Hizi ndio sababu BRT (Mwendokasi) kukosa mwekezaji, na hatatokea hadi marekebisho yafanyike

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,111
18,327
Mwendokasi sasa hivi inaendeshwa kwa hasara tena hasara kubwa, yamkini hata vipuri au mafuta yanatikana na mkono wa serikali.

Zipo sababu lukuki kwa nini shirika kama Udart kuendeshwa kwa hasara kwenye jiji lenye watu mil 5 na zaidi.

Wakati mwendokasi bado ipo chini ya uangalizi wa world bank mambo yalikua mazuri sana.

1. Fedha zote zilikusanywa kwa njia ya kieletronic na kampuni ya maxicom na ilikua audited.. kampuni hii ilikua na kazi moja tu ya kukusanya fedha(nauli)

2. Mwenye mabasi yeye alikua na kazi moja tu ya kuhakikisha abiria wanafika kwa wakati wanako kwenda.

3. Njia zote zinapo ambazo kuna mwendo kasi daladala, bajaji au chochote cha kubeba abiria hakikuruhusiwa na lengo lilikua na kuondoa msongamano na kupunguza pulution, na kuna wakati walitaka wajenge parking za magari madogo kimara, morocco na kariakoo ili watu waache magari hapo watumie public transport, na ulikua usafiri mzuri sana , nina kadi yao hadi leo.

Walikua wanapata makudanyo ya kutosha hata kuongeza mabasi kwa fedha zinazo tokana na mwendokasi.

Hali ipoje sasa.

1. Mapato yanakusanywa kwa mikono na ni cash.

2. Abiria wamepungua kwa sababu ya kuruhusu bajaji ambazo kisheria haziruhusiwi kufanya kazi kama public transport. Juzi nimekuta bajaji ya kutoka kimara hadi magomeni inapigiwa debe mchana kweupe.

3. Mapato yanakusanywa na wafanyakazi wa udart kitu ambacho kina palilia upigaji.

4. Serikali ina asilimia 80 kwenye udart hivyo udart ni UDA yenye rangi za blue badala ya rangi nyekundu.

Kwanini hatuwezi kupata mwekezaji

1. Serikali kuruhusu bajaji kufanya ruti kwenye ruti za mwendokasi kimepunguza sana abiria kiasi ambacho kwa mwekezaji mwenye akili hawezi kuja kutupa fedha sehemu ambayo haina utaratibu.

2. Serikali kuto weka kipaumbele matumizi ya public transport kwa kuweka miundo mbinu mizuri ya watu kuacha magari yao na kutumia mwendokasi, hakuna vituo vya kuacha magari wala pikipiki.

Hizo sababu mbili zisipo patiwa ufumbuzi, ni ngumu sana kupata mwekezaji serious, ukiona amepatikana ujue ni magumashi na ameoatikana kimagumashi.

Wito, serikali ituone huruma wananchi, tunahitaji maisha mazuri, kodi zinatumika kujenga miundo mbinu ambayo mwisho wa siku haitumiki.

Jiji lazima liwe na utaratibu, hata kama hakuna ajira hatuwezi kuachia jiji la ajabu chafu lisilo na mpangilio.

Wekeni utaratibu, bajaji na bodaboda ziwe feeder kutoka majumbani hadi kituoni.

Sasa hivi bodaboda na bajaji wote wanafanya kazi as public transport..

Asanteni.
 
Abiria wanajazana vituoni kwasababu ya ukosefu wa usafiri ajabu kule kwenye karakana yao kuna mabasi mengi yameozea kule baada ya kukaa muda mrefu bila kutengenezwa.

Hizo pesa zinazokusanywa kwenye huo mradi sijui zinafanyia kazi gani, serikali imelala sana wachache ndio wanajinufaisha na huo mradi huku wengi wakiumia.
 
Mwendokasi sasa hivi inaendeshwa kwa hasara tena hasara kubwa, yamkini hata vipuri au mafuta yanatikana na mkono wa serikali.

Zipo sababu lukuki kwa nini shirika kama Udart kuendeshwa kwa hasara kwenye jiji lenye watu mil 5 na zaidi.

Wakati mwendokasi bado ipo chini ya uangalizi wa world bank mambo yalikua mazuri sana.
Nimekuelewa sana bro

Hiyo pesa kutoka kukusanywa na Max malipo Hadi kukusanywa cash ni mipango ya watu Ili waibee kirahisi

Hi nchi ngumu sana
 
Sidhani kama upo SAWA hasa hapo kwenye BAJAJ+ BODABODA

Shida kwa mujibu wa waliokuwa wabunge wa UKAWA Dar+ Ex Dar Mayor Mwita,ni

1. Kuwepo kwa Magumashi toka huu mradi upo kwenye makaratasi..vitu vingi havikuwa kweli ,wawekezaji ,Kisena et al hawakuweka mitaji kama ilivyotakiwa,Najua unafahamu huyo mwizi Kisena ni Mfungwa kwa sasa

2.Bei ya mabasi iliongezwa na kumbuka ulikuwa ni MKOPO

3.Mabasi mengi yaliletwa mikweche.

