Misiba siku hizi.....'lawama tupu'.

Misiba siku hizi.....'lawama tupu'.

Labda pengine tujaribu pia kufikiri, kama ni sisi ndio tumefiwa tungependa kutendewa vipi na ndugu jamaa na marafiki? Itatosha kuchangiwa pesa tu? Vipi kama ukifiwa halafu jamaa zako wakakuchangia pesa na kisha kukuacha mwenyewe? Kama tunaamini pesa peke yake haitatosha, je ni kwa nini tunadhani kuwachangia pesa tu wenzetu inatosha?

Ukitizama kwa makini unaona kupotea/kutokuwepo kwa upendo wa dhati, ubinafsi na zaidi unafiki. Sawa tupo 'bize' na sababu nyingine, lakini vipi ikitutokea sisi na wenzetu wakasema wapo 'bize'?
 
Nakumbuka wakati baba yangu mzazi anafariki, iliambatana pia na tukio la harusi ya jamaa yangu (ambaye nafanya naye kazi), infact nilishindwa kuchangia harusi hiyo kwani gharama za kuuendesha msiba wa baba yangu zilikuwa zinanielemea, zaidi nililazimika kuisafirisha familia yangu yote kwenda kijijini (mkoa tofauti) ili wajukuu nao wapate wasaa wa kumzika babu yao, cha kushangaza mpaka leo jamaa naona hatuko naye vizuri eti kwa sababu sikuchangia katika harusi yake ambayo ilifanyika majuma mawili baada ya mazishi ya baba yangu!Lakini pia, hata yeye hakuona kama kuna umuhimu wa kunipa pole japo ya mdomo pamoja na kwamba ninakili ya kuwa alikuwa bize sana na shughuli za harusi yake! HII INANIFANYA NIAMINI YA KUWA SIKU HIZI WANADAMU TUMEINGIA KASUMBA YA KUZITHAMINI SAAANA HARUSI NA SHEREHE ZINGINEZO KULIKO MISIBA!
 
labda pengine tujaribu pia kufikiri, kama ni sisi ndio tumefiwa tungependa kutendewa vipi na ndugu jamaa na marafiki? Itatosha kuchangiwa pesa tu? Vipi kama ukifiwa halafu jamaa zako wakakuchangia pesa na kisha kukuacha mwenyewe? Kama tunaamini pesa peke yake haitatosha, je ni kwa nini tunadhani kuwachangia pesa tu wenzetu inatosha?

Ukitizama kwa makini unaona kupotea/kutokuwepo kwa upendo wa dhati, ubinafsi na zaidi unafiki. Sawa tupo 'bize' na sababu nyingine, lakini vipi ikitutokea sisi na wenzetu wakasema wapo 'bize'?

swali zuri hili
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Tena kijijini kwetu ukifiwa wala unakuwa huna mawazo ya kuwa mambo yataendaje. wewe kazi yako ni kulia na kushughulikia mambo machache sana.
wamama wanakuja na kuku na unga, na maharage, na kuni, na maji. watapika, na kufanya kila kitu.
Wababa watahakikisha kaburi limechimbwa na maandalizi yote ya mazishi yanakuwa sawa. muda ukifika ni kujinyanyua tu na kwenda kuzika.
Mjini tatizo mashauzi mengi, msibani ndo sehemu ya kuonyeshea mna uwezo kiasi gani, yaani hata wewe ukienda inabidi ukae kando maana usije ukaharibu, ni majanga.
nadhani watu sasa wanaona waende kufanya nini, ni hela inatakiwa atatuma kwa mpesa, muda wa kuzika tunakutana makaburini
Kibaya zaidi eti twataka tushone na sare za msibani, twende na saluni kupakwa poda na kutindanyusi, kweli zama za mawe zimepita huwa najiuli kweli unauchungu wa kuondokewa na mpendwa wako utawaza ya kwenda saluni au kushona sare.

Najua ziko sherehea tatu, na kila sherehe ina mandhari yake na msiba kiukweli una madhari yake lakini siku hizi kuiga ulaya kila kitu mpaka tunakodi eti watu wa kulia kwenye msiba. Kweli Mungu atuhurumie. kiufupi aliyefiwa na mpendwa wake ndiye pekee anayejua uchungu wa msiba. mengine madoido tu na kujishoo off.

