Misiba siku hizi.....'lawama tupu'.

Misiba siku hizi.....'lawama tupu'.

Mi nafkir tamaduni za makabila zinachangia sna katima hili!
Mngoni bana ili ajue umeenda kwenye msiba wake ulale!tena ulale chini kwenye mkeka!uondoke aljafiri!shurti mlango wa nyumba yenye msiba unakuwa mlango wazi full time,kwaya na nyimbo usiku kucha
na kama ni mfiwa shurti uwe na kilemba!ukae ile kufiwa hasa!sio maswala ya kutuletea fasheni !
iiila sasa kwa wakwe zangu na mashemeji zangu kina Nicas Mtei na Mkirua msibani tunavaa suti,tunakutana bar,tunachangisha hela!tunasubiri siku ya kupeleka mwili muhimbili tumsafirishe mgombani!
uuuuwih nawaone huruma sana ndugu zangu siku ya kuzikwa mimi!
wanaweza kukata rufaa kuwa sijatetendewa haki asee!msiba wa mtoto wao bar??
hivi tulikupeleka jumla?
si tulisema mtatenganishwa na kifo?
ukifa mnakuwa mmetengana, so tutakuchukua tivembayi mpaka mihu gamema ngo!
suti na msiba wapi na wapi, hakuna kuoga mpaka tutoke makaburini
 
mimi binafsi sijawahi ona umuhimu wala faida ya ku shoot jeneza kuingia kwenye kaburi

Ha ha ha...
Labda kwa kuwa huitaji tena kuona tukio hilo...

Au hujawaza kuwa kuna ndugu wa karibu sana wa marehemu ambao hukosa kufika mazishini au msibani kutokana na udhuru wa kuwepo ng'ambo...hivyo huwekewa japo kumbukumbu.
 
shangaa sasa muda wa kwenda bar na kwenye sherehe unavyopatikana, but msibani no.
yaani huwa najitahidi sana kuhudhuria misiba, hasa ya watu wangu wa karibu na majirani, hata kama nimen=banwa nitatafuta tu muda niende
kweli dear unakuwa na kimtandio kwenye pochi jioni ukitoka job unapitia kuonyesha sura kama the boss alivosema maisha yanaenda....hayo ya muda ni roho mbaya tu hakuna jingine
 
ila kuna nyumba wao pia hawahudhurii misiba ya wenzao, wanaenda kuonyesha sura tu na kutoa mshiko. watu huwa wanasoma sana na wanalipiziana kisasi.
kuna mama (kijijini) alikuwa hali kwenye misiba ya wenzake, siku akafiwa, watu wakajaa, wakapika vyakula kibao lakini hakuna aliyekula. Fikiria kijijini watu wanavyoshobokea wali na nyama lakini siku hiyo vya bure na hawakula

sijui niseme misiba ya siku hizi imekosa "huzuni/majonzi/uchungu" nilihudhuria msiba wa rafiki yangu mmoja, ningemtaja jina but mume wake ni member humu sitaki kumkumbusha machungu, mdogo wake na huyo marehemu alinishangaza sana sana, kwao wanawake ni wawili tu, dada yake amefariki lakini jamani alikuwa mkavu/mashauzi kwenye huo msiba balaa, yaani aligeuza msiba ndio sehemu yake ya kufanyia mashauzi yake ya kimjini mjini, (huwa ana mashauzi but siku hiyo aliyazidisha) sasa mtu unaona unaenda kwenye msiba kufanya nini wakati wafiwa wenyewe wana mida mpaka wa kufanya mashauzi na sio maombolezo!
 
kuna siku rafiki yetu alifiwa na kakake. sasa tupo wamama kama wa4 hivi tunaojua tupo karibu na huyo mama. mama wa watu katuambia kuwa kakake kafariki na wanategemea kusafirisha kama baada ya siku 4. siku ya kwanza kila mtu anatoa kisingizio. siku ya pili, bila bila.... sasa mimi nikawa sijisikii vizuri, napiga simu kwa kila mtu ana kisingizio, siku ya 3 nikawaambia mimi naenda peke yangu, siwezi hii aibu, hivi akirudi tutamwangaliaje? nikawaambia wote kuwa nina mpango wa kuondoka home saa fulani kwenda huko, hata kama nitakuwa alone. kufika huo muda kila mtu alikuja kwangu tukaanza safari ya kwenda huko.
Wakati mwingine watu siyo kama wanakuwa wamebanwa kihivyo ila tu naona kama misiba imepunguza mvuto, watu hawajali sana. mbona watu kwenye masherehe wanaenda? sijawahi hudhuria sherehe ikakosa wahudhuriaji, sijui kwa vile watu wanakuwa walichangia kwa hiyo wanaenda kula/kunywa hela zao?

