Miti inakua kutoka wapi? Mbona hatuoni shimo pale ulipotoka?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,052
12,421
Habari wakuu sana. Eti wakuu. Miti inakua kutoka wapi? Mbona unakuta mti mkubwa sana. Una kilo hata milioni moja(ukiwa mkavu), lakini pale ulipotoka hatuoni kama kuna kilo milioni moja zimetoka. Mti unatoka wapi?

General_Sherman_Tree_2013.jpg
800px-Adansonia_grandidieri04.jpg
Fony_baobab.jpg
800px-Adansonia_digitata_Baobab.jpeg
US_199_Redwood_Highway.jpg
 
Mti unatoka chini sana na ukitaka kujua unaanzia wapi usiukate hata mzizi wake mmoja ufuate kuelekea chini ndio utaona ulivyojishikilia na ukubwa wa shimo lakeView attachment 2418033View attachment 2418034
Sasa mbona unapotoka hatuoni shimo? Maana unatengeneza mzizi huko chini na kuinua shina kubwa huku juu. Tulitegemea ile ujazo
na hasa uzito wa shina, kuwe na shimo lenye ujazo/uzito kama huo chini pale.
 
Ngoja nisaidie mtoa mada kufanya watu wamwelewe.

Yaani anamaanisha kuwa mti huinyonya dunia (ardhi) katika ukuaji wake kwenda juu. Kama mti utakuwa na uzito wa tani 8 hivyo utakuwa umechukua tani nane ya udogo toka uliposimamia. Ni kama jengo la tani 8 ili lijengwe litasababisha shimo kwa ajiri ya udongo huo wa tani nane ulipotoka.

Sasa swali lake ni kuwa. Mti umechukua tani nane duniani ukazipandisha juu kama wajenzi wa majengo wafanyavyo. Je yale mashimo ya hiyo sehemu inayonyonywa na miti mbona hatuyaoni. Je mti hupata malighafi kutoka mbali na eneo ulipo kama majengo ya mjini yananyosombewa mchanga na magari toka mtoni ili yasimame hapo Nyerere road?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom