Mjadala huru! Ni sekta ipi inayoendeshwa na Serikali inafanya vizuri?

Serikali imefanikiwa Sana kwenye magereza.

Weekend moja tu ukiwa magerezani unakua umeelewa somo.
 
1. Mradi wa mwendokasi Dar. Huku mabasi hayafanyiwi maintainance, yanaharibika watu hawajali, kila siku watu zaidi ya laki 1 wanatumia mabasi haya na fedha zinakusanywa na mamlaka husika Ila kila siku mradi uko hovyo! Vituo vyake vinazidi kuchakaa na mabasi yanazidi kuchakaa. Haieleweki Kama waliopewa kazi ya kuendesha mradi hawawezi au la! Serikali ndo wanaendesha mradi

2. Bandari za Dar, Mtwara, Kigoma, Mwanza. Huku nako hakueleweki, mapato yanakusanywa Ila inaelezwa ni kidogo kuliko ilivopaswa! Ucheleweshwaji wa mizigo kila siku imekuwa wimbo. Serikali ndo wanaendesha mradi ingawa Kuna sehemu ndogo imewasha sekta binafsi ambayo inasemwa hii haina malalamiko sana!

3. Reli ya Kati. Hii imeanzia Dar , inaenda Mwanza, Kigoma na Katavi, huku nako hakufai. Treni zina hali mbaya , miundombinu nayo haifai. Kila siku ni bora ya jana na wasafiri wanaotumia usafiri huu wanaelewa hali ikoje.

4. Reli ya TAZARA. Hii aieleweki kama iko hai ama imekufa. Kwa ufupi haieleweki

5. Viwanja vya mpira mikoa yote ukiwemo uwanja wa Taifa. Hii nayo haifai iko hovyo kwenye hali mbaya kupindukia. Uwanja wa a Taifa ndo hadi watu wanakojoa kwenye masinki ya vyoo!

6. Vituo vya mabasi. Hivi viko hoehahe. Kila siku mapato makubwa yanakusanywa Ila haieleweki yanaenda wapi

Kwa mtazamo wangu naunga mkono Bandari ya Dar es Salaam kupatiwa mwekezaji binafsi kuiendesha. Serikali isimamie kitengo cha ulinzi wa Usalama tu. Pia katika kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye Bandari Bandari zote ziendeshwe kwa mfumo huo. Kikubwa apatikane mwekezaji wa maana tu kama Mwekezaji aliyepewa NMB na wawekezaji wengine makini ambao tumeona walivyofanya kazi nzuri!

Trafic kukusanya fine
 
Kazi ya serikali sio kufanya biashara,lazima mambo yaende hovyo.
Pole sana tena sana.

Ungejua China kafikia hapo alipo kwa serikali kufanya biashara.

Huo ujinga wa kubinafisisha kila kitu baadhi ya nchi za ulaya wanajilaumu.

Mi sikubaliani na mpango wa Mama, nitaupinga siku zote hata kama ukifanikiwa kwa sababu siyo sustainable.

Leo hii ukikichafua NMB akiondoka muwekezaji bank inakufa.

Namshauri Mama awe na uzalendo kama wa Dkt Magufuli, tusikalili njia za maendeleo kama za ulaya bali tuangalie mazingira yetu, ni afadhali hela wanazoiba akina Mwigulu au akina Nape maana wataziweka Tanzania na zitakuwa kwenye mizunguko lakini ukileta muwekezaji atakuwa anazihamisha
 
1. Mradi wa mwendokasi Dar. Huku mabasi hayafanyiwi maintainance, yanaharibika watu hawajali, kila siku watu zaidi ya laki 1 wanatumia mabasi haya na fedha zinakusanywa na mamlaka husika Ila kila siku mradi uko hovyo! Vituo vyake vinazidi kuchakaa na mabasi yanazidi kuchakaa. Haieleweki Kama waliopewa kazi ya kuendesha mradi hawawezi au la! Serikali ndo wanaendesha mradi

2. Bandari za Dar, Mtwara, Kigoma, Mwanza. Huku nako hakueleweki, mapato yanakusanywa Ila inaelezwa ni kidogo kuliko ilivopaswa! Ucheleweshwaji wa mizigo kila siku imekuwa wimbo. Serikali ndo wanaendesha mradi ingawa Kuna sehemu ndogo imewasha sekta binafsi ambayo inasemwa hii haina malalamiko sana!

3. Reli ya Kati. Hii imeanzia Dar , inaenda Mwanza, Kigoma na Katavi, huku nako hakufai. Treni zina hali mbaya , miundombinu nayo haifai. Kila siku ni bora ya jana na wasafiri wanaotumia usafiri huu wanaelewa hali ikoje.

4. Reli ya TAZARA. Hii aieleweki kama iko hai ama imekufa. Kwa ufupi haieleweki

5. Viwanja vya mpira mikoa yote ukiwemo uwanja wa Taifa. Hii nayo haifai iko hovyo kwenye hali mbaya kupindukia. Uwanja wa a Taifa ndo hadi watu wanakojoa kwenye masinki ya vyoo!