Hapo kwenye red. Utakuta wa dada wiki nzima wako busy kutafuta viwalo vya kuvaa siku ya sherehe
 
baadhi ya wakristo skuhzi wanatumia ule mstari wa "waache wafu wawazike wafu wao." ila pia inakera jaman mtu amefiwa, ndugu zake tunawafaham, wako jirani na kwake ila mnafka wao walengwa hawaji. wafiwa wengne wenzao walipofiwa walituma mchango kwa m-pesa ama tigo pesa, yakiwafika wao watategemea watu waje kuwamfariji!!?? Maeneo mengne marehem wakati wa uhai wake alikuwa mtu wa dharau, hapendi wengne, hahudhurii misiba wala sherehe, iweje afarki yeye watu wamjali?? Kawaida bnadam tunaroho za visasi..you do me, I do you.
 
Kwa kweli, mara ya kwanza naingia Dar kwa mafuriko ya el nino, nlishangaa sana misiba ya huku inavyoendeshwa. naongelea misiba inayotokea kwa majirani. Hakuna utaratibu maalumu wa kupeana taarifa kwa majirani, kama ni mtu bize utasikia "mzee fulani kafariki jana na tumezika', mie nikawa nabaki, how:yuck:?

Sehemu nilyoanzia kufanya kazi walinishangaa mno, niliacha kwenda kazini kisa next door kuna msiba, nikatoa tu taarifa kuwa siendi sababu nina msiba. Kutokana na nilikokulia, utaendaje kazini na next door kuna msiba? Tena jirani wa karibu ndie mtu anayehusika kusaidia kuhakikisha mambo yanaenda kama yalivyopangwa.
Sie akina mama ni kusimamia waombolezaji wanakula, chakula kinaiva kwa wakati, nyumba iko kwenye usalama(maana wafiwa wa karibu wengine huchanganyikiwa). Mwanamme nao wana ya aina hiyo kwa dizaini.

Lakini Dar, akina mama waviiiiiiivu, kupika tu wanategeana, usiongelee kuosha vyombo na au kuchota maji kama sehemu hiyo hawana. Mie nilichoka sana misiba ya Dar, nikagundua nilikotoka(tena shamba wala hatuna wasomi kivile, common sense tu) tulikuwa na utaratibu mzuri.

Anyway, misiba ya Dar ni majanga sana! Huu utamaduni wa Dar ushakuwa mchanganyiko sana, sijui wazawa zamani walikuwa wanafanyaje, maana wakuja tushawaharibia labda utaratibu ulokuwepo.
 
Ujue Nyamayao mie huwa nasema, 'kila msiba una mfiwa wake'. Na mfiwa si lazima awe ndugu au rafiki wa karibu. Katika msiba kuna mtu huwa anaguswa haswaa, hahitaji kupretend na wala hawaoni hata mloenda kuhani pale. Anakuwa kwenye majonzi kukweli kabisa.


Nikupe mfano, niliwahi kwenda msibani mahali. Nikapewa nafasi ya haitebo ya msiba kwa sababu kadha wa kadha, lakini sikuwa na amani rohoni maana nilijua kiti kile alitakiwa kupewa mtu mwingine na mtu huyo nilimwona na nikajua 'yeye ndio mfiwa'(she was devastated, na alikuwa kwenye dunia yake peke yake ya majonzi, sijui hata kama alikuwa anaona kuna watu wengine au alijiona yuko msituni peke yake, mbaya zaidi hakuna aliyemfikiria). Sometimes tunakuwa hatuwajui wafiwa wa kweli, tunaishia kufikiri fulani ndio mfiwa sababu ya 'uhusiano' uliopo na mfiwa awe kaka/dada/mme/mke/, lakini kumbe kuna watu huwezi kuainisha uhusiano wao formally lakini deep inside wana mahusiano makubwa zaidi ya haya tunayoyaona.