NI VEMA KUTENGA MUDA WA KUMSHUKURU MUNGU KWA KUWA UHAI WETU U MIKONONI MWAKE...........
 
Nakumbuka wakati baba yangu mzazi anafariki, iliambatana pia na tukio la harusi ya jamaa yangu (ambaye nafanya naye kazi), infact nilishindwa kuchangia harusi hiyo kwani gharama za kuuendesha msiba wa baba yangu zilikuwa zinanielemea, zaidi nililazimika kuisafirisha familia yangu yote kwenda kijijini (mkoa tofauti) ili wajukuu nao wapate wasaa wa kumzika babu yao, cha kushangaza mpaka leo jamaa naona hatuko naye vizuri eti kwa sababu sikuchangia katika harusi yake ambayo ilifanyika majuma mawili baada ya mazishi ya baba yangu!Lakini pia, hata yeye hakuona kama kuna umuhimu wa kunipa pole japo ya mdomo pamoja na kwamba ninakili ya kuwa alikuwa bize sana na shughuli za harusi yake! HII INANIFANYA NIAMINI YA KUWA SIKU HIZI WANADAMU TUMEINGIA KASUMBA YA KUZITHAMINI SAAANA HARUSI NA SHEREHE ZINGINEZO KULIKO MISIBA!

Kitu kimoja tu kitajengwa na haya yote ni upendo, utu na mshikamano. Hii siku zote itakuwa nii kauli mbiu yangu maana yalinigusa na mpaka leo siezi sahau na kila nikikumbuka majonzi hayanishi. pale nilipopigiwa simu na kuambiwa "my aunt passed away at Ubungo accident" unajua nilichojibu usiniambie ile ajali ya Ubungo yule mama aliyefariki ndiye................... sikuweza kuendelea zaidi ya kurukwa na akili na kuchanganyika ukizingatia kama masaa manne nilikuwa namhadithia mtu kuhusu ile ajali ya Ubungo na kuhusu yule mama pekee aliyefariki tena kwa........ bila kujua alikuwa ni mpendwa wangu wa damu ingawa sijui kwa nini kila mara kabla ya taarifa nilikuwa kila mtu namuuliza kama amesikia ile ajali ya Ubungo (kwa wanaoikumbuka ya lile tenka la mafuta) Ni huzuni isiyonisha mpaka kesho kila nikikumbuka. nabaki Kushukuru Mungu kwa kuwa ndiye mfariji wetu.

So ndugu ukiona mtu anajishebedua ndio hivyo kimpango na kutimiza wajibu lakini ukipatwa huwezi kumbuka ya kujishebedua sijui mara miwani ya giza, mara tisheti, mara sijui nini....... lakini ah! ndio hali labda kama wazazi tujitahidi vizazi hivi visiwe vibaya zaidi maana tuendako ni kubaya itafikia kukodi watu wa kuzika maana ndugu, jamaa, na rafiki hawana muda wako bize na maisha yapitayo kama waridi.
 
......e bana wee, itafikia zile za " mnazika? Nirushie vdo ya tukio kwa whatsapp!"

Yaani ili na yeye azike kupitia whatsapp ama? Hii kali, yaani mtu uko baa unarushiwa video then ghafla unakaa kimya washikaji wanakuuliza vipi mwenzetu, eti unazika rafiki yako kupitia whatsapp. Wabongo, yaani huko tunakokwenda mbona pana raha bin vituko.
 
.....ndio maana yake, tayari yapo haya!
 
.....ndio maana yake, tayari yapo haya!

Kweli? Yaani watu wanazika kwenye daladala na baa kupitia whatsapp? Basi mila na desturi yetu sasa inapotezwa na mitandao na kizazi fake (kipya).
 
Unazima simu ya nini mwishowe ukose madili hapa mjini, pokea mpe makavu live, ndo maisha, yeye si alikuwa busy wakati umefiwa, kha!

ila kuna watu wana roho mbaya tu ..mi nilivofiwa na mama kuna mtoto wa uncle yangu hakuja kwenye msiba wala hakunitumia sms ya pole...sijui kafukuzwa kazi juzi kanitumia sms anaomba hela ...nilizima simu wiki nzima...
kuna misiba kama una utu ndani yako hutokosa muda hata wa kwenda kuonyesha sura jamani
 
Back
Top Bottom