Maafande wa mchongo

Maafande wa mchongo

baharia 1

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2019
Posts
2,973
Reaction score
4,332
Wagambo na Sungusungu acheni ushamba! Mna uafande wa mchongo, sura za kauzu na njaa kali

Hawa Sungusungu/Wagambo (Nyungu) mbona wana roho mbaya hivi? Wakifanikiwa kuwa Maaskari kamili si watavunja watu viuno.

Wakuu wa jukwaa, kwanza salamu.

Leo nataka niwape makavu laivu Hawa viumbe, bila kuremba wala kuweka urembo wa aina yoyote.

Kuna hili kundi la watu wanaojiita ulinzi shirikishi, maarufu kama Sungusungu, Wagambo, au Nyungu.

Hivi hawa viumbe mbona wana roho mbaya na roho za kwanini kiasi hiki?

Unakuta mtu ni mlinzi tu wa mtaani lakini akikatiza mchana kweupe sura ameikunja kama amekunywa shubiri. Hawacheki na wowote, wamejaa kauzi utafikiri wanalipwa mamilioni.
Kichekesho sasa, wanapenda sifa za kijinga kufa mtu Ukikutana naye ukamwambia "Mambo vipi Afande?" au "Inakuwaje Kamanda/Soja?" basi utaona anachekelea hadi jino la mwisho. Anajiona yeye ndio CDF wa mtaa. Anakuwa rafiki yako kisa sifa za kijinga, roho mbaya inamshuka kidogo. Hivi hawa mbwa wana shida gani kichwani

Mfano Huyu Juma huyu Juma nilimpokea mimi mwenyewe kutoka kijijini miaka 7 iliyopita. Alikuja hana mbele wala nyuma, hata shule ya msingi la saba hakumaliza, hajui hata kusoma vizuri. Sasa hivi amefanikiwa kuingia kwenye hizi kamati za Nyungu za mtaani. Ohoo! Kujikuta sasa hivi kumepitiliza.

Mtaani hacheki na mtu kabisa, yani akipita anajiona yeye ndio mmiliki wa mji. Kumbe ukweli ni kwamba, elimu yenyewe hana, na hata angefika kidato cha nne Form 4 nchi hii ajira hakuna angeishia hapo hapo.

Cha kusikitisha sasa, huyu Juma na washirika wake wakiwa mtaani wanajifanya wajuaji mbele ya watu wasiojua sheria wala haki zao.

Wanawatishia raia, wanasingizia watu makosa, na kujifanya wao ndio mahakama na polisi kwa pamoja. Wananyanyasa watu wanyonge kisa tu wenevaa vile viraka vyao na kushika virungu

Wakikuotea Usiku Mkubwa Hapa sasa ndio utajua hawana tofauti na wanyama. Ole wako wakukute usiku mkubwa ukitoka kwenye mihangaiko yako au mtoko. Hawataki maelezo, hawataki kuelewa. Utawekwa chini ya ulinzi na kuanza kutembea nao mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba. Unakuwa kama mateka wao!

Utalinda nao doria usiku mzima kwenye baridi kali hadi asubuhi pasipo makosa yoyote ya msingi, kisa tu unakatalia kutoa hela ya sigara au "chai"

Wanakupelekesha utafikiri wewe ni mhalifu wa kimataifa, kumbe ni njaa tu inawasumbua. Wakikukuta na mpenzi wako ndio kabisa, wataanza kukutolea maneno machafu ya kashfa na kukutishia kuwapeleka polisi ili tu muwaongezee dau la rushwa.

Mna roho mbaya kwa sababu mnaumia kuona wenzenu wamepambana na wana maisha yao mazuri, wakati ninyi mnaambulia kulipwa posho za elfu mbili mbili za mchango wa ulinzi wa kila nyumba, tena kwa mbinde

Kazi yenu kubwa imebaki kuwa ni kukamata machokoraa, kufukuza kuku mtaani, na kukimbiza wamachinga wanaouza nyanya barabarani. Hiyo ndio "level" yenu ya juu kabisa ya uafande.

Mkishalewa viroba vya jioni mnaanza kujiona ninyi ni makomando wa JWTZ waliorudi kutoka vitani DRC. Amkeni ninyi! Hamna hadhi hiyo na hamtakuja kuipata kwa tabia zenu hizo za kishamba.

Hapa najiuliza swali moja la msingi sana, Hawa watu wenye njaa zao na elimu za kuunga-unga, wakija kufanikiwa kuvaa magwanda ya uaskari kamili wa JWTZ au Polisi, si watavunja watu miguu na viuno mitaani

Kama tu cheo cha kuvaa viraka na virungu vya miti kinawapa ulevi wa namna hii na kuwafanya wajione miungu watu, wakipewa SMG si watamaliza raia

Wagambo na Sungusungu acheni ushamba. Kazi yenu ni kulinda usalama wa raia na mali zao, sio kuleta uafande wa mchongo, unyanyasaji, na roho mbaya kwa watu waliowapokea mjini.

