Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 16,575
- 34,707
Mkuu the boss, kuna pande mbili za shilingi.
Life style tunayokwenda nayo ni ya kuiga na tumeruka baadahi ya hatua . Matokeo yake ni haya ya Ipad, Cellphone n.k. tukidhani ndio ustaarabu.
Vijijini ambako dola 1 ndio mlo n.k. watu wamesimama katika utu, likitokea janga watachangishana hadi sanda itoke. vijana wachimbe kaburi n.k.
Huku mjini sidhani kuwa ni ubize ni suala la kutojali tu na kunakotokana na aina ya ulimbukeni.
Upande wa pili wa shilingi,misiba imekuwa sehemu ya maisha ya kileo niseme.
Siku za nyuma msiba ukitokea watu wanakusanyika kufarijiana na kuangalia kinachofuata haraka. Ilikuwa rahisi kujua mipango ya mazishi, lini na nini kinahitajika.
Siku hizi kuna timu za maandalizi ikiwemo kamati ya ulinzi na usalama!
Si ulinzi na usalama wa kitu gani.
Kuna kuchapisha t-shirt na makando kando kibao. Msiba unachukua siku 10, 8 kati ya hizo ni vitu ninavyoweza kusema havina umuhimu wa msiba bali ufahari usio na maana.
Sasa nani atahudhuria msiba kwa siku 7 mfululizo tukielewa majukumu yanabaki pale pale?
Mambo ya teknolojia na maisha ya kileo yanatakiwa yatusadie kufanya mambo kwa urahisi, yasiwe msingi wa ubinadamu na utu wetu na wala yasiingilie tamaduni zetu nzuri za kiutu.

Last edited by a moderator: