Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,227
- 26,048
1. Mradi wa mwendokasi Dar. Huku mabasi hayafanyiwi maintainance, yanaharibika watu hawajali, kila siku watu zaidi ya laki 1 wanatumia mabasi haya na fedha zinakusanywa na mamlaka husika Ila kila siku mradi uko hovyo!
Vituo vyake vinazidi kuchakaa na mabasi yanazidi kuchakaa.
Haieleweki Kama waliopewa kazi ya kuendesha mradi hawawezi au la! Serikali ndo wanaendesha mradi
2. Bandari za Dar, Mtwara, Kigoma, Mwanza.
Huku nako hakueleweki, mapato yanakusanywa Ila inaelezwa ni kidogo kuliko ilivopaswa! Ucheleweshwaji wa mizigo kila siku imekuwa wimbo.
Serikali ndo wanaendesha mradi ingawa Kuna sehemu ndogo imewasha sekta binafsi ambayo inasemwa hii haina malalamiko sana!
3. Reli ya Kati. Hii imeanzia Dar , inaenda Mwanza, Kigoma na Katavi, huku nako hakufai. Treni zina hali mbaya , miundombinu nayo haifai.
Kila siku ni bora ya jana na wasafiri wanaotumia usafiri huu wanaelewa hali ikoje.
4. Reli ya TAZARA. Hii aieleweki kama iko hai ama imekufa. Kwa ufupi haieleweki
5. Viwanja vya mpira mikoa yote ukiwemo uwanja wa Taifa. Hii nayo haifai iko hovyo kwenye hali mbaya kupindukia.
Uwanja wa a Taifa ndo hadi watu wanakojoa kwenye masinki ya vyoo!
6. Vituo vya mabasi. Hivi viko hoehahe. Kila siku mapato makubwa yanakusanywa Ila haieleweki yanaenda wapi
Kwa mtazamo wangu naunga mkono Bandari ya Dar es Salaam kupatiwa mwekezaji binafsi kuiendesha.
Serikali isimamie kitengo cha ulinzi wa Usalama tu. Pia katika kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye Bandari Bandari zote ziendeshwe kwa mfumo huo.
Kikubwa apatikane mwekezaji wa maana tu kama Mwekezaji aliyepewa NMB na wawekezaji wengine makini ambao tumeona walivyofanya kazi nzuri!