Najua humu JF mmo wengi mnaofanya hii kazi ya Nyungu na mnasoma huu uzi mkiwa mmekunja sura zenu za kauzu. lakini ukweli ndio huo ushawafika kooni

MWISH
 
Unachosema baharia 1 ni kweli hawa jamaa wana misifa na ukatili wa hali ya juu, nakumbuka mwaka 2018 walinikamata maeneo ya Kigamboni ilikuwa mishale ya saa 8 usiku aisee walini harass sana , walinifanya kama Yesu alivyofanywa na Wayahudi tena siku hiyo nilikuwa ganzi (Hangover) na nilikuwa tayari nimeshanyoosha mikono ku surrender 😄

Nilijieleza vizuri kwamba nilikuwa na jamaa yangu tumepoteana bahati mbaya na sehemu tuliyokuwa nimepotea nisaidieni kunipeleka wakanipeleka kwenye ile Bar yaani kilichosaidia pale kulikuwa na jamaa tulisoma wote miaka ya nyuma japo alikuwa amenizidi kama madarasa matatu mbele. Na jamaa mwingine ni Mshua sana yale maeneo na wanamheshimu kwa sababu huwa anawarushia makombo kama mbwa (Hela, viatu na suruali ambazo jamaa kazichoka au zimepitwa na fashion) .

Jamaa ni makatili na hawa ubinadamu kabisa.
 
Unachosema baharia 1 ni kweli hawa jamaa wana misifa na ukatili wa hali ya juu, nakumbuka mwaka 2018 walinikamata maeneo ya Kigamboni ilikuwa mishale ya saa 8 usiku aisee walini harass sana , walinifanya kama Yesu alivyofanywa na Wayahudi tena siku hiyo nilikuwa ganzi (Hangover) na nilikuwa tayari nimeshanyoosha mikono ku surrender [emoji1]

Nilijieleza vizuri kwamba nilikuwa na jamaa yangu tumepoteana bahati mbaya na sehemu tuliyokuwa nimepotea nisaidieni kunipeleka wakanipeleka kwenye ile Bar yaani kilichosaidia pale kulikuwa na jamaa tulisoma wote miaka ya nyuma japo alikuwa amenizidi kama madarasa matatu mbele. Na jamaa mwingine ni Mshua sana yale maeneo na wanamheshimu kwa sababu huwa anawarushia makombo kama mbwa (Hela, viatu na suruali ambazo jamaa kazichoka au zimepitwa na fashion) .

Jamaa ni makatili na hawa ubinadamu kabisa.
Ndo walivyo
 
Sheria hawazijui wale watu wanakandamizaga kesi zao kwa kuangalia pesa ipo upande gani.

Na wengi wao ni masikin wamechokaaaa, na hao kuwa na maisha mazuri wasahau tu.

Huwa najiulza sijui ni laana ya mate ya watu kulalamika ndo maana hawatajikagi au elimu hawana?
weng maisha ni duni
 
Ndo walivyo uzeeni wanakuwa walinzi
 
Pole kwa kilichokukuta ndugu yangu.

Nakumbuka namimi 2017 huku vibaka walizidi sana mitaa yetu, leo limeibiwa duka pale kesho mtaa ule n.k. Wazee wakakubaliana kila familia yenye kijana tunapangiana zamu kulinda usiku kwa kushirikiana na hao migambo.

Nikiwa likizo nikapangwa zamu, mnagawana makundi yanapita kila mtaa, saa kumi na moja mnatawanyika.

Ilikuwa mbaya tukikutana na mtu, ilikuwa heri akimbie tu [ hapo yupo na piki piki anapigwa fimbo mgongoni, mawe n.k], akiwa kwa mguu ujieleze pasipo kueleweka ni utalinda usiku wote/ utapigwa.

Lakini ilikuwa ni ile hasira ya kukesha usiku, baridi. Vibaka nao wakiona hivyo wanajua hamuwezi fanya maisha yenu yote,wanaacha.

Haikuenda siku wazee wakakubaliana kutoa elf 2 ili wagambo ndiyo wawe wanafanya hiyo kazi usiku.

Ukikutana nao usiku ilikuwa ni mbaya
 
[emoji23]
 
[emoji23]

Kuna mzee wangu ni wa town kitambo, sasa kuna siku akajisahau akapita anaendesha baiskel stand acha mgambo wankamate na kudai faini ya 5000[ kipindi hicho].

Alilipa ila aliwazodoa utadhani aliyeleta maada hapa ni yeye "nyie kwanza mnatoka bush mna maisha magumu kichizi mnakuja kulete mambo gani haya, tutakutana huu mji"

Walimkazia alilipa😁😁😁,mpaka anafika home anatupa maneno
 
Kuna mzee wangu ni wa town kitambo, sasa kuna siku akajisahau akapita anaendesha baiskel stand acha mgambo wankamate na kudai faini ya 5000[ kipindi hicho].

Alilipa ila aliwazodoa utadhani aliyeleta maada hapa ni yeye "nyie kwanza mnatoka bush mna maisha magumu kichizi mnakuja kulete mambo gani haya, tutakutana huu mji"

Walimkazia alilipa[emoji16][emoji16][emoji16],mpaka anafika home anatupa maneno
Hahaha noma mzee
 
Back
Top Bottom