Misiba siku hizi.....'lawama tupu'.

Misiba siku hizi.....'lawama tupu'.

Aisee umenikumbusha juzi tu hapa kuna classmate wangu mmoja alifiwa na mama yake na kama alivyosema The Boss hapo juu ile kutokana na ratiba ya kuzika ilikuwa jumatatu hivyo baadhi ya jamaa wengine hawakufika ni mwendo wa kupeana updates whatsapp tu sasa ile kufika mida ya kuaga jamaa yetu mmoja akanitumia text "oyaaa nitumie picha basi" dah aisee sikumjibu chochote yule jamaa yangu

Nnachojiuliza huyu jamaa alikuwa anataka nimtumie picha ile iweje?

.....si nayeye ajione "katoa heshima ya mwisho!" .....heheh!
 
Last edited by a moderator:
Nina ndugu yangu amekulia ulaya, huwa anashangaa sana wafanyakazi wake "wakimwambia leo siji kazini kuna msiba kwa jirani" huwa anakasirika. vilevile kutokana na nature ya kazi zake huwa kuhudhuria misiba ni vigumu hivyo ndugu huwa hawamuelewi na yeye huwashaangaa jinsi wanavyopoteza muda kwenye misiba na kulala matanga nilijaribu kumuelewesha kuwa hii ni Africa unatakiwa kuhudhuria misiba hataki kuelewa anakwaambia ulaya siyo hivyo. so maisha yanabadilika itafika wakati ni ndugu tu wa karibu sna ndio watakuwa wanalala matanga.
ila na hao wafanyakazi wake wamezidi...yaani unaacha kabisa kwenda kazini? ...
 
ila kuna watu wana roho mbaya tu ..mi nilivofiwa na mama kuna mtoto wa uncle yangu hakuja kwenye msiba wala hakunitumia sms ya pole...sijui kafukuzwa kazi juzi kanitumia sms anaomba hela ...nilizima simu wiki nzima...
kuna misiba kama una utu ndani yako hutokosa muda hata wa kwenda kuonyesha sura jamani

huyu usimzimie simu, nialike tu nimfundishe pesa inapookotwa na utu unapouzwa.
 
Ha ha ha...
Labda kwa kuwa huitaji tena kuona tukio hilo...

Au hujawaza kuwa kuna ndugu wa karibu sana wa marehemu ambao hukosa kufika mazishini au msibani kutokana na udhuru wa kuwepo ng'ambo...hivyo huwekewa japo kumbukumbu.

picha za kawaida zinatosha sana
mnaweka mpiga picha mmoja tu inatosha
lakini sio kuona wau kumi au zaidi kila mtu yuko bize na simu yake ku shoot tukio
 
sijui niseme misiba ya siku hizi imekosa "huzuni/majonzi/uchungu" nilihudhuria msiba wa rafiki yangu mmoja, ningemtaja jina but mume wake ni member humu sitaki kumkumbusha machungu, mdogo wake na huyo marehemu alinishangaza sana sana, kwao wanawake ni wawili tu, dada yake amefariki lakini jamani alikuwa mkavu/mashauzi kwenye huo msiba balaa, yaani aligeuza msiba ndio sehemu yake ya kufanyia mashauzi yake ya kimjini mjini, (huwa ana mashauzi but siku hiyo aliyazidisha) sasa mtu unaona unaenda kwenye msiba kufanya nini wakati wafiwa wenyewe wana mida mpaka wa kufanya mashauzi na sio maombolezo!

kuna baadhi ya watu ustaarabu pia hawana
misiba ndo wanataka wafanye 'rusharoho' na kusutana pia
waswahili wana kazi....hii nayo inafukuza watu
 
Tena kwa simu yangu ya mkononi!

tulifiwa na rafiki yetu tuliyesoma nae chuo miaka ya nyuma, tukiwa msibani nilimnotice mskaji wanhu mmoja tuliyesoma nae pia sababu alikua amesimama juu ya kifusi cha kaburi la marehemu husika, alikua busy na simu SANA, tulipomaliza tu msiba wakt tunaondoka eneo la tukio nikawasha simu yangu zikaanza kuingia notification ya picha niyokua "tagged" ikiwa picha ya jeneza likishushwa kaburuni la rafk yangu kipnz ikiwa ni picha aliyoipost mshkaji wangu huyo dakk chache tu tena wakati hatujamaliza kuzika. Ukweli kila nikimuona nakumbuka alivyokua juu ya kifusi na "alivyokimbilia" kua wa kwanza kupost hito hbr FB. Sifurahii hii hali kwa sababu nikimuona nakumbuka alivyokua kaburini, na "anavyonikumbusha" rafk yangu aliyeteseka kwa kuugua Cancer muda mrefu.
 
Misiba sikuizi kama ni ya mtu mashuhuri au tajiri ndo utaona watu watajaa balaa. Manake wanakuwa wanajua kuwa ulabu na misosi iko level alafu kuchangishana na kidaftari hamna and then watu wakishapiga ulabu wakati wa usiku wanaanza kutongozana. Kwa aliyehuzuria msiba wa mtoto wa mzee mengi atanielewa au msiba wa huyu jaji mstaaafu aliyefariki juzi juzi sijui anaitwa nani. Kwetu wachovu msiba ni kimeo tu sikuizi ndo maana hatulazi. Ukifa asubuhi mchana tunakupiga chepe jioni tuko bar tunakula vyombo and life goes on.
 
