Sekta Binafsi Wakaribishwa Kuwekeza Katika Reli

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuboresha reli ya TAZARA pamoja na reli ya kutoka Dar es Salaam ,Tanga mpaka Kilimanjaro ili reli hizo ziweze kufanya kazi kwa ufanisi Mkubwa.

Kihenzile ameyasema hayo kwenye kongamano la Reli linalofanyika jijini Mwanza ambapo limewakutanisha wadau wa ndani nan je ya Nchi.

“Pamoja na serikali kuendelea na ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa vipande sita na vipande viwili vimeshakamilika vipande vya Dar es Salaam Morogoro na Morogoro Makutopora, Vilevile serikali ya awamu ya Sita inaendelea kuboresha reli ya TAZARA na Reli ya Dar es Salaam, Tanga mpaka Arusha ili iweze kubeba Mzigo wa kutosha.” Alisema Kihenzile.

Pia Kihenzile amewataka watanzani kutembea vifua mbele kwa miradi inayotekelezwa kwani zaidi ya kilometa 4700 za reli zinajengwa pia reli itajengwa kutoka Tabora kwenda Kigoma, Msongati mpaka Kindu DRC.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Uchukuzi Prof. Godius Kihyarara amesema wamefungua milango kwa sekta binafsi kuwekeza katika reli ili kuongeza ushindani na katika usafairishaji kutumia reli.

“ Tunakaribisha Sekta binafsi kuja kuwekeza katika reli, uje na Vichwa na Mabehewa ili tuongeze kasi ya usafirshaji na Sheria zetu zinaruhusu” Alisema Kahyarara

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha Mabehewa pamoja na vichwa vya treni hivyo kukaribisha Sekta binafsi kuwekeza kwenye Miundombinu ya Usafiri., Lengo kujenga Reli yenye urefu wa Kilometa zaidi ya 4700.

Huku Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amosi Makala amewataka wananchi na viongozi kujipanga katika kuhakikisha wanatumia vema bandari kavu ya fela katika kusafafirisha mizigo.

Kongamanao reli linafanyika kwa siku mbili jijini Mwanza kwa lengo la kukaribisha sekta binafsi kuwekeza kwenye reli, katika kongamanon hilo wawekezaji kutok nchi mbalimbali wamsehiriki pia wakuu wa mikoa ya Morogoro, Tabor ana Mwanza wamelezea fursa zilizopo katika mikoa yao katika sekta ya Reli.

GH5Sao1WMAAffNJ.jpg
GH54AJXWgAA8WlP.jpg
 
Ni wakati sasa matajiri wa mabasi kuungana pamoja na kuona wanafanyaje kuoperate mf, reli dar-tanga - moshi - arusha kwa ufanisi mkubwa!, wasiogope, waandae mpango kazi waanzishe bullet train la kaskazini! /
 
.Natamani kusikia Tenda ya Kuwakaribisha Sekta Binafsi ili Kuingia Ubia wa Kuendesha Serikali ikitangazwa, kwa sababu hicho ndio kiini cha matatizo karibu yote tuliyonayo hapa barani Afrika.
 
Back
Top Bottom