Heh! My dear, tembea Dar hii uone. Sikatai kuna misiba hapa Dar, unaweza jisahau ukabeba ndizi, pilipili na tuthipik kwenye pochi (ujue chakula cha watu wengi kinakuwa kitamu, hata kama kwako unapika kila siku, hasa muwe mmenda mashostito story zinaiva), maana ni bufee la maana.
Lakini, Dar hii hii kuna sehemu nilikuta msiba wanakunywa uji, Nilikuwa shocked.
Na kuna sehemu akina mama wanasaidia kupika vizuri tu, ila tatizo ni wavivu, wanafanya kazi kwa rimotu(midomo) tu. Sasa nyie kina mama vijana mtatumwa hadi mtie adabu, unasikia tu 'mama fulani hebu unga maharage hapo, ujue sie wazee sana'. Ila piga ua, hiwa sipiki ugali msibani, naogopa kupika ugali wa kisukuma watu wakabwe bure, umechambuka kama karanga.