Fahamu faida za Kushirikiana na Sekta Binafsi katika Uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam

Maryam Malya

Senior Member
Nov 29, 2021
115
258
1. Kuongeza ufanisi na tija katika Bandari ya Dar es Salaam

Hii ni pamoja na kupunguza muda wa meli kusubiri nangani kutoka siku 5 hadi masaa 24 na kupunguza muda wa kupakia na kupakua makasha kutoka siku 4.5 hadi siku 2.

2. Kuongezeka kwa Mapato ya Serikali

Ushirikiano huu utaongeza mapato kwa Serikali kutokana na ongezeko la wateja (shehena) na shughuli za kibandari kwa ujumla.

3. Kupungua kwa Gharama za Usafirishaji

Ushirikiano na Sekta binafsi utapunguza gharama za kuhudumia mizigo katika Bandari ya Dar es salaam kwa asilimia 50 na kuifanya Bandari yetu kuwa na gharama ndogo kulinganisha na majirani zetu jambo litakaloongeza idadi kubwa ya wateja.

4. Kudhibiti wakwepa Kodi

Ushirikinano na Sekta Binafsi utaziba mianya yote ya ukwepaji kodi katika Bandari ya Dar es salaam unaotokana na ukosefu wa mifumo ya kisasa na wateja wasio waamifu kutoa taarifa za uongo kuhusu mizigo (under declaration of goods) kwa kutumia mfumo wa Electronic Data Interchange (EDI) ambao utanasa taarifa sahihi za mizigo.

5. Kuongeza ushindani wa Bandari ya Dar es Salaam

Gharama kupungua kwa asilimia 50, ufanisi kuongezeka na ukiritimba kufutika katika Bandari ya Dar es Salaam kutaifanya iweze kushindana vizuri sokoni na kushinda deals nyingi kubwakubwa ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikienda kwa majirani zetu, hili litaongeza mapato ya Serikali na kunufaisha wananchi kupitia miradi lukuki ya maendeleo.

6. Kuongeza Ajira Serikalini

Ongezeko la wateja litakaloletwa na Sekta Binafsi litasababisha kuongezeka kwa ajira za maeneo mbalimbali Serikali yanayohusiana na shuguli za bandari kutoka waajiriwa 28,990 hadi waajiriwa 71,907 (direct and indirect jobs).

NB: Faida hizi ndizo zinazisababisha baadhi ya wananchi 'wakeshe wakiomba' Serikali imalizane na DP World mapema ili tuanze kunufaika kama Taifa.
 
Kwani kuna mtu anapinga sekta binafsi kuwekeza bandarini?
Tofautisha kati ya kuwekeza na kuuza!
 
Tunataka mkataba ambao utainufaisha nchi si kikundi cha watu wachache kama Rostam Aziz na genge lake la majangili.
 
Back
Top Bottom