Bora sie wachaga tunakutana bar kupanga mazishi lol

Hahahahaahahahaaaa!!!!! Hapo ndipo mnaponikosha shemeji zangu Loh!!! Tena wanaweka na matangazo kabisa kwenye redio kuwa kuna msiba kwa mzee masaawe lakini wanakutania Meeda Bar kupanga mazishi.
 
Its time haya mambo yapigwe marufuku
masuala ya kupiga picha yaachwe kwa 'mpiga picha rasmi'
ina udhi mno hasa ukimuona mtu ambae hata uchungu hana yuko bize na simu ku shoot..
 
Hahahahaahahahaaaa!!!!! Hapo ndipo mnaponikosha shemeji zangu Loh!!! Tena wanaweka na matangazo kabisa kwenye redio kuwa kuna msiba kwa mzee masaawe lakini wanakutania Meeda Bar kupanga mazishi.

Hahahaha nimecheka sana loh kumbe nikifa watu wanajikusanya bar??loh
 
ndo maisha hayo!
utu umetoweka ! ila kwenye sherehe watu wakialikwa wanawai na kukaa hadi mwisho wanywe biere!

Siku hizi tunapenda kunywa na kula na kucheza mziki. Ukiingia maofisini watu wanazungumzia michango ya harusi tu hukuti wakizungumzia michango ya kusomesha watoto!
 
ndo maisha hayo!
utu umetoweka ! ila kwenye sherehe watu wakialikwa wanawai na kukaa hadi mwisho wanywe biere!

Umesahau kitu kimoja mama Sherehe zinawekwa kwenye ratiba ndo maana tunazipangia mda na tunajipanga kushiriki, kama vipi tuambie lini utapatwa na msiba uone kama hatutahudhuria. Kiukweli misiba sasa hivi tumeanza kuichukulia poa kwasababu imekuwa mingi na huingiliana na ratiba zingine za kila siku.

Mimi nina jirani yangu mmoja mtu mzima sana ni mstaafu imefika mahala tumekosana kwasababu anachonga sana kuhusiana na ushiriki wangu kwenye misiba, Mimi nayeye tunaishi Tegeta sasa ni mara kibao hunishirkisha misiba ya ndugu zake, mingine inatokea Mbagara, Sinza, Tabata. Kibamba na misiba yenyewe ni ya binamu, mpwa nakadhalika sasa yeye anataka nihudhulie misiba yoote hii kisa ni jirani yangu,...Bfuuuuuuuuuuuuuuu
 
Zamani watu tulikuwa masikini zaidi
na tuna muda zaidi
siku hizi misibani magari tu yanapishana but watu wako too busy....
hawana time
kila mtu kaja 'kuzuga'
Right man, Tena siku hizi tuna classify na kuchagua Msiba wakuhudhuria upi na upi... Taazia ni by cm/email or calls !!
Mungu atusamehe...AMIN
 
Umesahau kitu kimoja mama Sherehe zinawekwa kwenye ratiba ndo maana tunazipangia mda na tunajipanga kushiriki, kama vipi tuambie lini utapatwa na msiba uone kama hatutahudhuria. Kiukweli misiba sasa hivi tumeanza kuichukulia poa kwasababu imekuwa mingi na huingiliana na ratiba zingine za kila siku.

Mimi nina jirani yangu mmoja mtu mzima sana ni mstaafu imefika mahala tumekosana kwasababu anachonga sana kuhusiana na ushiriki wangu kwenye misiba, Mimi nayeye tunaishi Tegeta sasa ni mara kibao hunishirkisha misiba ya ndugu zake, mingine inatokea Mbagara, Sinza, Tabata. Kibamba na misiba yenyewe ni ya binamu, mpwa nakadhalika sasa yeye anataka nihudhulie misiba yoote hii kisa ni jirani yangu,...Bfuuuuuuuuuuuuuuu

Uniaishi Tegeta halafu mtu anakwambia
shangazi wa mke wake kafariki,msiba upo gongo la mboto,hapo lawama..
 
hivi tulikupeleka jumla?
si tulisema mtatenganishwa na kifo?
ukifa mnakuwa mmetengana, so tutakuchukua tivembayi mpaka mihu gamema ngo!
suti na msiba wapi na wapi, hakuna kuoga mpaka tutoke makaburini

eheheheh yani wewe ndo utatia huruma mpka utanifanya nitamani kuamka!
chaaa!
 
Hahahahaahahahaaaa!!!!! Hapo ndipo mnaponikosha shemeji zangu Loh!!! Tena wanaweka na matangazo kabisa kwenye redio kuwa kuna msiba kwa mzee masaawe lakini wanakutania Meeda Bar kupanga mazishi.

we mi nikifikiria hiyo scenario ya msiba wangu kuwekwa baa!ujue natamani nijiwowe!
acha tu!
 
Misiba sikuizi kama ni ya mtu mashuhuri au tajiri ndo utaona watu watajaa balaa. Manake wanakuwa wanajua kuwa ulabu na misosi iko level alafu kuchangishana na kidaftari hamna and then watu wakishapiga ulabu wakati wa usiku wanaanza kutongozana. Kwa aliyehuzuria msiba wa mtoto wa mzee mengi atanielewa au msiba wa huyu jaji mstaaafu aliyefariki juzi juzi sijui anaitwa nani. Kwetu wachovu msiba ni kimeo tu sikuizi ndo maana hatulazi. Ukifa asubuhi mchana tunakupiga chepe jioni tuko bar tunakula vyombo and life goes on.

MSIBA WA MASKINI NI MZIGO KWA JAMII
bali MAZISHI YA TAJIRI NI SIKUKUU KWA MASKINI!
 
Back
Top Bottom