Mtu kama huyu jibu hili halimfai hawezi kukuelewa mkuuMkuu kama umeishia Kidato cha nne swali lako halina maana kwani tayari ungekuwa na majibu.
Ili mti ukue utahitaji mambo Yafuatayo;
I. Udongo
2. Maji
3. mwanga
1. Udongo
Kidato cha nne Kama sio cha tatu kuna topic inaitwa "Soil" Kwa Kiswahili ndio huitwa UDONGO.
Udongo Una components/composition zake kama
i. Mwamba wa asili/mother rock/inorganic materials, hii ndio hutoa Madini/mineral kama madini ya chuma, calcium n.k lakini pia ndio ita-determine rangi ya udongo husika. Kama ni mweusi, mwekundu, au mweupe utatokana na Rangi ya mwamba wa asili
ii. Organic material (mimea na wanyama waliokufa kwenye udongo) hawa husaidia mmea kupata chakula kitamu chenye virutubisho vya ukuaji wa haraka.
iii. Water/ Maji haya hutumika kulainisha na kufanya decomposition ya mchakato wa utengenezaji wa udongo na chakula kwaaajilo ya mimea Kwa kushirikiana na Jotoridi(temperature) kusababisha chemical reaction
iv. Living Organisms/viumbe hai. Hapa kuna viumbe wadogo kabisa wanaoishi ndani ya udongo(macro and micro Organism)
V. Air/ hewa especially oxygen. Kwenye Udongo pia kuna hewa ya Oxygen na Carbon dioxide. Hewa ya Oxygen inasaidia wadudu wadogo waishio udongoni kupumua na kuwafanya waishi vizuri wakiwa udongo. Hewa na maji huingia udongoni kupitia soil space ambazo huitwa Soil pores (Soil porosity).
N.k
Udongo ndio chakula cha mti. Kwenye udongo kuna madini ambayo yanaumuhimu katika mmea kulingana na Aina ya mmea.
Kuna madini ya chuma, sulphate, nitrogen, calcium etc.
Kuna kitu kinaitwa Soil Formation. Yaani Kwa kimatumbi Kujitengeneza Kwa udongo.
Majibu ya swali Lako ndio yapo hapa.
Udongo unatabia ya kujizalisha/kujitengeneza kama ilivyo Kwa viumbe vingine. Ingawaje udongo bado haujatanabaishwa Kama kiumbe hai lakini unabaadhi ya tabia za viumbe hai kama kujizalisha (Reproduction/kuji-zalisha)
Soil formation ndio hufanya mtu hata uking"olewa usione uwiano wa chakula kilichotolewa udongoni kwenda kwenye mti na lile shimo lililobakia ardhini baada ya mti kung'olewa.
Hii ni Kwa sababu mtu unapokula virutubisho vya udongo, udongo nao unajizalisha.
Zingatia, ukuaji wa mimea na Miri kwenye mimea ni moja ya sababu inayopelekea uzalishaji na ukuaji wa udongo Kwa haraka na urahisi zaidi.
Hii ni tofauti na Maeneo yasiyo na Miti au mimea haya udongo haujizalishi Kwa haraka na ni rahisi kupata madhara kwani udongo unakuwa uchi. Kumbuka mimea na Miti ndio vazi la udongo.
Ili udongo usipate madhara ya weathering, mass wasting, soil erosion, basi itapasa mimea na Miti iwe juu yake kui-cover.
Kwa hiyo jibu la swali lako itakupasa uwe na Concepts kuhusu Udongo katika mambo haya;
i. Soil
ii. Soil composition
iii. Soil components
iv. Soil Formation
v. Soil profile
Ni Kama kwenye ngozi yako, ukiumia na kuchimbika, mwili unafanya mchakato wa kujitengeneza eneo Hilo Kurudi kama awali
Nafikiri Kwa kiasi kidogo utakuwa umepata majibu.