So ukiona mtu anajishaua msibani, jua huyo si mfiwa wa huo msiba hata kama ni baba, mama, mke. au mme wa marehemu.
sijui niseme misiba ya siku hizi imekosa "huzuni/majonzi/uchungu" nilihudhuria msiba wa rafiki yangu mmoja, ningemtaja jina but mume wake ni member humu sitaki kumkumbusha machungu, mdogo wake na huyo marehemu alinishangaza sana sana, kwao wanawake ni wawili tu, dada yake amefariki lakini jamani alikuwa mkavu/mashauzi kwenye huo msiba balaa, yaani aligeuza msiba ndio sehemu yake ya kufanyia mashauzi yake ya kimjini mjini, (huwa ana mashauzi but siku hiyo aliyazidisha) sasa mtu unaona unaenda kwenye msiba kufanya nini wakati wafiwa wenyewe wana mida mpaka wa kufanya mashauzi na sio maombolezo!
 
Tena kijijini kwetu ukifiwa wala unakuwa huna mawazo ya kuwa mambo yataendaje. wewe kazi yako ni kulia na kushughulikia mambo machache sana.
wamama wanakuja na kuku na unga, na maharage, na kuni, na maji. watapika, na kufanya kila kitu.
Wababa watahakikisha kaburi limechimbwa na maandalizi yote ya mazishi yanakuwa sawa. muda ukifika ni kujinyanyua tu na kwenda kuzika.
Mjini tatizo mashauzi mengi, msibani ndo sehemu ya kuonyeshea mna uwezo kiasi gani, yaani hata wewe ukienda inabidi ukae kando maana usije ukaharibu, ni majanga.
nadhani watu sasa wanaona waende kufanya nini, ni hela inatakiwa atatuma kwa mpesa, muda wa kuzika tunakutana makaburini

Kwa kweli, mara ya kwanza naingia Dar kwa mafuriko ya el nino, nlishangaa sana misiba ya huku inavyoendeshwa. naongelea misiba inayotokea kwa majirani. Hakuna utaratibu maalumu wa kupeana taarifa kwa majirani, kama ni mtu bize utasikia "mzee fulani kafariki jana na tumezika', mie nikawa nabaki, how:yuck:?

Sehemu nilyoanzia kufanya kazi walinishangaa mno, niliacha kwenda kazini kisa next door kuna msiba, nikatoa tu taarifa kuwa siendi sababu nina msiba. Kutokana na nilikokulia, utaendaje kazini na next door kuna msiba? Tena jirani wa karibu ndie mtu anayehusika kusaidia kuhakikisha mambo yanaenda kama yalivyopangwa.
Sie akina mama ni kusimamia waombolezaji wanakula, chakula kinaiva kwa wakati, nyumba iko kwenye usalama(maana wafiwa wa karibu wengine huchanganyikiwa). Mwanamme nao wana ya aina hiyo kwa dizaini.

Lakini Dar, akina mama waviiiiiiivu, kupika tu wanategeana, usiongelee kuosha vyombo na au kuchota maji kama sehemu hiyo hawana. Mie nilichoka sana misiba ya Dar, nikagundua nilikotoka(tena shamba wala hatuna wasomi kivile, common sense tu) tulikuwa na utaratibu mzuri.

Anyway, misiba ya Dar ni majanga sana! Huu utamaduni wa Dar ushakuwa mchanganyiko sana, sijui wazawa zamani walikuwa wanafanyaje, maana wakuja tushawaharibia labda utaratibu ulokuwepo.
 
Kwa kweli, mara ya kwanza naingia Dar kwa mafuriko ya el nino, nlishangaa sana misiba ya huku inavyoendeshwa. naongelea misiba inayotokea kwa majirani. Hakuna utaratibu maalumu wa kupeana taarifa kwa majirani, kama ni mtu bize utasikia "mzee fulani kafariki jana na tumezika', mie nikawa nabaki, how:yuck:?

Sehemu nilyoanzia kufanya kazi walinishangaa mno, niliacha kwenda kazini kisa next door kuna msiba, nikatoa tu taarifa kuwa siendi sababu nina msiba. Kutokana na nilikokulia, utaendaje kazini na next door kuna msiba? Tena jirani wa karibu ndie mtu anayehusika kusaidia kuhakikisha mambo yanaenda kama yalivyopangwa.
Sie akina mama ni kusimamia waombolezaji wanakula, chakula kinaiva kwa wakati, nyumba iko kwenye usalama(maana wafiwa wa karibu wengine huchanganyikiwa). Mwanamme nao wana ya aina hiyo kwa dizaini.