4.Uongozi mbovu uliogubikwa na ufisadi,kuanzia kwenye mafuta + hizo tiketi

Kwa ufupi ni hayo,kafanye Homework yako vizuri..nimekupa na watu wakuwaona
 
2. Abiria wamepungua kwa sababu ya kuruhusu bajaji ambazo kisheria haziruhusiwi kufanya kazi kama public transport. Juzi nimekuta bajaji ya kutoka kimara hadi magomeni inapigiwa debe mchana kweupe.
Abiria wameopt for bajaj baada ya kukosa matumaini kwenye huo mwendokasi.

Ukitazama kwa umakini akili za viongozi ndizo zimekosa utashi kwakuwa wameondoa coasters na hiace na kuingiza vijidude vidogovidogo vingi ambavyo vinarudisha tatizo la traffic mjini kama zamani, sababu ya mwendokasi ilikuwa kuweka magari machache yenye kuchukua watu wengi kwa wakati mmoja

Moja ya sababu ya kuua mwendokasi ni kutengeneza ustawi wa biashara za wakubwa, hili ndilo linafanyika kila mji hivi sasa, hivyo vingi ya hivyo bajaj ni biashara za viongozi, kwahiyo ili wafanye biashara lazima waminye upande shindani na hayo ya kushindwa kwa mwendokasi ni juhudi za viongozi hawahawa
 
Tatizo la mwendokasi hakuna SERIOUS DEDICATED MANAGEMENT.
Mkuu wa Sasa alikua mkuu wa wilaya huko Rombo. Si ajabu maskini Kama kasomea uchumi au business management au ujuzi hata wa kusimamia daladala za Mbagala Mtoni Kijichi.

WHAT DO YOU EXPECT
 
Bajaji na bodoboda wala sio sababu, hayo mabasi yanavyojaza, bila bajaji na boda ingekuwaje.Ni sawasawa useme gari binafsi zinapelekea kufa kwa mwendokasi.Wao waboreshe watu wataamia tu
 
Sidhani kama upo SAWA hasa hapo kwenye BAJAJ+ BODABODA

Shida kwa mujibu wa waliokuwa wabunge wa UKAWA Dar+ Ex Dar Mayor Mwita,ni

1. Kuwepo kwa Magumashi toka huu mradi upo kwenye makaratasi..vitu vingi havikuwa kweli ,wawekezaji ,Kisena et al hawakuweka mitaji kama ilivyotakiwa,Najua unafahamu huyo mwizi Kisena ni Mfungwa kwa sasa

2.Bei ya mabasi iliongezwa na kumbuka ulikuwa ni MKOPO

3.Mabasi mengi yaliletwa mikweche.

4.Uongozi mbovu uliogubikwa na ufisadi,kuanzia kwenye mafuta + hizo tiketi

Kwa ufupi ni hayo,kafanye Homework yako vizuri..nimekupa na watu wakuwaona
Hakuna uhusiano na unacho kiongea kwa sababu hawa binafishi haya mabasi ya sasa, mqekezaji anakuja na mabasi yake.. tatizo hawezi kupata faida kwenye mazi gira kama haya ambayo hayasimamiwi ipasavyo
 
Bajaji na bodoboda wala sio sababu, hayo mabasi yanavyojaza, bila bajaji na boda ingekuwaje.Ni sawasawa useme gari binafsi zinapelekea kufa kwa mwendokasi.Wao waboreshe watu wataamia tu
Yanajaza kwa sababu ya uchache wa mabasi,
 
Tatizo la mwendokasi hakuna SERIOUS DEDICATED MANAGEMENT.
Mkuu wa Sasa alikua mkuu wa wilaya huko Rombo. Si ajabu maskini Kama kasomea uchumi au business management au ujuzi hata wa kusimamia daladala za Mbagala Mtoni Kijichi.

WHAT DO YOU EXPECT
Solution nyingine ni kuipeleka udart DSE
 
Nimekuelewa sana bro

Hiyo pesa kutoka kukusanywa na Max malipo Hadi kukusanywa cash ni mipango ya watu Ili waibee kirahisi

Hi nchi ngumu sana
Hahahahahah yeye alifikiri hilo limetokea bahati mbaya😁? Bongo mzalendo alikuwa Nyerere tu ila sahizi kila mtu jambazi mwenye vyeti vya chuo kikuu😂! Naskia watu wamebuni reciept zao kabisa wanajikusanyia mawe tu.
 
Mji haujapangika yaani watu wanaokaa ubungo ,kimara hiyo Morogoro road wote sio wastarabu.

Mpangilio upo hovyo ,watu ni wengi sana
 
Back
Top Bottom