vibaya mfumo huu kwa kupakia video zinazohamasisha ngono, mauaji, ubaguzi au kuiba na kupakia video amabazo hawazimiliki jambo ambalo ni kinyume na taratibu za Youtube na matokeo yake huwa ni channel yako kufungiwa au kupelekwa mahakamani.
 
Kuna Aina Nyingi Za Kuingiza Pesa Kupitia YouTube Channel.

1. Google Adsense
- Hii Ni Program Ya Google Wenyewe, Wana Kitengo Chao Cha Matangazo Kinaitwa Google Adwords (Hata Wewe Kama Una Biashara Yako Unaweza Kutangaza Pia), Kwahiyo Wafanyabiashara Wanapotangaza Kupitia Hiyo Program, Hayo Matangazo Unaweza Kuyafanya Yakawa Yanaonekana Kwenye YouTube Channel Yako Kupitia Setting (Utaona Kuna Kisehemu Kimeandikwa Monetize Your Account).

2.Direct Ads
- Hata Inatokea Kama Channel Yako Imekuwa Maarufu Sana ( Eg Diamond Platnumz & AyoTv ) Na Inatazamwa Na Watu Wengi Zaidi, So Makampuni Yanaweza Kutangazwa Kupitia Channel Yako Directly, Mfano. VodaCom Wanatangaza Directly Kwenye AyoTV Na Diamond Alipata Direct Ad Kutoka Kwa Dr Mwaka.

3.Affiliate Marketing
- Hii Mara Nyingi Ni Kwa Wale Ambao Hutengeza Tutorials, Unaweza Kufundisha Watu Kufanya Make Up, Then Ukawapa Direct Link Ya Amazon Ya Hizo Bidhaa Unazotumia, Wakizinunua Unapata Commission.

N.B: Hakikisha Video Ni Zako Na Ni Quality, Na Si Za Ubaguzi Au Ngono
 
Labda nami niulize ni jinsi gani wasanii wanavyoweka miziki yao YouTube maana huwa kuna kitu napenda nikiweke you tube
 
Wapendwa naomba kujua juu ya mitandao ulipwaji wake na faida zake mfano kama youtube nk ukilinganisha na biashara zisizo za mtandaoni.

Kichuguu,
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…