Lakini Dar, akina mama waviiiiiiivu, kupika tu wanategeana, usiongelee kuosha vyombo na au kuchota maji kama sehemu hiyo hawana. Mie nilichoka sana misiba ya Dar, nikagundua nilikotoka(tena shamba wala hatuna wasomi kivile, common sense tu) tulikuwa na utaratibu mzuri.

Anyway, misiba ya Dar ni majanga sana! Huu utamaduni wa Dar ushakuwa mchanganyiko sana, sijui wazawa zamani walikuwa wanafanyaje, maana wakuja tushawaharibia labda utaratibu ulokuwepo.

misiba ya siku hizi haipikwi na majirani/marafiki, labda uwe kapuku kama nyamayao hapa la sivyo ni wapishi wa kulipwa wanafanya kazi yao hapo, nyie mtaaombwa tu mkale bufee kama 6 hivi zimezunguka hapo msibani, my colleague alifiwa na mke wake tukaenda kiteto kuzika, jamani nilipenda maisha ya huko mbaya kabisa, wafiwa wao hawajigusi kabisaaaa, kila jirani anakuja na chochote, wafiwa hamtoi hata senti kumi yenu mpaka siku ya kuvunja matanga,msiba ukitokea tu wanajipanga wa kuandaaa kuanzia chai mpaka chakula cha usiku, haya ndio maisha.
 
hiyo ni kwako tu mkuu na wachache wa kaliba yako, ila bado kule vijijini na sehemu nyingine hapa mjini watu wanahudhuria misiba na hata kusafiri mikoani kuzika..utu umepungua kiasi kutokana na hali ya maisha lakini si katika kiwango cha kukuta msiba unakosa watu...
 
Bora msiba hata wanatuma pesa. Uugue sasa au uwe unauguza ni mwendo wa text tu, halafu hawa ndo marafiki wa karibu wengine akituma text alikuwa anawaza deal akakumbuka unaumwa ndo anakutumia pole.
Harusi zenyewe wanakuja ili akiwa na shughuli na wewe umchangie.
Bado kidogo tu, itakuwa msiba, ugonjwa, harusi ni familia tu ndo watakuwa wahusika pekee.

exactly the point
harusi ni kuwa na wao wanataka tu kuchangiwa
 
sijui niseme misiba ya siku hizi imekosa "huzuni/majonzi/uchungu" nilihudhuria msiba wa rafiki yangu mmoja, ningemtaja jina but mume wake ni member humu sitaki kumkumbusha machungu, mdogo wake na huyo marehemu alinishangaza sana sana, kwao wanawake ni wawili tu, dada yake amefariki lakini jamani alikuwa mkavu/mashauzi kwenye huo msiba balaa, yaani aligeuza msiba ndio sehemu yake ya kufanyia mashauzi yake ya kimjini mjini, (huwa ana mashauzi but siku hiyo aliyazidisha) sasa mtu unaona unaenda kwenye msiba kufanya nini wakati wafiwa wenyewe wana mida mpaka wa kufanya mashauzi na sio maombolezo!
unakumbuka ule uzi wangu kuhusu mdada niliyemkuta salon anajiremba sababu kafiwa na kakake?
mtu kama huyo unaweza kumweka kwenye kundi la "wafiwa"?
sidhani kama misiba imekosa msisimko, nadhani kuna baadhi ya watu tu wanashindwa kuelewa maana ya kuondokewa. dot com imewachanganya, wanaiga mambo ya wenzetu huko nje.
Kuna siku nilikuwa naongea na mama mmoja wa kijapani akawa analalamika kuwa anafurahi sana kwa sasa nchi yao ina maendeleo lakini anasikitika social life haipo tena, wana-miss social life, hii ambayo sisi tunayo wao hawana. hili hatutakuja kuliona sasa mpaka tutakapopoteza kabisa. Mtu kwenda kwa wazazi wako mwenyewe hata kusalimia tu lazima uombe na wao wakupangie masaa ambayo wanaweza kuonana nawe.....hao ni wazazi.
 
Back
Top Bottom