6. Vituo vya mabasi. Hivi viko hoehahe. Kila siku mapato makubwa yanakusanywa Ila haieleweki yanaenda wapi

Kwa mtazamo wangu naunga mkono Bandari ya Dar es Salaam kupatiwa mwekezaji binafsi kuiendesha. Serikali isimamie kitengo cha ulinzi wa Usalama tu. Pia katika kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye Bandari Bandari zote ziendeshwe kwa mfumo huo. Kikubwa apatikane mwekezaji wa maana tu kama Mwekezaji aliyepewa NMB na wawekezaji wengine makini ambao tumeona walivyofanya kazi nzuri!
KAKA UMWNENA VEMA,SIKUPINGI,ILA NIIJUAVYO BANDARI TUKIIWWKEA MBIA TUMEKWISHA.

HAKUNA MWAKA HATA MMOJA BANDARI HAIPELEKI RUZUKU. SECTOR ZINGINE NAKUUNGA MKONO.

ILA UMESAHAU TANESCO. HUKO NDO PAKUTAFUTIWA MBIA,NA WALA SI MBIA NI MAKAMPUNI YAPEWE FURSA YA KUGAWIA UMEME WANANCHI.

LA BANDARI NITAPINGANA NA WEWE DAIMA. MKIFANYA HIVYO MTACHEKWA.

NIONYESHE MFANO MMOJA TU WA BANDARI KUBWA ILIYOTAFUTIWA MBIA . KATIKA BANDARI ZA BAHATI KUU.
 
Ina maana hujui tatizo la hii nchi ni nini au unataka uambiwe alafu uite watu timu pinga pinga FC.
 
Pole sana tena sana. Ungejua China kafikia hapo alipo kwa serikali kufanya biashara. Huo ujinga wa kubinafisisha kila kitu baadhi ya nchi za ulaya wanajilaumu. Mi sikubaliani na mpango wa Mama, nitaupinga siku zote hata kama ukifanikiwa kwa sababu siyo sustainable. Leo hii ukikichafua NMB akiondoka muwekezaji bank inakufa. Namshauri Mama awe na uzalendo kama wa Dkt Magufuli, tusikalili njia za maendeleo kama za ulaya bali tuangalie mazingira yetu, ni afadhali hela wanazoiba akina Mwigulu au akina Nape maana wataziweka Tanzania na zitakuwa kwenye mizunguko lakini ukileta muwekezaji atakuwa anazihamisha
Kikubwa ni nchi kupata mapato stahiki!

Kama mwekezaji akiwa analeta mapato mengi kuliko tunavyopata sasa shida iko wapi?
 
KAKA UMWNENA VEMA,SIKUPINGI,ILA NIIJUAVYO BANDARI TUKIIWWKEA MBIA TUMEKWISHA. HAKUNA MWAKA HATA MMOJA BANDARI HAIPELEKI RUZUKU. SECTOR ZINGINE NAKUUNGA MKONO.ILA UMESAHAU TANESCO. HUKO NDO PAKUTAFUTIWA MBIA,NA WALA SI MBIA NI MAKAMPUNI YAPEWE FURSA YA KUGAWIA UMEME WANANCHI. LA BANDARI NITAPINGANA NA WEWE DAIMA. MKIFANYA HIVYO MTACHEKWA. NIONYESHE MFANO MMOJA TU WA BANDARI KUBWA ILIYOTAFUTIWA MBIA . KATIKA BANDARI ZA BAHATI KUU.
Bandari za New York, Singapore na Rotterdam zinaendeshwa na private sector hasa kwenye upande wa operations!
 
"5. Viwanja vya mpira mikoa yote ukiwemo uwanja wa Taifa. Hii nayo haifai iko hovyo kwenye hali mbaya kupindukia"

Mkuu, hilo kuhusu viwanja vya michezo, karibu vyote ni vya CCM.

Ijapokuwa vilijengwa na wananchi kwa kushirikiana na serikali, CCM iliamua kuvichukua vingi kama mali zake binafsi.
 
Viwanja vya mpira mikoa yote ukiwemo uwanja wa Taifa. Hii nayo haifai iko hovyo kwenye hali mbaya kupindukia. Uwanja wa a Taifa ndo hadi watu wanakojoa kwenye masinki ya vyoo!
Hivi vilitakiwa kuwa mali ya umma ila chama dola walijimilikisha tu kihuni.
 
Hivi vilitakiwa kuwa mali ya umma ila chama dola walijimilikisha tu kihuni.
Hi vizuri kuonesha huo uwezo wako kwa kujibu swali uliloulizwa!

Kushindwa kujibu swali ni kielelezo tosha kuwa huna uwezo wowote ule!
 
Mimi siku nikiwa rais wa hii nchi. ntabinafisha kila kitu na kuacha sekta muhimu km za maji, afya, usafiri na umeme...maana ishajihidhirisha serikali haiwezi kufanya biashara kutokana na incompetent culture ambayo imeshamiri miongoni mwa wafanyakazi wa serikali

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Wewe utauza mpaka urithi wetu (hifadhi za taifa zote), Kinapa, Ngorongoro n.k

Mungu atuepushe na mtu wa dizaini yako.
 
Hi vizuri kuonesha huo uwezo wako kwa kujibu swali uliloulizwa! Kushindwa kujibu swali ni kielelezo tosha kuwa huna uwezo wowote ule!
Ungekua umeuliza swali usingejijibu mwenyewe mwishoni.

Halikuwa swali hilo ila ni sehemu ya hoja ya kuhalalisha ubia wa kuendesha bandari.
 
Back
Top Bottom